upigaji kuraWananchi wa Tanzania waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wanaelekea katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kumchagua Rais wa awamu ya tano atakayemrithi Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake, Wabunge na madiwani. Kwa upande wa Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wazanzibari mbali na kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge, wanapiga kura kumchagua Rais wa Zanzibar na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania NEC imetangaza kuwa, maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika. Taarifa zaidi kutoka nchini Tanzania zinasema kuwa, usalama umeimarishwa kila kona ya nchi hiyo kuhakikisha kwamba, uchaguzi huo unafanyika katika mazingira ya amani na utulivu. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Ernest Mangu amesema kuwa, kikosi chake kimejiandaa kikamilifu kuhakikisha kwamba, usalama unakuweko na uchaguzi huo unafanyika kwa amani na utulifu kabisa. Amesema kuwa, kuna askari elfu sabini hadi themanini ambao wamepelekwa katika vituo vya kupigia kura huku kukiweko na askari wa doria ambao watakuwa wakipita huku na kule kulinda usalama. Mchuano mkali unatarajiwa kushuhudiwa katika kiti cha Urais kati ya mgombea wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli na wa Chadema anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa

Advertisements