MMChama cha wananchi CUF kimetoa wito kwa nchi wahisani na Jumuiya ya kimataifa kuwawekea vikwazo viongozi wa juu wa serikali kwa madai ya kuvuruga uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa Octoba 25 mwaka jana.

Mwenyekiti wa Kamati tendaji ya uogozi ya CUF Twaha Taslima amesema licha ya nchi hizo kuzuwia misaada yake kwa Tanzania lakini pia zinapaswa kuwawekea vikwazo viongozi aliowaita wabakaji wa demokrasia.

Akitoa maazimio yaliofikiwa na baraza kuu la uongozi la CUF kwa wandishi wa habari lilokutana Jumamosi na Jumapili mjini Zanizbar amesema chama hicho pia hakimtambui rais wa Zanzibar na serikali yake atakayoinda.

        Aidha Taslima amewataka wafuasi wa CUF kudai haki yao ya ushindi uliotokana na uchaguzi wa Octoba 25 kwa njia za amani na kikatiba huku viongozi wa juu wakiendelea kutafuta haki na kulinda maamuzi yao waliofanya kwenye uchaguzi huo.

Tayari nchi 10 za mataifa ya Mgaharibi likiwemo na shirika la MCC zimetangaza kusitisha misaada yao kwa Tanzania zikidai uchaguzi wa marudio uliofanyika bila ya kuwepo suluhisho la kisiasa.

Wakati huo huo katibu Mkuu wa CUF Malim Seif Sharif Hamad amesema kukutana kwake na viongozi wa CCM wakati akiwa mapumziko mjini Dar es Salaam haikuwa na maana ya kukisaliti chama hicho.

Katibu mkuu wa CUF Malim Seif Sharif Hamad

Katibu mkuu wa CUF Malim Seif Sharif Hamad

Amesema viongozi wa juu wa CCM waliomtembelea ni muendelezo wa utamaduni wa kujuliana hali hivyo amewataka wafuasi wa CUF kuiga mfano huo bila ya kujali itikadi za vyama vyao vya siasa.

Hata hivyo Malim Seif ambae ni makamu wa kwanza wa rais mstaafu amesema hayuko tayari kukutana meza moja na rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed  Shein kuzungumzia hali ya kisiasa inayoendelea.

Advertisements