Archive for October, 2015

UCHAGUZI MKUU ZANZIBAR UMEFUTWA

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha (kushoto)

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha (kushoto)

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Salim Jecha Salim ametangaza kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi visiwani humo akisema uchaguzi huo ulijaa kasoro nyingi.

Kulingana na mwanahabari wa BBC aliyeko hilo Sammy Awami, mwenyekiti huyo ametangaza hatua hiyo kupitia runinga ya serikali visiwani ZBC.

Bw Jecha amesema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki na kwamba kulikuwa na ukiukaji mkubwa wa sheria za uchaguzi, kwa mujibu wa taarifa ambayo baadaye imetumwa kwa vyombo vya habari.

Amesema baadhi ya makamishna wa tume hiyo, badala ya kutekeleza majukumu yao inavyotakiwa kikatiba “wamekuwa ni wawakilishi wa vyama vyao”.

“Kumegundulika kasoro nyingi katika uchaguzi huu miongoni mwa hizo ni kubainika kwa baadhi ya vituo hasa Pemba vimekuwa na kura nyingi kuliko daftari la wapiga kura wa kituo husika.”

Amesema hilo ni jambo la kushangaza ikizingatiwa kwamba “baadhi ya wapiga kura hawakwenda kuchukua vitambulisho vyao vya kupigia kura”.

Kadhalika, amesema kura hazikupata ulinzi mzuri hususan kisiwani Pemba ambako amesema kuwa baadhi ya mawakala wa baadhi ya vya vyama vya siasa katika kisiwa hicho walifukuzwa.

Ameongezea kuwa vijana katika eneo hilo walivamia vituo vya kupigia kura kwa lengo la kutaka kuzua ghasia, na pia vyama vya siasa vilionekana “kuingilia majukumu ya tume ikiwemo kujitangazia ushindi na kupelekea mashindikizo kwa tume.”

  Hii ni sehemu ya taarifa ya Bw Jecha tar

“Nimeridhika kwamba uchaguzi huu haukiwa wa haki na kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu za uchaguzi,” amesema Bw Jecha.

“Hivyo, kwa uwezo nilionao natangaza rasmi kwamba uchaguzi huu na matokeo yake yote yamefutwa na kwamba kuna haja ya kurudia uchaguzi huu.”

Tangazo la mwenyekiti huyo limetolewa huku hali ya wasiwasi ikiendelea kutanda visiwani humo.

Siku moja baada ya uchaguzi kufanywa, mgombea wa chama cha upinzani cha Civic United From (CUF) Seif Sharif Hamad alijitangaza kuwa mshindi, hatua iliyokemewa na chama cha CCM ambacho mgombea wake Dkt Ali Mohamed Shein amekuwa rais wa visiwa hivyo muhula unaomalizika.

Tume ya uchaguzi visiwani humo pia ilishutumu hatua ya mgombea huyo. Kabla ya kufutiliwa mbali kwa matokeo ya uchaguzi, tume hiyo ya uchaguzi ilikuwa imetangaza matokeo ya majimbo 31 kati ya majimbo 54 visiwani humo.

Hayo yakijiri Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania inaendelea kutoa matokeo ya uchaguzi wa urais. Kufikia sasa imetoa matokeo ya majimbo 155 kati ya majimbo 264.

MGOMBEA URAIS ZANZIBAR KUPITIA CCM DR. ALI SHEIN AMEPIGA KURA.

Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ali Mohammed Shein, tayari ameshapiga kura yake kwenye Kituo cha Skuli ya Bungi kusini mwa kisiwa cha Unguja, majira ya saa moja asubuhi  Shein  amewaambia  waandishi  wa  habari   kuwa amejipigia kura mwenyewe na ana matumaini makubwa yakushinda

Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ali Mohammed Shein, tayari ameshapiga kura yake kwenye Kituo cha Skuli ya Bungi kusini mwa kisiwa cha Unguja, majira ya saa moja asubuhi Shein amewaambia waandishi wa habari kuwa amejipigia kura mwenyewe na ana matumaini makubwa yakushinda

UCHAGUZI MKUU TANZANIA-2015: Usalama umeimarishwa.

upigaji kuraWananchi wa Tanzania waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wanaelekea katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kumchagua Rais wa awamu ya tano atakayemrithi Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake, Wabunge na madiwani. Kwa upande wa Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wazanzibari mbali na kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge, wanapiga kura kumchagua Rais wa Zanzibar na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania NEC imetangaza kuwa, maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika. Taarifa zaidi kutoka nchini Tanzania zinasema kuwa, usalama umeimarishwa kila kona ya nchi hiyo kuhakikisha kwamba, uchaguzi huo unafanyika katika mazingira ya amani na utulivu. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Ernest Mangu amesema kuwa, kikosi chake kimejiandaa kikamilifu kuhakikisha kwamba, usalama unakuweko na uchaguzi huo unafanyika kwa amani na utulifu kabisa. Amesema kuwa, kuna askari elfu sabini hadi themanini ambao wamepelekwa katika vituo vya kupigia kura huku kukiweko na askari wa doria ambao watakuwa wakipita huku na kule kulinda usalama. Mchuano mkali unatarajiwa kushuhudiwa katika kiti cha Urais kati ya mgombea wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli na wa Chadema anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa

MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI KWA AJALI YA GARI

21d41b82b5f5b45940a70fdf67821279_LMwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia leo alfajiri kwa ajali ya gari katika Kijiji cha Msolwa huko Chalinze, mkoani Pwani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jaffar Mohamed amethibitisha tukio hilo na kusema, taarifa zaidi zitatolewa na familia ya mwanasiasa huyo. Mohamed amesema Mtikila alikuwa akitokea Morogoro kuelekea Dar es Salaam na alikuwa na watu wengine watatu katika gari hilo ambao wamejeruhiwa. Amesema chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa. Mchungaji Mtikila alikuwa maarufu kutokana na siasa zake zilizozungukwa na utata na kutokana na msimamo wa chama chake cha DP wa kujitambulisha kama chama cha Tanganyika na hivyo kukataa kuwasajili wanachama kutoka Visiwani Zanzibar. Ingawa alibadilisha msimamo huo katika miaka ya hivi karibuni, lakini chama chake hakikuweza kuwavutia wanachama wengi. Kiongozi huyo wa DP aliyefariki dunia mapema leo aliwahi kugombea urais mwaka 2005 na kupata asilimia 0.27 ya kura zote zilizopigwa