congoSerikali ya Tanzania imeanza kuwasiliana na maafisa wa Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo DRC kufuatia madai ya kutekwa mashekhe Sita na waasi wa nchi hiyo FDRR

Naibu katibu wa jumuiya ya wanazuoni nchini Mohamed Issa amesema wamepata mshutuko mkubwa baada ya baada ya kusitikia taarifa za mashehe hao waliotekwa nyara na madereva wao

Hivyo amesema waislamu wameitaka serikali kuwasiliana na waasi hao ili kuona mashehe hao wanachiwa huru wakiwa salama

Hadi sasa hakuna taaria zaidi ya juu ya mateka hao na majina yao, lakini serikali ya Tanzania imesema inawasiliana na serikali ya DRC ili kujua hatma ya masheikh hao

Msemaji wa serikali ya Tanzania Mende Kasije amesema serikali imeanza mawasiliano kupitia balozi wake alioko mjini Kinshasa.

Hata hivyo kuna taarifa kwamba waasi wa FDRR wanadai kutaka kulipwa fidia ili kuwachia mashekhe hao.

Advertisements