Archive for August, 2017

Kongamano la Kimataifa la Nne la Diaspora Zanzibar Hotel ya Sea Cliff Zanzibar

 

Mwakilishi wa Kampuni ya TIC  Godfrey Mwambe akitowa Mada kuhusiana na Diaspora kuwekeza katika Jamii Nchini, akizungumza wakati wa Kongamano la Nne la Diaspora linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar.
Mwakilishi wa TPSF akizungumzia Mada kuhusiana na fursa kwa WanaDiaspora kuwekeza nyumbani akitowa mada hiyo kwa Watanzania Wanaoishi Nje kutumia fursa hiyo kuwekeza nyumba.
Baadhi wa WanaDiaspora wakifuatilia Kongamano hilo linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Manowari ya jeshi la Marekani, USS Indianapolis, iliyozama miaka 72 iliyopita yapatikana

Image caption USS Indianapolis – picha ya mwaka 1937

Manowari ya jeshi la Marekani ya USS Indianapolis ambayo ilizama wakati wa vita vya pili vya dunia, imepatikana kwenye bahari ya Pacific, Miaka 72 baada ya kuzamishwa na nyambizi wa Japan.

USS Indianapolis ilikuwa ikirejea kutoka oparesheni ya siri ya kupeleka sehemu za kunda bomu la atomic ambalo baadaye lilitumiwa huko Hiroshima.

Manowari hiyo ilipatikana kilomita 5.5 chini ya bahari.

Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft Paul Allen, ambaye aliongoza kikosi cha kutafuta manowari hiyo alisema ugunduzi huo ni wa kutia moyo.

USS Indianapolis iliharibiwa tarehe 30 Julai mwaka 1945 katika habari ya Ufilipino kati ya Guam na Leyte baada ya kugongwa na kombora kutoka kwa nyambizi ya Japan.

Haki miliki ya picha Paul G Allen
Image caption Picha ya Indianapolis baharini

Kilikuwa kisa kibaya zaidi cha kupotea kwa maisha kulikumba jeshi la wanamaji wa Marekani.

Kulikuwa na wanajeshi 1,196 ndani ya manowari hiyo na ni kati ya wanajeshi 800 na 900 walinusurika kuzama.

Lakini manowari hiyo haikutuma ishara na hadi wakati masura walipatikana siku nne baadaye ni watu 316 tu waliopatikana wakiwa hai katika eneo hilo lenye papa wengi.

Meli hiyo ni maarufu kwa kufanya safari ya siri ya kusafiirjha sehemu za kuunda bomu la atomic lilifahamika kama “Little Boy” .

Haki miliki ya picha Paul G Allen
Image caption Sehemu za USS Indianapolis

Bidhaa hizo zilipelekwa katika kisiwa cha Tinian kwenye kambi ya jeshi la Marekani ambayo ilifanya shambulizi la kwanza na bomu la nyuklia.

Siku nne baadaye Indianapolis ilizama chini ya wiki moja kabla ya bomu hilo la nyuklia ililosaidia kuunda kuharibu mji wa Hiroshima.

Sawa na bomu lenye jina “Fat Man” lililoangushwa mji wa Nagasaki, ambalo liliilazimisha Japan kuachana na vita na kumalizika kwa vita vya pili vya Dunia.

Picha: Ziara ya Rais Dkt. Shein wilayani Magharibi A

Picha: Ziara ya Rais Dkt. Shein wilayani Magharibi A

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dtk. Ali Mohamed Shein ameendelea na ziara yake ya kikazi, amefika na kuzindua miradi mbali mbali katika wilaya ya Magharibi A.

DSC_9755

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana Viongozi mbali mbali wakati alipowasili katika viwanja vya Skuli ya msingi Kihinani Jimbo la Mfenesini kuweka jiwe la msingi Jengo jipya la Skuli hiyo leo akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo

DSC_9852

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akifungua pazia kama ishara ya   kuweka jiwe la Msingi Jengo jipya la Skuli ya msingi Kihinani leo akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo

DSC_9886

Baadhi ya wananchi na Wazee wa Wanafunzi wa Skuli ya msingi Kihinani jimbo la Mfenesini wakiwa katika sherehe za ufunguzi wa Jengo jipya la Skuli hiyo leo iliyowekwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani )akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,

DSC_9918

Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Kihinani walipokuwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani ) alipokuwa akizungumza na Wanafunzi hao pamoja na Wazee wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo jipya katika Skuli hiyo leo,akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo

DSC_9919

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza na Wananchi,Wazee na Wanafunzi   wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo jipya katika Skuli ya msingi Kihinani jimbo la Mfenesini  leo,akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,(kulia) Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma na (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud

DSC_9933

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza na Wananchi,Wazee na Wanafunzi   wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo jipya katika Skuli ya msingi Kihinani jimbo la Mfenesini  leo,akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,

DSC_9964

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipofika kutembelea Ofisi ya Walimu mara baada ya kuweka  Jiwe la Msingi Jengo jipya katika Skuli ya msingi Kihinani jimbo la Mfenesini  leo,akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,(kulia) Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma na (kushoto) Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo  Bi.Mafunda Juma Khamis,

DSC_0022

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” Nd,Mwinyiussi (katikati) wakati alipofika kutembelea Mradi wa Visima vya Maji Safi na salama katika Shehia ya Bumbwisudi leo alipofanya ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,(kulia) Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe.Salama Aboud Talib,

DSC_0036

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipofuatana na Viongozi mbali mbali  wakati alipofika kutembelea Mradi wa Visima vya Maji Safi na salama katika Shehia ya Bumbwisudi leo alipofanya ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,

DSC_0073

Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira, Salama Aboud Talib alipokuwa akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) wakati alipotembelea Mradi wa Visima vya Maji Safi na salama katika Shehia ya Bumbwisudi leo alipofanya ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi ”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM. Mhe. Shaka Ziarani Kisiwani Pemba ya Kikazi Kukagua Maendeleo ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020 Pemba.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Agosti 15, 2017 akisalimiana na Wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake mara baada ya kuwasili Visiwani Pemba-Zanzibar kwa Ziara ya kikazi.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba Ndg Abdallah Rashid Ali akielezea namna Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inavyotekeleza ilani ya CCM mbele ya Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na maafisa wa serikali pamoja na  Viongozi Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC)(kulia) akizungumza na viongozi wa kikundi cha Vijana wa Jasiriamali  wa mboga mboga (Mtaji wa masikini)wadi ya pujin mara maada ya kukagua mazao mbali mbali yanayolimwa na kikundi hicho.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba Ndg Abdallah Rashid Ali (kulia)akielezea jambo kwa  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua mradi wa kikundi cha Vijana wa Jasiriamali  wa mboga mboga (Mtaji wa masikini)wadi ya pujin
Meneja Mradi wa Barabara yenye urefu wa km 35  ya ole ngeneja  Amin khalid abdallah akitoa ufafanuzi juu ya maendeleo ya mradi huo kwa  ndg:Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) alipokwenda kukagua ujenzi wa barabara hiyo.
Daktari dhamana katika hospitali ya chakechake Dkt.Ali Habib Ali akimpokea ndg: Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) alipowasili hospitalin hapo kuangalia wagonjwa na kuwafariji.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akimpatia baadhi ya vifaa tiba mama mzazi wa mtoto Bi,Salha Issa Nassor alipokwenda kuangalia wagonjwa na kuwafariji katika hospitali ya Chake chake wilayan chakechake.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC(KWANZA KULIA)) akiwasili katika ukumbi wa mkutano Tawi la CCM Wawi kuzungumza na Vijana wa CCM wilayani Chake Chake Mkoa wa Kusini pemba
 Vijana wakifuatilia mkutano huo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Vijana wa CCM wilayani Chake Chake Mkoa wa Kusini pembakatika ukumbi wa mkutano Tawi la CCM Wawi
 ”Watumishi wa umma mmepewa dhamana kubwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe.Dkt,John Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar DktAli Shein hivyo ni matarajio ya chama cha mapinduzi na serikali,watumishi wote kusimamia na kuwajibika ili kutekeleza ilani kwa uimara”Alisema ndg: Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  wakati akizungumza na maafisa wadhamini,wadhamini wa mabaraza ya mji na madiwani,katika ukumbi wa skuli ya chekechea mdungu wilayani Chake Chake Mkoa wa Kusini pemba.
 Maafisa wadhamini,wadhamini wa mabaraza ya mji na madiwani wakimsikiliza ndg: Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
”Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo chini ya CCM hinyo kila kiongozi alieajiriwa na serikali ana jukumu moja kubwa la kutekeleza ilani kwa maslahi mapana na umakini mkubwa”Aliendelea kusisitiza ndg: Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  wakati akizungumza na maafisa wadhamini,wadhamini wa mabaraza ya mji na madiwani,katika ukumbi wa skuli ya chekechea mdungu wilayani Chake Chake Mkoa wa Kusini pemba.
(Picha na Fahadi Siraji)

Uchaguzi Kenya 2017: Odinga kupinga ushindi wa Kenyatta mahakamani

Odinga anadai mitambo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa kumfaa Kenyatta
Image captionOdinga anadai mitambo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa kumfaa Kenyatta

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametangaza kwamba muungano wake wa National Super Alliance utawasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumanne wiki iliyopita.

Bw Odinga alikuwa amesema ingawa muungano huo ulikuwa umeapa kutowasilisha kesi kortini wakati huu, wameona ni heri kufanya hivyo “kufichua uovu uliotokea wakati wa uchaguzi mkuu.”

“Tumeamua kwenda kortini kufichua jinsi uongozi wa kompyuta ulivyofanikishwa,” amesema Bw Odinga akiwahutubia wanahabari mtaa wa Lavington, Nairobi.

“Hawa ni viongozi wa kompyuta. Kompyuta ndiyo iliwataga, kompyuta iliangulia, kompyuta iliwatoa. Vifaranga vya kompyuta.”

Kiongozi huyo amesisitiza msimamo wa NASA kwamba uchaguzi haukuwa huru na wa haki.

Amesema mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi IEBC ilidukuliwa na matokeo kuvurugwa kumfaa Bw Kenyatta ambapo kulikuwa na pengo kiasi fulani kati yake na Bw Odinga muda wote wa kutangazwa kwa matokeo.

“Mtindo huu ulitokea pia katika maeneo mengi na kwenye uchaguzi wa ugavana. Jambo kama hili halijawahi kutokea katika uchaguzi wa kidemokrasia pahala pengine popote duniani. Lakini ilitokea hapa,” alisema.

Bw Odinga amesema udukuzi huo una uhusiano na kuuawa kwa meneja wa teknolojia katika tume hiyo Chris Msando ambaye aliuawa wiki moja kabla ya uchaguzi.

Matokeo na mshindi kila kaunti uchaguzi wa urais 2017

Bofya kwa maelezo zaidi

Chanzo: IEBC

Aidha, kiongozi huyo ameishutumu tume ya uchaguzi akisema imekuwa ikitangaza matokeo ya uchaguzi bila kutoa Fomu 34A za kuonyesha matokeo yalivyokuwa katika vituo vya kupigia kura.

Bw Odinga mesema uchunguzi wa muungano huo umebaini udanganyifu mwingi ulitokea, na akawashutumu waangalizi wa uchaguzi ambao walisema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.

Waziri mkuu huyo wa zamani amesema upinzani uliwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo mwaka 2013 lakini hawakutendewa haki, na kusema “Uhuru (Kenyatta) alishinda 100%, nasi tukashindwa 100%.”

“Mahakama inaweza kutumia hii kama nafasi ya pili ya kujitakasa, au inaweza kuamua kuharibu mambo kabisa,” amesema.

Jamii ya kimataifa ilikuwa imehimiza upinzani, pamoja na wagombea wengine ambao hawakuwa wameridhishwa na uchaguzi, kutumia mifumo iliyowekwa kikatiba kutafuta haki.

Kwa mujibu wa matokeo ya IEBC, Rais Kenyatta alipata kura 8,203,290 huku naye Raila Odinga akipata kura 6,762,224.

Lipumba Amwangukia Maalim Seifu…….Amtaka Arudi Ofisini, Wakutane na Kumaliza Tofauti Zao

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kurudi wafanye mazungumzo na kumaliza tofauti.
Profesa Lipumba amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya ofisi za Chama Cha Wananchi (CUF) zilizopo Buguruni.
 Lipumba amemtaka Katibu Mkuu huyo kurudi wafanye mazungumzo na atambue kuwa yeye ndiye Mwenyekiti wa CUF na ndiye boss wake.
“Maalim analalamika lakini malalamiko yake hayana msingi, yeye ni Katibu Mkuu anapaswa kufuata misingi ya Mwenyekiti, anatambua kuwa Mwenyekiti ni boss kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Mwenyekiti nipo yeye aje kufanya kazi hapa. Maalim ni mkongwe wa siasa tunataka kuwa na maelewano, nampigia simu hapokei, nasikia saizi akija Dar es Salaam anakwenda uchochoroni huko Magomeni wakati tuna ofisi hapa nzuri, Katibu Mkuu unauzoefu wa kisiasa tufanye majadiliano ofisi zetu ziko hapa njoo tuzungumze” alisisitiza Lipumba
Aidha Lipumba amesema kama Katibu Mkuu wa CUF hatakuja ofisini kwa ajili ya majadiliano na mazungumzo kwa lengo la kumaliza migogoro yao basi Naibu Katibu Mkuu ataendelea kukaimu nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba yao ya CUF.
“Katibu Mkuu akishindwa kutekeleza majukumu yake Naibu Katibu Mkuu anafanya kazi kwa kufuata maelekezo ya Mwenyekiti ataendelea Kukaimu nafasi hiyo mpaka pale Katibu Mkuu atakapokuwa tayari kuja hapa ataruhusiwa kufanya kazi na ofisi yake ipo hapa, akiwa anakuja ofsini anafuata utaratibu na kufuata maelekezo yangu mimi sina shida ila kama hatakuja basi Naibu Katibu Mkuu ataendelea kufanya kazi”alisema Lipumba
Mbali na hilo Lipumba amesema kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) toka kimempokea Mhe. Edward Lowassa wameacha ajenda ya ufisadi na wameiweka kando ajenda hiyo na kusema sasa hivi wao ndiyo ajenda yao hiyo.

Msimu wa Uchumaji karafuu kisiwani Pemba

 Baadhi Wachumaji wa karafuu wakiwa katika harakati za kuchambuwa karafuu walizochuma huko Ngomeni Wilaya ya Chake Chake Pemba.
  Baadhi Wachumaji wa karafuu wakiwa katika harakati za kuchambuwa karafuu walizochuma hukoa katika Ngomeni Wilaya ya Chake Chake Pemba.
 Karafuu ambazo zimeanikwa kwa  mfumo unaotakikana kisheria katika majamvi huko Ngomeni Chake Chake Pemba, ambapo uhalisia na ubora wake haupotei.
 Karafuu ambazo zimeanikwa kwa  mfumo unatakikana kisheria katika majamvi huko Ngomeni Chake Chake Pemba, ambapo uhalisia na ubora wake haupotei.
Picha na Hanifa Salim , Pemba