Archive for May, 2016

WATU WASIOJULIKANA WAVAMIA MSIKITI WA MASJID RAHAMN MWANZA NA KUUWA WAUMINI WATATU

MSIKITIWaumi watatu wameuwawa na mwengine amejeruhiwa kwa kukatwa na mapanga katika msikiti wa masjid Rahman usiku wa kuamkia leo uliopo Ibanda wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wakati waumini walipokuwa wakisali sala ya isha.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi amesema tukio hilo limefanywa na watu wasiojulikana wapatao 15 wakiwa wamevalia mavazi ya kuficha uso wakiwa na mapanga, shoka na bendera nyeusi yenye maandishi meupe waliingia ghafla katika msikiti huo.

Amesema watu hao walipoingia msikitini humo walizima taa na kutoa sauti wakisema kwa nini mnasali wakati wenzetu na wanashikiliwa na polisi na na hapo hapo wakaanza kuwashambuliwa kwa kwa mapanga

Jeshila la polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu watatu kwa ajili ya kuwahoji kuhusiana na tukio hilo, huku msako mkali wa kuwasaka watu wengine walio husika na mauaji hayo ukiwa bado unaendelea

Huduma ya mabasi ya mwendo wa kasi yaanza Dar es Salaam

Image captionMabasi ya mwendo wa kasi TZ

Huduma ya mabasi ya uchukuzi yanayoenda kwa kasi BRT nchini Tanzania imeanza rasmi siku ya jumanne katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam.

Abiria watalipa shilingi 400 na 800 huku wanafunzi wakilipa 200 kulingana na mamlaka ya uchukuzi wa barabarani na majini SUMATRA.

Image captionKituo cha mabasi ya mwendo wa kasi Tanzania

Mkurugenzi mkuu anayesimamia mamlaka hiyo bw Giliard Ngewe amewaambia maripota mjini humo kwamba nauli zitakuwa shilingi 400 kwa uchukuzi wa barabara ndogo,650 kwa barabara kuu na shilingi 800 kwa uchukuzi wa barabara kuu na ndogo huku wanafunzi wakilipa shilingi 200 kwa kila safari.

Image captionAbiria wakiwa wamepanda basi la BRT

ASiku ya Jummanne na Jumatano mabasi hayo yatahudumu kati ya saa kumi na moja alfajiri na saa sita mchana.

Image captionKituo cha mabasi ya BRT Tanzania

Tunawaonya wanaoendesha pikipiki na madereva wa magari mengine kutotumia barabara za mradi wa BRT,alisema akiongezea kwamba bado wanazungumza na washikadau kutafuta njia nzuri ya kupanga barabara zitakazotumiwa na BRT na mabasi mengine ya abiria.

Kulingana na yeye,mfumo huo wa BRT hauyaruhusu mabasi mengine kutoa huduma pamoja na mabasi ya BRT kwa hivyo abiria walioko katika barabara za BRT hawataruhusiwa kutumia mabasi mengine.

MAGAZETI YALIOTUFIKIA LEO

BONYEZA HAPA: http://www.mpekuzihuru.com/2016/05/habari-zilizopo-katika-magazeti-ya-leo_4.htmlBONYEZA

 

Zanzibar Press Club Yaadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo Habari kwa Kongamano la Waandishi Zanzibar.

Katibu wa Zanzibar Press Club Ndg Mwinyimvua akizungumza wakati wa Kongamano la Waandishi wa Habari Zanzibar kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani huadhimishwa kila mwaka 3 Mei, maadhimisho hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Zanzibar Press Club Ndg Abdulla Abdurahaman akizungumza na waandishi wa habari wa Zanzibar wakati wa Kongamano la kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani lililowashirikisha Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Serikali na Binafsi, lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohammed akifungua Kongamano wa Waandishi wa Habari kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar, na kuwataka waandishi wa habari kufuata maadili ya Kazi zao wanaporipoti habari kwa Wananchi bila ya kuwa na upendeleo wanapotoa taarifa kwa Wananchi, Waandishi ni kioo cha jamii na kuelimisha.
Mhe Hamad Rashid Mohammed akisisitiza jambo wakati wa hutuba yake ya Ufunguzi wa Kongamano la Waandishi wa Habari Zanzibar kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Waandishi wakiwa makini kusikiliza hutuba ya mgeni rasmin Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe Hamad Rashid Mohammed ikiwa ni Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani huadhimishwa kila mwaka 3 Mei.
Waandishi wakimsikiliza Mgeni rasmin akitowa nasaha zake kwa Waandishi wa Habari wakati swa Ufunguzi wa Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari, lililoandaliwa na Zanzibar Press Club katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Mkuu wa Chuo cha Waandishi wa Habari Zanzibar Dk Abubakar Rajab,akitowa Mada katika Kongamano hilo la kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Akiwasilisha Mada yaMiaka 22 ya Azimio la Windhoek (Namibia) Kuhusu Uhuru wa Vyombo vya Habari. Wajibu wa Mamlaka za Umma Kustawisha Uhuru wa Vyombo vya Habari Kama Nyenzo ya Kukuza Utawala Bora na Uwajibikaji Nchini ( Zanzibar)
22 Anniversary of Windhoek (Namibia) Declaration on Freedom of Press : Public.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

RAIS WA ZANZIBAR DR. ALI MOHAMED SHEIN AAPISHWA RASMI KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein leo asubuhi tarehe 02 Mei, 2016 ameapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake ndani ya Baraza hilo.

Rais Shein ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, tukio ambalo limeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Viongozi wengine walioshuhudia tukio hilo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo mchana ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Mawaziri, uliopo Ofisi ya Rais TAMISEMI Mjini Dodoma.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
02 Mei, 2016

RAIS MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto) akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichofanyika leo katika ukumbi wa Tamisemi Mjini Dodoma,(wa pili kushoto) ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]