Archive for January, 2016

MALIM SEIF ALITOA SIRI ZA MAZUNGUMZO BILA YA KUMALIZIKA-DR. SHEIN

isMakamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein amesema chama hicho kitaingia kwenye uchaguzi wa marudio licha ya umoja wa Ulaya kusikitishwa na uwamuzi wa kurejewa uchaguzi huo.

Akizungumza na wana CCM katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM amesema kurejewa kwa uchaguzi ni suala la demokrasi inayongozwa na katiba na sheria.

 

Amesema taasisi zinazosimamia uchaguzi ndio zenye malaka ya kusimamia na kutangaza uchaguzi na hivyo sio utashi wa chama cha Mapinduzi……

Dr. Shein amesema mazungumzo ya kumaliza mgogoro wa kisiasa Zanzibar yaliowashirikisha viongozi wakuu yalikuwa yakiendelea vizuri, lakini alishangazwa na kauli ya kujitoa kwa Malim Seif Sharif Hamad.

Amesema aliheshimu mazungumzo hayo baada ya kuombwa na kujadili mgogoro huo kwa njia za amani uliojitokeza baada ya tume ya uchaguzi Zanzibar kufuta uchaguzi wa Octoba mwaka jana.

Hata hivyo Dr. Shein amesema Zanzibar itaendelea kuwa na amani na yule atakaefanya vitendo vya fujo serikali itawachukuliwa hatua za kisheria…….

Mabalozi wa nchi zinazounda Umoja wa Ulaya (EU) na Marekani wameeleza kusikitishwa na kitendo cha Tume ya Uchaguzi (ZEC) kutangaza tarehe ya marudui ya Uchaguzi na kumtaka Rais John Magufuli kutumia nafasi yake ya uongozi kutatua mgogoro wa kisiasa Zanzibar.

Tamko hilo la EU limetolewa siku saba baada ya mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha kutangaza uchaguzi wa rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani utarudiwa Jumapili ya Machi 20, lakini siku tano baadaye CUF ilitoa tamko la kutoshiriki uchaguzi huo wa marudio.

Advertisements

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU UGONJWA WA ZIKA

Mtoto mwenye ugonjwa Zika akionesha kuwa na kichwa kidogo.

Mtoto mwenye ugonjwa Zika akionesha kuwa na kichwa kidogo.

1. Utangulizi
Kumekuwepo na taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya Kitaifa na Kimataifa kuhusu Homa ya Zika ambao ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi kijulikanacho kama “Zika Virus”.
Ugonjwa huu uligundulika kwa mara ya kwanza nchini Uganda katika miaka ya 1947 kwenye wanyama aina ya sokwe/nyani (rhesus macaque) ndani ya Misitu ya Zika, karibu na Ziwa Victoria.
Mnamo mwaka 1952, ugonjwa wa zika uligundulika kwa binadamu nchini Uganda na Tanzania, na mwaka 1968 uligunduliwa nchini Nigeria.
Kuanzia mwaka 1951 hadi 1981, ugonjwa huu umeshatolewa taarifa katika nchi takribani sita (6) za Afrika ambazo ni Afrika ya Kati, Egypt, Gabon, Sierra Leone, Tanzania na Uganda.
Vile vile, ugonjwa huu umeshatolewa taarifa katika nchi za India, Indonesia, Malaysia, Philipine, Thailand na Vietnam na pia nchi za Amerika na Pacific.
Kuanzia mwezi Mei 2015, ugonjwa huu ulianza kutolewa taarifa ambapo hadi sasa umeathiri zaidi Bara la Amerika ya Kusini. Kuna takribani nchi 22 ambapo Wagonjwa wamethibitishwa kimaabara kuwa na ugonjwa wa Zika. Nchi hizo ni Brazil (Majimbo 14 yameathirika),  Colombia, Suriname, El Salvador, Guatemala, Paraguay, Mexico, Venezuela, Panama, Cape Verde, Honduras, Panama, France (French Guiana na Martinique, United States of America (Puerto Rico), Guyana, Barbados, Ecuador, Bolivia, Haiti, Ujerumani, France (Saint Martin and Guadeloupe na Dominican Republic.
Ugonjwa huu unaenezwa na mbu aina ya Aedes ambaye (huwa ana tabia ya kuuma asubuhi na pia nyakati za mchana/jioni). Aina hii ya kirusi ipo katika familia ya “Flavirus” ambapo pia wapo virusi vya ugonjwa wa Dengue, Homa ya Manjano (Yellow Fever), Japanese ancephalitis na West Nile Virus.
Kirusi cha homa ya Zika kama kile cha Dengue kinaambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa kuumwa na mbu wa jamii ya Aedes hasa Aedes aegypti. Mbu huyu anaishi katika mazingira ya makazi ya binadamu, huuma wakati wa mchana ndani ya nyumba au kwenye maeneo yenye viwili, hususani majira ya asubuhi na jioni kabla ya jua halijazama.
Mbu huyu anazaliana katika maji yaliyotuama hasa kwenye vyombo vya nyumbani, makinga maji ya paa za nyumba, matairi ya gari, ndoo, makopo nk.
2. Dalili za Homa ya Zika
Dalili za ugonjwa huu zinafanana na za homa ya Dengue, ambazo ni homa, kuumwa na kichwa, maumivu ya viungo, macho kuwa mekundu na vile vile kupata vipele vidogo vidogo kama harara (Skin rashes).
Dalili hizi huanza kujitokeza kuanzia kati siku ya 2 hadi 7 tangu mtu alipoambukizwa kirusi cha homa ya Zika.
Uko uwezekano, ambao haujathibitishwa rasmi, kwamba wakati mwingine wagonjwa wanaweza kupata matatizo katika ubongo (Neurological Complications) na miguu kupooza (Gullein Barre Syndrome), na wajawazito huweza kujifungua watoto wenye ulemavu wa kichwa yaani kichwa kuwa kidogo kulingana na umri wa mtoto (microcephaly).
Kwa wakati mwingine dalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria. Hivyo basi, natoa rai kwa wananchi kuwa, wakati wanapojisikia homa au wamepata homa wahakikishe wanapima ili kugundua kama wana vimelea vya malaria au la, kwa kuwa dalili za ugonjwa wa Zika zinaweza kufanana sana na dalili za malaria.
Homa ya Zika inaweza kutibika kama mgonjwa atapelekwa hospitali mapema na kupatiwa matibabu ya haraka. Hakuna dawa maalum ya ugonjwa huu wala chanjo bali mgonjwa anatibiwa kutokana na dalili zitakazoambatana na ugonjwa huu kama vile homa, kupungukiwa maji na damu.

 

Mara tu baada ya kuwepo kwa taarifa juu ya ugonjwa huu, Serikali kupitia Wizara ya Afya imefanya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini pamoja na mipakani kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa (surveillance system ya Wizara).
Tumejiridhisha kuwa ugonjwa wa homa ya Zika kwa sasa haujaingia nchini kwetu. Hivyo, Wananchi wasiwe na hofu ila waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu pamoja na magonjwa ya Dengue na Malaria kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuzingatia yafuatayo:-
(i)  Kuangamiza mazalio ya mbu kwa:
kufukia madimbwi ya maji yaliyotuama au kunyunyizia viuatilifu vya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo.
kuondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile; vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.
kufyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu.
Kuhakikisha kuwa maua yanayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama.
 Kufunika mashimo ya maji taka kwa mfuniko imara.
kusafisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama.
(ii)  Kujikinga na kuumwa na mbu kwa;-
Kutumia viuatilifu vya kufukuza mbu “mosquito repellants”
Kuvaa nguo ndefu ili kujikinga na kuumwa na mbu.
Kutumia vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu (kwa wale wanaolala majira ya mchana hasa watoto).
kuweka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi.
4. Hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Wizara ni pamoja na:-
1.Tanzania ikiwa ni nchi mwanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) inaendelea kuwasiliana na kushirikiana kwa karibu na Shirika la afya Duniani – Ofisi ya Tanzania kwa lengo la kupata Taarifa na maelezo zaidi ya kukabiliana na ugonjwa huu. Kamati ya Dharura ya Miongozo ya Kimataifa ya Afya  ya WHO yaani “International Health Regulations Emergency Committee” itakutana siku ya Jumatatu ya tarehe 1/2/2016, mjini Geneva,Uswisi ili kufanya tathmini ya ugonjwa huo na kutoa tamko na maelekezo zaidi ya namna ya kudhibiti Ugonjwa huu kwa nchi wanachama.
Baada ya tamko/Mwongozo huo wa WHO, Wizara ya Afya itaandaa Taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kwa ajili ya kusambazwa kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya Tanzania Bara. Aidha, taarifa hii itajumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (ainisho la Ugonjwa), “Ukweli Kuhusu Ugonjwa” (Fact Sheet), Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli. Vipeperushi vinavyoelezea jinsi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu vitatolewa.
2. Wizara itaanza kutoa elimu kwa wananchi kupitia Radio na Runinga kuhusu ugonjwa huu sambamba pia na ugonjwa wa Dengue ambao uambukizi wake unasababishwa na Mbu aina ya Aedes.
3. Kuendelea kutoa vyandarua vyenye uatilifu katika Mkoa yote Tanzania ili kufikia lengo la asilimia 95.
4. Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na mipakani kupitia mfumo wa surveillance ya Wizara. Aidha, Wizara inatoa maelekezo kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya hapa nchini kutoa taarifa za watoto watakaozaliwa wakiwa na ulemavu wowote wa kichwa ikiwemo “microcephaly” au “anencephaly”.
5.Kufuatilia kwa karibu ongezeko la wagonjwa wenye homa isiyokuwa ya malaria kwa Mikoa na Wilaya zote nchini ili kuweza kufanya uchunguzi wa kina iwapo kuna ugonjwa huu.
6. Kuimarisha uwezo wa kutambua ugonjwa huu kwa kina kupitia maabara ya Taifa iliyopo katika Taasisi ya uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Wizara itashirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO) na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa (Centre for Disease Control (CDC) katika kuhakikisha kuwa vitendanishi vya kutambua ugonjwa huu vinapatikana.
7. Kushirikisha program ya Malaria na NIMR katika kudhibiti mbu kwa kupulizia na kunyunyizia  viuatilifu. Hii inalenga  kuangamiza mbu wapevu na viluwiluwi.
5. Hitimisho
Ugonjwa wa Homa ya Zika bado haujaingia Tanzania. Wananchi waondoe hofu juu ya uwepo wa ugonjwa huu. Hata hivyo, ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya Zika, Dengue na malaria ambayo huenezwa kwa namna inayofanana.
Aidha, mvua hizi kubwa zinazoendelea kunyesha hapa nchini zinaweza kuchangia kuongezeka kwa mazalio ya mbu. Hivyo, utupaji, uzoaji na uhifadhi wa taka katika vijiji na miji yetu ni lazima uimarishwe katika kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa salama kwani bila ya kuzingatia hayo, tunatoa fursa kwa mazalio ya mbu kuongezeka na hata kuwa karibu zaidi ya makazi ya binadamu.
Wizara ya Afya itaendelea kutoa taarifa za mara kwa mara kwa wananchi ili waweze kuelewa kuhusu ugonjwa huu na kuchukua hatua stahiki.
Imetolewa na:-
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
31/1/2016

Hatutashiriki Uchaguzi-Baraza kuu CUF

imagesKWAMBA Chama Cha Wananchi (CUF) hakitoshiriki katika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 kwa sababu uchaguzi huo si halali kwani uchaguzi halali ulishafanyika.

AZIMIO LA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA KUHUSU TANGAZO LA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR LA KUITISHA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi), likiwa ndiyo chombo cha juu cha maamuzi katika Chama baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa, limefanya kikao cha dharura leo, tarehe 28 Januari, 2016, katika Ofisi Kuu ya CUF, mjini Dar es Salaam. Kikao hicho kilikuwa na ajenda moja tu, ambayo ni kufanya maamuzi kuhusiana na tangazo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar la kuitisha uchaguzi wa marudio.

Baada ya kujadili kwa kina tamko hilo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, la kuitisha uchaguzi wa marudio tarehe 20 Machi, 2016 na mwenendo mzima wa hali ya kisiasa Zanzibar tokea alipotoa tamko lake batili la tarehe 28 Oktoba, 2015 kudai kwamba amefuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na matokeo yake, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:

 1. KWAMBA Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar umeshafanyika tarehe 25 Oktoba, 2015, ambapo kwa upande wa uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani ulikwisha kamilika na washindi wote kupewa shahada za kuwathibitisha na kuwatambua kama washindi halali. Kwa upande wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, matokeo yalikwisha bandikwa nje ya vituo vya majumuisho vya majimbo yote 54. Kilichokuwa kinaendelea baada ya hapo ni kuhakiki matokeo hayo kutoka majimboni na kazi hiyo ilikwishakamilika kwa majimbo 40 na katika hayo, matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa majimbo 31 yalikwishatangazwa kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jecha Salum Jecha, kutangaza isivyo halali kwamba ameufuta uchaguzi huo.
 2. KWAMBA Chama Cha Wananchi (CUF) hakitoshiriki katika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 kwa sababu uchaguzi huo si halali kwani uchaguzi halali ulishafanyika.
 3. KWAMBA linatoa wito kwa Wazanzibari wote wanaoipenda nchi yao na ambao wanaamini katika utawala wa sheria, demokrasia na kuheshimu Katiba na Sheria za nchi yetu kutoshiriki katika uchaguzi huo usio halali wa marudio.
 4. KWAMBA sababu kuu ya Baraza Kuu kufikia maamuzi haya ni kutokana na matamko yote mawili ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, kutokuwa halali na kwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984. Hakuna kifungu chochote cha Katiba ya Zanzibar au Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar kinachotoa uwezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na hata kwa Tume yenyewe kufuta uchaguzi au kuitisha uchaguzi wa marudio.
 5. KWAMBA linazipongeza na limetiwa moyo sana na taasisi na jumuiya zote za kimataifa na kikanda zikiwa ni pamoja na Jumuiya ya Madola (The Commonwealth), Umoja wa Ulaya (European Union), Umoja wa Afrika (African Union), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nchi za Marekani na Uingereza kwa msimamo wao wa kuungana na Wazanzibari na kutetea haki yao ya kidemokrasia na maamuzi halali waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kutaka mchakato wa uchaguzi huo ukamilishwe na matokeo yake kutangazwa.
 6. KWAMBA linazipongeza na kutiwa moyo pia na taasisi za hapa nchini zikiwemo taasisi na jumuiya za kidini, taasisi za haki za binadamu, vyombo huru vya habari, vyama vyengine vya siasa na Wazanzibari na Watanzania wote wanaopenda amani na demokrasia kwa msimamo wao wa kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kuendelea kusisitiza haja ya kuheshimu na kufuata Katiba na Sheria za nchi yetu na pia haja na umuhimu wa kutunza amani ya nchi yetu kwa kutaka haki itendeke. Baraza Kuu linazihakikishia taasisi na jumuiya hizo zote na pia kuwahakikishia Wazanzibari na Watanzania wote kwamba CUF itaendelea kusimama kidete katika kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi yetu na pia kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015.
 7. KWAMBA limesikitishwa na kushangazwa na kitendo cha Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kuandika barua na kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kutaka vyama vya siasa vishiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 bila ya kujali kwamba uchaguzi huo ni haramu na unakiuka matakwa ya Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984. Baraza Kuu halikutarajia mtu mwenye hadhi ya Ujaji kufanya kazi ya kutumikia maslahi ya watawala ambao wameamua kuvunja Katiba na Sheria za nchi yetu na kukanyanga misingi ya haki na demokrasia huku akishindwa kukemea uhuni mkubwa uliofanywa wa kubaka demokrasia na haki za watu.
 8. KWAMBA limesikitishwa na kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli, kukwepa dhamana na wajibu wake kama Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuiacha njiani kazi aliyoianza ya kutafuta ufumbuzi wa mkwamo wa uchaguzi Zanzibar. Baraza Kuu linamtaka Rais Magufuli kujitathmini na kujiuliza anajiweka vipi na kutoa taswira gani mbele ya macho ya Watanzania na jumuiya ya kimataifa kutokana na kutosimamia ahadi yake aliyoitoa mbele ya Watanzania wakati akilizindua Bunge jipya kwamba atafanya kazi na vyama vya CUF na CCM ili kuupatia ufumbuzi mkwamo huu.
 9. KWAMBA linalaani matumizi ya nguvu kubwa ya vyombo vya ulinzi na usalama vya Jamhuri ya Muungano na Vikosi vya SMZ dhidi ya wananchi wasio na hatia na ambao wamekuwa watulivu licha ya vitendo vingi vya uchokozi wa makusudi na hata mashambulizi ya hujuma dhidi yao yanayofanywa na makundi ya vijana wa CCM waliowekwa katika makambi kadhaa kisiwani Unguja.
 10. KWAMBA linaitaka jumuiya ya kimataifa na hasa taasisi zinazosimamia haki za binadamu na zinazopambana na makosa ya jinai kimataifa ikiwemo Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (International Criminal Court – ICC) kufanya uchunguzi wa kauli na matendo ya uhalifu, uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu na ubaguzi ambao umekuwa ukifanywa dhidi ya wananchi wa Zanzibar na kuchukua hatua dhidi ya watu walio nyuma ya maamuzi na utekelezaji wa matukio hayo.
 11. KWAMBA linawapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuonesha ukomavu wa hali ya juu na kuwa watulivu licha ya machungu makubwa waliyoyapitia na wanayoendelea kuyapitia tokea pale maamuzi yao yalipopinduliwa na CCM kwa kumtumia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha. Baraza Kuu linatoa wito kwa Wazanzibari wote kuungana pamoja chini ya chama chao cha CUF walichokipa ridhaa halali kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 kutetea maamuzi yao waliyoyafanya kupitia sanduku la kura kwa njia za amani. Baraza Kuu linawasisitiza tena Wazanzibari kwamba waendelee kutunza amani ya nchi yetu na kutambua kwamba kutunza amani si udhaifu bali ni jambo linaloipa nguvu jumuiya ya kimataifa kufuatilia haki za kidemokrasia za wananchi wa Zanzibar.
 12. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawatahadharisha CCM na watawala wasiowajali na kuwaheshimu wananchi kwamba zama za utawala wa mabavu usioheshimu Katiba na Sheria za nchi hazina nafasi tena katika dunia ya leo. Baraza Kuu lina imani kwamba HAKI ITASHINDA.

LIMETOLEWA NA:
BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)
DAR ES SALAAM
28 JANUARI, 2016

 

UKAWA KUTOA MSIMAMO WAO JUU YA KUREJEWA UCHAGUZI ZANZIBAR

isUMOJA wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umesema utatoa msimamo juu ya hali ya siasa ya Zanzibar baada ya kikao cha kamati tendaji kuketi na kutoa msimamo. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma.
Alisema walifanya mazungumzo ya mashauriano ya hali ya siasa ya Zanzibar, yaliyohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa nyama vya upinzani, wakiongozwa na aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowasa.
“Januari 28 keshokutwa kutakuwa na kamati ya utendaji na kikao hicho, kitatoa msimamo wa kitu gani kifanyike kuhusiana na siasa za Zanzibar,” alisema. Pia, alisema Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), litatoa msimamo wake kuhusu suala la Zanzibar.
Mbunge wa Malindi kwa tiketi ya CUF, Ally Salehe alisema wanaamini Rais John Magufuli, anaweza kuingilia mgogoro wa Zanzibar na kuupatia ufumbuzi

TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR YATANGAZA TAREHE YA KURUDIWA UCHAGUZI

TUMETume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi visiwani humo baada ya matokeo ya uchaguzi uliopita kufutwa.

Uchaguzi huo sasa utafanyika Jumapili tarehe 20 Machi.

Tangazo hilo limefanywa na mwenyekiti wa ZEC Jecha Salim Jecha.

Bw Jecha amesema tarehe hiyo iliamuliwa na tume baada ya mkutano hapo jana.

“Uchaguzi huo utahusisha uchaguzi wa Rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani na hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya kampeni,” amesema Bw Jecha.

“Wagombea wote walioteuliwa hapo awali wataendelea kuwa wagombea katika uchaguzi huu.”

Chama cha Wananchi (CUF) kimekuwa kikipinga kurudiwa kwa uchaguzi. Chama hicho mapema mwezi huu kilionya kwamba hatua hiyo inaweza kusababisha vurugu.

Viongozi wa chama hicho walisusia maadhimisho ya Siku ya Mapinduzi wiki iliyopita.

Chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa tayari kimewashauri wanachama wake visiwani wajiandae kwa marudio ya uchaguzi, tangazo lililoshutumiwa vikali na viongozi wa CUF.

MAGAZETI YA LEO TAREHE 19 JAN. 2016

1KUSOMA ZAIDI BONYEZA HAPA

MATOKEO YA MITIHANI DARASA LA KUMI ZANZIBAR 2016

MATOKEO YA MITIHANI DARASA LA KUMI ZANZIBAR 2015/2016