Archive for August, 2015

WAZIRI MKUU WA ZAMANI TANZANIA FEDERICK SUMAYE AJIUNGA NA UKAWA

Waziri mkuu wa zamani Tanzania Federick Sumaye

Waziri mkuu wa zamani Tanzania Federick Sumaye

Waziri mkuu mstaafu Fedrick Sumaye ametangaza rasmi leo kukihama chama cha Mapinduzi CCM na kujiunga na muungano wa vyama vya siasa vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA.

Akizungumza na wandishi wa habari mjini Dar es Salaam Sumaye amesema amefikia uwamuzi huo kwa kile alichokita kuendelea na nia yake ya kuwahudumiwa watanzania.

Hata hiyvyo Sumaye hakutaja chama alichojiunga, lakini amesema amejiunga na Ukawa.

Hatua hiyo ya Sumaye ya kumunga mkono aleikuwa waziri mkuu mwenzake Eduward Lowasa kuteuliwa kugombea urais wa Tanzania kupitia CHADEMA imekuja huku tume ya uchaguzi NEC ikitangaza leo kuanza rasmi kampeni za uchaguzi kwa wagombea wa vyama vya siasa kwa muda wa siku 63.

Federick Sumaye aliezaliwa mwaka 1950 alietuliwa kuwa waziri mkuu wa Tanzania Novemba 28 mwaka 1995 hadi 2005, aligombea nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano kwa vipindi viwili kupitia CCM, lakini jina lake lilienguliwa katika hatua za awali.

TUWAPE POLE NDUGU ZETU WA KICHINA

Hivi ndivyo miripuko ya kwenye bohari ilivyoteketeza gari zilizokuweko barabarani

Hivi ndivyo miripuko ya kwenye bohari ilivyoteketeza gari zilizokuweko barabarani

UKAWA KULIKONI

11866406_874189309297371_3631352832951018787_n (1)

MASHEIKH SITA WA KISLAMU WATEKWA NYARA DRC

congoSerikali ya Tanzania imeanza kuwasiliana na maafisa wa Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo DRC kufuatia madai ya kutekwa mashekhe Sita na waasi wa nchi hiyo FDRR

Naibu katibu wa jumuiya ya wanazuoni nchini Mohamed Issa amesema wamepata mshutuko mkubwa baada ya baada ya kusitikia taarifa za mashehe hao waliotekwa nyara na madereva wao

Hivyo amesema waislamu wameitaka serikali kuwasiliana na waasi hao ili kuona mashehe hao wanachiwa huru wakiwa salama

Hadi sasa hakuna taaria zaidi ya juu ya mateka hao na majina yao, lakini serikali ya Tanzania imesema inawasiliana na serikali ya DRC ili kujua hatma ya masheikh hao

Msemaji wa serikali ya Tanzania Mende Kasije amesema serikali imeanza mawasiliano kupitia balozi wake alioko mjini Kinshasa.

Hata hivyo kuna taarifa kwamba waasi wa FDRR wanadai kutaka kulipwa fidia ili kuwachia mashekhe hao.

PROFISA LIPUMBA AJITOA CUF

Profisa Ibrahim Lipumba akiwa na katibu wa CUF Malim Seif Hamad

Profisa Ibrahim Lipumba akiwa na katibu wa CUF Malim Seif Hamad

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) cha nchini Tanzania Prof. Ibrahim Haruna Lipumba leo ametangaza kujiuzulu uwenyekiti wa chama hicho. Tamko hilo la Prof. Lipumba linahitimisha siku mbili za minong’ono na tetesi zilizogubika medani ya kisiasa nchini kuwa kiongozi huyo anaondoka katika chama hicho hali iliyolazimu wananchama, wapenzi na mashabiki wa kiongozi huyo kufurika makao makuu ya chama hicho Buguruni Dar es Salaam jana ili kujua hatma ya kiongozi wao huyo. Akizungumzia sababu za kujiuzulu kwake, Profesa Lipumba amesema amekerwa na hatua ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao CUF ni chama shiriki kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo. Amesema Ukawa ulianzishwa kulinda maslahi ya wananchi yaliyoainishwa kwenye Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba, na kwamba nafsi yake inamsuta hivi sasa kuendelea na uongozi huku waliokuwa wanaipinga Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba wakikaribishwa kuwania uongozi wa nchi kupitia umoja huo. Prof. Lipumba amesema baada ya kujiuzulu atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo. Lipumba ametangaza uamuzi huo leo Mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam na kusema atabaki kuwa mwanachama wa kawaida wa CUF

NANI ZAIDI HAPA CCM OR UKAWA-2015

ccm-chadema