sheRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Nd. Bakari Khamis Muhidin ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi.

Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya Raslimaliwatu ni ndugu Khamis Haji Juma na Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Pemba Nugu Masoud Ali Mohamed.

Katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za Serikali Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ni Ndugu Daima Mohammed Mkalimoto.

Wizara ya Fedha na Mipango alieteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi ni Ndugu Ali Bakari Ishaka, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Barabara ni Ndugu Mwalim Ali Mwalim na Ofisa Mdhamini wa Wizara hiyo Pemba ni Ndugu Ibrahim Saleh Juma.

Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Kamishana wa Kazi ni Ndugu Fatma Iddi Ali, Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa wazee Ndugu Wahida Maabad Mohamed na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Ndugu Mwanaidi Mohamed Ali.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Wanawake na Watoto Ndugu Nasima Haji Choum na Ofisa Mdhamini, Wizara ya Kazi Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Pemba Ndugu Khadija Khamis Rajab.

Dkt. Fadhil Mohamed Abdullah anakuwa Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Wizara ya Afya na Mkurugenzi wa Huduma za Hospitali ni Dkt. Mohammed Dahoma.

Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Naibu Katibu Mkuu (Mifugo na Uvuvi) ni Dkt. Islam Seif Salum.  Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti ni Ndugu Sheha Idrissa Hamad na Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi Ndugu Noah Saleh Said.

Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo ni Ndugu Mohamed Khamis Rashid, Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka Ndugu Yussuf Haji Kombo wakati Dkt. Bakari Saad Assed anakuwa Mkurugenzi wa Chuo cha Kilimo, Kizimbani.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, Kizimbani ni Dkt. Suleiman Shehe Mohammed, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Ndugu Mussa Aboud Jumbe, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mifugo Dkt. Yussuf Haji Khamis na Ofisa Mdhamini, Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Pemba ni Ndugu Sihaba Haji Vuai.

Katika Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Ndugu Hassan Abdalla Mitawi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu (Habari), Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti Ndugu Mahmoud Omar Hamad.

Ndugu Imane Duwe ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ZBC ni Nassra Mohammed Juma.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji ni Ndugu Rafii Haji Makame, Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Ndugu Yussuf Khamis Yussuf, Mkurugenzi wa Habari (Maelezo) Ndugu Hassan Vuai.

Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari ni Chande Omar Omar na Ofisa Mdhamini, Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Pemba Ndugu Khatib Juma Mjaja.

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi ni Ndugu Bimkubwa Abdi Nassib. Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti Ndugu Khatib Mohamed Khatib na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini ni Ndugu Abdalla Hussein Kombo.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Mkurugenzi wa Baraza la Mitihani katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ni Ndugu Zubeir Juma Khamis.

 

Ofisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Pemba ni Ndugu Juma Bakari Alawi na  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) ni Dkt. Said Seif Mzee.

Mwisho

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIB