Archive for March, 2016

WAFADHILI WASITISHA MISAADA KWA TANZANIA

Image copyrightStatehouse Tanzania
Image captionRais wa Tanzania John Magufuli.

Kundi la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi wametangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania.

Hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada la serikali ya marekani kuondoa msaada wa dola 472 wa kufadhili miradi ya maendeleo kutokana na jinsi uchaguzi wa kisiwa cha Zanzibar ulivyoendeshwa.

Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania ilitegemea msaada mwaka uliopita, kwa hivyo hatua hizo za hivi punde ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya.

Advertisements

DR. SHEIN KUZINGATIA USAWA WA KIJINSIA KATIKA UTEUZI WA NAFASI ZA UONGOZI SERIKALINI-TAMWA

tamwaRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein ametakiwa kuangalia usawa wa kijinsia wakati wa uteuzi wa viongozi mbali mbali katika serikali.

Hayo ni kutokana na kuwa tayari Rais ameshachagua makamo wa pili wa rais Balozi Seif Ali Idd hivyo kuonesha kuwa utawala wa juu wa nchi unashikiliwa na wanaume pekee.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya TAMWA kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa wanawake wamekuwa wakiachwa nyuma katika Nyanja nyingi ikiwemo siasa, uchumi na kijamii.

Inaaminika kuwa uwingi wa wanawake katika vyombo vya maamuzi utaweza kupunguza matatizo katika Nyanja nyengine kwa vile yatakuwa yakijadiliwa kutokana na uzoefu na ujuzi na kuweza kuchukuliwakwa  hatua muafaka.

 

Katika vipindi vilivyopita nafasi ya wanawake katika Baraza la Mawaziri na nafasi za uteuzi wa Rais pia hazikuwa nyingi kulinganisha na wenzao na hivyo kuendelea kuwa na pengo la usawa wa kijinsia.

 

Hadi Baraza linamalizika kulikuwa na mawaziri 4 wanawake kati ya 19 wakiwa ni sawa na asilimia 21 wakati awali walianza na nafasi mbili.

Nafasi za uteuzi ambapo kwa kawaida huwa ni 10 kwa Rais, wanawake walikuwa ni 4 hadi mwisho sawa na asilimia 40.

 

Hivyo TAMWA inamuomba Rais ukumbuke kuwa usawa wa kijinsia ni kipaumbele katika mipango mbali mbali ya nchi na ulimwengu ikiwemo ya Malengo ya Uendelezaji wa Maendeleo (SDGs) pamoja Mpango wa Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA).

 

Kukosekana kwa usawa wa kijinsia katika vyombo vya maamuzi pia kunarejesha nyuma maendeleo ya nchi kiuchumi na kielimu hasa kwa vile wanawake ndiyo wanawakilisha zaidi ya asilimia 50 ya wananchi wote.

 

Mzuri Issa

Mratibu

TAMWA,Zanzibar.

Tanzania yasikitika kunyimwa pesa za MCC

Image captionTanzania imehuzunishwa na hatua ya bodi ya shirika la changamoto za milenia (MCC) kusitisha msaada

Tanzania imehuzunishwa na hatua ya bodi ya shirika la changamoto za milenia (MCC) kusitisha msaada wake wa awamu ya pili wa dola milioni 472.8 ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja pesa za Tanzania.

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw Augustine Mahiga ameelezea kushtushwa kwake na hatua hiyo ya bodi ya MCC akisema “imepuuza hatua kubwa tu zilizopigwa kidemokrasia” nchini humo.

”Inasikitisha kuwa demokrasia yetu inatathminiwa tu na matokeo ya uchaguzi wa visiwani Zanzibar,”

Image copyrightAFP
Image captionWaziri wa mambo ya nje bwana Augustine Mahiga

Kuhusiana na uchaguzi wa Zanzibar Bw Mahiga anasema kuwa Tanzania, ilifanya kila kitu kuambatana na sheria na katiba ya nchi wala hakuna tatizo ama ukiukwaji wa sheria.

Mahiga anasema kuwa huo ni uamuzi wao na kwa sababu hela hizo ni zao wanauhuru wa kuzitumia watakavyo ila anahoji kwanini uamuzi huo uliafikia bila ya majadiliano na serikali ya muungano ya Tanzania.

Image copyrightStatehouse Zanzibar
Image captionBw Mahiga amesisitiza kuwa Tanzania ilifwata katiba yake kuhusiana na uchaguzi wa Zanzibar

Kuhususiana na kupitishwa kwa sheria ya uhalifu wa mitandao bwana Mahiga anasema sheria hiyo ilikuwa inalenga kupambana dhidi ya ugaidi.

Waziri huyo ameonya kuwa watu wanaoishi vijijini ndio watakaoathirika zaidi kwani fedha hizo zilikuwa zimepangiwa kueneza umeme mashinani.

Katika kutoa uamuzi wake, Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) ilisema kuwa Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea msaada wa awamu ya pili.

Image captionBodi hiyo aidha imesema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao “haukushirikisha wote na wala haukuakisi maoni ya wote

Kupitia taarifa, bodi hiyo ilisema kuwa: “Serikali ya Tanzania haijachukua hatua za kuhakikisha kuheshimiwa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika katika utekelezwaji wa sheria ya Uhalifu wa Mtandao.”

Bodi hiyo aidha imesema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao “haukushirikisha wote na wala haukuakisi maoni ya wote, licha ya malalamiko kutoka kwa serikali ya Marekani na jamii ya kimataifa.

MAREKANI YASITISHA MSAADA WA MABILIONI YA PESA KWA TANZANIA.

Shirika la ufadhili la serikali ya Marekani limesitisha msaada wake kwa serikali ya Tanzania likilalamikia matukio kuhusu uchaguzi wa Zanzibar na kutekelezwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao.

Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) imesema Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea msaada wa awamu ya pili ambao ulikuwa wa jumla ya Dola 472.8 milioni ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja za Tanzania.

Kupitia taarifa, bodi hiyo imesema: “Serikali ya Tanzania haijachukua hatua za kuhakikisha kuheshimiwa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika katika utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.”

Bodi hiyo aidha imesema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao “haukushirikisha wote na wala haukuakisi maoni ya wote, licha ya malalamiko kutoka kwa serikali ya Marekani na jamii ya kimataifa.”

Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Ali Mohammed Shein alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani, Chama cha Wananchi (CUF).

MCC imesema kwamba huwa inatilia mkazo sana demokrasia na kujitolea kwa nchi kufanikisha uchaguzi huru na wa haki.

“Uchaguzi uliofanyika Zanzibar na kutekelezwa nwa Sheria ya Uhalifu wa Mitandao vinaenda kinyume na hili,” imesema.

Tanzania ilipokea Dola 698 milioni katika awamu ya kwanza.

Pesa za MCC hutumiwa kufadhili miradi ya maji, barabara na nishati.

Maalim Seif Sharif Hamadi Arejea Zanzibar Baada ya Kukaa Mapumzikoni Serena Hoteli Kwa Siku 17

isSiku chache baada ya Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein kuapishwa baada ya kushinda uchaguzi wa marudio uliosusiwa na baadhi ya vyama vya upinzani, Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amerejea Zanzibar.
Maalim Seif ambaye alikuwa mapumzikoni katika hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es Salaam kwa takribani siku 17, jana alirejea Zanzibar kuendelea na mapumziko yake.
Maalim Seif alilazwa katika Hospitali ya Hindu Mandal ya jijini Dar es Salaam,mara baada ya kuruhusiwa March 8 mwaka huu alishauriwa na Daktari wake kupata mapumziko ya muda mrefu.
Kurejea kwa Maalim Seif visiwani humo kunazidisha shauku na kiu ya baadhi ya Wazanzibar kutaka kusikia atakachokisema kiongozi huyo wa upinzani mwenye ushawishi mkubwa kwenye jamii.
Maalim Seif aliugua wakati Wazanzibar wakiwa katika maandalizi ya kurudia uchaguzi mkuu uliofanyika March 20, mwaka huu baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25  mwaka  jana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar( ZEC), Jecha Salim Jecha kwa madai kuwa uligubikwa na dosari nyingi.
Gharama za Hotelini
Taarifa zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari siku chache zilizopita zilidai kuwa kila siku aliyokaa kwenye hoteli hiyo, Maalim Seif alikuwa akitumia wastani wa Sh. 6,162,500.
Kutokana  na  takwimu hizo, hadi kufikia jana, Maalim Seif atakuwa ametumia kiasi kisichopungua sh. Milioni 92.4
Chumba alichokuwa akilala Maalim Seif katika Hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota tano kinalipiwa dola za Marekani 2,500 kwa usiku mmoja.
Maalim Seif alikuwa akiishi hotelini hapo na wasaidizi wake watano, ambao wote gharama zao zinalipwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ

WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI VITI MAALUM WANAWAKE-CCM

baraza la wawakilishiTume ya uchaguzi Zanzibar imetangaza majina 22 ya wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM walioteuliwa kuwa wajumbe wa baraza la wawakilishi kwa kipindi cha miaka mitano.

Walioteuliwa ni Salama Abod Talib, Shadya Mohamed Suleiman, Bihindi Hamad Khamis, Salma Mussa Bilal, Mwanaid Kassim Mussa, Panya Ali Abdalla, Mgeni Hassan Juma na Zainab Abdallah Salum.

Wengine ni Salha Mohamed Mwinyijuma, Zulfa Maka Omar, Lulu Msham Abdalla, Wanu Hafidh Ameir, Saada Ramadhan Mwenda, Tatu Mohamed Usi na Amina Idd Mabrouk.

Wengine ni Chum Kombo Khamis, Mtumwa Suleiman Makame, Mwantatu Mbaraka Khamis,Riziki Pembe Juma, Viwe Khamis Abdalla, Hamida Abdalla Issa na Hidaya Ali Makame.

MH JAMAA KAUFYATA

-PAXP-deijE