Waziri mkuu wa zamani Tanzania Federick Sumaye

Waziri mkuu wa zamani Tanzania Federick Sumaye

Waziri mkuu mstaafu Fedrick Sumaye ametangaza rasmi leo kukihama chama cha Mapinduzi CCM na kujiunga na muungano wa vyama vya siasa vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA.

Akizungumza na wandishi wa habari mjini Dar es Salaam Sumaye amesema amefikia uwamuzi huo kwa kile alichokita kuendelea na nia yake ya kuwahudumiwa watanzania.

Hata hiyvyo Sumaye hakutaja chama alichojiunga, lakini amesema amejiunga na Ukawa.

Hatua hiyo ya Sumaye ya kumunga mkono aleikuwa waziri mkuu mwenzake Eduward Lowasa kuteuliwa kugombea urais wa Tanzania kupitia CHADEMA imekuja huku tume ya uchaguzi NEC ikitangaza leo kuanza rasmi kampeni za uchaguzi kwa wagombea wa vyama vya siasa kwa muda wa siku 63.

Federick Sumaye aliezaliwa mwaka 1950 alietuliwa kuwa waziri mkuu wa Tanzania Novemba 28 mwaka 1995 hadi 2005, aligombea nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano kwa vipindi viwili kupitia CCM, lakini jina lake lilienguliwa katika hatua za awali.

Advertisements