Ibada tukufu ya Hija

Bismillahir Rahmanir Rahim

Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Hii ni makala maalumu ya kuzungumzia ibada tukufu ya Hija. Ni matumaini yetu itakunufaisheni vya kutosha.

***

Hija ni ibada inayokusanya mambo mengi yanayomkurubisha mja kwa Mola wake Karima. Ni shule ya kutoa malezi na maarifa kwa waja kwa msingi wa tawhidi na kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Safari ya Hija huanza kwa kuwekwa nia safi na ikhlasi na kukamilika kwa ibada na amali makhsusi.
Kwa mara nyingine tena imewadia safari ya uja na mapenzi kuelekea katika ardhi tukufu ya Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada tukufu ya Hija. Ni safari fupi lakini iliyojaa nembo na siri kubwa. Ni safari ya siku chache lakini yenye matunda na manufaa makubwa mno. Ni safari ambayo wenye uwezo wa kifedha na kiafya ndio wanaoweza kuitekeleza baada ya kupata tawfiki ya Mwenyezi Mungu. Ni safari ya kuelekea katika kitovu cha Wahyi; ardhi ambazo ni mahala pa maarifa , mlima wa mahaba na mahala pa uja na unyenyekevu. Mbali na kutekeleza ibada ya kimaanawi na kisiasa ya ibada ya Hija, akiwa Makka hujaji hupata fursa ya kujionea athari muhimu za Uislamu. Katika safari hii ya kimaanawi Hujaji hupata nafasi ya kunufaika kihistoria na kimaanawi na athari za Uislamu katika mji wa Makka na Madina.
Kwa hakika al-Kaaba ni nyumba ya Mwenyezi Mungu iliyobarikiwa na yenye uongofu. Mwenyezi Mungu anasema katika aya ya 96 ya Surat al-Imran kwamba, “Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ajili ya ibada ni ile iliyoko Makka, iliyobarikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote.” Wanahistoria wana kauli moja kuhusiana na kujengwa nyumba ya al-Kaaba katika zama za Nabii Adam AS. Imekuja katika kitabu cha Taarikh al-Yaaqubi kwamba, baada ya Nabii Adam kumaliza kujenga al-Kaaba alifanya tawafu. Katika kipindi chote cha historia, Kaaba ikawa ni mahala pa kufanya ibada manabii wengi wa Mwenyezi Mungu. Nabii Ibrahim aliamrishwa na Mwenyezi Mungu aikarabati al-Kaaba. Mwenyezi Mungu anasema katika aya za 26 na 27 za Surat al-Haj kwamba, “Na pale tulipomweka Ibrahim pahala penye ile Nyumba tukamwambia: Usinishirikishe na chochote; na isafishe Nyumba yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kut’ufu, na wanaokaa hapo kwa ibada, na wanao rukuu, na wanaosujudu. Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali.”
Hivyo basi Kaaba ni nembo ya wanatawhidi na wampwekeshao Mwenyezi Mungu na jambo hilo lilikuwa hivyo katika kipindi chote cha historia. Nafasi muhimu iliyobainishwa na Qur’ani kuhusiana na al-Kaaba ni ile hidaya na kuongoza kwake watu. Mwanzoni mwa Uislamu al-Kaaba hakikuwa kibla cha Waislamu. Kwa muda wa miaka kumi na tatu aliyokuwa mjini Makka na muda kidogo mjini Madina, Mtume SAW na wafuasi wake walikuwa wakisali ibada zao wakielekea Baytul Muqaddas.
Hii ni katika halia ambayo, wananchi wa Makka walikuwa wameigeuza Kaaba na kuwa nyumba ya waabudu masanamu. Nyumba ya Mwenyezi Mungu al-Kaaba ina nafasi muhimu katika ibada za Kiislamu na vile vile uhai wa kijamii wa Waislamu. Waislamu kwa siku huelekea mara tano upande wa al-Kaaba wakati wa kusali. Hii kwamba, kwa siku mamilioni ya watu usiku na mchana na kwa wakati maalumu tena kwa pamoja husali na kuelekea upande wa al-Kaaba, kwa hakika hili ni jambo ambalo huzifanya nyoyo za Waislamu kuwa pamoja na kuzikurubisha zaidi.
Mwenyezi Mungu amewataka Waislamu popote watakapokuwa kuelekea upande wa Makka wakati wa ibada zao, kwa sababu nyumba ya al-Kaaba daima inapaswa kuwa mhimili na kitovu cha kukusanyika wanatawhidi wote. Fadhila muhimu ya Al-Kaaba ni kuwa, nyumba hii, ni nyumba ya tawhidi na haina msukukumo mwingine usiokuwa wa Kimwenyezi Mungu katika kupatikana kwake na katika kuendelea kwake kuweko. Mahujaji wakiwa katika nyumba ya Mwenyezi Mungu hufanya tawafu katika mahala ambapo malaika wanatufu na mahala ambapo Mitume wa Mwenyezi Mungu na mawalii wake walikuwa kando ya eneo hilo na kumhimidi Mwenyezi Mungu.
Bwana Mtume SAW anasema: Mwenyezi Mungu anajifakharisha na watu wanaofanya tawafu, na laiti ingelikuwa imeamuliwa kwamba, malaika wapeane mikono na mtu, basi wangepeana mikono na wenye kufanya tawafu katika nyumba ya Mwenyezi Mungu. Kaaba ni mahala pa amani na usalama kwa wanaadamu wote. Mwenyezi Mungu anasema katika Suratul Baqara aya ya 125 kwamba,
“Na kumbukeni tulipo ifanya ile Nyumba (ya Alkaaba) iwe pahala pa kukusanyikia watu na pahala pa amani.” Hivyo basi kila mtu atakayekuwa kando ya Kaaba, anakuwa yuko katika amani kimwili na kiroho na huwa na utulivu. Usalama na amani ya Nyumba hii ya Mwenyezi Mungu unatokana na dua aliyoiomba Nabii Ibrahimn AS kama inavyosema aya ya 126 ya Suratul Baqarah, “Na alipo sema Ibrahim: Ee Mola wangu Mlezi! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.” Mwenyezi Mungu aliijibu dua ya Ibrahim AS. Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana kwa karne nyingi, al-Kaaba imesalimika na shari ya waitakiao mabaya. Kisa cha Abraha na jeshi lake la askari waliokuwa wamepanda tembo ni jambo linaloweka wazi uhakika huu.
Abraha Aliyeandaa jeshi kubwa lililokuwa limesheheni tembo wengi ili kwenda kuivunja al-Kaaba na yeye mwenyewe alikuwa amempanda tembo mkubwa sana kuliko wote alikumbwa na hatima mbaya. Waarabu wa Makka waliliogopa sana jeshi lile. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu alilishushia jeshi la Abraha, jeshi la ndege lililodondosha mawe. Mtu yeyote aliyepatwa na jiwe alisagikasagika yeye na tembo wake na kuwa kama majani yaliyoliwa na kutapikwa kama tunavyosoma katika Qur’ani.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullah Wabarakaatuh

————————————————————————————

MAKALA MAALUM-IBADA TUKUFU YA HIJJA Faida
Ibada ya Hijjah ndio inayozikamilisha nguzo tano za Uislamu, amesema Allah Mola Mwenyezi: “…NA ALLAH AMEWAWAJIBISHIA WATU WAFANYE HIJJAH KATIKA NYUMBA HIYO; YULE AWEZAYE KUFUNGA SAFARI KWENDA HUKO…” [3:97] Na akasema tena: “NA (tukamwambia): UTANGAZE KWA WATU KHABARI ZA HIJJAH, WATAKUJIA (wengine) KWA MIGUU NA (wengine) JUU YA KILA MNYAMA ALIYECHOKA (kwa machofu ya njiani) WAKIJA KUTOKA KATIKA KILA NJIA YA MBALI. ILI WASHUHUDIE MANUFAA YAO NA (ili wakithirishe) KULITAJA JINA LA ALLAH KATIKA SIKU ZINAZOJULIKANA…” [22:27-28] Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah-Allah amuwiye radhi-amesema-Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amesema: “Enyi watu! Hakika Allah amekufaradhishieni Hijjah, basi hijini (nendeni Hijjah). Atakayehiji kwa ajili tu (ya kutaka radhi za) Allah na asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu, atatoka katika madhambi yake kama siku aliyozaliwa na mama yake. Na Umrah moja mpaka nyingine ni kafara ya madhambi ya kipindi kilicho baina ya (Umrah) mbili hizo na Hijjah yenye kukubaliwa haina jazaa (malipo) ila pepo”. Bukhaariy & Muslim-Allah awarehemu.

Katika mithili ya masiku kama haya kila mwaka, macho, masikio na nyoyo za waislamu ulimwenguni kote huelekezwa nchini Saudi Arabia. Khususan katika mji Mtakatifu wa Makkah; mahala ambapo ipo nyumba takatifu na kongwe ya Allah, nyumba inayotajwa na kauli tukufu ya Allah: “KWA YAKINI NYUMBA YA KWANZA ILIYOWEKWA KWA AJILI YA WATU (kufanya ibada) NI ILE ILIYOKO MAKKAH, YENYE BARAKA NA UONGOZI KWA AJILI YA WALIMWENGU WOTE. HUMO MNA ISHARA ZILIZO WAZI (za kuonyesha utukufu wake na ukongwe wake. Miongoni mwa hizo ni) MAHALA ALIPOKUWA AKISIMAMA IBRAHIMU, NA ANAYEINGIA (Haram) ANAKUWA KATIKA SALAMA…” [3:96-97]

Waja wa Allah huuitikia wito wa Mola wao katika masiku haya kwa kufunga safari kutoka pande mbalimbali za dunia kuielekea nyumba hii tukufu ya Allah. Huenda huko kwa ajili tu ya kuitekeleza ibada ya Hijah ambayo ni nguzo ya tano ya Uislamu; dini na mfumo wao sahihi wa maisha. Ibada hii tukufu huwakutanisha pamoja ndugu wa imani wa mataifa, lugha, hadhi na rangi mbalimbali. Huu ni mkutano na mkusanyiko usio na mithali yake katika ulimwengu huu, ulimwenguni kote haujapata na wala hautapata kutokea mkusanyiko unaowakusanya watu wengi na wa mataifa mengi kama huu wa Hijjah. Kutokana na utukufu na umuhimu wa ibada hii tukufu ya Hijjah, Website yako (WEBSITE UISLAMU) inajifakharisha kwa mara nyingine tena kuifanyia kazi kauli tukufu ya Allah: “…NA SAIDIANENI KATIKA WEMA NA TAQWA, WALA MSISAIDIANE KATIKA MADHAMBI NA UADUI”. [5:2] Ili kukusaidia wewe ndugu mpenzi Hajji kuitekeleza kauli ya Allah Mola Mlezi wako: “NA TIMIZENI HIJJAH NA UMRAH KWA AJILI YA ALLAH…” [2:196] Website yako inakuletea maelezo haya mukhtasari inayopenda kuyaita (MUONGOZO WA HIJJAH NA UMRAH) huku ikiamini kwa yakini kwamba inachangia katika suala zima la kusaidiana katika WEMA na TAQWA. Ni matumaini ya Website Uislamu kwamba utaupokea muongozo huu kwa mikono miwili na kupupia kuusoma kwa nia ya kujifunza, kujua na kuutumia katika kipindi chote cha kuitekeleza kwako ibada hii tukufu. Kadhalika ni matarajio ya Website Uislamu kuwa muongozo huu utakupa msaada mkubwa utakaokuwezesha kuitekeleza ibada hii  kwa UJUZI WA KWELI. Website Uislamu inawatakia mahujaji wote Hijjah njema iliyotakasika kwa ajili ya Allah. Haya sasa karibu katika MUONGOZO WA HIJJAH NA UMRAH, kwa jina la Allah na kwa kuutaraji mno msaada na taufiq yake tunaanza kwa:

 

  1. USIA MUHIMU:

Enyi mahujaji, Website yenu (WEBSITE UISLAMU) inapenda kuitumia fursa hii adhimu kumuhimidi Allah aliyekuwafikisheni kwenda kuhiji katika nyumba yake tukufu. Kama alivyokuwafikisheni kuhiji tunamuomba akutakabalieni ibada yenu hii na baki ya amali nzenu njema, Aamiyn! Ili kuhakikisha kuwa unafuzu katika kuitekeleza ibada hii, tunapenda kwa mapenzi ya Allah kukupa wasia muhimu kama ifuatavyo:

a)      Kumbukeni kwamba nyinyi kama mahujaji mumo katika safari tukufu yenye baraka tele za Allah. Pia mumo katika Hijrah; mnaiacha miji yenu, watu wenu na shughuli zenu kwa ajili tu ya kuuitika wito wa Mola wenu. Fahamuni-Allah akurehemuni-kwamba safari yenu hii ina ujira adhimu, kwani Hijjah yenye kukubaliwa haina jazaa ila pepo.

b)     Tahadharini na adui yenu mkuu shetani asije kutusha baina yenu mjadala na mabishano yatakayosababisha uadui na chuki baina yenu: “HIJJAH NI MIEZI MAALUMU, NA ANAYEKUSUDIA KUFANYA HIJJAH KATIKA (miezi) HIYO, BASI ASISEME MANENO MACHAFU WALA ASIFANYE VITENDO VICHAFU WALA ASIBISHANE KATIKA HIYO HIJJAH…” [2:197]

c)      Waulizeni wanazuoni wenu mlioambatana nao mas-ala tata yanayokutatizeni katika utekelezaji mzima wa ibada yenu ili muweze kuitekeleza kama itakiwavyo na sheria: “…BASI WAULIZENI WENYE KUMBUKUMBU (wenye kujua) IKIWA NYINYI HAMJUI”. [16:43]

d)     Eleweni kwamba Allah ametufaradhishia baadhi ya mambo na kutusunishia mengine. Ni dhahiri shahiri kwamba Allah hazikubali sunah za mtu aliyezivunja na kuzipoteza fardhi. Baadhi ya mahujaji hughafilika na ukweli huu, wakawakera na kuwaudhi waumini wenziwao na pengine kuhatarisha maisha yao kwa ajili tu ya kutaka kulibusu “Hajarul-Aswad”. Au kwa ajili tu ya kutaka kwenda jarambe katika Twawaafu au kuswali nyuma ya “Maqaamu Ibrahiym” au kunywa maji ya Zamzam. Fahamuni kwamba mambo yote haya ni SUNAH na kuwaudhi waumini ni HARAMU, vipi basi tunatenda la haramu kwa ajili ya kupata la Sunah?!

e)      Tambueni kwamba haitakikani mwanamume kuswali pembeni ya mwanamke au nyuma yake ndani ya msikiti mtukufu au mahala pengine kwa sababu yo yote ile iwayo, ikiwa kuna imkani ya kuliepuka hilo basi liepuke kadiri uwezavyo. Na enyi mahujaji wanawake pupieni sana kuswali nyuma ya wanamume kama mtakiwavyo na sheria tukufu.

f)       Ni kheri kwenu nyinyi ikiwa mtakumbuka kwamba milango na maingilio ya Haram (eneo takatifu) ni njia ambazo si halali kwa ye yote miongoni mwenu kuziziba. Asiizibe milango/maingilio hayo kwa kuswali hapo hata kama ikiwa ni kwa ajili ya kuidiriki swala ya jamaa.

g)      Haijuzu kuzuia/kuchelewesha utekelezaji wa ibada ya Twawaafu kwa kukaa pembezoni mwa Al-Ka’abah au kwa kuswali karibu yake au kwa kusimama katika “Hijri-Ismail” au “Maqaamu Ibraahiym”. Kuwa kwako au kuswali maeneo hayo husababisha kero na usumbufu mkubwa usio wa lazima kwa wenzako wanaotufu khasa wakati wa msongamano.

Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo Website yako {WEBSITE UISLAMU} imeonelea ni vema ikakukumbusha ili uweze kuitekeleza ibada yako ya Hijjah kwa ufanisi mkubwa.

 

2.         NAMNA YA KUITEKELEZA IBADA YA HIJJAH NA UMRAH:

Ewe Haji-Allah akutakabalie Hijjah yako-kabla hatujaanza kukuelekeza utekelezaji wa ibada mbili hizi; Hijjah na Umrah, ni vema tukajifunza kwanza pamoja:

a)     Aina za utekelezaji wa Hijjah na Umrah:

Kuna aina tatu za namna ya utekelezaji wa ibada za Hijjah na Umrah kama zilivyofundishwa na Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-kwani yeye ndiye aliyesema: “Twaeni kwangu ibada zenu” – yaani nitakavyofanya mimi nanyi mfuate hivyo.

TAMATUI: Hii ndio aina ya kwanza, nako ni kuhirimia Umrah kwenye Miiqaati (Ihram site) katika miezi ya Hijjah ambayo ni Shawwaal (Mfunguo mosi), Dhul-Qa’adah (Mfunguo pili) na Dhul-Hijjah (Mfunguo tatu). Baada ya kutekeleza ibada hii ya Umrah na kupata “Tahalul” (Release from Ihram) ndipo tena mtu atahirimia Hijjah Makkah au karibu ya Makkah siku ya Tar-wiyah (mwezi 8 Mfunguo tatu) katika mwaka ule ule aliofanya Umrah. Kwa kuitekeleza kwake ibada ya Umrah na Hijjah kwa njia hii ya TAMATUI, kutamlazimu kuchinja mnyama “Hadiyu” – (a voluntary sacrifice animal). Atamchinja mnyama huyu Minaa au sehemu nyingine yo yote ya Haram siku ya kuchinja (mwezi 10 Mfunguo tatu) au baada yake katika siku za “Tashriyq”. Siku za Tashriyq, hizi ni siku za kuanika nyama nazo ni zile siku tatu zinazoiandamia Eidil-Hajji, yaani mwezi 11, 12 na 13. Kama hana mnyama wa kuchinja basi na afunge siku kumi; tatu kule kule Makkah na saba atakaporudi nyumbani, amesema Allah Mola Mtukufu: “…BASI MWENYE KUJISTAREHESHA (tamatui) KWA KUFANYA UMRAH KISHA NDIO AKAHIJI, BASI ACHINJE MNYAMA ALIYE SAHILIKA (nae ni mbuzi) NA ASIYEPATA, AFUNGE SIKU TATU KATIKA HIJJAH NA SIKU SABA MTAKAPORUDI (kwenu); HIZI NI KUMI KAMILI”. [2:196]

QIRAANI: Hii ndio aina ya pili, huku ni kuhirimia Hijjah na Umrah pamoja. Mwenye kuzitekeleza ibada mbili hizi; Hijjah na Umrah hapati Tahalul yaani ahalalikiwi na yale yote yanayokuwa haramu kwake kuyatenda baada tu ya kuhirimia ila siku ile ya kuchinja. Atapata Tahalul siku hiyo ya mwezi 10 Mfunguo tatu baada ya kutupia mawe “Jamratul-Aqabah” na kunyoa au kupunguza. Huyu nae kutamlazimu kuchinja mnyama (Hadyu) Minaa au sehemu nyingine yo yote ya Haram.

 

IFRAAD: Hii ndio aina ya tatu, huku ni kuhirimia Hijjah peke yake katika Miiqaat (vituo vya kuhirimia), kisha Hajji ataendelea kubakia na Ihramu yake mpaka siku ya kuchinja. Halafu ndio atafanya ibada ya Umrah.

 

Mukhtasari wa kauli:

Þ    Ifraadi ni mtu kuhiji kwanza kisha ndio afanye Umrah.

Þ    Tamatui ni mtu kufanya Umrah kwanza kisha ndio ahiji.

Þ    Qiraani ni mtu kuhirimia Hijjah na Umrah; zote mbili kwa pamoja.

 

A.       NAMNA YA KUFANYA UMRAH:

F     Utakapofika kwenye Miiqaati (vituo vya kuhirimia) koga na ujitie manukato likikuwepesikia hilo. Kisha vaa nguo za Ihraam ambazo ni shuka mbili; moja ya kujifunga kiunoni na nyingine ni ya kujitanda na ni bora sana ikiwa zote zitakuwa nyeupe. Ama mwanamke yeye atavaa nguo zo zote za sitara azitakazo zisizo dhihirisha pambo lake. Kisha ndipo unuie kuhirimia Umrah moyoni mwako kwa kusema:              

“NAWAYTUL-UMRATA WA AHRAMTU BIHAA LILLAAHI TAALA”.

Kisha utasema: 

“LABBAYKA UMRATAN [LABBAYKAL-LAAHUMMA LABBAYKA, LABBAYKA LAA SHARIYKA LAKA LABBAYKA, INNAL-HAMDA WAN-NI’IMATA LAKA WAL-MULKU, LAA SHARIYKA LAKA”.

Wanaume wataijihirisha (wataileta kwa sauti) Talbiyah hii na wanawake wataisirisha. Kisha kithirisha kuleta Talbiyah, Dhikri, Istighfaari, kuamrisha mema na kukataza maovu.

 

F     Kisha utaondoka hapo katika kituo chako cha kuhirimia na kuelekea Makkah. Ukifika Makkah itufu Al-Ka’abah mara saba (Twawaafu ya Umrah). Utaanzia kutufu kwenye “Hajarul-Aswad”, huku ukileta Takbira; yaani ukisema Allaahu Akbar na kumalizia hapo, hiyo ni mara moja. Utafanya hivi hivi kwa  mara nyingine zilizobakia mpaka zitimie saba. Wakati wa kutufu utamdhukuru Allah na kumuomba kwa dhikri na dua yo yote uiwezayo. Lakini ni bora ukaikhitimisha kila mara (mzunguko mmoja) kwa kusema:

“RABBANAA AATINAA FID-DUNYAA HASANATAN WAFIL-AAKHIRATI HASANATAN WAQINAA ADHAABAN-NAARI”.

Katika utekelezaji wa zoezi zima la Twawaafu hakikisha unachunga mambo yafuatayo:

a)      Kulibusu “Hajarul-Aswad” kama inamkinika, kama haimkiniki kunatosha kuligusa kwa mkono tu. Hili pia kama likishindikana, kunakutosha kuliashiria kwa mkono pamoja na kukabiri (kuleta Takbira). Kumbuka hakujuzu kuwazonga na kuwaudhi watu kwa ajili ya kulibusu au kuligusa “Hajarul-Aswad”.

b)     Kutufu kwa nyuma ya “Hijril-Ismaail” na wala si ndani yake kwani hiyo ni sehemu ya Al-Ka’abah. Ukimaliza kutufu swali rakaa mbili za Twawaafu nyuma ya “Maqaamu Ibraahiym”, likiwepesika hilo kama haikuwezekana basi swali mahala po pote msikitini.

 

F     Ukimaliza kuswali, ondoka ukiendee kilima Swafaa, panda juu yake (zoezi hili ni kwa mwanamume pekee na wala halimkhusu mwanamke). Elekea Qiblah, muhimidi Allah na umkabiri mara tatu ilhali umeinua mikono yako ukiomba dua, kisha sema:

 

“LAA ILAAHA ILLAL-LAAHU WAHDAHU LAA SHARIYKA LAHUU, LAHUL-MULKU WALAHUL-HAMDU WAHUWA ‘ALAA KULLI SHAIN QADIYRU. LAA ILAAHA ILLAL-LAAHU WAHDAHU ANJAZA WA’ADAHU WANASWARA ‘ABDAHU WAHAZAMAL-AHZAABA WAHDAH”.

Yakariri maneno haya mara tatu, kisha shuka kilimani ili uanze kufanya Sa’ayi ya Umrah mara saba. Anzia hapo Swafaa na kuishia Mar-wa, hiyo ni mara moja. Halafu toka hapo Mar-wa kurudi Swafaa, hii ni mara ya pili. Endelea kufanya hivi kwa mara nyingine zilizobakia mpaka zitimie saba. Nenda mwendo wa kawaida mpaka ukifika kwenye alama ya kijani utakwenda matiti (jaramba/mbio) mpaka uifikie alama ya pili ya taa ya kijani, hapo utatembea mwendo wa kawaida. Kumbuka zoezi hili linamkhusu mwanaume tu (yaani huku kwenda matiti) na sio mwanamke. Angalia ukifika Mar-wa utapanda juu yake kiasi na utayafanya yote uliyoyafanya Swafaa.

TANBIHI: Twawaafu na Sa’ayi hazina adhkari (nyiradi) makhsusi za wajibu, bali mtu ataleta dhikri na dua zinazomuwepesikia au atasoma Qur-ani.

F     Ukishaikamilisha Sa’ayi yako, nyoa au punguza nywele. Mpaka hapa Umrah yako itakuwa imekamilika, hivi ni iwapo umeifanya ibada yako kwa njia ya Tamatui. Kwa kitendo chako cha kunyoa au kupunguza utakuwa umepata “Tahalul”, yaani utakuwa umepata uhalali wa kuyafanya yale yote yaliyokuwa haramu kuyafanya kwa sababu ya Ihraamu (things unlawful while in Ihraam). Ama mtu aliyechagua kufanya ibada mbili hizi kwa njia ya Ifraadi au Qiraani, yeye ataendelea kubakia na Ihraamu ya ibada ya Hijjah, wala hatapata Tahalul mpaka siku ya kuchinja (mwezi 10 Mfunguo tatu). Huu ndio utaratibu wa kuitekeleza ibada ya Umrah, sasa tuangalie yafuatayo:

 

Nguzo za Umrah.

Nguzo za Umrah ni kama zifuatazo:

1.         Ihraamu: Hii ni NIA ya kuingia katika ibada husika kwa kutamka moyoni: NAWAYTUL-UMRATA WA AHRAMTU BIHAA LILLAAHI TAALA.

2.         Twawaafu: Hili ni zoezi la kuizunguka Al-Ka’abah tukufu mara saba kwa namna ilivyoelezwa katika vitabu vya sheria.

3.         Sa’ayi: Hili ni zoezi la kwenda na kurudi mara saba baina ya vilima Swafaa na Mar-wa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria.

4.         Kunyoa au kupunguza: Hili ni zoezi linalohusisha uondoshaji wa nywele zote kichwani au baadhi yake tu. Bora kwa mwanamume ni kunyoa na kwa mwanamke ni kupunguza kidogo tu.

B.       NAMNA YA KUHIJI:

 

F     Ikiwa wewe umechagua kuifanya ibada ya Hijjah kwa njia ya Ifraadi au Qiraani, basi hirimia Hijjah katika Miiqaati (Ihraamu sites) unayoingilia Makkah. Iwapo hauko katika Miiqaati, basi hirimia ulichokinuia mahala ulipo ndani ya mipaka ya Haram. Na ikiwa umechagua njia ya Tamatui, basi utahirimia Hijjah mahala ulipo siku ya Tarwiyah ambayo ni mwezi 8 Mfunguo tatu.

F     Baada ya kuhirimia, koga na ujitie manukato likikuwepesikia hilo. Kisha vaa vazi la Ihraamu, halafu sema:

“LABBAYKA HAJJAN, LABBAYKAL-LAAHUMMA LABBAYKA, LABBAYKA LAA SHARIYKA LAKA LABBAYKA, INNAL-HAMDA WAN-NI’IMATA LAKA WAL-MULKU LAA SHARIYKA LAKA”.

F     Halafu ondoka uelekee Minaa na uswali hapo swala za Adhuhuri, Alasiri, Maghribi, Ishaa na Alfajiri ya mwezi tisaa. Utazikusuru swala za rakaa nne kwa kuziswali rakaa mbili mbili katika nyakati zake bila ya kuzijumuisha.

F     Litakapochomoza jua mwezi tisaa Mfunguo tatu, ondoka Minaa na uelekee katika viwanja vya Arafah kwa utulivu bila ya kuwaudhi mahujaji wenzio. Utaswali hapo swala za Adhuhuri na Laasiri kwa kuzijumuisha mjumuisho wa kutanguliza na kuzikusuru (yaani kuziswali rakaa mbili mbili badala ya nne nne). Ni wajibu uhakikishe kuwa umeingia na umo ndani ya mipaka ya Arafah, uwe makini sana khususan upande wa Kaskazini na Mashariki. Arafah yote ni mahala pa kusimama isipokuwa mahala panapoitwa “Batwni Arinah”. Ni kheri kwako ikiwa utafahamu kwamba kusimama Arafah ndio nguzo kuu ya Hijjah kutokana na kauli yake Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie: “Hijjah ni Arafah”. Kutokana na kauli hii ya Mtume wa Allah itakuwazikia kwamba mtu ambaye hakusimama katika viwanja vya Arafah mchana baada ya swala ya Adhuhuri au usiku mpaka kuchomoza kwa Alfajiri ya siku ya kuchinja (mwezi 10), hana Hijjah mtu huyo. Cha kufanya hapo Arafah ni kukithirisha mno kuleta adhkaari na dua, ilhali umeelekea Qiblah ukiwa umenyanyua mikono yako kama alivyofanya Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie. Endelea kubakia hapo Arafah mpaka kuchwa kwa jua.

F     Jua likishazama, shika njia kuelekea Muzdalifah kwa upole na utuvu mkubwa huku ukileta Talbiyah na tahadhari usiwaudhi mahujaji wenzako: “…NA MTAKAPORUDI KUTOKA ARAFAATI MTAJENI (mdhukuruni) ALLAH PENYE MASH’ARIL HARAAM…” [2:198] Utaswali hapa Muzdalifah swala za Maghribi na Ishaa kwa kuzijumuisha mjumuisho wa kuakhirisha, yaani uziswali swala mbili hizo zote; Maghribi na Ishaa katika wakati wa Ishaa. Utaziswali kwa adhana moja na Iqaamah mbili; Iqaamah moja kwa ajili ya Maghribi na nyingine kwa ajili ya Ishaa. Utabakia hapa mpaka kuswali Alfajiri ukikithirisha dhikri na dua.

F     Kisha ondoka kabla ya kuchomoza kwa jua la siku hii ya mwezi 10 Mfunguo 3; siku ya Eidil-Adh-haa uelekee Minaa huku ukileta Talbiyah. Ukiwa una udhuru, mathalan umeambatana na wanawake au madhaifu (wakongwe, walemavu n.k.) si vibaya ikiwa utaanza kuelekea Minaa tangu baada ya saa sita usiku. Chukua hapa Muzdalifah vijiwe saba (pebbles) kwa ajili ya kwenda kutupia  “Jamratul-Aqabah”, vijiwe vingine utachukua huko huko Minaa.

F     Ukishafika Minaa unatakiwa kufanya mambo yafuatayo:

1.      Kitupie/kipige mawe kinara cha Jamratul-Aqabah, hiki ni kile kilicho karibu na Makkah. Utakipiga mawe saba, yenye kufuatana moja baada ya jingine huku ukileta Takbiri na sio kuyatupa yote kwa mkupuo mmoja tu.

2.      Chinja mnyama (hadyu) ikiwa umelazimikiwa kutokana na kuifanya ibada ya Hijjah na Umrah kwa njia ya Tamatui au Qiraani. Ule sehemu ya nyama hiyo wewe mwenyewe na iliyobakia walishe mafakiri.

3.      Nyoa au punguza nywele, lakini kunyoa ni bora zaidi kwa mwanamume na mwanamke yeye atapunguza nywele kiasi kidogo tu.

Baada ya kutupia mawe Jamratul-Aqabah na kunyoa au kupunguza utakuwa umepata Tahalul ya kwanza, yaani utakuwa umepata uhalali wa kuyafanya yale yote uliyokuwa umezuiwa kwa sababu ya Ihraamu ila kumuingilia mkeo.

4.      Kisha teremka Makkah na utufu “Twawaaful-Ifaadhwah” mara saba, hii ni Twawaafu ya nguzo, kwani Hijjah yako haitimii ila kwa kuileta/kuitenda. Halafu ufanye Sa’ayi baina ya Swafaa na Mar-wa mara saba, hii ni iwapo ulichagua kufanya ibada mbili hizi; Hijjah na Umrah kwa njia ya Tamatui. Kadhalika kutampasa kufanya Sa’ayi yule aliyeichagua njia ya Qiraani au Ifraadi, iwapo hakufanya Sa’ayi baada ya Twawaful-Quduum. Baada ya Sa’ayi hii, ndipo utapata Tahalul ya pili ambayo itakuhalalishia mambo yote hata kumuingilia mkeo.

5.      Baada ya kutufu Al-Ka’abah Twaaful-Ifaadhwah siku ya kuchinja, rejea Minaa na ulale hapo usiku wa mwezi 11, 12 na 13 (masiku ya kuanika nyama – Ayyaamut-tashriyq). Kunajuzu pia kulala nyusiku mbili tu, yaani usiku wa mwezi 11 na 12. Hapa utavitupia mawe vinara vyote vitatu kila siku baada ya kupinduka jua, kila kinara utakitupia mawe saba; moja baada ya jingine huku ukileta Takbira kwa kila jiwe unalotupa. Utaanza kukitupia mawe kinara cha kwanza, siku ya mwezi 11, hiki ni kile kinachouandamia msikiti wa Hunayfi. Kisha utakitupia kinara cha kati na utamalizia na Jamratul-Aqabah. Utafanya hivi katika siku inayofuatia, yaani mwezi 12. Ikiwa una haraka, utaondoka kuelekea Makkah baada ya kuvitupia mawe vinara siku hiyo ya mwezi 12. Kuondoka huku ni sharti kuwe kabla ya kuzama kwa jua, ikiwa utachelewa mpaka jua likazama ukawa bado haujaondoka Minaa, basi kutakulazimu kulala hapo hapo Minaa na uvitupie mawe vinara baada ya kupinduka kwa jua siku ya mwezi 13. Hapo sasa ndio unaweza kuondoka Minaa kurudi Makkah: “NA MTAJENI ALLAH KATIKA ZILE SIKU ZINAZOHISABIWA, LAKINI AFANYAYE HARAKA KATIKA SIKU MBILI (akarejea) BASI SI DHAMBI JUU YAKE, NA MWENYE KUKAWIA PIA SI DHAMBI JUU YAKE, KWA MWENYE KUMCHA ALLAH…” [2:203] Baada ya kumaliza amali zote hizi za ibada ya Hijjah na Umrah na ukaazimia kufunga safari ya kurudi nyumbani, kunakuwajibikia kutufu “Twawaaful-Wadaai” ambayo hasameheki kuiacha ila mwanamke mwenye damu ya hedhi au nifasi tu. Mpaka hapa utakuwa umeikamilisha Hijjah yako.

 

Nguzo za Hijjah.

Ibada ya Hijjah imesimama juu ya nguzo zifuatazo:

1.         Kuhirimia.

2.         Kutufu “Twawaaful-Ifaadhwah”,

3.         Kusa’ayi baina ya Swafaa na Mar-wa.

4.         Kusimama Arafah.

5.         Kunyoa au kupunguza.

 

Waajibaati za Hijjah.

1.         Kuhirimia katika Miiqaati.

2.         Kulala Muzdalifah usiku wa Idi.

3.         Kulala Minaa katika masiku ya Tashriyq.

4.         Kutupia mawe vinara.

5.         Kutufu “Twawaaful-Wadaai”.

6.         Kujiepusha na Muharamaati za Ihraamu (mambo yaliyo haramishwa kwa sababu ya Ihraamu).

7.         Kunyoa au kupunguza.

Elewa na uzingatie kwamba Haji akiacha mojawapo ya nguzo za Hijjah, Hijjah yake hiyo haitasihi kisheria ila kwa kuitenda hiyo nguzo aliyoiacha. Na akiacha mojawapo ya Waajibaati zake, Hijjah yake itasihi lakini kutamlazimu kuchinja mnyama Makkah.

 

Yanayomuwajibikia mwenye kuhirimia.

Yanamuwajibikia mtu mwenye kuhirimia ibada ya Hijjah na Umrah mambo yafuatayo:

1.         Ajilazimishe kuyatenda yale yote aliyowajibishiwa na Mola wake katika fardhi za dini yake kama vile kuswali swala kwa nyakati zake tena katika jamaa.

2.         Ajiepushe na yale yote aliyokatazwa na Allah, asiseme maneno machafu, asifanye vitendo vichafu (ufasiki), asifanya mjadala muovu utakaopelekea uadui, na….. na……

3.         Ajiepushe na Muharaamati za Ihraamu (things unlawful while in Ihraam). Mambo yanayomuharamikia mwenye kuhirimia kwa sababu ya huko kuhirimia kwake Hijjah ni kama yafuatayo:

a)         Kunyoa/kukata nywele au kucha hata kidogo tu.

b)        Kujitia manukato mwilini au nguoni. Haidhuru athari ya manukato aliyojitia kabla ya kuhirimia.

c)         Kuwinda na kumuua mnyama au ndege wa bara au kumsaidia mtu kufanya hivyo.

d)        Kukata au kung’oa mimea ya Haram.

e)         Kuposa au kufunga ndoa yeye mwenyewe au kwa ajili ya mtu mwingine.

f)          Kumuingilia mkewe.

Haya yanawakhusu wote; mwanamume na mwanamke. Haya yafuatayo yanamkhusu mwanamume tu:

a)      Kufunika kichwa chake kwa kuvaa kitu mithili ya kofia au kilemba. Ama kutumia mwavuli si vibaya.

b)     Kuvaa nguo zilizoshonwa (sewn garments).

Ama mwanamke, yeye anakhusika na yafuatayo:

a)      Kuvaa gloves mikononi.

b)     Kufunika uso.

Kunajuzu kwa mwenye kuhirimia kuvaa kandambili/viatu, pete, miwani, saa na mkanda wa kuhifadhia pesa.

 

———————————————————————————————————

bada Ya Hijja Muongozo Kwa Binaadamu.

1 October 2010

Al- Kaaba ndio chimbuko la kwanza la muongozo kwa ulimwengu wote. Muongozo
ambao ni kwa watu wote katika dunia. Iwapo watu wataweka mazingatio yao katika
Al- Kaaba, basi bila shaka itakuwa ndio kuongoka kwao katika njia iliyonyooka.
Muongozo huu umeletwa duniani kwa kuelekezwa Al- Kaaba. Muongozo huu ni ule ule
tunaomwelekeze Mwenyeezi Mungu (s.w.t) kwa kumwomba katika sala zetu za kila siku
kwa kusema:

“Ihdinaa Siraatal Mustaqiim” – Yaani, “Tuongoze katika njia iliyonyooka”

Njia hii ni ile ambayo imejaa Baraka za dunia na hatimaye kufuzu katika maisha ya
baadae ya Akhera. Sote waislam tunaelekeza nyuso zetu kila siku mara tano mbele ya
Al- Kaaba popote tulipo, na inatuwajibikia kutanabahi kwa nini ikaitwa ni nyumba ya
Mwenyeezi Mungu hali tunafahamu na kuelewa vilivyo kuwa yeye hana upunguvu
wa kukadiriwa kuwapo mahala maalum palipowekwa mipaka apate kuabudiwa na
kuelekezewa?

Hivyo ni wazi na hakika ya kwamba kuna lengo na shabaha fulani katika utekelezaji wa
jambo hili na kwa yeyote mwenye kusali huku anayelekea katika nyumba hii anakuwa
ni mwenye kusudio la kumkurubia Mola wake ili kupata mwongozo halisi. Nyumba hii
si ya watawala au wafalme, bali ni nyumba ya Tawhiid (umoja wa Mwenyeezi Mungu)
na imejengwa kwa ajili ya wanatawhiid (wanaoamini umoja wa Mwenyeezi Mungu).

Wakati Nabii Ibrahim (a.s) alipovunja masanamu pamoja na jisanamu lililokuwa na
nguvu zaidi (Namrud) na hatimaye alifanikiwa kuwashinda waabudia masanamu hapo
ndipo akaanza kazi ya kuijenga Al – Kaaba.

Nyumba hii ni huru kutokana na misingi ya rangi, kabila, taifa au chochote anachoweza
mtu kujifikiria kuwa nacho. Ni nyumba ya watu wote kutoka pande zote za dunia.
Ni hifadhi ambayo wote hukimbilia na Mwenyeezi Mungu (s.w.t) ameahidi na kufanya
kuwa ni mahala salama kwa mwenye kuingia. Kunapatikana aya na hadithi nyingi zenye
kutaja taadhima za Al- Kaaba na utekelezaji wa ibada ya Hijja ambazo zimethubutu
katika vitabu vya tafsiri na riwaya.

Je, tunadhani kuwa ibada ya Hijja katika uislam ni ibada inayotekelezwa kwa kusudio
la kupata malipo ya Akhera tu? Au yamkinika mtu kudhani kuwa utekelezaji wa Hijja
kila mwaka katika wakati makhsusi hakuna jukumu katika mwelekeo kwa umma wa
kiislamu?

Katika kuielezea Al- Kaaba, Mwenyeezi Mungu amesema ndani ya Qur’an tukufu kuwa:

“Mwenyeezi Mungu ameifanya Kaaba hii nyumba tukufu kuwa ni tengenezo la (maisha
ya) watu na akaifanya ile miezi minne mitukufu (pia tengenezo la maisha ya watu) na
kule kupeleka wanyama Makka, na kujitia vigwe (vya kuonyesha kuwa wao ni Mahujaji;
yote hayo ni kwa ajili ya tengenezo la Maisha ya watu. Amefanya haya kwa sababu
mjue ya kwamba Mwenyeezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyopmo katika
ardhi, na kwamba Mwenyeezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu” (Surat Al – Maidah: 97).

Kwa ubainifu wa aya hii, je hakuna mafungamano yoyote ya watu na maisha yao
kutokana na Hijja?

Hivyo, ni dhahiri kwamba tunaweza kufaidika na kufahamu falsafa ya Hijja kwa kupitia
katika aya mbalimbali toka katika kitabu kitufu cha Mwenyeezi Mungu.

Ameeleza tena Allah (s.w.t) kuwa:

“Na (kumbukeni habari hii pia) tulipoifanya nyumba (Al- Kaaba) iwe mahali pa
kuendewa na watu na mahali pa salama. Na mahali aliposimama Ibrahim pafanyeni
pawe ni pa kusalia. Na tulimwusia Ibrahim na Ismail (tukawaambia); itakaseni
(isafisheni nyumba yangu kwa ajili ya wale wanaoizunguka na kutufu na kwa
wanaokaa hapo na wanaorukuu na kusujudu hapo pia” (Surat Al – Baqarah: 125)

“Katika (wanyama) mnaowapeleka Makka (kuchinjwa) mnayo (ruhusa kutumia)
manufaa yake mpaka muda maalum; (nao ni hapo inapopasa kuchinjwa). Kasha mahali
pa kuchijiwa kwake ni (karibu na) ile nyumba kongwe ya kale” (Surat Al- Hajj: 33)

Kusudio la aya hizi mbili hapa ni suala zima la umoja baina ya waislamu wote pindi
wanapokuwa katika ibada ya Hijja, kwani ni lazima tufahamu pia lengo la mkusanyiko
kwa ibada hii muhimu na maalum ni kwa ajili ya kuunganisha umma na kujenga umoja
baina yao bila ya kuonyesha ubaguzi wa aina yoyote na kuleta nguvu na kujenga ngome
imara katika dini tukufu ya uislam dhidi ya maadui.

Enyi ndugu katika uislam! Katika masiku haya ambayo wengi wenu mnakusudia kwenda
Hijja kama Mahujaji hebu zingatieni mliyoyaandalia katika safari hii takatifu. Ni ujumbe
gani mlioubeba kama zawadi kwa ndugu zako wengine waislamu? Utaufikisha vipi
ujumbe huu uliojaa huba, udugu na mazingatio yake kwa Mahujaji wenzako ili upate
kuwafikia waislamu wote duniani? Utaoanisha vipi mapendekezo yako na ya wengine ili
kupatikane fahari, uelewano wenye masikilizano na utangamano wenye mapenzi katika
ulimwengu wa kiislamu?

Kwako ngugu yangu, pindi haya yatakuwa ndio lengo na shabaha ya kutekeleza ibada hii
muhimu, na kufikiria namna ya utekelezaji katika kongamano hili ambalo yamsarifu kila
mwenye uwezo hata kama ni mara moja katika uhai wake, itakuwa ndio hatua ya kwanza
katika kuukomboa umma wa kiislamu kutokana na shida na matatizo yanayoukabli na
ndiko kutakuwa kuafikiwa kwa lengo la Hijja.

Mwisho, Ewe dada yangu na ewe kaka yangu mwislamu, iwapo wewe ni miongoni mwa
Mahujaji mwaka huu, tunakutakia Hajj Maqbulan (yenye kukubalika) na ikiwa si mmoja
wao, basi Mwenyeezi Mungu atakuwafikisha kuwa miongoni mwa wenye kuhiji Bei-ul-
Allah al –haram mwakani, Insha-Allah.

Imetayarishwa na kikundi cha wanawake cha:
Hazrat Zahra (a.s) Foundation of Tanzania.

 

————————————————————————————————————-

UFAFANUZI  WA IBADA YA HAJJ

BISMILLAHIR RAHMAANIR RAHIIM

Tunamshukuru mwenyezi mungu mola wa walimwengu wote,na rehma na amani ziwe juu ya mtume muaminifu, na juu Aali zake na maswahaba wake walio wema na watakasifu.

Mwenyezi mungu mtakasifu amesema (( Na ni haki ya mwenyezi mungu  juu ya  watu kuhiji  (  kuitembelea)  nyumba hiyo kwa  mwenye kuiweza njia ya kwendea. Na anaekataa, basi mwenyezi mungu si muhitaji kwa walimwengu )).  Suratu al-imraan aya 97.

Kisha amesema : Na watangazie watu hijja  watakujia (wengine)  kwa miguu na (wengine) juu ya kila mnyama  wakija toka kila njia ya mbali* Ili washuhudie manufaa yao na kulitaja  jina la mwenyezi mungu katika  siku maalum juu  ya yale  aliyowaruzuku,  nao ni  wanyama wenye miguu mine,  na  kuleni katika  wanyama hao na walisheni wenye shida, mafakiri. suratul haji aya 27-28.

Pia mwenyezi mungu amesema: Hijja ni miezi maalum, na atakayewajibikiwa  kufanyahijja katika (miezi) hiyo, basi asiseme maneno machafu  wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hijja. Na kheri yoyote mnayoifanya menyezi mungu anaijua. Na chukueni masurufi, hakika masurufi bora niucha mungu, na nicheni mimi enyi wenye akili. (Suratul baqarah 197.)

Swadaqallahul adhiim.

Ufuatao ni muhtasari na ufafanuzi wa ibada ya hijja na faida zake kwa mujibu wa fat’wa za marjiu wa kidini ayatullahi

Ali hussein Sistaniy.

Na hebu tutaje  hapa baadhi ya hadithi zilizo pokelewa  kuhusiana  na umuhimu wa Hajji na baadhi ya siri zake:

Amesema imam swadiq (a.s) Mwenye kuhiji na mwenye kufanya umrah ni wageni  wa  mwenyezi mungu, wakimuomba, huwapa, na wakimuita huwaitika, na wakimuomba uombezi huwakubalia uombezi wao, na wakinyamaza yeye huwaanza, na hupewa badala ya kila dirham moja  dirham elfu mia moja.

Na Mtume (s.a.w) amesema: Wageni wa mwenyezi mungu ni wa aina tatu  Mwenyekuhiji (Al-haji) na mwenye kufanya umrah na mpiganaji kwenye njia ya mwenyezi mungu, mwenyezi mungu aliwaita wakamuitika, na wakamuomba akawapa.

Na imam Ali bin Hussein  (a.s) amesema: Fanyeni hijja na umra miili yenu itapata swiha na Afya, na riziki zenu zitapanuka na kuzidi, na mtaweza kukidhi mahitaji ya familia zenu.

Na imepokelewa kutoka kwa imam swadiq (a.s): amesema (Yeyote mwenye kufariki bila kufanya hijja ya kiislaam na hapakuwa na tatizo lolote lililo mzuwia  kufanya hivyo  au lililo kuwa likimsumbua au  kuwa na ugojwa  ambao ulimzuwia kufanya hijja  au mtawala wa kumzuwia  basi akifa atakufa akiwa yahudi au mkiristo).

Na imepokelewa katika Hadithi nyingine: Mwenye kuichelewesha hijja  hadikikamfikia kifo mwenyezi mungu atamfufua siku ya kiama akiwa yahudi au mkiristo.

Na imepokelewa kutoka kwao amani iwe juu yao: Umejengwa uislaam juu ya misingi mitano  Swala, Zaka, Hajji ,Funga, na wilaya ya Ahlul bayti.. (yaani kuwatawalisha Ahlul bayti)

Na imepokelewa kutoka kwa imam swaadiq (a.s.) kuhusia na kauli yake mwenyezi mungu alie takasika ( Yule ambae katika dunia hii atakuwa kipofu basi na katika Akhera atakuwa kipofu na mpotofu wa njia) yaani yule ambae huichelewesha Hajji (Hijjatul islaam) mpaka akafikiwa wa mauti.).

Pamoja na kuwa Hajji ni nguzo moja wapo kati ya nguzo za uislaam, haimpasi mwislaam na muumini isipokuwa kuitekeleza faradhi hii tukufu-ikiwa masharti ya kuwajibika kwake yatakamilika-.

Na Hijja ni  ibada amabyo mja hupata kheri za dunia na thawabu za Akhera kupitia ibada hiyo, Hijja si ibada ya kiroho tu kiasi kwamba mtu anaisahau dunia na kuipa mgongo moja kwa moja, kama ambavyo si matendo ya kimadi pekee kiasi mbacho huitupilia mbali Akhera, bali ni mchanganyiko ambao huangalia upande wa kimadi kama ambavyo ina angalia upande wa kiroho, na kila upande kwa kisi chake.

Na jambo la kwanza kabisa liangaliwalo katika ibada hii ya Hijja ni kuwa, hijja ni kongamano la kimataifa la mwaka na la watu wote, na hukusanyika na kukutana kwenye kongamano hilo  makundi yote ya wanadamu  na wote wakiwa sawa tajiri na masikini bwana na mtumwa na wengineo, na nilazima kufanyike kati yao mazungumzo ili waweze kufahamu habari na mambo muhimu ambayo inampasa kuyafahamu kila muislaam wa  nchi yoyote ile, na nilazima baadhi yao kufikiria japokuwa  kidogo- ufumbuzi wa mabao yanayo wahimu waislaam katika maisha yao ya kidini na mengineyo.. na kwa kufanya hivyo kutakuwa na kheri zote kwa ujumla, ikiwa muislaam atafahamu kuhusiana na yanayo msibu nduguye muislaam na kufahamu yaliyo muhimiza na kutilia hima mambo yake na kuweza kumnusuru  kutokana na misukusuko na matatizo na kumletea saada.

Imam swadiq (a.s) anasema: akimjibu Hisham pale alipo muuliza kuhusu sababu ya kufanya hijja: (( Akaifanyahijja iwe ni mkusanyiko wa watu kutoka mashariki na magharibi ili waweze kuelewana, na lau kama watu wa kila nchi wangelikuwa wakizungumza kuhusu nchi yao pekee na yanayo tokea  humo wange angamia na nchi zinge haribika na vivutio vinge anguka na kusinge patikana faida na habari zisinge julikana au zinge potoshwa na wasinge yaelewa hayo)).

Je mahujaji hatuwaoni wakivua mavazi yao  na kuvua kila aina ya pambo na kuvaa nguo mbili za ihram, je hili halijulishi ya kuwa watu wote ni sawa na wako kwenye mustawa mmoja hakuna alie bora kuliko mwingine katika shakli na umbo au mandhari, maefu yote haya ya mahujjjaji huko waliko toka wameacha mapambo ya aina tofauti ya kidunia na vitu mbali mbali vya kifakhari na wakaja wakiitika wito wa mwenyezi mungu na huku wakisoma takbira na kumtukuza allah na wakitoa mandhari yenye kuvutia na mazuri ya usawa wa kikweli kweli na wakidhati usawa ambao haukuchanganyika na aina yoyote ya kujitweza na kujiboresha.

Hakika mandhari hayo ni mandhari matukufu na ambayo humuondoshea mwanadamu aina zote za tofauti na iitibari zisizo na msingi, na huwa mnyenyekevu na kufikia hatua ya kuwaona  watu walioko pande zote za dunia kuwa ni ndugu zake na nilazima awasaidie na ashirikiane nao katika furaha zao, na huona na kujihisi ya kuwa hakuna kitu kimuinuacho daraja na kumfanya kuwa bora kuliko nduguye au kuwa na nafasi ya juu kabisa kuliko rafiki yake.

Imama Ali (a.s) amesema katika hotuba yake: (Hakika wameacha nguo zao na suruali zao huko waliko toka na kuzipa mgongo, na wakashikwa na hisia kwa kunyoa vichwa vyao, na huo ukiwa ni mtihani mkubwa, na majaribio mengi, na kukitoa kiburi kwenye nyoyo zao, na kuzituliza nyoyo zao kwa kuziingizia unyenyekevu).

Mji wa makkatul mukarramah na Madinatul munawwarah ndio chimbuko la kuenea ujumbe wa kiislaam, na miji hiyo miwili ndio chanzo cha kuenea nuru ya uislaam,na kuenea pembe zote za dunia, na kwenye miji hiyo ndiko kwenye athari za mtume wa uislaam (s.a.w), na kwenye miji hiyo ndio kuliko na sehemu na muhali ambapo humrejesha hajji kwenye zama za mwanzo za uislaam….

Hakika huweza kuona kwenye miji hiyo pango la Hiraa mahala pa kwanza ambapo mtume alitelemshiwa wahyi na sheria mahala hapo, na huuona mlima wa Thawr sehemu ya kwanza alipo simama mtume (s.a.w) kwa ajili ya kufikisha wito wa mwenyezi mungu, na Kaaba tukufu ni sehemu tukufu ambayo ameielekea mtume na waislaam, na masjidul haraam ni nukta na sehemu  muhimu sana ambapo mwenyezi mungu mtukufu huabudiwa, na msikiti wa mtume ni madrasa kubwa kabisa ya kiislaam iliyoweza kufahamika katika historia ya waislaam, na kaburi la mtume (s.a.w) ni kaburi tukufu kabisa litembelewalo na waislaam (hufanyiwa ziara), na makaburi ya maimamu watokanao na kizazi chake ni mahala patukufu kabisa pakusudiwapo na watu wema na wenye utakasifu wa moyo..,  mambo yote haya na mandhari yote haya na mengineyo mengi humkumbusha na kumpatia kumbu kumbu ya visimamo vya mtume (s.a.w) na jihadi yake ambayo haikuteteleka dhidi ya shirki na humkumbusha juhudi alizo zifanya katika njia ya kuliinua neno la mwenyezi mungu na kulifuta neno la kufru na ushirikina.

Hakika hajji anapo rudi kutoka kwenye safari hii hurudi akiwa amejawa na imani kamili na yenye nguvu kutokana na aliyo yaona yamtiayo kila mtu athari ya imani na nguvu.

Imama Jaafari swadiq (a.s) amesema akibainisha sababu ya kuwekwa sheria ya hajji: ( Na ili watu waweze kuelewa athari za mtume (s.a.w) na waweze kufahamu habari zake, na akumbukwe wala asisahaulike).

Na katika upande wa kiuchumi, ni kwamba mamilioni ya pesa huyatumia mahujjaji katika safari yao je hii sio harakati ya kiuchumi yenye kuendelea kila mwaka na kunufaika nayo watu wa matabaka tofauti, je unafahamu vema hali ya kibiashara ambayo hufanyika kwenye msimu huu wenye baraka  wa hijja, hakika wakulima na wafanya kazi na wafanya biashara wakubwa wakubwa pia wafanya biashara wadogo wadogo na wafugaji na wamiliki wa majumba  na mahoteli na wengineo ambao ni wenge hupata faida kubwa sana katika masiku haya machache bali baadhi yao hujipatia matumizi ya mwaka mzima katika masiku haya machache pekee, ukiongezea idadi kubwa ya mahujaji wafanyao biashara katika safari yao hii  kila mmoja kulingana na shughuli yake na kazi yake, na huenda ikawa ni njia moja wapo ya kutanbuana  na kujuana katika nyanja za kiuchumi na kibiashara moja kumjua mwenziwe, jambo lipelekealo kukuza na kupanua nyanja za kimaisha na kibiashara katika jamii mbali mbali za wanadamu na nchi mbali mbali  za kiislamm.

(Na watangazie watu hijja  watakujia (wengine)  kwa miguu na (wengine) juu ya kila mnyama  wakija toka kila njia ya mbali* Ili washuhudie manufaa yao na kulitaja  jina la mwenyezi mungu katika  siku maalum juu  ya yale  aliyowaruzuku,  nao ni  wanyama wenye miguu mine,  na  kuleni katika  wanyama hao na walisheni wenye shida, mafakiri.) suratul haji aya 27-28.

Imama swadiq (a.s) amesema katika hadithi yake:( Na ili kila watu wapate faida kutokana na biashara zitokazo nchi moja kwenda nchi nyingine, na ili waweze kunufaika kwa kufanya hivyo …….

Ewe mheshimiwa hajji, hizi ni baadhi tu ya faidia za hajji  na siri zake kwa mtazamo wa haraka  haraka ambazo huzifahamu kutokana na hadithi tukufu, na kuyaelewa yote kiukamilifu inahitaji nafasi na muda mrefu  ambao hatukujaaliwa kuupata kwenye utangulizi huu mfupi ambao huwekwa kwenye kijitabu kama hiki cha mas’ala ya kisheria.

Tunamuomba mwenyezi mungu awape tawfiq waislaam wote yakuweza kufanya matendo yao kwa mujibu wa hukumu za kiislaam, hakika yeye ndie mbora wa watoao tawfiq na msaidizi bora.

TUNAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU MOLA WA VIUMBE WOTE NA REHMA NA AMANI ZIWE JUU YAKE NA AALI ZAKE WATUKUFU.

Haji ni wajibu kwa kila mukallafu alie timizi masharti yafuatayo, na kuwa kwake wajabu kumethibiti kwa mujibu wa kitabu kitukufu na sunna iliyo thibiti kutoka kwa mtume (s.a.w). Na haji ni nguzo moja wapo kati ya nguzo za dini, na wajibu wake ni miongoni mwa mambo ya lazima katika dini, na kuiacha hajji pamoja na kukubali kuthibiti kwake- ni maasi makubwa, kama ambavyo kupinga asili ya kuwepo kwa faradhi hii –ikiwa kupinga huko hakukujitegemeza kwenye shubha ni kufru.

Mwenyezi Mungu amesema katika kitabu chake kitukufu: ((( Na ni haki ya mwenyezi mungu  juu ya  watu kuhiji  (kuitembelea)  nyumba hiyo kwa  mwenye kuiweza njia ya kwendea. Na anaekataa, basi Mwenyezi Mungu si muhitaji kwa walimwengu )).

Na Shekh Kulayniy amepokea –kwa njia muutabar – kutoka kwa Abi abdillahi  (a.s) amesema: Yeyote mwenyekufa huku akiwa hakuhiji hijja ya islaam,na hakuna kulicho mzuwia kufanya hivyo tatizo lolote au hajja yoyote yenye kumtatiza, au ugonjwa ambao haukumuwezesha kufanya hijja, au  mtawala mwnye kumzuwia, basi akifa na afeakiwa yahudi au mkiristo.

Na kuna riwa zingine nyingi ambazo ni dalili tosh juu ya kuwajibika kwa hajji na kuitilia umuhimu  hatukuweza kuzielezea kwa kutaka kufupisha, na aya tulio itaja pia riwaya tuliyo itoa inatoshelrza kuthibitisha uwajibu huo.

Na nivema ukaelewa kuwa hijja iliyowajibu kwa kila mukallafu –katika sheria ya kiislaam- ni mara moja tu, na hijja hijyo huitwa (Hijjatul islaam).

MAS’ALA 1: Ni wajibu kuitekeleza ibada ya hijja kwa haraka iwezekanavyo baad ya kukamilika  masharti yake, na itakuwa ni lazima kuitekeleza katika mwaka  wa kwanza wa kupatikana uwezo, na ikiwa mtu  ataiacha kuitekeleza kwenye mwaka huo basi itamlazimu katika mwaka wa pili na kuendelea ikiwa hakuweza kwenye mwaka wa pili.

Lakini uharaka wa kuiteleza kwake je niwakisheria – kama isemavyo kauli iliyo mashuhuri- au niwa kiakili na ni katika kufanya ihtiyaati- ili isije kumlazimu hali ya kuuchelewesha wajibu au kuutia wajibu kasoro bila ya udhuru na kwa kufanya hivyo akastahili adhabu kwa kuto utekeleza wajibu- hapa kuna pande mbili: iliyo ahwatu ni ya kwanza, na yenye nguvu zaidi ni ya pili, na ikiwa hakuharakia kuitekeleza bila ya kuwa na uhakika au matumaini ya kuwepo uwezekano wa kuitekeleza baada ya hapo atakuwa ni  (mutajarriya) mwenye kukusudia kuacha jambo lililo thibiti kisheria ikiwa atalifanya au kulitekeleza baadae, na atakuwa ni aasi au muasi na mwenye kufanya madhambi makubwa ikiwa hakuweza kuitekeleza kamwe  baada ya kuwa imempita.

MAS’ALA 2: Ikiwa itawajibika kutoka kwenda hijja itawajibika pia kukamilisha vitangulizi vya safari hiyo ya hajji na kuandaa nyenzo za safari kiasi kwamba ataweza kuitekeleza ibada hiyo katika wakati wake ulio pangwa, na lau kuta kuwa na watu kadhaa au vikundi kadhaa anavyo weza kufuatana navyo kwenye safari na akawa na uhakika wa kuidiriki ibada hiyo ya hajji  kwa kufuatana na msafara wowote ule atakuwa na hiyari ya kufuatana na msafara wowote ule, japokuwa ni bora kuchagua msafara ambao atakuwa na uhakika zaidi ya kuidiriki ibada hiyo.

Na ikiwa kati ya misafara hiyo kuna mmoja tu ambao anauhakika kuwa kwa kufuatana nao ataweza kuidiriki ibada hiyo, haitajuzu wakati huo kuchelewa kutoka isipokuwa ikiwa atakuwa na uhakika kuwepo kwa msafara mwingine, na kukawa na uwezekano wa kuanza safari na kuweza kuidiriki ibada ya hijja ikiwa atafuatana na msafara huo.

Na hali ni hiyo hiyo katika mambo mengine yahusianayo na utokaji kwa ajili ya safari, kama ikiwa safari ni kwa njia ya bara (nchi kavu) au bahari au anga na mfano wa hayo.

MAS’ALA 3: Ikiwa utapatikana uwezo na ikawajibika kuharakia kuitekeleza ibada hiyo ya hijja katika mwaka ambao uwezo umepetikana na akachelewa kutoka kwenda kuitekeleza kwa kuwa na uhakika wa kuidiriki pamoja na kuwa kuchelewa pia, lakini ikatokea kwamba hakuweza kuidiriki kwa sababu ya kuchelewa kutoka, atakuwa ni mwenye udhuru katika kuchelewa kwake, na kwa kauli yenye nguvu ni kuwa haitathibiti kwake ibada ya hijja.

Na hali ni hiyo hiyo katika sehemu zingine ambazo itashindikana kuidiriki hajji kwa sababu ya matukio ya ghafla ambayo yako nje ya uwezo wake bila ya yeye kuzembea katika kupitwa kwa ibada hiyo au kusababisha ucheleweshaji huo.

Si wajibu kwenda hijja kwa mtu ambae hajafikia baleh yaani ukubwa wa kisheria, hata kama atakuwa mefikia ujana, na lau kama mtoto au kijana atakwenda hijja, basi hijja hiyo haitakuwa imemuondolea na kutosheleza katika hijja ya kiislaam, hata kama hijja yake itakuwa sahihi kwa kauli iliyo na nguvu.

MAS’ALA 4- Ikiwa mtoto atatoka na kwenda hijja na akawa balehe au kufikia utu uzima kabla ya kuvaa ihram kwenye miiqaati (vituovya kuvalia ihram)  na akawa ni mwenye uwezo -hata kama atakuwa kwenye sehemu hiyo- hakuna shaka yoyote kuwa hijja yake ni hijja ya kiislaam.

Na ikiwa atava ihram na akawa baleeh baada ya kuvaa ihram na kabla ya kusimama muzdalifa ataitimiza hijja yake na hijja hiyo itakuwa ni hijja ya kiislaam pia kwa kauli yenye nguvu.

MAS’ALA 5: Ikiwa ata hijji hijja ya sunna akiitakidi ya kuwa hajawa baleeh, kisha ikabinika baada ya kuitekeleza hijja hiyo au wakati akitekeleza na kabla hajamaliza ya kuwa amebaleeh, hijja hiyo itahesabika kuwa ni hijja ya kiislamm na atatosheka na hijja hIyo na hakuna ulazima wa kufanya hijja nyingine.

MAS’ALA 6: Ni sunna kwa mtoto mwenye kutambua (mumayyiz) kufanya hijja, lakini kauli iliyo mashuhuri ni kuwa ni sharti katika kusihi kwake  kupata idhini ya wali wake, na kauli hiyo haiko mbali na ukweli.

MAS’ALA 7: Haizingatiwi idhini ya wazazi wawili katika kusihi kwa hijja ya mtoto alie fikia baleeh kamwe. Ndio ikiwa kutoka kwake kwa ajili ya hijja ya sunna kutasababisha maudhi kwa wazazi wawili au mmoja wao kwa kumuonea huruma kutokana na hatari na taabu za njiani kwa mfano haitajuzu kwake kutoka.

MAS’ALA 8: Ni sunna kwa walii kumpeleka hijja mtoto ambae si mumayyiz- pia mtoto wa kike ambae si mumayyiz- na katika hijja hiyo atamvisha nguo mbili  za ihram  na kumuamrisha kufanya talbiya (yaani kusema labbayka allahumma labayka) na kumtamkisha maneno hayo- ikiwa kunauwezekano wa kuyatamka maneno hayo laa sivyo  walii atamtamkia kwa niaba yake- na kumuepusha na mambo yaliyo haramu kwa mtu alie vaa ihram kujiepusha nayo, na inajuzu kuchelewesha kumvua nguo zake zilizo shonwa na mfano wa hizo mpaka kwenye sehemu ya fakh- ikiwa ni mwenye kupita njia hiyo- na inambidi kumuamuru kutekeleza kila analo weza kulitekeleza kati ya matendo ya hijja, na atamfanyia yeye matendo ambayo hawezi kuyatekeleza, na atafanya twawaaf pamoja nae, na atafanya saai kati ya safa na marwa, na atasimama nae katika Arafa na katika mash’aril haraam, na atamuamuru kutupa mawe ikiwa ataweza kufanya hivyo, la sivyo atamsaidia kutupa mawe, vilevile kusali sala ya twawaf, na atanyoa nywele na atafanya matendo mengine.

MAS’ALA 9: Hakuna shaka yoyote walii kumvalisha  ihram  mtoto hata kama yeye mwenyewe si mwenye kuvaa ihram.

MAS’ALA 10: Kauli iliyo adh’har ni kuwa walii ambae ni sunna kumfanyisha hajji mtoto asie kuwa mumayyiz ni kila mwenye haki ya kumlea kama wazazi wawili au wengineo kama ilivyo fafanuliwa kwenye mas’ala ya nikaha (ndoa).

MAS’ALA 11: Matumizi ya hijja ya mtoto  yanayo zidi matumizi ya kawaida ya nyumbani ni juu ya walii si juu ya mtoto. Ndio, ikiwa kumhifadhi mtoto kunategemea au ni lazima kusafiri nae, au ikwa katika kusafiri nae kuna maslahi kwake, matumizi ya safari yenyewe yatakuwa kwenye mali yake si matumzi ya kuhijji nae ikiwa matumizi yatazidi. 

MAS’ALA 12: Thamani ya mnyama wa kuchinja wa mtoto ambae si mumayyiz ni juu ya walii, vile vile kafara ya kuwinda kwake, ama kafara ambazo hufanyika au huwa wajibu kuzitekeleza kwa kufanya jambo kwa makusudi kauli iliyo dhahiri ni kuwa haitawajibika kwa kitendo cha mtoto – hata kama ni mumayyiz- si juu ya walii wala si wajibu kwenye mali ya mtoto. 

SHARTI LA PILI: KUWA NA AKILI TIMAMU

Si wajibu kwa mwenda wazimu au majnuni kufanya  ibada ya hajji, ndio ikiwa wazimu wake ni wa vipindi na wakati anapo zindukana hawezi  kutekeleza matendo ya hajji na utangulizi wake, na alikuwa ni mwenye uwezo, itamuwajibikia kuhijji  hata kama atakuwa  kwenye hali ya umajnuni katika muda mwingine, kama ambavyo lau akijua ya kuwa kipini chake cha kujiwa na uwazimu kitakutana na matendo au ibada ya hijja kwa wakati wote itakuwa ni wajibu kwake kumuweka  mtu amfanyie hijja baada ya kuzindukana kwake
———————————————————————————————–

Ibada ya Hijja ni chemchemi safi inayoweza kuwatakasa mahujaji na uchafu wa madhambi

Monday, 21 June 2010 15:10 TzChalii
E-mail Print PDF

HIJA NA UMUHIMU WAKE

MAKALA HII IMEANDIKWA NA: BARAZA

 
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI

WA REHEMA MWENYE KUIREHEMU.

ASSALAAM ALIKUM WARAHMATULLAH TAALA WABARAKAATUH.

Msimu wa Hija ni machipuo ya umaanawi na kung’ara kwa tauhidi katika upeo wa Dunia; na ibada ya Hija, ni chemchemi safi inayoweza kuwatakasa mahujaji na uchafu wa madhambi na mghafala, na kurejesha ndani ya nyoyo na nafsi zao atia ya Mwenyeezi Mungu ya nuru ya fitra na maumbile. Kulivua vazi la majivuno na la kujipambanua na wengine katika makutano ya Hija, na kuvaa vazi la pamoja na la rangi moja la Ihramu, ni alama na nembo ya kuwa na hali moja umma wa Kiislamu, na ni hukumu ya dhihirisho la umoja na kuwa kitu kimoja Waislamu wa sehemu zote duniani.
Msimu wa Hija ni machipuo ya umaanawi na kung’ara kwa tauhidi katika upeo wa dunia; na ibada ya Hija, ni chemchemi safi inayoweza kuwatakasa mahujaji na uchafu wa madhambi na mghafala, na kurejesha ndani ya nyoyo na nafsi zao atia ya Mwenyezi Mungu ya nuru ya fitra na maumbile. Kulivua vazi la majivuno na la kujipambanua na wengine katika makutano ya Hija, na kuvaa vazi la pamoja na la rangi moja la Ihramu, ni alama na nembo ya kuwa na hali moja umma wa Kiislamu, na ni hukumu ya dhihirisho la umoja na kuwa kitu kimoja Waislamu wa sehemu zote duniani. Upande mmoja wa Sha’ar ya Hija ni
فَإِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ فَلَهُ أَسْلِمُوا وَبَشِّرِ الْمُخْبِتِينَ
“Basi Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Jisalimishieni Kwake tu, na wabashirie wanyenyekevu.” Na upande wake wa pili ni
وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ الَّذِي جَعَلْنَاهُ لِلنَّاسِ سَوَاء الْعَاكِفُ فِيهِ وَالْبَادِ
“Na Msikiti Mtakatifu, ambao tumeufanya kwa ajili ya watu wote sawasawa, kwa wakaao humo na wageni.” Na ndivyo hivyo, kwamba al Kaaba, mbali ya kuwa ni kiwakilishi cha kalima ya tauhidi, ni dhihirisho pia la tauhidi ya kalima, udugu na usawa wa Kiislamu.

Waislamu waliokusanyika hapa kutoka pembe nne za dunia wakiwa na shauku kubwa ya kutufu al Kaaba na kuzuru Haram ya Mtume Muhammad SAW wanapaswa kuithamini na kuitumia ipasavyo fursa hii kwa ajili ya kuimarisha mfungamano wa kidugu baina yao, ambao ni dawa ya masononeko makubwa uliyo nayo umma wa Kiislamu. Leo hii tunajionea waziwazi jinsi mkono wa wasioutakia mema ulimwengu wa Kiislamu unavyofanya kazi zaidi ya ulivyokuwa huko nyuma, ya kuwafarakanisha Waislamu. Na hii ni katika hali ambayo leo hii umma wa Kiislamu unahitajia mshikamano na kuwa kitu kimoja, zaidi ya ilivyokuwa huko nyuma.

Leo makucha yaliyoroa damu ya maadui, yanaonekana hadharani yakiendelea kuleta maafa katika sehemu mbali mbali za ardhi za Kiislamu; Palestina iko kwenye mateso na madhila yanayoongezeka kila uchao, ya ukandamizaji wa kikhabithi wa Wazayuni; msikiti wa al Aqsa unakabiliwa na hatari kubwa; baada ya mauaji yale ya kimbari yasiyo na mfano, wananchi madhulumu wa Gaza wangali wanaendelea kuishi katika hali ngumu kabisa; Afghanistan iliyoko chini ya ukandamizaji wa kijeshi wa wavamizi, kila siku inapatwa na maafa na masaibu mengine mapya; wananchi wa Iraq wamekuwa hawana raha kutokana na machafuko na kukosekana amani nchini humo; na mauaji baina ya ndugu na ndugu nchini Yemen yameutia jeraha jengine jipya moyo wa umma wa Kiislamu.

Waislamu wa dunia nzima wakae na kutafakari, fitna na vita hivi, na milipuko na mauaji haya ya kigaidi na ya kiholela, ambayo yamekuwa yakijiri katika miaka ya hivi karibuni katika nchi za Iraq, Afghanistan na Pakistan yanatokea vipi na yanapangwa na kuratibiwa wapi? Kwa nini hadi kabla ya uingiaji wa kijeuri na wa kujifanya wamiliki, wa majeshi ya Magharibi katika eneo hili wakiongozwa na Marekani, wananchi wa mataifa haya hawakushuhudia misiba na masaibu yote haya? Kwa upande mmoja wavamizi wanazipa harakati za mapambano za wananchi wa Palestina, Lebanon na maeneo mengine jina la magaidi, na kwa upande mwingine wanaratibu na kuongoza ugaidi wa kinyama wa kimapote na kikaumu kati ya mataifa ya eneo hili. Katika kipindi kirefu, na kwa zaidi ya miaka mia moja, nchi za eneo la Mashariki ya Kati na la Kaskazini mwa Afrika zilikuwa katika madhila, uvamizi na unyonyaji wa madola ya Magharibi, ya Uingereza, Ufaransa na mengineyo, na baadaye Marekani; maliasili zao ziliporwa, moyo na hisia za kujihisi kuwa ni binadamu huru zilizimwa, na wananchi wao wakafanywa mateka wa uchu na tamaa za madola machokozi ya kigeni.
Na mara baada ya madhalimu wa kimataifa kung’amua kwamba haiwezekani tena kuendeleza hali hiyo kutokana na mwamko wa Kiislamu na harakati za mapambano za mataifa, na baada ya kuona kuwa suala la kuwa tayari kufa shahidi na katika njia ya Mwenyezi Mungu limeingia tena katika damu ya Jihadi ya Kiislamu likiwa ni fikra madhubuti isiyo na mithili, (madhalimu hao wa kimataifa) waliamua kutumia mbinu za hila na ujanja, na hivyo ukoloni mamboleo ukachukua nafasi ya mbinu za huko nyuma.

Lakini leo hii zimwi lenye nyuso kadhaa la ukoloni, limeamua kutumia nguvu na uwezo wake wote ili kuupigisha magoti Uislamu kwa kutumia vikosi vya kijeshi, mkono wa chuma na uvamizi wa waziwazi, mlolongo wa kazi za kishetani za propaganda, maelfu ya mifumo ya uenezaji uwongo na uvumi; kuandaa makundi ya kufanya ugaidi na mauaji ya kikatili, kusambaza vitu vya kushamirisha ufuska na maovu ya kiakhlaqi; kueneza mihadarati na kuharibu azma, nyoyo na akhlaqi za vijana, kuanzisha mashambulio na hujuma za kisiasa za kila upande dhidi ya ngome za mapambano, kuamsha na kuchochea ghururi za kikaumu na taasubi za kimapote, pamoja na kuanzisha uadui baina ya ndugu wa Kiislamu. Ikiwa upendo, dhana njema na masikilizano yatatawala baina ya mataifa ya Kiislamu, madhehebu za Kiislamu na kaumu za Waislamu, badala ya dhana mbaya na kutizamana kwa jicho la uadui ambayo ndiyo matakwa ya maadui, Waislamu wataweza kuzima sehemu kubwa ya njama na mipango ya wale wasiowatakia mema, na kutibua mipango yao miovu ya kutaka kuendelea kuuweka umma wa Kiislamu chini ya udhibiti wao.

Hija ni mojawapo ya fursa bora kabisa kwa ajili ya kufikia lengo hili tukufu.
Waislamu waelewe kwamba kwa kushirikiana na kushikamana na misingi yao mikuu ya pamoja ambayo imeelezwa na Qur’an na Sunna wataweza kuwa na nguvu na uwezo wa kukabiliana na shetani hili lenye nyuso kadhaa na kulishinda kwa imani na irada zao. Iran ya Kiislamu ni mfano dhahiri wa istikama iliyofanikiwa kutokana na kushikamana kwake na mafunzo ya Imam Khomeini (MA). Wameshindwa katika Iran ya Kiislamu. Kwa miaka thelathini sasa maadui hao wanafanya njama mbali mbali dhidi ya Iran ya Kiislamu. Kuanzia kujaribu kufanya mapinduzi hadi vita vya miaka minane vya kujihami kutakatifu. Kuanzia vikwazo na kutaifisha mali hadi vita vya kisaikolojia na kipropaganda vinavyofanywa na vyombo vyao vya habari vilivyojipanga safu moja. Kuanzia njama zao za kuizuia Iran isipate maendeleo ya kisayansi na teknolojia za kisasa kama vile teknolojia ya nyuklia hadi kufanya uchochezi na kuingilia waziwazi katika masuala ya uchaguzi uliofana kabisa wa hivi karibuni nchini Iran. Lakini njama na vitimbi vyote hivyo vya maadui vimeshindwa na hivyo kuwalazimisha maadui hao wachanganyikiwe na wachukue maamuzi ya hasira na pupa. Kwa mara nyingine ile aya ya Qur’ani tukufu inayosema:
إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا
Hakika vitimbi vya shetani ni dhaifu… imethibiti kivitendo na kwa uwazi kabisa mbele ya macho ya Wairani. Katika sehemu nyingine yoyote pia, ambako istikama iliyotokana na azma na imani imewawezesha wananchi kusimama na kukabiliana na Waistikbari wenye majigambo, ushindi umewaendea waumini, na kipigo na fedheha imekuwa ndiyo hatima ya uhakika iliyowafika madhalimu. Ushindi wa dhahiri wa vita vya siku 33 nchini Lebanon na jihadi ya kujivunia na ya ushindi ya Gaza katika miaka mitatu ya hivi karibuni, ni shahidi hai wa kuthibitisha uhakika huo.

Nasaha zangu ninazozitilia mkazo kwa mahujaji wote waliopata saada , hususan maulamaa na makhatibu wa nchi za Kiislamu ambao wamehudhuria katika makutano haya matukufu, na makhatibu wa Ijumaa wa Haramain tukufu, ni kwamba wawe na uelewa sahihi wa hali halisi, na kulitambua leo hii jukumu walilo nalo linalohitaji kutekelezwa kwa haraka. Kwa uwezo wao wote wawabainishie wasikilizaji wao njama za maadui wa Uislamu, na kuwalingania watu wito wa upendo na umoja.

Wajihadhari sana na kila kinachosababisha Waislamu kudhaniana dhana mbaya; na kwa kadiri ya motisha waliyo nayo, na kwa kiasi wawezavyo kupaza sauti zao, wafanye hivyo dhidi ya Waistikbari, maadui wa umma wa Kiislamu na viranja wa fitna zote, yaani Uzayuni na Marekani na wadhihirishe kwa maneno na matendo yao kujibari na kujiweka mbali kwao na washirikina. Kwa unyenyekevu, ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atupe mimi na nyinyi nyote uongofu, taufiki, msaada na rehma Zake. Wassalaamu Alaykum
Sayyid Ali Husseini Khamenei
3 Dhilhijjatul Haram 1430 Hijria

MWISHO WA MAKALA.

————————————————————————————————————–

Wajibu Na Shuruti Za Hajj

 

Imefasiriwa na Ummu ‘Abdil-Wahaab

 

 

Allah Amewaamrisha waja Wake kuitekeleza ibada ya Hijja kwenye Nyumba Tukufu, na kuwalipa malipo mema kutokana na ibada hiyo. Yeyote mwenye kuitekeleza Hijja kwenye Nyumba hiyo (Ka’abah) na akawa hakumkaribia mkewe kwa matamanio ya nafsi yake, wala hakutenda dhambi yoyote, basi atatoka kwenye ibada hiyo hali ya kuwa hana dhambi yoyote mfano wake ni kama mtoto mchanga ambaye ndio kwanza amezaliwa na mama yake. Hijja iliyokubaliwa (Al-Hajj Al-Mabruur) malipo yake si chochote ila ni Pepo.

Enyi watu! Muogopeni Allah na jitahidini kuutekeleza wajibu wa Hijja, ambao Allah Amekuamrisheni juu yenu. Allah amesema:

((إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ))

(( فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا وَلِلّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلاً وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ الله غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ))

((Hakika Nyumba ya kwanza waliowekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka, iliyobarikiwa na yenye uongofu kwa walimwengu wote))

 

((Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi – masimamio ya Ibraahiym, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allah imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakayekanusha basi Allah si mhitaji kwa walimwengu)) [Al-‘Imraan: 96-97]

 

Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((Uislaam ni kushuhudia ya kwamba Hapana Mola anaestahiki kuabudiwa kwa haki ila Allah na Muhammad ni Mjumbe wa Allah, kusimamisha sala, kutoa Zakaah, kufunga mwezi wa Ramadhaan, na kuhiji kwenye Nyumba Tukufu kwa mwenye uwezo)) [Muslim]

Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema Uislaam umejengeka kutokana na hizi nguzo tano na endapo yoyote miongoni mwa nguzo hizi tano ikikosekana basi, Uislaam hautimii. ‘Umar Ibnul-Khattaab (Radhiya Allahu ‘anhu) amesema; “Nilikuwa karibu nitume wajumbe katika miji kuchunguza wale walio na uwezo wa kufanya Hijjah lakini hawafanyi, ili niwaamrishe walipe kodi, hao si Waislamu, hao si Waislamu”.

Wajibu wa Hijja umethibitishwa katika Kitabu cha Allah na Sunnah za Mjumbe wa Allah (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na vile vile kwenye makubaliano ya wanavyuoni wa Kiislaam. Mtu yeyote anaepinga wajibu huu, huyo hana dini, na yeyote anaeacha wajibu huu eti kwa sababu ya kutojali, japo kuwa mtu huyo anaamini, huwa yupo kwenye ukingo wa ukafiri.

Baada ya kubainisha (kuainisha) Wajibu wa Hijja, Allah Anasema

(( فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا وَلِلّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلاً وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ الله غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ))

((Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi – masimamio ya Ibraahiym, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allah imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakaye kanusha basi Allah si mhitaji kwa walimwengu)) [Al-‘Imraan: 97]

Huwaje kwa Muislamu akajihisi kasalimika hali ya kuwa kaipuuza Hijja na ilhali ana uwezo wa kuitekeleza kiafya na kifedha, na anafahamu kuwa Hijja ni wajibu, na ni moja miongoni mwa nguzo za Kiislaamu?

Huwaje kwa Muislaamu kujizuia fedha kuzitumia kwa ajili ya Hijja, na hali ya kuwa anazitumia fedha hizo kwa mambo ya anasa za kidunia?

Huwaje kwa Muislaamu akajihifadhi kutokana na uchovu wa Hijja, lakini anajitahidi kwenye mambo (ya kipuuzi) ya kidunia?

Huwaje mtu akawa mvivu katika kuitekeleza Hijja, hali ya kuwa ibada hii imeamrishwa mara moja tu katika uhai wake?

Huwaje mtu akaakhirisha kuitekeza Hijja, na ilhali hajui kuwa uhai wake utafikia angalau siku moja ijayo au la?

Hivyo, Muogopeni Allah enyi waja, na timizeni wajibu wa Hijja ambao umeamrishwa juu yenu, tekelezeni kwa dhati ya kumpenda Yeye, yakubalini maamrisho Yake na fanyeni hima na hamu ya kumtii Yeye, ikiwa nyinyi ni waumini wa kweli.  Allah Anasema:

((وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا))

((Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Allah na Mtume Wake wanapokata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Allah na Mtume Wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi)) [al-Ahzaab:36]

Ikiwa Muumini ataitekeleza ibada ya Hijja mara moja tu baada ya kufikia balegh, basi itatosheleza na atakuwa ameutimiza msingi muhimu wa Uislaamu. Hatotakiwa tena kutekeleza Hijja wala Umrah baada ya hapo, isipokuwa ikiwa kama aliweka nadhiri ya kutekeleza moja kati yake, basi atawajibika kuitekeleza nadhiri yake kama tulivyofundishwa na Mtume wetu (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth ifuatayo:

Kutoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah (Radhiya Allahu ‘anhaa kwamba Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote atakayeweka nadhiri ya kumtii Allah basi amtii. Na yeyote atakayeweka nadhiri kumuasi Allah basi asimuasi)) [Al-Bukhaariy]

Advertisements