Archive for December, 2015

C.U.F YASUSIA SHEREHE ZA MAPINDUZI ZA MIAKA 52 ZANZIBAR

Tunahitaji tuwe hivi sio mifarakano

Tunahitaji tuwe hivi sio mifarakano

Chama cha Wananchi kimesema hakitashiriki maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi visiwani Zanzibar kutokana na utata kuhusu matokeo ya uchaguzi.

 Chama hicho kupitia taarifa kimesema maadhimisho hayo yatafanyika “Serikali ikiwa inaongozwa na viongozi ambao hawana uhalali na ridhaa ya wananchi”.

“CUF tumesisitiza mara zote kwamba hatukubaliani na uamuzi (wa kufuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar),” inasema taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Mshauri wa Katibu Mkuu wa CUF Mansoor Yussuf Himid.

“Tunapenda kutumia fursa hii kuwaeleza wananchi wa Zanzibar kwamba viongozi wetu hawatoshiriki katika shughuli walizopangiwa katika ratiba ya sherehe hizi.”

Siku ya Mapinduzi huadhimishwa kila mwaka tarehe 12 Januari kukumbuka tarehe 12 Januari, 1964, siku ambayo Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ilitangazwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.

Serikali ya visiwani ilikuwa imetangaza ratiba ya kufanyika kwa shughuli mbali mbali zenye lengo la kuadhimisha Mapinduzi hayo kuanzia tarehe 2 Januari hadi kilele tarehe 12 Januari katika sherehe kuu Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar.

“Kiuataratibu, kilele cha sherehe huongozwa na Rais ambaye yupo kikatiba. Kushiriki katika sherehe hizo ni kuhalalisha kipindi cha uongozi ambacho hakipo tena kikatiba,” taarifa ya CUF imesema.

MzozoImage copyrightZanzibar Electoral Commission
Image captionMazungumzo ya kutafuta suluhu ya mzozo huo yanaendelea

“Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wenziwe ndani ya Chama waliokuweko Serikalini hadi tarehe 2 Novemba, 2015 hawako tayari kuhalalisha uvunjaji wa Katiba ya Zanzibar ambayo ndiyo sheria kuu ya nchi.”

Mapema wiki hii, Chama cha Mapinduzi (CCM) kiliwataka wanachama wake wajiandae kwa marudio ya uchaguzi Zanzibar, hatua hiliyoshutumiwa na CUF

Advertisements

JE? MAMBO SAFI ZANZIBAR

1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mazungumzo hayo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema lengo la mazungumzo hayo ilikuwa ni kumpa taarifa Rais Magufuli juu ya hali ya mazungumzo ya kisiasa yanayoendelea huko Tanzania Zanzibar baada ya uchaguzi Mkuu.
Rais Shein amesema mazungumzo juu ya hali ya Zanzibar yanaendelea chini ya kamati maalum ambayo yeye ndiye mwenyekiti na wengine wakiwa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungo wa Tanzania Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu ya sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume na Rais Mstaafu wa awamu ya tano wa Zanzibar Dkt. Salmin Amour.
Amesema tayari kamati hiyo imeanza mazungumzo tangu tarehe 09 Novemba, 2015 na kwamba mazungumzo hayo yamelenga kujadili hatma ya Zanzibar baada ya uchaguzi Mkuu.
Rais Shein amebainisha kuwa mazungumzo hayo bado yanaendelea.
“Kwa hiyo nimekuja kumpa taarifa Mheshimiwa Rais Magufuli kuhusu maendeleo ya mazungumzo yetu ili aweze kujua kinachoendelea akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo Zanzibar ni sehemu yake, na sisi ni jukumu letu kumpa taarifa hiyo” Alisema Rais Shein.

Aidha Rais Shein ameongeza kuwa mazungumzo hayo yatakapokamilika wananchi watajulishwa

SHEREHE ZA MAULID YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD S.W.A ZIMEFANA ZANZIBAR

55637

POLISI WAUANA KWA RISASI JIJINI MWANZA WAKIWA LINDONI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha

ASKARI Polisi wa Kituo cha Polisi Nyamagana jijini Mwanza, Konstebo Daud Masunga Elisha, amemuua askari mwenzake, Konstebo Petro Saimon Matiko kwa risasi na baadaye kujiua kwa risasi na kufa papo hapo.

Tukio hilo lilitokea jana saa 8.30 mchana jijini Mwanza katika eneo la Benki ya Posta Tawi la Pamba wilayani Nyamagana huku chanzo cha mauaji hayo kikiwa hakijulikani.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alisema kitendo hicho si cha kawaida ndani ya jeshi hilo, na kufafanua jinsi mazingira ya tukio lilivyotokea na kusababisha taharuki kwa wananchi na wateja waliokuwa ndani na nje ya benki hiyo.
“Ni kweli kuna askari wawili wamefariki eneo la Benki ya Posta. Katika eneo la benki hiyo kulikuwa na askari wawili waliokuwa lindoni ambao ni PC Elisha na PC Remigius Alphonce mwenye namba H 4291, wakiwa wanaendelea na lindo alifika askari mwingine aliyekuwa amevaa kiraia PC Matiko na kuwasalimia kisha kuingia ndani ya benki kuchukua fedha,” alieleza Kamanda Kamugisha na kuongeza:
“Baada ya dakika tano, Matiko alitoka nje na kuwaeleza askari wenzake kwamba mtandao unasumbua, wakati akieleza hivyo, ghafla askari PC Elisha aliweka chemba risasi ambapo mwenzake PC Alphonce alimhoji mbona unaweka risasi katika hali ya utayari wa kutumika na alijibiwa kwa ufupi kwamba ‘achana na mimi.’
“Ghafla alimfyatulia risasi PC Matiko na kumpiga eneo la bega la kushoto na kutokeza mgongoni na kuanguka chini, kitendo hicho kilimfanya PC Alphonce kukimbilia Benki ya Barclays ili kuomba msaada kwa askari wenzake waliokuwapo lindoni hapo.
“Kabla ya askari hao kufika, ilisikika sauti ya mlio wa risasi na baada ya kurudi alimkuta PC Elisha akiwa amejipiga risasi kwenye paji la uso na kutokea nyuma ya kisogo, tayari akiwa amepoteza maisha.”

WAZIRI WA AFYA AMSIMAMISHA KAZI KAIMU MKURUGENZI WA TAASISI YA OCEAN ROAD DK.DIWAN MSEMO.

ummy mwalim

WAZIRI wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

WAZIRI wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk.Diwani Msemo ili kupisha uchunguzi pamoja na mambo mengine ili kubaini  mgongano wa kimaslahi ulioathiri utendaji wa taasisi  hiyo chini ya kaimu mkurugenzi huyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto mwenye Wizara hiyo, Ummy Mwalimu imesema kuwa kutokana na ziara alizofanya Rais Dk. John Pombe Magufuli inaonyesha kukosekana kwa dawa katika hospitali za Serikali huku vituo vya afya vya  binafsi vikiwa na dawa.
Taarifa ya Waziri huyo imesema kuwa upungufu wa dawa umeendelea kujitokeza kwa karibu zaidi na baadhi ya wagonjwa walieleza kwa uchungu jinsi wanavyopata dawa kwa tabu hatazile wanazotakiwa wapate kwa bei ya ruzuku au zilezinazotakiwa kutolewa bure na serikali.
Kwa msingi wa uwazi na uwajibikaji ameagiza watendaji wote wa sekta ya afya hususani wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya, Wafamasia, Wauguzi na Waganga Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya kukiri kwa maandishi kwa ngazi zao za uwajibikaji endapo wanamiliki Hospitali, Zahanati, Kiliniki, Maduka ya Dawa ndani ya siku 21 kuanzia leo Desemba 23 mwaka huu ambapo  agizo hilo limeotolewa.
Aidha taarifa hiyo imedai kuwa kufanya hivyo kutaziba mianya ya upotevu wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya umma.

Bodi ya Taasisi ya Ocean Road imeagizwa kutafuta mtu atakayekaimu nafasi iliyoachwa wazi na Dk.Msemo anayefanyiwa uchunguzi

DR. MAGUFULI AKAMILISHA SAFU YA MAWAZIRI.

MAGURais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano yautawala wake

Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;

  1. Profesa Jumanne Maghembe -Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
  2. Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).
  3. Mhandisi Gerson Lwenge – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
  4. Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi.(Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)
  5. Mheshimiwa Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
  6. Prof. Makame Mbarawa –Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano

Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu

MAGUFULI ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli

RAIS WA JAMHURI YA MUUGANO WA TANZANIA DKT JOHN MAGUFULI AMETANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LENYE WIZARA 18 LIKIWA NA MAWAZIRI 19

KATIKA UTEUZI HUO BAADHI YA WIZARA BADO HAZIJATAJA MAWAZIRI  WAKE AMBAPO  BARAZA HILIO LINA MAWAZIRI MCHANGAYIKO WAKIWEMO WAPYA NA WALIOKUWA KATIKA AWAMU ILIYOPITA.

MAWAZIRI  WALIOTEULIWA NI OFISI YA RAIS  TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWAL BORA MH GEORGE SIMBA CHAWENE  MANAIBU  WAKE NI MH ANGELA KAIRUKI NA MH JAFO SELEMANI JAFO.

WIZRA YA MUUNGANO NA MAZINGIRA AMETEULIWA MH JANUARI MAKAMBA NA NAIBU WAKE MH. LUHAGA JARSSON MPINA, AFISI YA WAZIRI MKUU  WIZARA YA VIJANA AJIRA NA ULEMAVU  NI MHE JENISTA MHAGAMA MANAIBU WAKE MH. POSY ABDLLA NA MH. ANTONY MAVUNDE

WIZRA YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI MHE  MWIGULU NCHEMBA NAIBU WAKE NI WILLIAM OLE NASHA, WIZARA YA UJENZI UCHUKUZI NA MAWASIIANO WAZIRI BADO HAJATANGAZWA NA NAIBU MHANDISI EDWIN  NGONYANI.

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WAZIRI BADO HAJATANGAZWA NA NAIBU WAKE MHE ASHANTU KIZACHI, WIZARA YA NISHATI NA MADINI PROF MUHONGO NAIBU WAKE MH MEADALED KAREMALIGO, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA MH HARISSON MWAKIYEMBE

WIZARYA MBAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA YA MASHARIKI  BALOZI AGUSTINO MAHIGA NAIBU WAKE NI DR. SUZAN KOLIMBA, WIZARA YA ULINZI AMEPEWA DKT HUSSEN MWINYI, WIZARA YA  MAMBO YA NDANI MHE CHARLES KITWANGWA.

WIZRA YA ARDHI NYUMBA NA  MAKAZI MH WILLIAM LUKUVI NA NAIBU WAKE MHE ANGELINA MABULA, WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAZIRI WAKE BADO HAJATANGAZWA NA NAIBU WAKE MHANDISI. RAMOL MAKANI.

WIZARAYA VIWANDA NA BIASHARA MHE  CHARLES MWIJAGE, WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA UFUNDI WAZIRI HAJATANGAZWA NA NAIBU WAKE MHANDISI STELA MANYANYA, WIZAR YA AFYA MAENDELEO YA  JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO MH UMMY MWALIMU NAIBU WAKE HAMIS KIGWANGALA

WIZARA YA HABARI NA UTAMADUNI, WASANIII NA MICHEZO MH. NAPE NAUYE  NAIBU WAKE MH. ANASTASIA WAMBURA, WIZARA YA MAJI UMWAGILIAI PROF MAKAME MBARAWA NAIBU WAKE MHANDISI ISSACK KAMWELA