sheRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza dhamira ya kweli ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano na Serikali na wananchi wa Marekani.

Akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mheshimiwa Wilson Masilingi Ikulu leo, Dk. Shein alisema Zanzibar inajivunia uhusiano wake na Marekani ambao ulianzia tangu miaka 1844-5 kwa Marekani kufungua kituo chake cha biashara Zanzibar.

Dk. Shein aliongeza kuwa uhusiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nchi hiyo umedumu kwa miaka mingi ambapo historia inaonesha nchi hizo zimekuwa zikishirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo afya, miundombinu na nishati.

Chini ya ushirikiano huo Marekani imeweza kusaidia ujenzi wa barabara kisiwani Pemba, kugharimia uwekaji wa waya wa umeme wa baharini kutoka  Tanzania Bara hadi Zanzibar na kusaidia katika kuangamiza ugonjwa wa malaria ambapo Zanzibar sasa ugonjwa huo uko asilimia 0.6.

Alimtaka Balozi Masilingi kufanya kila jitihada zaidi kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano huo kwa kuangalia maeneo mengi ya ushirikiano yakiwemo ya uwekezaji na biashara kama utalii.

Kwa upande wake Balozi Masilingi amemhakikishia Dk. Shein kuwa atatekeleza kwa vitendo Sera ya Diplomasia ya Uchumi kwa kuhimiza wawekezaji kutoka nchi hiyo kuja Tanzania kushiriki katika kuinua uchumi

Advertisements