Archive for September, 2016

Madereva Wa Tanzania Watekwa Nchini DRC

 

Baadhi ya magari yanayodaiwa kuchomwa moto

Baadhi ya magari yanayodaiwa kuchomwa moto

Baadhi ya magari yanayodaiwa kuchomwa moto.

Chama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo nchini Tanzania (TATOA) kinaripoti kwamba, waasi wa Mai Mai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamewateka nyara madereva wa Tanzania na kuchoma baadhi ya magari ya mizigo. Waasi hao wanadai dola za Kimarekani elfu nne (karibu shilingi za Kitanzania milioni tisa) kwa kila dereva ama sivyo watawapiga risasi madereva wote. Pia waasi hao wametoa siku ya mwisho (deadline) ya majeshi yanayolinda amani nchini humo kuondoka.

TATOA inasema imezungumza na mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics,  Azim Dewji,  ambaye amethibitisha taarifa hizi na pia balozi wa Tanzania DRC  na Wizara ya Mambo ya Nje.  Serikali inashughulikia suala hili. Jumla ya magari yaliyotekwa ni 12 kati ya hayo magari 8 ni ya Tanzania na 4 ya Kenya. Magari 4 ya Tanzania yamechomwa moto na madereva wote walichukuliwa na waasi lakini bahati nzuri madereva wawili wa Tanzania walifanikiwa kuwatoroka. Tukio hilo limetokea sehemu inayoitwa Kasebebena na Matete, wastani wa kilomita 30 kutoka mji wa Namoya.

TATOA inawashauri wanachama waliopakia mzigo kuelekea huko kuwasiliana na madereva wao ili wasitishe safari, kusubiri taarifa ya hali ya usalama kutolewa.

Mai Mai Kata ni kundi la waasi nchini DRC ambalo linadai kupigania uhuru wa jimbo la Katanga, na linaongozwa na Gédéon Kyungu Mutanga, ambaye aliunda kundi hilo mara tu alipotoroka kutoka gerezani mwaka 2011.

Advertisements

Tetemeko la ardhi lakumba Tanzania

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.7 kwa kipimo cha rishta limeikumba mikoa ya kanda ya ziwa nchini Tanzania na kusini mashariki mwa Uganda na kusababisha maafa ya vifo na majeruhi na hasara ya mali.

Habari zinaarifu kwamba mikoa ya Mwanza na Kagera nchini Tanzania ndiyo imeshuhudia madhara makubwa kutokana na majengo mengi kubomoka huku baadhi ya habari zikieleza kuwa, baadhi ya watu wameuawa.

Majeruhi wa tetemeko la ardhi leo nchini Tanzania

Maeneo yalioathirika zaidi kwa Tanzania ni, Bukoba na Nsuga yaliyoko Kagera na baadhi ya maeneo ya Mwanza. Wakazi wa mikoa ya Kagera, Mwanza, Tabora, Geita na Katavi wameshuhudia mtetemeko huo kwa uzito tofauti.

Nyumba iliyoharibiwa kwa tetemeko la leo

Mbali na Mikoa hiyo ya Tanzania, tetemeko hilo limeikumba pia baadhi ya miji nchini Uganda ikiwemo Kampala na Mbarara Kusini Mashariki mwa nchi hiyo. Taarifa iliyotolewa na uongozi wa hospitali ya rufaa ya Mjini Bukoba, imeeleza kuwa watu 10 wamepoteza maisha kuokana na janga hilo la kimaumbile, huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa vibaya.

Majeruhi wakiendelea kupatiwa huduma ya kwanza hospitali ya Bukoba

Hadi tunaingia mitamboni bado kulikuwa hakujatolewa taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo.