tamwaRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein ametakiwa kuangalia usawa wa kijinsia wakati wa uteuzi wa viongozi mbali mbali katika serikali.

Hayo ni kutokana na kuwa tayari Rais ameshachagua makamo wa pili wa rais Balozi Seif Ali Idd hivyo kuonesha kuwa utawala wa juu wa nchi unashikiliwa na wanaume pekee.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya TAMWA kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa wanawake wamekuwa wakiachwa nyuma katika Nyanja nyingi ikiwemo siasa, uchumi na kijamii.

Inaaminika kuwa uwingi wa wanawake katika vyombo vya maamuzi utaweza kupunguza matatizo katika Nyanja nyengine kwa vile yatakuwa yakijadiliwa kutokana na uzoefu na ujuzi na kuweza kuchukuliwakwa  hatua muafaka.

 

Katika vipindi vilivyopita nafasi ya wanawake katika Baraza la Mawaziri na nafasi za uteuzi wa Rais pia hazikuwa nyingi kulinganisha na wenzao na hivyo kuendelea kuwa na pengo la usawa wa kijinsia.

 

Hadi Baraza linamalizika kulikuwa na mawaziri 4 wanawake kati ya 19 wakiwa ni sawa na asilimia 21 wakati awali walianza na nafasi mbili.

Nafasi za uteuzi ambapo kwa kawaida huwa ni 10 kwa Rais, wanawake walikuwa ni 4 hadi mwisho sawa na asilimia 40.

 

Hivyo TAMWA inamuomba Rais ukumbuke kuwa usawa wa kijinsia ni kipaumbele katika mipango mbali mbali ya nchi na ulimwengu ikiwemo ya Malengo ya Uendelezaji wa Maendeleo (SDGs) pamoja Mpango wa Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA).

 

Kukosekana kwa usawa wa kijinsia katika vyombo vya maamuzi pia kunarejesha nyuma maendeleo ya nchi kiuchumi na kielimu hasa kwa vile wanawake ndiyo wanawakilisha zaidi ya asilimia 50 ya wananchi wote.

 

Mzuri Issa

Mratibu

TAMWA,Zanzibar.