Archive for February, 2016

WAGOMBEA WOTE HALALI KATIKA UCHAGUZI WA MARUDIO-JECHA

Capture catoonTume ya uchaguzi Zanzibar ZEC imesema wagombea wote walioshiriki uchaguzi uliopita ngazi ya urais, uwakilishi na udiwani wana  uhalali na watakuwemo katika taratibu zote za uchaguzi wa marudio.

Mwenyekiti wa ZEC Jecha Salim Jecha amesema tume itaendelea kuwahesabu wagombea hao ni halali kutokana na kutofuata utaratibu wa kisheria za  kujitoa kwenye uchaguzi huo.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari amesema sheria ya uchaguzi nambari 11 ya mwaka 1984 inatoa sharti la kuwepo wadhamini wa wagombea na hakuna chama kilichoiandikia tume kuwa kimefuta udhamini wa wagombea wake kushiriki katika uchaguzi huo

Aidha Jecha amesema pamoja na wagombea wa CUF kuandika barua ofisi za wilaya lakini hakuna barua hata moja iliyowasilishwa ya kufuta udhamini wa wagombea……

Aidha ZEC imesema maandalizi ya uchaguzi wa marudio yamefikia hatua nzuri na  kazi ya uchapishaji wa daftari la wapiga kura itakuwa imekamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi huu..

Tangazo hilo la tume limekuja huku zaidi ya vyama 10 vya siasa vilivyoshiriki kwenye uchaguzi wa Octoba 25 mwaka jana vikisusia kushiriki katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika March 20 mwaka huu.

MATOKEO YA KIDATU CHA NNE 2015

http://tanzania.go.tz/matokeo_2015/Olevel.htm

MATOKEO YA KIDATU CHA NNE 2015

BONYEZA HAPA http://tanzania.go.tz/matokeo_2015/Olevel.htm

Ajali ya basi na lori yaua 11 Tanga

Watu 11 wamepoteza maisha katika ajali mbaya ya basi la abiria na lori la mizigo iliyotokea Alhamisi, asubuhi mkoani Tanga, nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoani humo Hassan Hashim, majeruhi walipelekwa katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza ambapo wanapatiwa matibabu.

​Hashim anasema ajali hiyo ilitokea kutokana na dereva wa lori kutokuwa makini wakati alipoamua kupita gari lingine na kwenda kuligonga basi hilo usoni linalo milikiwa na kampuni ya Simba Mtoto.

Miongoni mwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni madereva wote wa lori na basi hilo lililokuwa likutokea mkoani Tanga na kuelekea jijini Dar es salaam.

Mpaka hivi sasa hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu hali ya majeruhi ama kama idadi ya vifo imeongezeka

MGOGORO WA KISIASA ZANZIBAR UTAMALIZWA KWA MAREJEO YA UCHAGUZI-RAIS MAGUFULI

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli

Rais wa Tanzania Dr. John Magufuli amesema njia pekee ya kupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa Zanzibar ni kufanyika tena kwa uchaguzi utakaokuwa wa huru na haki.

Akizungumza na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini pamoja na wakuwa wa taasisi za umoja wa mataifa Ikuliu mjini Dar es Salaam amesema mfumo wa kisiaza Zanzibar ni tofauti kutokana na kuwa na uchaguzi unaojitegemea na katiba.

Amesema busara na mazungumzo ya kukwamua mkwamo wa kisiasa Zanzibar pamoja na kurudia uchaguzi huo ndio utakuwa suluhisho.

Rais Magufuli amesema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ya kikanda Dr. Agostino Mahiga katika hafla ya kukaribisha mwaka mpya kwa mabalozi na wakuu wa mashirika na taasisi za umoja wa mataifa zilizopo nchini.

LOWASA AUNGA MAAMUZI CUF KUTOSHIRIKI UCHAGUZI ZANZIBAR

Waziri mkuu wa Tanzania Eduward Lowasa

Waziri mkuu wa Tanzania Eduward Lowasa

Ni dhahiri kuwa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema bado ana ndoto za kuwa rais wa Tanzania baada ya kurudia kauli yake ya kwenda Ikulu, lakini safari hii akisema chama hicho kitaingia Ikulu bila ya kumwaga damu.

Lowasa alisema hayo jana katika mkutano ulioandaliwa na Baraza la Wazee wa Chadema, tawi la Ubungo kwa ajili ya kumpongeza kwa ushupavu aliounyesha baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.
 
“Siku moja tutaingia Ikulu bila kumwaga damu. Msiwe na wasiwasi kwa sababu mimi, dunia na Watanzania wanafahamu kuwa tulishinda katika uchaguzi uliopita,” alisema Lowassa ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne kabla ya kujiuzulu.
Lowasa alisema ingawa ana uhakika kuwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita yalichakachuliwa, aliweka mbele amani.
“Nawashukuru Watanzania kwa kunisikiliza, walikuwa wananisikiliza mimi tu baada ya uchaguzi. Ningeweza kuwaambia twende barabarani, sikufanya hivyo kwa sababu najua amani ni muhimu,” alisema.
Uchaguzi wa Zanzibar 
Waziri huyo mkuu wa zamani pia alizungumzia uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza kurudiwa kwa uchaguzi wa rais, wawakilishi na madiwani Machi 20, akitahadharisha kuwa suala hilo linaweza kusababisha mpasuko.
 
“Hali ya Zanzibar isiposhughulikiwa kwa umakini na umahiri, italeta matatizo makubwa nchini,” alisema.
Alimtaka Rais John Magufuli, akiwa kiongozi wa Tanzania, kuchukua uamuzi na kuhakikisha suala la Zanzibar linatatuliwa.
Alisema UKAWA  inaunga mkono maamuzi ya  CUF kupinga uchaguzi huo kurudiwa kwa kuwa hakuna ushahidi wa kukiukwa kwa taratibu zozote za uchaguzi wa mwaka jana.
“Nashauri wakae chini wazungumze, kwa nini hili la sasa linashindikana wakati CUF walikubali Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwa miaka mitano?” alihoji.
Alisema amani ni jambo la muhimu na linatakiwa lipewe kipaumbele kabla ya uamuzi mwingine kufanyika.
Kuhusu mikakati ya kukiboresha chama, Lowassa, ambaye alipata kura milioni 6.07 na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Magufuli aliyepata kura milioni 8.8, alisisitiza uamuzi wake wa kufanya ziara nchi nzima kuwashukuru Watanzania wote ambao walimpigia kura na ambao hawakumpigia.
Lowassa pia alizungumzia uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), akiituhumu kuwa inaendeshwa na chama tawala.
Alisema katika uchaguzi uliopita, NEC ilipotosha matokeo na kuharibu mchakato wa uchaguzi.
“NEC ilifanya mambo ya hovyo, walipaswa kufukuzwa, ni uongo kusema kuwa ipo huru,” alisema.
Awali, kabla ya Lowassa kusema hayo, mwenyekiti wa wazee hao wa Chadema, Enock Ngombale alisoma risala ambayo ilimpongeza kwa ushupavu aliounyesha kabla na baada ya uchaguzi.
Katika risala hiyo, Ngombale alisema Watanzania wanajua kuwa Lowasa alishinda uchaguzi, lakini walishangazwa na matokeo.
“Wewe ni kiongozi imara, shupavu na mahiri. Watanzania waliamini kuwa ulishinda lakini kilichofanyika ni uchakachuzi,” alidai.
Kadhalika, risala hiyo ilisema Serikali ya Rais Magufuli haifuati sheria na kanuni za utawala bora.
 
“Tumeona unyanyasaji mkubwa kwa wafanyabiashara, bomobomoa ambayo haifuati misingi ya haki za binadamu,” alisema.

Pia, wazee hao walimshauri Lowassa mambo mbalimbali ya kukiimarisha chama.