Posts by skaska

Maalim Seif Shariff Hamad amelishutumu Jeshi la Polisi kwa kile alichodai kuvuruga mikutano

954495-01-02

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi – CUF Maalim Seif Shariff Hamad amelishutumu Jeshi la Polisi kwa kile alichodai kuvuruga mikutano inayoandaliwa na wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono Katibu Mkuu huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Maalim Seif Shariff Hamad amedai kushangazwa na nguvu kubwa inayotumiwa na Polisi
katika kuzuia mikutano ya ndani inayoandaliwa na wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono, huku wakiruhusu ile inayoandaliwa na Mwenyekiti wa chama hicho Prof Ibrahim Lipumba.

Aidha, Katibu Mkuu huyo pia amezungumzia suala la kuachiwa huru watuhumiwa wa utekaji nyara wa viongozi na wanachama wa CUF akidai ni ukiukaji wa hakim, huku akimtala waziri wa mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kuingilia kati.

Madereva Wa Tanzania Watekwa Nchini DRC

 

Baadhi ya magari yanayodaiwa kuchomwa moto

Baadhi ya magari yanayodaiwa kuchomwa moto

Baadhi ya magari yanayodaiwa kuchomwa moto.

Chama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo nchini Tanzania (TATOA) kinaripoti kwamba, waasi wa Mai Mai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamewateka nyara madereva wa Tanzania na kuchoma baadhi ya magari ya mizigo. Waasi hao wanadai dola za Kimarekani elfu nne (karibu shilingi za Kitanzania milioni tisa) kwa kila dereva ama sivyo watawapiga risasi madereva wote. Pia waasi hao wametoa siku ya mwisho (deadline) ya majeshi yanayolinda amani nchini humo kuondoka.

TATOA inasema imezungumza na mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics,  Azim Dewji,  ambaye amethibitisha taarifa hizi na pia balozi wa Tanzania DRC  na Wizara ya Mambo ya Nje.  Serikali inashughulikia suala hili. Jumla ya magari yaliyotekwa ni 12 kati ya hayo magari 8 ni ya Tanzania na 4 ya Kenya. Magari 4 ya Tanzania yamechomwa moto na madereva wote walichukuliwa na waasi lakini bahati nzuri madereva wawili wa Tanzania walifanikiwa kuwatoroka. Tukio hilo limetokea sehemu inayoitwa Kasebebena na Matete, wastani wa kilomita 30 kutoka mji wa Namoya.

TATOA inawashauri wanachama waliopakia mzigo kuelekea huko kuwasiliana na madereva wao ili wasitishe safari, kusubiri taarifa ya hali ya usalama kutolewa.

Mai Mai Kata ni kundi la waasi nchini DRC ambalo linadai kupigania uhuru wa jimbo la Katanga, na linaongozwa na Gédéon Kyungu Mutanga, ambaye aliunda kundi hilo mara tu alipotoroka kutoka gerezani mwaka 2011.

Tetemeko la ardhi lakumba Tanzania

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.7 kwa kipimo cha rishta limeikumba mikoa ya kanda ya ziwa nchini Tanzania na kusini mashariki mwa Uganda na kusababisha maafa ya vifo na majeruhi na hasara ya mali.

Habari zinaarifu kwamba mikoa ya Mwanza na Kagera nchini Tanzania ndiyo imeshuhudia madhara makubwa kutokana na majengo mengi kubomoka huku baadhi ya habari zikieleza kuwa, baadhi ya watu wameuawa.

Majeruhi wa tetemeko la ardhi leo nchini Tanzania

Maeneo yalioathirika zaidi kwa Tanzania ni, Bukoba na Nsuga yaliyoko Kagera na baadhi ya maeneo ya Mwanza. Wakazi wa mikoa ya Kagera, Mwanza, Tabora, Geita na Katavi wameshuhudia mtetemeko huo kwa uzito tofauti.

Nyumba iliyoharibiwa kwa tetemeko la leo

Mbali na Mikoa hiyo ya Tanzania, tetemeko hilo limeikumba pia baadhi ya miji nchini Uganda ikiwemo Kampala na Mbarara Kusini Mashariki mwa nchi hiyo. Taarifa iliyotolewa na uongozi wa hospitali ya rufaa ya Mjini Bukoba, imeeleza kuwa watu 10 wamepoteza maisha kuokana na janga hilo la kimaumbile, huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa vibaya.

Majeruhi wakiendelea kupatiwa huduma ya kwanza hospitali ya Bukoba

Hadi tunaingia mitamboni bado kulikuwa hakujatolewa taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo.

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA MAZIKO YA AL-HAJ ABOUD JUMBE

sawa sawa mgomo unaendelea

sawa sawa mgomo unaendelea

RAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR ABOUD JUMBE AMEFARIKI DUNIA

JUMBAliyekuwa Rais wa pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kati ya tarehe 7 Aprili 1972 hadi 30 Januari 1984, Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia mchana wa leo nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar es Saalam baada ya kuugua kwa muda mrefu na anatarajiwa kuzikwa kesho Zanzibar. Kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe kimethibitishwa na mmoja wa wanafamilia wa marehemu.

Jumbe atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuiongoza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akichukua nafasi ya aliyekuwa rais wa visiwa vya Zanzibar marehemu Abeid Aman Karume aliyefariki mwaka 1972.

 Enzi za uhai wake Aboud Jumbe alipotembelewa na jamaa mbalimbali akiwemo Dakta Gharib Bilal mwenye koti jeusi

Enzi za uhai wake Aboud Jumbe alipotembelewa na jamaa mbalimbali akiwemo Dakta Gharib Bilal mwenye koti jeusi

Enzi za uhai wake akiwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar alishirikiana na rais wa wakati huo wa Tanzania na Mwenyekiti wa chama cha TANU marehemu Julius Kambarage Nyerere kuanzisha Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kuvunja vyama vya TANU na ASP na kuunda chama kimoja cha CCM.

Enzi za uhai wake Aboud Jumbe alipotembelewa na jamaa mbalimbali akiwemo Dakta Gharib Bilal mwenye koti jeusi

Rais wa Zanzibar Dk Shein, Akutana na Ujumbe wa Kampuni ya Huawei Ikulu Zanzibar

H 1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbali mbali za serikali.

Wateule hao ni Dk. Juma Yakout Juma kuwa naibu Katibu Msaidizi wa Baraza la Mapinduzi na Mwadini Makame Haji kuwa Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala bora, walioteuliwa ni Abdulla Issa Mgongo kuwa Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti na Shaibu Ally Mwazema kuwa Mkurugenzi wa Miundombinu ya Taasisi, Utumishi na Maslahi ya watumishi.
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ, Khalid Omar Abdulla anakuwa Mkurugenzi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakati Mashaka Hassan Mwita ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Magharibi A.

Katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,  Issa mlingoti Ally anakuwa Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ Dar es salaam, Ameir Makame Ussi, Mkurugenzi Idara ya Mipango, Sera na Utafiti na Khalid Bakari Amran, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali.

Wengine ni Riziki Daniel Yussuf aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Idara ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa huku Ali Salim Matta akipewa nafasi ya Ofisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba.

Wizara ya Afya walioteuliwa ni Ramadhan Khamis Juma kuwa Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti na Ofisa Mdhamini Pemba ni Ali Bakari Ali.
Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Haji Hamid Saleh anakuwa Mkurugenzi Umwagiliaji Maji.

Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo, ni Dk. Omar Abdulla Adam anakuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni.

Katika  Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, walioteuliwa ni Abdulla Mwinyigogo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba na Ramadhan Mussa Bakari kuwa Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo, ambapo  Omar Ali Omar Bhai anakuwa  Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi katika
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira, walioteuliwa ni Tahir M. K. Abdulla kuwa Naibu Katibu Mkuu, na Hemed Salim Hemed anakuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Huduma za Maji na Nishati (ZURA).

Nana Mwanjisi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko.

Imetolewa na idara ya habari maelezo-zanzibar
Julai 20,  2016

Kinana atoa Masharti Endapo Rais Magufuli Atamhitaji Aendelee Kuwa Katibu Mkuu wa CCM

kinanaKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ametoa neno endapo Rais John Magufuli atamhitaji kuendelea na wadhifa huo, huku akibainisha kuwa amekutana na changamoto nyingi katika nafasi hiyo kiasi kwamba wakati mwingine alikata tamaa.

Mwanasiasa huyo maarufu ndani ya CCM na nchini, anatarajiwa kuhitimisha uongozi wake wiki hii wakati Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa, Rais John Magufuli atakapokabidhiwa uenyekiti huo na kuunda Sekretarieti yake mpya ambayo haijulikani kama itaongozwa tena na Kanali huyo wa zamani wa Jesh

Akizungumza jana na waandishi wa habari baada ya kukagua Ukumbi wa Mkutano Maalumu wa CCM utakaofanyika keshokutwa Jumamosi, Kinana ambaye amekuwa katika nafasi hiyo kwa miaka mitatu na nusu, alisema aliombwa katika nafasi hiyo baada ya kuwa aliamua kustaafu, lakini akakumbana na changamoto mbalimbali.
CCM kuwa mbali na wananchi 
Alisema kuna wakati aliona kama vile chama kiliacha kwenda kwa wananchi na kwamba hakikuwa karibu sana nao.
“Ninyi ni mashahidi, ikabidi kubuni utaratibu mzuri wa kwenda kwa wananchi ili chama kiwe karibu na wananchi, kiwasikilize na kuwa sauti ya wananchi kifuatilie matatizo yao kisimamie utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi,” alisema Kinana na kuongeza kuwa katika kufanya hivyo amekuwa akiwasiliana na Rais na Waziri Mkuu kwa ajili ya matatizo kutatuliwa.
 
“Changamoto ya pili ya kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya chama, hapo nyuma kulikuwa na misukosuko kidogo ya umoja na mshikamano, kushutumiana na kulaumiana,” alisema na kuongeza kuwa kazi nyingine aliyofanya ni kuimarisha umoja ndani ya chama, kushirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha chama kinajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kurejea katika misingi yake ya awali katika maeneo ya uadilifu, uwajibikaji na utendaji kazi kwa ufanisi.
Azuiwa ziarani
Kinana alisema amekwenda wilaya zote, majimbo, mikoa na nusu ya kata za nchi na amesafiri zaidi ya kilometa 192,000, kufanya mikutano zaidi ya 3,700 ya aina mbalimbali ya ndani na nje na haikuwa kazi rahisi
 “Changamoto nilizokutana nazo ambazo lazima nikiri ni pale nilipotaka wakati mwingine kufanya ziara kwenye maeneo fulani fulani niliambiwa ni hatarishi siwezi kwenda kwa hiyo ilibidi nibishane na viongozi na watendaji wakuu wa serikali…nikasema hapana nimeamua kwenda lazima niende,” alisema Kinana.
Katibu huyo akitoa mfano alisema kuna wakati aliamua kutoka kwa boti kutoka Nyamisati wilayani Rufiji kwenda Mafia, viongozi wa Mkoa wa Pwani walifikiri si njia salama ya kusafiri na kumpelekea ujumbe asisafiri kwa boti, bali asafiri kwa ndege, lakini alisema hapana ataondoka kwa boti.
“Walichofanya wakakaa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na wakaniandikia barua rasmi kwamba tunakushauri usisafiri kwa boti safiri kwa ndege kwa maana nyingine walikuwa wanajivua lawama kwa yatakayotokea, lakini vile vile kunitisha kidogo kwamba si salama zaidi nikawasisitiza hapana,” alieleza Kinana.
Ashitakiwa kwa JK
“Baadaye Rais mstaafu Kikwete alikuwa Msoga, viongozi wa Mkoa wa Pwani wakaenda kumwambia tumezungumza na Katibu Mkuu wako naona hasikii tumemuandikia barua ya kumuomba asisafiri na boti hasikii, Rais akaandika meseji ndefu sana…nikamjibu rais nakuheshimu mamlaka yako ni makubwa si vizuri nikakukatalia, lakini niruhusu nikukatalie kwa sababu hata wananchi wanaosafiri kwenye boti hii wanahatarisha maisha yao, ni vizuri na mimi nikahatarisha maisha yangu hata kidogo… akaniambia nimekuelewa endelea,” alibainisha.
Alisema zipo changamoto nyingi sana nyingine, kwa mfano Mbambabay kwenda Kyela, mkuu wa mkoa akamuambia boti haifai kusafiri akasema mara haiwezi kusafiri imeharibika.
“Nikazungumza na Mwakyembe akapeleka mafundi wakatengeneza, safari haikuwa rahisi, lakini changamoto zilikuwa nyingi sana, kwingine Lupingu kule ni gari moja tu ndio inayoshuka chini hakuna kupishana magari nikaambiwa nisiende nikasema nina kwenda,” alisema na kuongeza kuwa kulikuwa na ubishi mwingi wakati mwingine alionekana mtu mmoja kidogo ambaye hasikilizi ushauri sana.
Pia nyingine zinazotokana na changamoto za wananchi kutolipwa mazao yao kwa wakati, mbolea kutofika kwa wakati, halmashauri kutopata fedha za maendeleo kwa wakati, watumishi wa umma wanaohamishwa kwenda vijijini hawaendi vijijini kwenda kuwahudumia wananchi, tatizo kubwa la migogoro kati ya wakulima na wafugaji kati ya wananchi na hifadhi za taifa.
“Ndio maana mnaniona siku hizi nimenyamaza kwa sababu yale yote niliyokuwa nikiyaombea yanafanyika, umangimeza haupo watu wachape kazi wawahudumie wananchi, uadilifu unapigwa vita, rushwa inapigwa vita, uwajibikaji na uadilifu unahimizwa, utendaji kazi unatakiwa na hayo yasipofanyika mtu anaondolewa mara moja,” alifafanua Kinana ambaye kuanzia mwaka 2014 hadi mwanzoni mwa mwaka jana alitembea kote nchini akikisafisha chama chake na kuibana serikali.
Kurejea kwake CCM
“Yalitokea mazingira ambayo niliombwa na viongozi wastaafu na viongozi wa chama kuniomba niwe mtendaji mkuu wa chama chetu. Si nafasi ambayo niliipenda, bali niliitwa na nikakalishwa wakanisihi na mimi nikakubali sababu ni wito na kwa kuwa ni watu ninaowaheshimu na wana dhamana kubwa kwenye nchi yetu, nikakubali kufanya kazi hiyo,” alisema Kinana akizungumzia jinsi alivyoteuliwa kushika nafasi hiyo.
Alisema amekuwepo katika uongozi ndani ya chama kwa muda mrefu (miaka 25) ndani ya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa, na alihisi ni wakati muafaka wa kung’atuka.
“Mwanasiasa mzuri ni yule anayejua wakati wa kuingia na wakati wa kutoka. Ni wakati mzuri wa kung’atuka kuachia waingie wenye umri wa kati na umri wa vijana kuachia waongoze chama na kuwaamini,” alieleza.
Alisema moja ya mambo ambayo walikubaliana wakati ule akajitahidi kukiimarisha chama, kusimamia na kumsaidia mwenyekiti kusimamia mchakato wa kuwapata wagombea kwenye nafasi zote za Urais, Ubunge na Udiwani. Pia alijitahidi kuendesha shughuli za kampeni na uchaguzi na utakamalizika.
 
“Uchaguzi umekwisha niruhusiwe kupumzika, na wote waliafiki na kukubali sasa muda umefika kwa hiyo nimewakumbusha yale tuliyokubaliana muda wake umefika sasa wengine wakaniuliza hivi ndivyo tulivyokubaliana nikawaambia wazee hamjawa wazee kiasi cha kusahau ndio haya tuliyokubaliana,” alieleza.
Akiombwa na JPM
Alipoulizwa kama akiombwa na Rais Magufuli aendelee kwa Katibu Mkuu, Kinana alisema, “Niseme hajasema, hatujazungumza hilo, likitokea tutaangalia, tutakaa naye kikao kama akiniomba, tutakuwa na kikao na mazungumzo muda utakapofika kama nilivyokuwa na mazungumzo na kikao kama kwa wale walioniomba mwaka 2012.”
Waliokisaliti chama
Akizungumzia walioisaliti CCM katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana, mtendaji huyo wa CCM alisema msaliti yeyote adhabu yake ni mbaya sana, hata kwenye chama cha siasa.
“Kwenye CCM wapo watu walioyumba, kulikuwa na wimbi kubwa mwaka jana, watu waliyumba hivi kidogo wakakaa mguu upande huku hawapo na kule hawapo, wako ambao sio tu waliyumba, bali walikiuka maadili na hawakushiriki kwenye shughuli za kampeni,” alisema.
Pia alisema wapo ambao hawakushiriki, hawakusaidia na wakasaidia upinzani na kila mtu atakuwa na adhabu yake kulingana na makosa yake.

“Kama mmekuwa mkifuatilia kuna waliochukuliwa hatua ngazi za wilaya na mikoa. Kwa mfano, Shinyanga 123 walichukuliwa hatua. Wapo wanaotakiwa kuchukuliwa hatua kwenye ngazi za juu, sasa jambo moja mtu yeyote kabla ya kuchukuliwa hatua lazima aelezwe mashtaka yake, apewe fursa ya kusikilizwa, kwa hiyo hawa wote watasomewa mashtaka, watasikiliza na kupewa adhabu kwa kadri itakavyostahili, lakini hatua zitachukuliwa mara baada ya Mkutano Mkuu kumalizika,” alieleza