bbbbWake wa viongozi wa jumuiya ya Uamsho ambao waume zao wamewekwa ndani kwa zaidi ya miezi tisa wametaka kuchukuliwa hatua za kisheria katika uendeshaji wa kesi hiyo badala ya utashi wa kisiasa.

Wakizunguma na waandishi wa habari kiongozi wa wake hao 16 Asha Idd amesema uwamuzi wao huo sio kuingilia kazi za mahakama, lakini wanawajibu wa kukumbusha utekelezaji wa sheria kwenye kesi hiyo.

Amesema kitendo hicho cha kuwekwa ndani waume zao licha ya kuathiri familia zao kisaikolojia, lakini pia kinarudisha nyuma taaluma ya dini ya kislamu kutokana na waislamu wengi walihudhuria katika darsa zao..

Aidha Asha ameziomba taasisi za haki za binadamu ndani na nje ya nchi na rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein kuangaliwa mwenendo wa kesi za waume zao ili kuona haki inatendeka

 

 

—————————————————————————————————————————

Mufti mkuu wa Oman, Sheikh, Ahmed bin Hamed

 

 

———————————————————————————————-

Mufti mkuu wa Oman, Sheikh, Ahmed bin Hamed , amewataka Waislamu kisiwani Pemba kuitumia Misikiti kwa  ajili ya kuamrishana mema na kuakatazana maovu.

Akifungua msikiti huko Mkanjuni amesema khitilafu ziliopo miongoni mwa waumini wadini hiyo isiwe chanzo cha kuleta migogoro kwani lengo lao kuu ni kwa ajli ya kumuabudu mwenyeezi Mungu mmoja.

Akizungumzia suala la kuimarisha misikiti amewataka waislamu kujenga uhusiano baina ya Msikiti na Msikiti ilikukuza Udugu na umoja katika kuipigania Dini ya kislamu.

Mufti huyo yupo Kisiwani Pemba, kwa zira maalum iliyoandaliwa na Jumuiya ya Istiqaama Pemba, na kupata fursa ya kuangalia shughuli zinazofanywa na jumuiya hiyo ya kidini.

————————————————————————————————–

WANAZUONI FANYENI UTAFITI JUUYA MUANDAMO WA MWEZI-DR. MWINYI

Waziri wa Ulinzi na

Dr.

Jeshi la kujenga Taifa nchini Dk. Hussein Mwinyi amewataka wanazuoni wa kislamu kufanya utafiti zaidi ili kuusaidia Uislamu kusimama katika misingi yake iliyowekwa na Mwenyezi Mungu.

Waziri huyo ameyasema hayo mjini Dar es Salaam wakati akizindua kitabu chenye maudhui ya mwezi upi sahihi wa kitaifa au wa kimataifa kilichoandikwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislamu mkoani Morogoro Profesa Juma Mikidadi.

Amesema katika uzinduzi huo suala la muandamo wa mwezi hasa wa Ramadhani limekuwa likiwagawa Waislamu pasipo sababu za msingi hali inayosababisha umoja baina yao kutokuwepo.

Awali akizungumzia kuhusu kitabu hicho, Profesa Juma Mikidadi, amesema ni aibu kwa Waislamu kuitana majina mabaya kwa sababu ya kuhitilafiana katika kufunga na kufungua jambo ambalo alisema linawezekana kupatawa muafaka.

————————————————————————————————–

Seif Sharif Hamad

Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad amewata waumini wa dini ya kiislamu nchini kujenga maelewano,umoja na mshikamano katika kutafuta mbinu bora za kuuendeleza uislamu.

 

Maalim Seif ameyasema hayo huko katika viwanja vya Fyssabilillah Markadh Ole Kianga wakati akiwahutumia waumini wa dini ya kiislam kutoka maeneo tofauti ya Afrika Mashariki katika ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa.

 

Amesema kuwa taasisi za dini zimekuwa na mchango mkubwa katika kuiunganisha jamii inapokubwa na mifarakano,huku akitolea mfano juhudi zilizofanywa na viongozi wa dini katika kutatua mifarakano ya kisiasa iliyokuwa imeikumba Zanzibar .

 

Amesema kuwa jamii inashughulia kazi kubwa zinazofanywa na viongozi na mashekh,maulamaa na taasisi za dini kwa umma ikiwemo kuwaelimisha juu ya kujenga tabia njema,kuhimiza uadilifu na uwajibikaji kwa viongozi wa serikali na wananchi wake.

 

Makamo wa kwanza amesema kuwa juhudi zinazofanywa na viongozi hao zimetoa mchango mkubwa kwa amani na utulivu wa nchi na zinapaswa kuungwa mkono na waumini wote kwa faida ya waumini hao na Taifa kwa kupiga vita matendo maovu.

 

Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Ijitimai Kitaifa Amir Hafidh ameeleza kusikitishwa kwake kuona ni waumini wachache wa Visiwa vya Unguja na Pemba ambao walikuwa wakishiriki katika kufanya kazi mbali mbali za matayarisho za Ijitimai hiyo.

 

Amesema kutojitokeza kwao kwa wengi kulipelea kamati hiyo kuelemewa na majukumu mengi,huku waumini hao wakikosa fadhila zilizopatikana kutokana na kazi hizo.

 

Aidha ameiyomba serikali ya Zanzibar kutafuta njia za kuisadia Jumuiya ya Fyssabilillah Zanzibar kwa kuwapatia gari ambalo litawasaidia katika kazi zao za maandalizi kwa vile wamekuwa wakipata tabu sana kwa kukosa usafiri.

 

Miongoni mwa waumini walioshiriki katika ijitimai hiyo mwaka huu ni pamoja na kutoka Rwanda,Malawi,Uganda, Burundi, Kenya, DRC kwa nchi jirani na Mikoa 18 ya Tanzania bara na waumini wa visiwa vya Unguja na Pemba ambapo ijitimai hiyo itakamilika tarehe 18 mwezi huu.

————————————————————————————————

MALIM SEIF AFUNGUA MADRASA TOMONDO

Malim Seif akifungua Madrasa ya Qadiriyatul Iman ya Tomondo.

MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad, amesema kuporomoka kwa maadili, ni moja kati ya matatizo makubwa yanayowakabili Wazanzibari, hususan vijana, wakati huu.

Maalim Seif amesema hayo jana huko Tomondo, Wilaya ya Magharibi Unguja, alipozungumza na wazazi, walimu na wanafunzi katika hafla ya uzinduzi wa Madrasa ya Qadiriyatul Iman.

Amewataka masheikh na walimu  wa vyuo na madrasa kuzingatia wajibu wao mkubwa katika kuwaandaa vyema watoto na kuwarudisha katika maadili mema waliyorithi kutoka kwa wazazi wao.

Aidha amewataka wazazi na walezi wa watoto hao kuwa na mashirikiano ya karibu na walimu na kuelewa jukumu  lao katika kuiendeleza madrasa hiyo kwa kutoa michango yao ya hali na mali kwa maslahi yao na  watoto wao.

Alisema biashara ilio nzuri kwao ni ile ya kutanguliza mbele kheir kwa minajil kuwa mafao yake watayakuta huko waendako.

Akizungumza kwa masikitiko, alisema kuwa Zanzibar iliokuwa ikisifika sana hapo zamani, kwa kuwa na watu wema, wakarimu na mahala patukufu pa kujifunza elimu ya dini ya Kiislamu, imeanza kupoteza haiba na sifa hizo kutokana na na kuporomoka kwa maadili ya watu wake.

Alisema Zanzibar ilijuilikana katika ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati kama kituo muhimu cha kujifunza uislamu na kuwafanya wanazuoni kutoka nchi mbali mbali (ambao leo ni mashuhuri) kuja kujifunza dini hiyo.

Alisema kutokana na vijana kukosa mafunzo ya dini, wamejikuta wakijiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya, na kufikia kuwa janga la Taifa hivi sasa.

Aidha alisema mbali na vijana hao kuwa tatizo katika jamii kutokana na vitendo vyao viovu ikiwemo wizi, lakini pia Taifa limepoteza rasilimali yake muhimu katika kuimarisha uchumi wake.

Alifafanua kuwa janga hilo limeziweka familia zote za Wazanzibari katika hali ya mashaka, kwani hakuna hata familia moja inayoweza kujinasibu kuwa iko salama kwa kukosa kijana anaetumia uraibu huo.

Katika hatua nyingine Makamu wa kwanza wa Rais, aliwakumbusha wazazi na walimu hao juu ya janga la ukimwi ambalo limekuwa likiwaathiri zaidi vijana na kuanisha kuwa chanzo chake ni zinaa iliotapakaa katika kila pembe ya miji na vijiji.

Alisema njia pekee ya kuondokana na maambukizo ya ugonjwa huo ni kurudi katika misingi ya maadili ya Kizanzibari na kutekeleza kwa vitendo maamrisho ya Mwenyezi Mungu.

Aliwapongeza viongozi na walimu wa Madrasa hiyo kwa juhudi kubwa wanayoichukua kuwaendeleza vijana hao katika elimu za aina zote ikiwemi ile ya dunia na akhera.

Maalim Seif aliahidi kuchangia Shilingi Laki tano, kusaidia maendeleo ya madrasa hiyo.

Mapema katika risala yao, wanafunzi wa madrasa hiyo walimweleza Makamu wa kwanza wa Rais changamoto mbali mbali zinazowakabili, ikiwemo ufinyu wa jengo,vikalio,computet, printer, mishahara ya walimu, mashirikiano duni kati ya wazazi na walimu  pamoja na fedha za kununua kiwanja kipya na gharama za ujenzi wake.

Madrasatul Qadiriatul Iman ilioanzishwa 1993 ina wanafunzi 250, ambapo miongoni mwa masomo yanayofundishwa ni Fikhi,Sira,Tahfidh –l- Qoraan pamoja na kuendesha masomo ya ziada (tuition) kwa wanafunzi wanaokabiliwa na mitihani ya Taifa.

———————————————————————–

MAHAKAMA ZANZIBAR YATOA KIFUNGU CHA MIEZI 24 KWA MTU ALIECHOMA QUR-ANI

Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe imemuhukumu Ramadhan Handa Tuma mwenye umri wa miaka 28 kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miezi 24 kwa kupatikana na  kosa la kuchoma moto Msahafu na Juzuu za dini ya Kiisilamu.

Hukumu hiyo imetolewa na hakimu Khamis Ali Simai  mara baada ya kumtia hatiani mshitakiwa huyo dhidi ya mashitaka ya kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani pamoja na kukashifu dini.

Akitoa hukumu hiyo, hakimu Khamis amesema shitaka la kwanza la kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani atalipa faini ya shilingi 200,000 na endapo atashindwa atatumikia Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miezi sita.

Kosa la pili lililomkabili mshitakiwa huyo ni kukashifu dini, mahakama hiyo imempa adhabu ya kutumikia Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miezi 18, na kufahamisha kuwa adhabu zote hizo zitakwenda sambamba.

Upande wa mashitaka ulioongozwa na Raya Issa Mselem, amesema haukuridhishwa na Hukumu hiyo na kusema kwamba anakusudia kukata rufaa dhidi ya adhabu iliyotolewa kwa shitaka la pili la kukashifu dini.

Hata hivyo Mwendesha mashitaka Raya Mselem ameomba itolewe adhabu kali dhidi ya mshitakiwa huyo  kutokana na kitendo alichokifanya ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hiyo.

Kwa upande wake mshitakiwa huyo aliomba apunguziwe adhabu kwa madai ana familia inayomtegea akiwemo mke na mtoto, pamoja kusumbuliwa na maradhi ya tumbo.

Kwa mujibu wa mahakama hiyo, Ramadhan Handa Tuma alifanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani Novemba 16 mwaka jana Mombasa zanzibar ambapo kwa makusudi na bila ya halali alichoma moto msahafu pamoja na juzuu za dini ya Kiisilamu .

—————————————————————————

——————————————————————————-

MTU ALIECHOMA MOTO QUR-ANI TUKUFU HUKUMU YAKE KUTOLEWA FEB. 21, 2011

Mahakama ya wilaya ya Mwanakwerekwe  inakusudia kutoa hukumu dhidi ya Mshtakiwa Ramadhan Hamda Tuma Februari 21 mwaka huu  anatuhumiwa kuohoma juzuu za msaafu na kukashifu dini ya kiislam.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya hakimu Khamis Ali Simai kufunga kusikiliza ushahidi hii leo ambapo mashahidi wawili walitoa ushahidi upande wa utetezi na mashahidi saba walitoa ushahidi upande wa mashtaka.

Waendesha Mashtaka wa kesi hiyo Raya Mselem na Khamis Jafar wamedai mbele ya mahakama hiyo kwamba mshitakiwa huyo ametenda kosa hilo  Novemba 16 huko Mombasa Wilaya ya Magharib .

Mshitakiwa huyo ametenda kosa hilo la kukashifu dini kinyume na kifungu cha sheria na kufanya kitendo kinachopelekea uvunjifu wa amani kwa mujibu wa sheria za Mapinduzi Zanzibar.

Katika kesi hiyo Mshatakiwa huyo amekuwa akijijitetea mwenyewe huku akishindikizwa na ulinzi mkazi wa Polisi mwenye Silaha.

Hata hivyo mamia ya waumini waliohuduria mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo wamesema

WAISLAMU KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA ZANZIBAR

Waislamu nchini wametakiwa kuongeza bidii katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuliletea maendeleo taifa lao wakati huu wakiingia katika mwaka mpya wa kislamu wa 1432 Hijiria.

Katibu afisi ya musti Zanzibar Sheikh FAdhili Sora ametoa wito huo katika kuukaribisha mwaka mpya wa kislamu.

Amesema uislamu unahimiza kufanya kazi kwa bidii na niharamu kwa mtu kupokea malipo ambayo hakuyafanyia kazi.

Amewataka waislamu kumshukuru mwenzi mungu kwa kuwafikisha kuanza mwaka mpya wa kislamu na kuwataka kujitathimi kwa kiasi gani wameza kujikurubisha kwa mwenyezi mungu kwa kufanya mambo mema.

Amesema huu ni wakati muafaka kwa wailslamu kutubia madhambi yao huku wakiadhimia kutorudia tena kuyafanya madhambi hayo……CLIPS….(SAVED-SORAGA)

Aidha sheikh Soraga amesema Zanzibar inaingia katika mwaka mpya wa kislamu wa 1432 Hijiria wakati nchi ikiwa katika amani na utulivu na kusema neema hiyo ni wajibu wa waislamu kuishukuru na kuienzi

KESI YA MTU ALIECHOMA MOTO QUR-ANI TUKUFU IMEANZA KUSIKILIZWA ZANZBIAR

Mamia ya waislamu Decemba 2 walihudhuria katika mahakama ya wilaya Mwanakwerekwe kusikiliza kesi  ya mtu aliechoma moto Qur-ani tukufu katika maeneo ya Tomondo wilaya ya magharibi.

Mtuhumiwa huyo  Ibrahi ambae alisilimu na baadae kurudi kwenye ukiristo alichoma moto Qur-ani hiyo Novemba 2010.

Awali kijana huyo alisilimu kwa hiari yake na kupewa nyumba ya kuishi. Mahakama ya Mwanakwerekwe imeahirisha kesi hiyo hadi Decemba 13 mwaka 2010.

Kijana huyo anaedaiwa kuchoma moto Qur-ani hiyo alikuwa na mtindo wa kwenda kanisani na baada ya kuonekana na mwenendo huo muislamu aliempa nyumba yake kwa ajili ya kuishi alimwambia ahame na ndipo mkewe ambae hajasilimu alimshawishi kuichoma moto Qur-ani.

Kitabu hicho kitakatifu kilichomwa moto pamoja na taka zilizosafishwa kwenye nyumba anayoishi Ibrahim katika eneo la Tomondo.

Inasemekana mtoto mmoja aliekuwa akipita njia alikiona kitabu cha Qur-ani kikichomwa moto na kutoa taarifa kwa waisalmu wanaoishi eneo hilo.

Baada ya kupata taarifa hizo waislamu walimkamata Ibrahim na kumpeleka kituo cha polisi cha Mazizini na kufunguliwa kesi katika mahakama ya wilaya Mwanakwerekwe.

Wakizungumzia kesi hiyo baadhi ya walislamu waliohudhuria wamesema iwapo kesi hiyo itazunguushwa hawatavumilia

——————————————————————————————————–

Waislamu Tanzania waaswa kuenzi umoja na mshikamano

Print E-mail
Saturday, 11 September 2010
Sample ImageWaislamu nchini Tanzania wametakiwa kujenga umoja miongoni mwao na pia kuhakikisha vijana wao wanaishi maisha yanayopendeza katika jamii ili kuwa na maadili mema.Mwito huo umetolewa na Mufti wa Tanzania, Shehe Mkuu Issa bin Shaaban Simba mara baada ya kumalizika sala ya Idi ‘l-Fitr ambayo Kitaifa ilisaliwa katika Msikiti wa Riyadh wa mkoani Tanga.Gazeti la Serikali la Habari Leo limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, sala hiyo ilisalishwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi na kuhudhuriwa na Rais Jakaya Kikwete.Mufti Simba amesema, Waislamu wanatakiwa kujenga umoja miongoni mwao kama alivyoelekeza Mtume Muhammad (SAW), kuwa jamii ya Kiislamu inapaswa kuishi kwa umoja, kushirikiana na kushikamana.Vile vile amesema, wazazi wa Kiislamu wanapaswa kuhakikisha vijana wao wanaishi maisha mema na kufuata misingi ya dini yao badala ya kushuhudia vijana wa kiume wakivaa hereni na kusuka nywele

—————————————————————-

Obama ataka waumini kuvumiliana.

Wakati leo ikitimia miaka tisa tangu kutokea kwa shambulio la kigaidi mjini New York, Septemba 11 2001, Rais Barack Obama wa Marekani ametoa wito wa kuwepo kuvumiliana kwa waumini wa dini tofauti.

Ameyasema hayo jana, katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Washington, Rais Barack Obama amesema pia kwamba nchi yake haiwezi kugawanyika kwa misingi ya dini.

Rais Obama ametoa kauli hiyo jana, wakati nchi yake ikiwa katika wakati mgumu, kufuatia mipango iliyotangazwa awali na kasisi wa kanisa moja nchini Marekani Tery Jones ya kutishia kuchoma moto nakala za kitabu kitukufu cha waislamu, Koran leo, kama kuadhimisha kumbukumbu ya miaka tisa tangu kutokea shambulio la kigaidi la Septemba 11, mwaka 2001..

Kasisi Terry Jones, asitisha mipango yake ya kuchoma nakala za Koran.Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift:  Kasisi Terry Jones, asitisha mipango yake ya kuchoma nakala za Koran.Aidha rais Obama alifafanua pia kwamba hawako katika vita na Uislamu ila wako katika vita na makundi ya kigaidi, ambayo yamepotosha  uislamu ama kutumia dini hiyo kufanya maovu yao.

Na katika kile kilichoonekana kugusia mipango ya ujenzi wa msikiti karibu na eneo llilipotokea shambulio la Septemba 11, Rais Obama alisema waislamu pia wana haki ya kujenga popote na kwamba Marekani inatoa uhuru sawa kwa watu wote wanawake kwa wanaume na haki yao ya kuabudu.

Wananchi wa Afghanistan wakiandamana kupinga mipango ya kasisi Terry Jones.Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift:  Wananchi wa Afghanistan wakiandamana kupinga mipango ya kasisi Terry Jones.Serikali ya Marekani imekuwa na wasiwasi kuwa mpango huo wa kuchoma moto nakala za Koran utahatarisha maisha ya wanajeshi wao, wanaohudumu nchini Afghanistan na Iraq.

Katika hatua nyingine, Imam Feisal Abdul Rauf ambaye anaongoza juhudi za ujenzi wa msikiti katika eneo lililokaribu na kilipokuwa kituo cha biashara kilichoteketezwa katika shambulio la bomu la Septemba 11, mwaka 2001 nchini Marekani, amesema hana mipango yoyote ya kukutana na kasisi Terry Jones ambaye ametishia kuchoma moto nakala za kitabu kitukufu cha waislamu,Koran.

Imam Feisal Abdul Rauf.Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift:  Imam Feisal Abdul Rauf.Awali Kasisi huyo pamoja na wafuasi wake, kwa siku kadhaa walipanga kuchoma moto nakala za koran, kwa kile alichodai kuadhimisha kumbukumbu hiyo ya leo.

Kasisi huyo amekubali kuachana na mipango yake hiyo, na kutaka kukutana na Imam Rauf ambaye amedai kuwa amekubali kuhamisha ujenzi katika eneo hilo na kwamba wao wamekubali kufuta mpango wao wa kuchoma moto nakala za Koran leo.

Watu wakiangalia ujenzi unavyoendelea katika eneo lililokuwa na kituo cha biashara cha kimataifa kilichoteketezwa katika shambulio la Septemba 11, mwaka 2001.Bildunterschrift: Watu wakiangalia ujenzi unavyoendelea katika eneo lililokuwa na kituo cha biashara cha kimataifa kilichoteketezwa katika shambulio la Septemba 11, mwaka 2001.Hata hivyo Imam Feisal Abdul Rauf, ambaye anaongoza ujenzi wa msikiti huo alikanusha taaraifa hizo, kwa kusema kuwa hajawahi kuwasiliana na kasisi huyo.

————————————————————————————————————-

Uchomaji wa Koran washutumiwa duniani kote

TERRY JONES

Mpango wa kuchoma nakala za kitabu kitakatifu cha Waislamu cha Koran katika jimbo la Florida nchini Marekani umezusha shutuma kali duniani kote
Mpango  wa  kuchoma  nakala  za  kitabu  kitakatifu  cha Waislamu  cha  Koran   katika  jimbo  la  Florida  nchini Marekani  umezusha  shutuma  kali  duniani  kote.

Mkuu  wa  masuala  ya  kigeni  wa  umoja  wa  Ulaya Catherine  Ashton  ameshutumu  kwa  jumla  tukio  hilo linalopangwa,  ambapo  mkuu  wa  jumuiya  ya  nchi  za Kiarabu  Amr Mussa  amemueleza  mkuu  wa  kanisa  hilo mchungaji  Terry  Jones   kuwa  ni  shabiki  tu,  na kuliambia  shirika  la  habari  la  AFP  kuwa  anawataka Wamarekani  kupinga  vikali  hatua  kama  hiyo.

Kituo   cha  kanisa  linaloongozwa  na  mchungaji  Jones kinachojulikana  kama ” njiwa  anayewafikia  watu  wote duniani “, cha  mjini  Gainesville, Florida  kimeapa kuchoma  nakala  za  Koran  wakati  wakiwakumbuka  kiasi watu  3,000  waliouwawa  na  watu  walioteka  nyara  ndege kutoka  katika  kundi  la  Al-Qaeda.

Baraza  la  Kikatoliki  linalohusika  na   madahalo  baina  ya dini  limesema  katika  taarifa  kuwa , kila  dini, pamoja  na vitabu  vyake  vitakatifu  na  alama  zake , ina  haki  ya kuheshimiwa  na  kulindwa.

Rais  Barack  Obama  amezungumzia   kwa  mara  ya kwanza   leo  kuhusiana  na  mpango  huo  wa   mchungaji kutoka  Florida  kutaka  kuchoma  nakala  za  Koran , akisema  kuwa  itakuwa  ni  bahati  kubwa  kwa  al-Qaeda, na  kumuomba   mchungaji  huyo  kubadili  mawazo  yake.

Lakini  akijibu  miito  ya  maafisa  wa  ngazi  ya  juu  wa mambo  ya  kigeni  kutoka  India, Pakistan  na  kwingineko kuwa  serikali  ya  Marekani  inapaswa  kuzuwia  kuchomwa kwa  nakala  hizo, Obama  amedokeza   katika  mahojiano na  shirika la  habari  la  ABC  kuwa   mikono  yake imefungwa  na  katiba  ya  Marekani.

Mchungaji  huyo  Terry  Jones, anaweza  kutajwa  tu  kuwa alifanya  tukio  hilo, Obama  amesema. Jones  na  kundi lake  dogo  la  waumini   katika  mji  wa  Gainesville , wanapanga   siku  ya  Jumamosi  kufanya  kumbukumbu ya  mwaka  wa  9  wa  shambulio  la  kigaidi  dhidi  ya Marekani   kwa  kuharibu  kitabu  hicho  kitakatifu   cha Waislamu. Halmashauri  ya  jiji  hilo  imekataa  kumpa kibali  cha  kuchoma  moto, na  unajitayarisha  na  hatua za  usalama  kwa  ajili  ya  tukio  hilo.  Kamanda  wa majeshi  ya  NATO  nchini  Afghanistan  jenerali  David Petraeus  ameonya  kuwa   kuchoma  nakala  za  Koran kutatoa  nafasi  kwa  propaganda  ya  wapiganaji  wa Taliban.

“Tuna  wasi  wasi  kuwa  picha  za  kuchoma nakala  za Koran , zitatumiwa  kwa  njia  ile  ile, kama  wale  watu wenye  msimamo  mkali  wa  kidini  walivyotumia  picha  za jela  ya  Abu  Ghraib. Kwa  maana  nyingine  picha  hizo zitakaa  milele  katika  mtandao  na  zitatumiwa  na  wale ambao  hawatutakii  mema  kuchochea  ghasia   na   hasira miongoni  mwa  watu  wa  kawaida  dhidi  yetu  na  ujumbe wetu  hapa  Afghanistan  pamoja  na  ujumbe  mwingine duniani.

Viongozi  wa  kidini  wa  Marekani   pamoja  na  watu wengine, wanapanga   kwenda  Gainesville  kupinga uchomaji  wa  Koran.

Katika  miongo   ya  hivi  karibuni, mahakama  kuu  ya Marekani  imeweza  kutoa  haki  kwa  Wamarekani   hata kuchoma  bendera  ya   nchi  hiyo  kama  tukio  la  uhuru wa  kujieleza  unaolindwa   chini  ya  katiba  ya  Marekani.

Wizara  ya  mambo  ya  kigeni  ya  Marekani  imezitaka balozi  zake  zote  nje  ya  nchi   kufanya  mikutano  na kutathmini  hatari  wanayokabiliana  nayo  Wamarekani , iwapo  kanisa  hilo  nchini  Marekani  litakaidi  maoni  ya dunia  na  kuchoma  nakala  hizo  za  Koran.

Mwandishi : Sekione  Kitojo / DPAE/ AFPE

Mhariri : Mohammed  Abdul Rahman

—————————————————————————

TATIZO LA SOMALIA NI UINGILIAJI KATI WA MATAIFA YA KIGENI-HIZB UT-TAHARIR

Jumuiya ya kislamu ya kimataifa ya Hiz Ut-Tahrir imepinga ungiliaji kati unaofanywa na mataifa ya kigeni katika mzozo unaoendelea nchini Somalia kati ya wanamgambo wa Al-shabab na serikali ya mpito ya nchi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa naibu mwakilishi wa wa vyombo vya habari vya Jumuiya hiyo Afrika Mashariki Massoud Mselem amesema mzozo wa Somalia hauhitaji nguvu za kijeshi bali ni kuangalia kiini cha tatizo lenyewe.

Amesema suluhisho la amani ya Somalia sio kupambana na wanamgambo wa Al-Shabab bali ni kupinga uingiliaji kati wa masuala ya nchi hiyo dhidi ya mataifa ya kigeni

Akizungumzia mateso na vitendo viovu wanavyofanyiwa waislamu wa Tajikistan Masoud ameitahadharisha dola hiyo na kusema iwapo hasara itatokea itarejea upande wa taifa hilo na kusema chama hicho kitajitolea kulingania utukufu wa mwezi mungu.

Amesema serikali ya Tajikistan inafanya makosa hayo huku ikiungwa mkono na madola ya magharibi na taasisi zinazodai kutetea haki za binadamu zikiwa zimekaa kimya.

Masoud amefahamisha zaidi ya waislamu 300 wa Tajikistan wanaendelea kusulubiwa kwa mateso, uonevu na vifungo vya muda mrefu.

Amesema Hiz ut-Tahrir Afrika Mashariki inalaani mateso na uharamia wanaofanyiwa waislamu wasiokuwa na hatia na utawala wa nchi hiyo  unaongozwa na rais Rahmanov.

Jumuiya ya Hiz ut-Tahrir ni chama cha kislamu cha kimataifa chenye malengo ya kurejesha tena uislamu kupitia dola ya Helaf iliyoangushwa mwaka 1924.

August 29, 2010 skaska Leave a comment Edit this
Categories: Uncategorized

RAIS KARUME AFUNGUA NYUMA YA WATOTO YATIMA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume amewataka wazazi na walezi kuchukuwa tahadhari ya kutowachia watoto wao kudhubaa mitaani.

Akifungua nyumba mpya ya kulelea watoto huko Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar mesema tabia hiyo itawajenga watoto kuishi maisha ya taabu na yasiokuwa na malengo yao ya baadae.

Dr. Karume amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar haiwezi kuiachia hali hiyo ikitokea kwa vile wazanzibari wote ni familia moja na wanadhamana ya kuwalea watoto wote.

Amesema mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 rais wa kwanza Abeid Karume ameanzisha kituo cha kulelea watoto huko Forodhani ili kuona watoto hao wanalelewa katika mazingira mazuri

Aidha Dr. Karume amesema serikali imeamuwa kuwahamisha watoto wanaolelewa katika kutuo cha Forodhani kutokana na mazingira yaliopo katika eneo hilo hayafai tena kulelea watoto.

Amesema jengo hilo la Forodhani litaendelea kuwa mali ya serikali na kutumika kwa shughuli za makumbusho ya usafiri wa bahari ya Hindi chini ya usimamizi wa taasisi ya Agakhan Foundation.

Akizungumza katika ufunguzi wa kituo hicho katibu wa afisi ya Mufti mkuu Zanzibar Sheikh Fadhili Soraga amewataka waislamu kuendelea kuwatunza watoto yatima kulingana na mafundisho ya dini yao.

Amesema watu wanaowadhulumu watoto yatima kwa kula mali zao ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya kislamu na watu hao tayari wameshabashiriwa kuingia motoni

Nyumba hiyo mpya ya kulelea watoto yenye ghorofa moja, vyumba vya kuishi watoto 80 kwa wakati mmoja, ukumbi wa mikutano, vyumba vya kompyuta, kusomea, na zahanati ujenzi wake umesimamiwa na taasisi ya ZAYADESA na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 883.

————————————————————————————————————

MUFTI MKUU WA ZANZIBAR AFARIKI DUNIA NCHINI INDIA

Mufti mkuu wa Zanzibar Sheikh Harith bin Khelef Khamis amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nchini India katika hospital ya Meyot ambapo alikuwa anapata matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Mufti imesema kwamba Mufti amefariki dunia jana asuhuhi katika hospitali ya Meyot Mjini Chanay nchini Idia

Katibu wa Mufti Sheikh Fadhil Suleiman Soraga amesema Zanzibar imepata msiba mkubwa kwa kuondokewa na kiongozi wake huku akisisitiza wananchi kuwa na subra katika msiba huo.

“Nchi yetu imepatwa na msiba mkubwa sana kwa kuondokewa na kiongozi mkuu wa dini visiwani ambaye alikuwa matibabuni kwenye hospitali ya Meyot Mjini Chenay nchini India” alisema Sheikh Soraga.

Soraga alisema mipango ya kusafirisha mwili wa mrehemu inaendelea kwa mashirikiano makubwa na ubalozi wa Tanzania nchini India huku maandalizi ya kuupokea mwili wa marehemu kwa heshima zote za kitaifa yanaendelea.

Alisema wananchi wataelezwa rasmi juu ya suala hilo lilipofikia baada ya kuwasili kwa maiti na muda wa mazishi hayo yatapangwa baada ya kufika Zanzibar mwili wa marehemu.

“Kwa taarifa hii waumini na wananchi wote kwa ujumla wanaombwa kuwa watulivu na kuungana pamoja katika kuukabili msiba huu mkubwa kitaifa” alisema taarifa hiyo iliyosainiwa na katibu wa Mufti Sheikh Soraga.

Licha ya kuwa taarifa ya serikali haikueleza Mufti alipelekwa nchini India kwa ugonjwa gani lakini taarifa za undani zinasema kwamba alipelekwa baada ya kuugua kwa muda mfupi akisumbuliwa na matatizo ya figo.

Akizungumza bila ya kutaka kutajwa jina lake gazetini kwa madai kwamba sio msemaji wa familia alisema wakati wa uhai wake Sheikh Harith alikataa kusafirishwa kupelekwa India kutokana na hali yake lakini baada ya kuonekana hali yake imezidi kuzorota ilimshauri kumpeleka matibabuni India.

Hatika hatua nyengine takriban misikiti yote leo Zanzibar imetoa tangazo la kifo cha Mufti na kuwataka waumini wamuombee dua katika kipindi hiki muhimu cha mwezi mtukufu wa ramadhani.

“Tuna masikitiko makubwa kwa kuondokewa na kiongozi wetu msomi wetu na muumini mwenzetu Mufti wa Zanzibar Sheikh Harith Bin Khelef huko nchini India alipokwenda kwa matibabu kwa hivyo tumuombeeni sana dua Mwenyeenzi Mungu amsameh madhambi yake” alisema Sheikh Abrahaman Habshi imamu mkuu wa msikiti wa Jibril Mkunazini.

Mufti Khelef mwenye umri wa miaka 80 ni miongoni mwa wasomi na wanazuoni wakubwa ambao wamebahatika kusoma katika chuo kikuu maarufu cha Kiislamu kiliopo Misri Al-Azhar katika miaka ya 1960.

Chuo kikuu cha Al-Azhar ni maarufu sana katika bara la Afrika na duniani ambacho hutoa elimu mbali mbali za dini ya kiislamu pamoja na masomo mengine ya lugha za kiarabu.

Marehemu Khelef aliteuliwa kuwa Mufti mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mwaka 1995 wakati wa uongozi wa rais mstaafu Dk Salmin Amour Juma.

Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kutoka India inafanywa na ofisi ya mufti wa Zanzibar ambayo ipo chini ya Wizara ya nchi Ofisi ya Rais Katiba na Utawala bora—————————————————————————————–

Watu nusu milioni watembelea maonyesho ya Qurani Tehran

Print E-mail
Sunday, 22 August 2010
Sample ImageZaidi ya watu nusu milioni hadi sasa wametembelea Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qurani Tukufu yanayoendelea katika Ukumbi Mkubwa wa Sala wa Imam Khomeini mjini Tehran. Maonyesho ya mwaka jana yalihudhuriwa na watu milioni moja na nusu na inatazamiwa kuwa washiriki katika maonyesho ya mwaka huu yatakayomalizika tarehe 23 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wataongozeka kwa asilimia 25. Mbali na mashirika 340 ya uchapishaji nchini Iran yanayoshiriki, vile vile kuna mashirika 15 ya kimataifa ya uchapishaji yanayoshiriki. Aidha kuna mashirika 90 ya programu za kompyuta kuhusu Qurani Tukufu yanayoshiriki katika maonyesho haya. Kuna nchi 28 zinazoshiriki katika maonyesho hayo katika kitengo cha Qurani na Mataifa ya Kiislamu. Maonyesho ya Kimataifa ya Qurani yanafanyika nchini Iran kwa lengo la kuhimiza utamaduni wa Qurani katika jamii

——————————————————–

Risala

Barack Obama
Rais wa Marekani

IKULU YA MAREKANI


21 Agosti, 2009

RISALA YA RAIS BARACK OBAMA
KATIKA KUUKARIBISHA MWEZI WA RAMADHAN

Kwa niaba ya watu wa Marekani – ikiwa ni pamoja na jumuiya za Waislamu katika majimbo yote hamsini ya Marekani – ninapenda kuwatakia kheri Waislamu wote wa Marekani na duniani kote. Ramadhan Kareem.

Ramadhan ndio mwezi ambao Waislamu wanaamini kuwa Korani ilifunuliwa kwa Mtume Muhammad, ikianzia na neno rahisi – iqra. Hivyo huu ni wakati ambao Waislamu hutafakari kwa kina kuhusu hekima, miongozo na mafundisho ya imani yao na wajibu ambao wanadamu wanao kwa wanadamu wenzao na kwa Mungu.

Kama ilivyo kwa watu wengi wa imani tofauti ambao wameshuhudia Ramadhani katika jamii na familia zetu, ninafahamu kuwa huu ni wakati wa furaha – wakati ambapo familia hukusanyika na kula pamoja. Lakini ninajua pia kuwa Ramadhan ni wakati wa ibada, tafakari na maombi ya kina – ni wakati ambao Waislamu hufunga wakati wa mchana na usiku wakisali tarawih, wakisoma na kusikiliza Korani yote katika kipindi chote cha mwezi huu mtukufu.

Ibada hizi zinatukumbusha misingi inayotuunganisha pamoja na nafasi muhimu ya Uislamu katika kujenga na kuimarisha haki, maendeleo, hali ya kuvumiliana na heshima kwa wanadamu wote.

Mathalani, dhana ya kufunga inapatikana katika imani nyingi – ikiwa ni pamoja na imani yangu ya Kikristo – ikitambuliwa kama njia ya kuwaweka karibu waja na Mola wao na kuwakumbuka wale miongoni mwetu wenye njaa. Aidha, msaada ambao Waislamu wanautoa kwa wengine katika kipindi hiki, unatukumbusha wajibu wetu katika kutoa fursa na kuwezesha ustawi wa watu wengine mahali pote. Kwani ni muhumu kwetu kukumbuka kuwa dunia tunayotaka kuijenga – na mabadiliko tunayotaka kuyafanya – ni lazima yaanzie ndani ya mioyo yetu na katika jamii zetu wenyewe.

Katika kipindi hiki cha majira ya joto, watu wengi hapa Marekani wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali za kusaidia jamii zao – ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa watoto, kuhudumia wagonjwa, na kuwasaidia wale wenye shida mbalimbali. Taasisi za kidini, ikiwa ni pamoja na taasisi za Kiislamu, zimekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma hizi za kijamii. Katika kipindi hiki ambapo tunakabiliwa na changamoto nyingi, ni lazima tuuendeleza moyo huu wa kujitolea na kuwahudumia wengine, si katika mwezi huu tu bali pia katika miezi na miaka ijayo.

Ni azma yetu kutekeleza kwa dhati wajibu wetu wa kujenga dunia yenye amani na usalama zaidi sio tu ndani bali hata nje ya mipaka ya Marekani. Ni kwa sababu hiyo ndiyo tunahitimisha vita nchini Irak kwa namna nzuri inayohakikisha uwajibikaji. Ni kwa sababu hiyo ndiyo tunayatenga makundi yenye msimamo mkali na ya kigaidi huku tukijenga uwezo wa watu katika maeneo kama Afghanistan na Pakistan. Hii ndiyo sababu tunaunga mkono kwa dhati haki ya Waisraeli na Wapalestina kuishi kwa amani na usalama. Na ni kwa sababu hiyo ndipo wakati wote tutasimama kidete kulinda na kutetea haki ya watu wote kutoa maoni yao, kuabudu na kutekeleza mafundisho ya dini yao, kuchangia kikamilifu katika jamii zao na kuwa na imani katika utawala wa sheria.

Jitihada zote hizi ni sehemu ya dhamira ya dhati ya Marekani ya kushirikiana na Waislamu na nchi za Kiislamu kwa misingi ya kuheshimiana na kujali maslahi ya pande zote. Katika kipindi hiki muhimu cha ibada na kujiimarisha kiimani, ninapenda kusisitizia dhamira yangu ya dhati ya kuwa na mwanzo mpya kati ya Marekani na Waislamu duniani kote.

Kama nilivyosema katika hotuba yangu ya Cairo, ni lazima mwanzo mpya utokane na jitihada za kudumu za kila upande kusikiliza na kujifunza kutoka kwa upande mwingine. Aidha, ni lazima mwanzo huu ujengwe katika misingi ya kuheshimiana na kutafuta mambo yanayotuunganisha. Ninaamini kuwa kusikiliza ni sehemu muhimu ya jitihada hizi. Katika miezi miwili iliyopita Balozi za Marekani duniani kote zimekuwa zikikutana sio to na serikali bali pia moja kwa moja na wananchi katika nchi za Kiislamu ili kupata maoni yao. Na kutoka duniani kote, tumepata maoni mengi kuhusu namna ambavyo Marekani inaweza kushirikiana na nchi hizo kwa kuzingatia matarajio ya watu.

Tumesikiliza. Na kama ilivyo kwenu, tunaelekeza jitihada zetu katika kuanza kuchukua hatua mahsusi – kuhusu masuala ya kisiasa na kiusalama niliyoyaelezea hapo awali, na katika maeneo ambayo mmetuambia yataleta mabadiliko yenye manufaa zaidi katika maisha ya watu. Tunaamini kuwa baada ya muda jitihada hizi zitaanza kuleta mabadiliko.

Mashauriano haya yanatusaidia kutekeleza ubia ambao niliupendekeza mjini Cairo – ili kupanua program za mabadilishano ya kielimu; kuimarisha ujasiriamali na kukuza ajira; na kuongeza ushirikiano katika nyanja ya sayansi na teknolojia huku tukisaidia mafunzo ya ufundi. Tunaendelea kushirikiana na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) na nchi wanachama wa OIC ili kutokomeza polio. Aidha, tunashirikiana kwa karibu na jumuiya ya kimataifa katika kukabiliana na changamoto za pamoja kuhusu masuala ya afya kama vile Mafua ya Nguruwe – ambayo najua ni kitisho kwa Waislamu wengi wanaojiandaa kwenda kushiriki ibada ya hija.

Jitihada zote hizi zinalenga katika kutimiza matarajio yetu ya pamoja ambayo ni pamoja na kuishi kwa amani na usalama; kupata elimu na kazi zenye heshima, kupenda familia, jamii na imani zetu. Haya yote yatahitaji muda, jitihada na subira kubwa. Hatuwezi kubadilisha mambo kwa siku moja, lakini tunaweza kuazimia kwa dhati kufanya yale yanayotupasa kufanya, wakati tukijielekeza katika mwelekeo mpya – tukielea kule ambako tungependa kuelekea sisi na watoto wetu. Hii ni safari ambayo ni lazima tusafiri pamoja.

Ninatarajia kuendelea na mjadala huu muhimu na kuubadilisha kuwa hatua mahsusi za utekelezaji. Na leo ninapenda kuwatakia Waislamu wote wa Marekani na duniani kote mwezi wenye Baraka mnapoupokea mwezi mtukufu wa Ramadhan. Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi.

————————————————————————————————–

SERIKALI YA MSETO Z’BAR YAUNGWA MKONO NA WAISLAM

Na Mauwa Mohammed-Zanzibar

ZANZIBAR:

Jumuiya ya Maimamu Zanzibar JUMAZA imesema inaunga mkono kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kama hatua moja wapo ya kuimarisha amani na utulivu nchini.

Katibu Mtendaji wa JUMAZA sheikh Muhdin Zuber Muhdini amesema hatua hiyo ni kuzishukuru neema za mwenyezi mungu zilizoondosha siasa za chuki zilizoleta mirafarakano na uadui

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa amesema serikali ya umoja wa kitaifa ndio suluhisho la kuleta amani, hivyo amewataka wananchi kushiriki katika kura ya maoni ili kutoa ridhaa ya kuundwa serikali hiyo

Hata hivyo Sheikh Muhidin amesema jumuiya hiyo haiwezi kuwalazimisha wananchi kutumia uhuru wao wa kuamua, lakini jumuiya za waislamu zinajukumu la kuielekeza jamii umuhimu wa kulinda amani na utulivu.

Aidha jumuiya hiyo pia imewataka wananchi kuendeleza amani na utulivu uliopo hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa kuwachagua viongozi mbali mbali wa nchi.

Tamko hilo la JUMAZA la kuunga mkono kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa limefikiwa katika kikao chake kilichofanyika June 12 mwaka huu na kuzishirikisha jumla ya taasisi 18 za kislamu

Ufaransa kuchunguza vitendo vya kibaguzi dhidi ya Waislamu

"Barack

Print E-mail
Saturday, 19 June 2010
Sample ImageSerikali ya Ufaransa imeahidi kushughulikia haraka iwezekanavyo vitisho vinavyotolewa na makundi yanayofurutu ada nchini humo dhidi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu. Serikali ya Ufaransa imekuwa ikikosolewa kwa kushindwa kuzingatia kilio cha Waislamu ambao wanalalamikia kuvunjiwa heshima vituo vya Kiislamu vya nchi hiyo. Serikali ya Paris imekubali kutiliana saini makubaliano na Baraza la Kiislamu nchini humo na kuahidi kuchukua hatua za kukabiliana na vitisho vinavyotolewa dhidi ya Waislamu nchini humo. Hadi sasa vimeshafanyika vitendo kadhaa vya kuwavunjia heshima Waislamu, vituo vya Kiislamu, misikiti na maeneo ya makaburi ya Waislamu nchini humo, lakini serikali ya nchi hiyo bado haijachukua hatua zozote za kukabiliana na vitendo hivyo. Brice Hortefeux, Waziri wa Mambo ya Ndani amesisitiza kuwa atashirikiana na Muhammad al Mussawi Mkuu wa Baraza la Waislamu la Ufaransa kwa shabaha ya kuchunguza vitendo hivyo. Kuna Waislamu wapatao milioni kumi wanaoishi nchini Ufaransa, wengi wao wakitokea nchi za kaskazini mwa Afrika

————————————————————————————————————————————————–

OIC yataka kuchukuliwa hatua za kimataifa dhidi ya utawala wa Kizayuni

Print E-mail
Monday, 07 June 2010
Sample ImageJumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC imetaka kubuniwe kamati ya wataalamu wa kisheria kwa lengo la kuwafikisha kizimbani viongozi wa utawala haramu wa Israel waliohusika na hujuma dhidi ya msafara wa meli za misaada Jumatatu iliyopita.Uamuzi huo umechukuliwa baada ya kikao cha dharura cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu mjini Jeddah. Kikao hicho kiliitishwa na Iran na Uturuki kwa lengo la kujadili hujuma ya utawala wa Kizayuni dhidi ya msafara wa meli za misaada ya kibinaadamu zilizokuwa zikilekea Ghaza. Duru za Palestina zinasema watu karibu 20 waliuawa katika hujuma hiyo.OIC imeitaja hujuma hiyo ya Israel kuwa ni ugaidi wa kiserikali na uharamia.(chanzo radio iran idhaa ya kiswahili)———————————————————————————————————————————————————-

Pakistan yazindua tovuti mbadala ya Facebook ya Waislamu

Print E-mail
Sunday, 30 May 2010
Sample ImagePakistan imezindua tovuti mbadala ya Facebook baada ya tovuti hiyo kupigwa marufuku nchini humo kutokana na kuanzisha shindano la vijikatuni vya kumvunjia heshima Mtume Mohammad SAW.
Tovuti hiyo mpya inayojulikana kama Millatfacebook inawaunganisha zaidi ya Waislamu Billioni moja laki tano pamoja na wafuasi wa dini nyinginezo. Aidha tovuti hiyo ya kijamii ya Waislamu inatoa huduma mbadala ya tovuti ya Kimarekani ya Facebook ambayo inalaumiwa kwa kutoheshimu faragha ya watumizi wake. Mamia ya maelfu ya wananchi wa Pakistan wamekuwa wakiandamana wiki za hivi karibuni kupinga ukurasa wa Facebook uliowahimiza watumizi wake kutuma taswira zinazomvunjia heshima Mtume Mohammad SAW. Serikali ya Pakistan iliwaamuru wanaotoa huduma za intaneti kuizuia tovuti ya Facebook baada ya mawakili wa Kiislamu kushinda kesi iliyoitaka serikali kupiga marufuku tovuti hiyo ya kijamii yenye makao yake Marekani. Anwani ya tovuti mpya ya Kijamii ya Waislamu ni http://www.millatfacebook.com

……………………………………………………………………………

NI KWELI WANASAYANSI WANAWEZA KUUMBA UHAI? SOMA HABARI HII

Wanasayansi Marekani ‘waumba uhai’

Seli sanisiaSeli sanisia

Wataalamu huko Marekani kwa mara ya kwanza wamefanikiwa kuunda seli hai kwa kutumia asidi nasaba, DNA iliyounganishwa na vitu mbalimbali.

Wataalamu hao waliunda programu ya vinasaba na kuvipandikiza ndani ya seli pokezi.

Matokeo yake yakazaa vijiumbe maradhi vinavyofuata nyenzo za ileile DNA iliyounganishwa.

Ufanisi huu uliochapishwa katika jarida maarufu ‘science’, umeshangiliwa na ulimwengu wa sayansi kama hatua kubwa, ingawa wakosoaji wanasema viumbe sanisia vinaweza kusababisha madhara yasiyoelezeka.

Wengine wanasema kuwa manufaa ya teknolojia hii yametiwa chumvi.

Lakini wataalamu wana nia ya kuunda seli za bakteria hiyo ambayo itasaidia katika utengenezaji wa dawa na mafuta halikadhalika kumeza gesi zinazochafua mazingira.

Kundi hilo la wataalamu lililongozwa na Dr Craig Venter kutoka chuo cha J.Craig Venter huko Maryland na Carlifornia nchini Marekani.

Dr Craig VenterDr Craig Venter

Kabla ya hapo yeye na wenzake waliunda bakteria kwa kuchanganya zaidi ya kitu kimoja na baadaye kuoanisha mfumo waliotumia mwanzoni.

Sasa wametumia njia hiyo hiyo kwa kuunganisha bakteria ya awali na kuunda seli yenye chembechembe ambayo ina uhai na uwezo wa kujenga ramani ya kiumbe.

Dr Venter alifananisha mafanikio haya na ujenzi wa mtambo mpya wa programu ya kujengea seli na kuongezea kuwa mtambo huu unapoanza kazi yake moja kwa moja huanza kuzalisha nakili za chembechembe za ramani.

Dr Venter alisema, hii ni mara ya kwanza kwa programu ya DNA kuweza kumiliki seli, na nadhani ni fursa kubwa katika mabadiliko ya sayansi ya viwanda.

Tayari Dr Venter na wenzake wanashirikiana na makampuni ya dawa na mafuta kuunda na kujenga kromosomu za bakteria ambazo zitaweza kutengeneza mafuta yenye manufaa pamoja na dawa mpya.

Hata hivyo wakosoaji wamejitokeza kwa kusema kuwa manufaa ya uvumbuzi huu yametiwa chumvi mno.

Dr Helen Wallace wa shirika la Greenwatch linalosimamia maendeleo ya teknolojia ya maumbile nchini Uingereza, ameiambia BBC kuwa bakteria iliyoundwa kwa mchanganyiko wa vitu vingi inaweza kuwa na hatari.

Unapoweka viumbe wapya katika mazingira unaweza kusababisha janga.

Kwa kuweka bakteria hawa wapya hewani ili kumeza uchafu kutoka viwandani, ukweli ni kwamba unasababisha uchafu zaidi. Hatuelewi ni jinsi gani vijidudu hivi vitaishi katika mazingira

…………………………………………………………………………………………………………..

SMZ KUFUATILIA NYENDO ZA MAHUJAJI DHIDI YA HOMA YA MAFUA YA NGURUWE

baadhi ya mahujaji wakionekana kurejea nyumbani baada ya kumalizika kwa ibada tukufu ya Hijja mjini Mecca, Saud Rabia

1 12 2009

ZANZIBAR:

Wizara ya afya na ustawi wa jamii imeandaa mpango wa kufuatilia afya za mahujaji wa Zanzibar waliokwenda kutekeleza ibada ya hijja mjini Mecca, Saud Arabia kutokana na wasiwasi wa homa ya mafua ya nguruwe.
AkizWILAYA YA MAGHARIBI:
Bei za mazao ya kilimo zimeripotiwa kupungua katika soko la Mwanakwerekwe, wilaya ya Magharibi ikilinganishwa na miezi miwili iliyopia.
Akizungumza na Zenj Fm Radio mkuu wa soko hilo Bw Khamis Mohamed Zahor amesema mazao hayo yameshuka bei kutokana na kupungua mahitaji yake ikilinganishwa kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadahani.
Ameyataja baadhi ya mazao yaliyoshuka bei ni ndizi, ambapo chana moja inauzwa kwa shilingi elfu mbili hadi elfu mbili na 500 wakati zamani ikiuzwa shilingi elfu tatu hadi 4,000.
Mazao mengine yalioshuka bei ni nazi kutoka shilingi elfu moja ambapo kwa sasa inauzwa kati ya shilingi 250 hadi 500 wakati mazao mengine kama vile muhugo, viazi vukuu na vidogo ziko katika hali ya wastani.
Akizungumzia kuhusu suala la usafi wa mazingira katika soko hilo bw Zahor amesema hali ya usafi hivi sasa ni ya kuridhisha kutokana na ushirikiano uliopo baina ya uongozi wa soko hilo na wafanyabiashara.
ungumza na Zenji fm Radio mkurugenzi wa afya ya jamii Zanzibar Juma Rajab amesema chini ya utaratibu huo mahujaji wote mara baara ya kuwasili Zanzibar watalazimika kujaza fomu maalum zitakazoonesha sehemu wanazoishi.
Amesema mahujaji hao pia watapewa maelekezo endapo wataona dalili za homa kali au maumivu ya kichwa waripoti katika vituo vya afya.
Bw. Rajab amesema kabla ya kuondoka mahujaji hao walipewa mafunzo maalum ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe pamoja na kufuatana na madaktari watatu.
Aidha amesema wizara ya afya imejiandaa kukabiliana na ugonjwa huo ambapo baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo Unguja na Pemba wameshapatiwa mafunzo ya kujikinga na homa hiyo

————————————————————————————————————————————————————————————

HATARINI KUKUMBWA NA UKAME-KARUME

  • Wananchi watakiwa kuomba dua ya kuomba mvua
  • Kudhibiti matumizi ya chakula na maji

Rais Karume akisalimiana na wananchi waliofika katika viwanja vya ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kupokea mkono wa Idd wakiwemo wanawake wenye ulemavu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume amewataka wananchi wa Zanzibar kuchukua tahadhari ya kukabiliana na ukame  unaonza kujitokeza katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba kutokana na ukosefu wa mvua uliojitokeza kwa muda mrefu hapa nchini.

Amesema ukosefu wa mvua umeathiri kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa mazao ya kilimo, mazao ya bishara, mimea pamoja na mifugo, hivyo amewataka wananchi kudhibiti matumizi ya maji na chakula kutokana na kuwepo kwa tishio la kukumbwa na ukame iwapo mvua hazitanyesha kwa siku za hivi karibuni.

“Wakati serikali inajiandaa kukabiliana na hali yoyote ya ukame itakayojitokeza ni wajibu wa kila mmoja wetu kuchukua tahadhari ya kutosha ya kudhibiti hali hiyo na kudhibiti matumizi ya raslimali zetu zikiwemo maji na chakula”. Alisisitiza rasi Karume.

Rais Karume ambae alikuwa akizungumza katika baraza la Eid-el-fitri hivi karibuni huko nyumba ya wananchi Forodhani mjini hapa amesema serikali yake hivi sasa inaendelea kukabiliana na hali ukame iliyojitokeza na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kukata miti ovyo na kuharibu vianzio vya maji kwani ndio chanzo chake.

Aidha rais Karume amewataka wananchi kumuomba mwenyezi mungu aijaalie Zanzibar kupata mvua za kutosha, huku serikali kwa upande wake ikiendeleza juhudi za kuimarisha kilimo cha umwagiliaji maji ambacho ndio mkombozi na kuwasaidia wakulima kuwapatia mbegu na pembejeo nyengine kwa njia ya ruzuku ili kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Akizungumzia hali ya kudorora kwa uchumi duniani iliyoikumba mataifa mengi hivi karibuni rais Karume amesema, suala la kuimarisha kilimo, uwekezaji katika sekta ya utalii na biashara, miundo mbinu na huduma za kijamii kwa Zanzibar ni mambo yanayohitaji kupewa umuhimu mkubwa katika juhudi za kukabiliana na kuzorota kwa uchumi duniani.

Hivyo amewataka wananchi kuchukua fursa hiyo ya mageuzi ya uchumi yanayofanywa na serikali kwa kujijengea misingi ya uchumi endelevu kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzidi kujituma.

Kwa mujibu wa bajeti ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 2008/2009 itaelekeza nguvu zake zaidi katika shughuli za maendeleo kwa nia ya kuwashirikisha wananchi wake kuwaekea miundo mbinu ya kuimarisha kilimo na utali ili kuongezeka ajira na kujenga misingi imara ya ukuwaji wa uchumi hapo baadae

____________________________________________________________________________________________________________________

Advertisements