Waandishi wakiwa makini kupata habari kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Janii Zanzibar hayuko pichani

Waandishi wakiwa makini kupata habari kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Janii Zanzibar hayuko pichani

Jeshi la polisi Zanzibar  limewakamata  watuhumiwa  wanne  wanaodaiwa kuhusika na shambulio la mabomu yaliyoripuliwa katika nyumba ya kamishina na sehemu nyengine za matukio kama hayo.

Akizungumza na Waandishi wa habar Naibu  Mkurugenzi  Upelelezi Makosa ya jinai Zanzibar Salum Msangi  amesema  wamewakamata watu hao   ambao wamekiri kuhusika na  matukio ya uripuaji wa mabomu hayo

Jeshi la polisi limesikitishwa na tukio hilo ambao watu wanao husika na tukio hilo ni  wafuasi wa chama cha CUF na ni viongozi wa chama hicho ambao ni Omar Bakari Nassor Miaka 26 mkaazi wa bububu,Hassan Omar Issa Miaka 67 ni Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Magharibi ‘A’ mkaazi wa mfenesini,Saleh Mohamed Saleh Miaka 34 Katibu wa CUF Wilaya ya Magharibi ‘A’ Mkaazi wa bububu na Suleiman Mohamed Bakari Miaka 50 Katibu wa CUF jimbo la mfenesini.

Watuhumiwa hao wamekamatwa na mabomu  matano yaliyotengenezwa  kienyeji ambapo mtuhumiwa wa kwanza alikiri kutupa bomu katika nyumba ya kamishna akiwa na wenzake ambao bado wanatafutwa  na jeshi la polisi na wengine kati  yao wanakiri kuratibu zoezi hilo la uripuaji  wa mabomu katika maeneo mbalimbali.

Kutokana na matukio hayo jeshi la polisi limejipanga  kikamilifu  katika Nyanja za  kumsaka anaetengeneza  mabomu hayo  hapa Zanzibar

Advertisements