Kuku wa Peduu kutoka Brazil

Kuku wa Peduu kutoka Brazil

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatarajia kuongeza kodi ya uingizaji wa kuku kutoka nje ya nchi kwa asilimia 100 ili kulinda soko la wafugaji wa ndani.
Hatua hiyo ya serikali imekuja baada ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kuitaka serikali kupiga marufuku kuingizwa kuku wa Peduu kutoka nchini Brazil wanaodaiwa kushusha soko la wafugaji wa ndani.
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais Mohammed Aboud Mohammed amesema kuwekewa kodi kubwa kuku hao kutasaidia kulinda soko hilo kutokana na wanachi wengi  kujiajiri katika sekta hiyo.
Hata hivyo amesema serikali itaandaa mkutano wa kitaifa wa kujadili athari za kupiga marufuku kuku hao kuingizwa nchini baada ya kuonekana soko la ndani halitoshelizi mahitaji na kuathiri sekta ya utalii.
Nae waziri wa mifugo na uvuvi Abdilahi Jihad Hassan amesema serikali inatarajia kujenga soko kubwa litakalofanana na soko la Fery mjini Dar es Salaam katika eneo la Malindi kwa ufadhili wa serikali ya Japan.
Akijibu hoja za wajumbe wa baraza la wawakilishi waliochangia hotuba ya  bajeti ya wizara hiyo amesema ujenzi wa soko hilo  unatarajiwa kuanza Julai mwakani baada ya serikali ya Japan kupitisha mradi huo.
Hata hivyo hotuba ya bajeti ya wizara hiyo imeshindikana kupitishwa kufuatia kuzuka hoja ya kuitaka serikali kupiga marufu uingizaji wa kuku kutoka Brazil, madai yanayopingwa na serikali

—————————————————————————————————————————————————————————————————————————————————————-

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR KUSUBURI DNA

ZANZIBAR                      GGWizara ya afya Zanzibar imesema inasubiri sehemu nyingine mbili za mashine ya kupimia vinasaba zitakazogharimu zaidi ya shiligi milioni 600 ili kusaidia ushahidi wa kesi mahakamani.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi naibu waziri Dr. Sira Ubwa Mwamboya amesema wizara inafanya taratibu za kuzipata sehemu hizo kupitia kwa washirika wa maendeleo.

Amesema sehemu ya kwanza ya mashine hiyo imetolewa msaada na taasisi moja ya Marekani kupitia chuo kikuu cha MarekaniBrownUniversity.

Amesema mashine za DNA zinatumika zaidi kwa kesi za mzazi anaemkataa mwanawe.

Aidha amesema kwa kesi za ubakaji na kulawiti hazinaulazimu wa kutumia mashine ya DNA, iwapo mlalamikaji anao ushahidi wa kitaalamu unaotakiwa.

Hata hivyo amesema tatizo linalokwamisha kesi za kulawiti na kubaka liko katika vituo vya polisi na wananchi wenyewe kukataa kutoa ushahi kwa kuogopa aibu au uhasama na familia.

…………………………………………………………………..

Waziri wa sheria na katiba Zanibar Aboubakar Khamis Bakary

Waziri wa sheria na katiba Zanibar Aboubakar Khamis Bakary

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IMESEMA ITAENDELEA KUSIMAMIA MATAKWA YA WANANCHI WA ZANZIBAR KATIKA MABADILIKO YA KATIBA MPYA WATAKAYOKUBALIANA KWENYE MABARAZA YA KATIBA.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA ABOUBAKAR KHAMIS BAKAR AMETOA KAULI HIYO ALIPOKUWA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA WAWAKILISHI, CHUKWANI.

AMEESEMA BAADHI YA MABADILIKO HAYO YATACHUKUA MUDA NA KUWATAKA WANANCHI KUWA WASTAHAMILIVU.

AIDHA BAKARY AMESEMA ZANZIBAR INAHITAJI KATIBA ITAKAYOBADILISHA HALI YA KISIASA, KIUCHUMI NA KIJAMII, HIVYO AMEWATAKA WAJUMBE WA BARAZA HAYO KUJALI MSLAHI YA NCHI YAO

AKIZUNGUMZIA UTENDAJI WA MAHAKAMA AMESEMA WIZARA IMECHUKUA HATUA YA KUFANYAMABADILIKO YATAYONGEZA UFANISI WA UTOWAJI WA MAAMUZI YA KESI.

AMESEMA IKIWEMO CHA UTOWAJI WA MAAMUZI YA KESI MAHAKAMANI HAKIRIDHISHI AMBAPO MWAKA 2012/2013 KESI ELFU MBILI, 874 ZEMETOLEWA KATI YA KESI ELFU NANE, 913.

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA IMEOMBA KUIDHINISHWA MATUMIZI YA SHILINGI BILIONI NANE NA MILIONI 188 KWA KAZI ZA KAWAIDA NA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDA 2013/2014.

………………………………………………………………………………………….

………………………………………………………………………………………..

SMZ HAINA TAARIFA WAZANZIBARI WANOFANYA KAZI NJE YA NCHI KINYUME NA MAADILI

Waziri wa kazi, uwezeshaji wananchi kiuchumi na Ushirika Haroun Ali Suleiman

Waziri wa kazi, uwezeshaji wananchi kiuchumi na Ushirika Haroun Ali Suleiman

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema haina taarifa kuwa baadhi ya vijana wa kike wa Zanzibar walikwenda kufanya kazi katika nchi za Kiarabu inayokwenda kinyume na maadili.

Waziri wa kazi, uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika Haroun Ali Suleiman amesema asilimia 90 ya wanawake hao wanafanya kazi za majumbani, lakini hakuna taarifa za kufanyakazi zisizostahiki.

Akijibu saala katika kikao cha baraza la wawakilishi amesema serikali iko katika hatua za miwisho za kusaini mikataba na nchi za Oman na Qatar ili kuwalinda wanzibari wanaofanyakazi katika nchi hizo.

Jumla ya vijana mia nne na 89 wakiwemo wanawake mia nne na 18 wamepata fursa za ajira nje ya nchi tokea mwaka 2011 baada ya serikali kuanza utaratibu wa kuwatafutia ajira wananchi katika nchi za kiarabu.

Wanawake hao wanaodhaniwa kufanyakazi zinazokwenda kinyume na maadili wako katika nchi za Saud Arabia, Qatar, Oman na Falme za kiarabu.

…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….

SMZ KUWALIPISHA GHARAMA ZA MASOMO VIJANA WANAOKATAA KUFANYAKAZI ZANZIBAR

DUNIOMARWizara ya afya imeaanda mpango wa kuwalipisha gharama za masomo wafanyakazi waliodhaminiwa na serikali waliokataa kurejea nyumbani kufanyakazi baada ya kumaliza masomo yao.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi waziri wa afya Juma Duni Haji amesema serikali inatumia fedha nyingi kuwasomesha wafanyakazi kutokana na ukosefu wa wataalamu katika sekta ya afya.

Amesema baadhi yao wanakataa kurudi nyumbani baada ya kumaliza masomo yao wakidai maslahi duni, lakini amesema mpango huo utasaidia kuwadhibiti wafanyakazi wengine.

Hata hivyo amesema serikali inaendelea kuwaonezea maslahi wafanyakazi ili kupunguza wimbi la kwenda kufanyakazi nchi za nje….CLIPS…(SAVED-DUNI)

Nae waziri wa nchi ofisi ya rais, utumishi wa umma na utawala bora Haji Omar Kheir amesema serikali inafanya utafiti kujuua idadi ya vijana waliodhaminiwa na serikali waliokataa kurudi nyumbani kufanyakazi.

Madaktari wengi wa Zanzibar wanakwenda kufanyakazi katika nchi za Malaysia, Bostwana na Tanzania bara wakilalamikia maslahi duni wanayolipwa na serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Advertisements