she

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein ametangaza baraza jipya la mawaziri lenye wizara 13 badala ya 16 za zamani wakiwemo mawaziri watatu wa zamani.

Baraza hilo lenye mawaziri wanawake wanne na manaibu watatu wanawake kati ya saba pia linajumuisha wajumbe wawili wa baraza la mapinduzi wenye hadhi ya mawaziri kutoka vyama vya upinzani.

Akitangaza baraza hilo jipya kwa wandishi wa habari Ikulu mjini Zanzibar Dr. Shein amesema serikali yake itaendeshwa kwa uwazi na ukweli na kutenda haki kwa wananchi wote.

WAJUMBE WA BARAZA HILO NI

Ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi – Issa Haji Ussi Gavu.
2). Katiba na Sheria Utumishi wa Umma – Haroun Ali Sleiman.
3). Tawala za Mikoa na Idara maalum – Haji Omari Kheir.
4). Makamo wa 2 wa Rais – Mohamed Aboud.
5). Waziri wa Fedha na Mipango – Dk. Khalid Salum Mohamed.
6). Afya – Mahmoud Thabit Kombo.
7). Wizara ya Elimu – Riziki Pembe Juma.
8). Viwanda na Masoko – Amina Salum Ali.
9). Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi – Ali Karume.
10). Habari Utalii Utamaduni na Michezo – Rashid Ali Juma.
11). Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi – Hamad Rashid Mohamed.
12). Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mauldine Castiko.
13). Maji Ardhi Nishati na Mazingira – Salama Aboud Talib.
MANAIBU N I
1). Naibu waziri wa afya -Harusi Said Suleiman
2). Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali ni Mmanga Mjengo Mjawiri
3). Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi-Mohamed Ahmed Salum
4). Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi-Lulu Msham Khamis
5). Habari Utalii Utamaduni na Michezo-Chum Kombo Khamis
6). Maji Ardhi Nishati na Mazingira-Juma Khamis Makungu
7). Katiba na Sheria Utumishi wa Umma-Khamis Juma Maalim

Dr. Shein anatarajiwa kuliapisha baraza hilo la mawaziri kesho asubuhi katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.

Advertisements