Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.7 kwa kipimo cha rishta limeikumba mikoa ya kanda ya ziwa nchini Tanzania na kusini mashariki mwa Uganda na kusababisha maafa ya vifo na majeruhi na hasara ya mali.

Habari zinaarifu kwamba mikoa ya Mwanza na Kagera nchini Tanzania ndiyo imeshuhudia madhara makubwa kutokana na majengo mengi kubomoka huku baadhi ya habari zikieleza kuwa, baadhi ya watu wameuawa.

Majeruhi wa tetemeko la ardhi leo nchini Tanzania

Maeneo yalioathirika zaidi kwa Tanzania ni, Bukoba na Nsuga yaliyoko Kagera na baadhi ya maeneo ya Mwanza. Wakazi wa mikoa ya Kagera, Mwanza, Tabora, Geita na Katavi wameshuhudia mtetemeko huo kwa uzito tofauti.

Nyumba iliyoharibiwa kwa tetemeko la leo

Mbali na Mikoa hiyo ya Tanzania, tetemeko hilo limeikumba pia baadhi ya miji nchini Uganda ikiwemo Kampala na Mbarara Kusini Mashariki mwa nchi hiyo. Taarifa iliyotolewa na uongozi wa hospitali ya rufaa ya Mjini Bukoba, imeeleza kuwa watu 10 wamepoteza maisha kuokana na janga hilo la kimaumbile, huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa vibaya.

Majeruhi wakiendelea kupatiwa huduma ya kwanza hospitali ya Bukoba

Hadi tunaingia mitamboni bado kulikuwa hakujatolewa taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo.

Advertisements