POLISIMaafisa wanne wa polisi na raia waatu wameuawa baada ya watu wasiojulikana kuvamia kituo cha polisi mjini Dar es salaam.

Polisi wamesema shambulizi hilo limetokea katika kituo cha polisi kilichoko Ukonga wakati wavamizi hao walipotekeleza shambulizi hilo la kuvizia usiku wa kuamkia leo.

Watu hao wanaosadikiwa majambazi waliwafyatulia risasi maafisa wa polisi katika kituo hicho na kuua wanne.

Aidha inasemekana kabla ya kuuliwa polisi hao majambazi hao waliba silaha 30 za polisi na idadi ya risasi isiyojulikana.

Hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kufuatia shambulizi hilo huku maafisa wa upelelezi wanaendelea na uchunguzi.

Advertisements