————————————————————-

Tukio la Israa Na Mi’iraaj

Imekusanywa na Ummu ‘Abdillaah

Kutoka katika Vitabu Zaadul Ma’ad na Ar-Rahiyqul Makhtuum

Kutokana na umuhimu wa tukio hili ambalo Allaah سبحانه وتعالى Kalielezea katika Kitabu Chake Kitukufu pale Aliposema:

“Ametakasika Aliyemchukua mja Wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyouzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara Zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona” [Al-Israa: 1]

na ni Mu’ujizah mkubwa kabisa wa Nabii yetu kipenzi صلى الله عليه وآله وسلم baada ya Mu’ujizah wa Qur-aan Tukufu, kuna haja ya kukieleza tena japo kimekwishaelezwa na kuandikwa na wengi.

Tukio hili adhimu, limeelezwa na wanahistoria kwa kauli mbalimbali wakati hasa lilipotukia:

1.      Inasemekana Israa ilikuwa katika ule mwaka ambao Allaah سبحانه وتعالى Alimkirimu ndani yake Utume, Ameichagua kauli hii Atw-Twabariy.

2.    Inasemekana Israa ilikuwa baada ya kupewa Utume kwa miaka mitano, Kauli hii imepewa nguvu na Al-Nawawiy na Al-Qurtwubiy.

3.    Inasemekana Israa ilikuwa usiku wa ishirini na saba katika mwezi wa Rajab, Mwaka wa kumi wa Utume, Kauli hii imepewa nguvu na mwanachuoni mkubwa Al-Mansuur Forty.

4.    Inasemekana Israa ilikuwa kabla ya Hijra kwa miezi kumi na sita yaani katika mwezi wa Ramadhaan mnamo mwaka wa kumi na mbili wa Utume.

5.    Inasemekana Israa ilikuwa kabla ya Hijra kwa mwaka mmoja na miezi miwili yaani Muharram mnamo mwaka wa kumi na tatu wa Utume.

6.    Inasemekana Israa ilikuwa kabla ya Hijra kwa mwaka mmoja yaani Rabi’u Ath-Thaaniy mnamo mwaka wa kumi na tatu wa Utume.

Kauli tatu za mwanzo zimepingwa kwa sababu Mama wa Waumini Khadiyjah رضي الله عنها alifariki mwezi wa Ramadhaan mwaka wa kumi wa Utume na kifo chake kilitokea kabla ya kufaradhishwa kwa Swalaah tano na hakuna tofauti kuwa Swalaah tano zilifaridhishwa katika usiku wa Israa. Ama kuhusu kauli tatu zilizobaki hakikupatikana kile ambacho kingetumika kutia nguvu moja katika kauli hizo isipokuwa mtiririko wa Surat Al-Israa, Ambao unafahamisha kuwa Israa ilichelewa sana. Wanachuoni wa Hadiyth wamepokea ufafanuzi wa tukio hili na hapa chini tunauleta kwa ufupi katika maneno yafuatayo:

Ibn Al-Qayyim amesema; “Mjumbe wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم, kwa kauli sahihi, alipelekwa kimwili akiwa amempanda Buraaq, akifuatana na Jibriyl عليه السلام kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Baytul Al-Maqdis, akamfunga Buraaq katika kikuku cha mlango wa Msikiti, Na kisha kuswali pamoja na Mitume, Yeye akiwa Imaam. Baada ya hapo, usiku huo huo kutoka Baytul Al-Maqdis akapandishwa katika uwingu wa Dunia akifuatana na Jibriyl عليه السلام aliyekuwa akibisha hodi kwa ajili yake, akafunguliwa na huko akamuona Aadam عليه السلام baba wa watu wote, akamsalimia, akamkaribisha na akamjibu salaam yake na akaukubali Utume wake. Allaah سبحانه وتعالى Akamuonyesha roho za watu wema zikiwa upande wake wa kuume na roho za watu waovu zikiwa upande wake wa kushoto. Baada ya hapo akapandishwa uwingu wa pili, Jibriyl عليه السلام akaomba kuingia, akafunguliwa na hapo akamuona Yahya bin Zakariya na ‘Iysa bin Maryam عليهما السلام, akakutana nao, akawasalimia, na wao wakamjibu salaam yake, Wakamkaribisha na kisha wakaukubali Utume wake. Kisha akapandishwa mpaka uwingu wa tatu, hapo akamuona Yuusuf عليه السلام, akamsalimia, naye akamjibu salaam yake, akamkaribisha na akaukubali Utume wake. Baada ya hapo akapandishwa uwingu wa nne ambako alimkuta Idriys عليه السلام, akamsalimia, naye akamjibu salaam yake, akamkaribisha na akaukubali Utume wake. Kisha akapandishwa uwingu wa tano, Na hapo akamuona Haaruun bin ‘Imraan عليه السلام, akamsalimia, naye akajibu salaam yake na kumkaribisha na kuukubali Utume wake.

Baada ya hapo akapandishwa katika uwingu wa sita na akamkuta hapo Muusa bin Imraan عليه السلام, akamsalimia, naye akajibu salaam yake, akamkaribisha na akaukubali Utume wake. Alipompita, Muusa عليه السلام alilia na alipoulizwa ni jambo gani linalimliza? Akajibu, “Ninalia kwa sababu kijana amepewa Utume baada yangu, Na katika Ummah wake wataingia peponi kuliko watakaoingia peponi kutoka katika Ummah wangu.” Kisha akapandishwa kwenye uwingu wa saba, ambako alikutana na Ibrahiym عليه السلام, akamsalimia naye akajibu salaam yake, akamkaribisha na akaukubali Utume wake. Baada ya hapo ndipo akanyanyuliwa na kupelekwa Sidratul-Muntahaa, Kisha akanyanyuliwa hadi Baytul Ma’amuur, naye akapandishwa kupelekwa kwa Allaah Mwingi wa Utukufu, Akasogea Mtume صلى الله عليه وآله وسلم mpaka umbali wa kiasi cha masafa ya Qawsayn (pinde mbili) au karibu zaidi kuliko hivyo, Allaah سبحانه وتعالى Akayafunua kwa Mja wake yale Aliyoyafunua, Na Akamfaradhishia Swalaah Khamsini. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Akazipokea na kuanza kurejea mpaka alipofika mahali alipo Muusa عليه السلام ambaye alimuuliza; “Umepewa amri ya jambo gani? Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akamueleza, “Ameniamrisha Swalaah Khamsini”, Muusa عليه السلام akamwambia, “Kwa hakika Ummah wako hawataweza kutekeleza jambo hilo, Rejea kwa Mola wako na umuombe Akupunguzie iwe takhfifu kwa Ummah wako”. Akageuza uso na kumuangalia Jibriyl عليه السلام kwa jicho la kumtaka ushauri katika jambo hilo, naye akampa ishara ndio kama ukitaka. Akapanda naye Jibriyl عليه السلام mpaka akafika kwa Allaah سبحانه وتعالى na hali ya kuwa Yeye Yu Mahali Pake; (Tamko hili ni la Al-Bukhaariy). Katika mapokezi mengine, Akampunguzia Swalaah kumi kisha akateremshwa mpaka mahali alipokuwa Muusa عليه السلام na akamueleza idadi ya Swalaah zilizopunguzwa. Muusa عليه السلام akamwambia, “Rejea kwa Mola wako na umuombe Akupunguzie tena. “Inasemekana kuwa hakuacha kwenda na kurudi kwa Muusa عليه السلام na Allaah سبحانه وتعالى mpaka Swalaah zikabaki tano. Muusa عليه السلام akamtaka arejee kwa Allaah tena na kuomba kupunguziwa, Hapo Mtume akajibu; “Kwa hakika ninamuonea hayaa Mola wangu na sasa mimi ninaridhia na ninakubali Swalaah nilizopewa.” Alipokwenda umbali kidogo, Alilingania mlinganiaji; “Nimezipitisha faradhi Zangu na nimewapunguzia waja Wangu.”

Ibnul Qayyim amejadili kuhusu suala hili la Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kumuona Mola wake, Allaah Aliyetukuka mwenye Utukufu na kisha akayataja maneno ya Ibn Taymiyah kuhusu suala hili. Matokeo ya utafiti ni kuwa, “Kumuona Allaah سبحانه وتعالى kwa macho ni jambo ambalo halikuthibiti kabisa. Hiyo ni kauli ambayo haikusemwa na yeyote katika Maswahaba. Na kile tunachokisema kutoka kwa Ibn ‘Abbaas kuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alimuona Allaah سبحانه وتعالى moja kwa moja. Ni kuwa alimuona kwa moyo si kwa macho, Kauli ya kwanza haipingani na ya pili.” Kisha akasema: “Ama kuhusu kauli yake Allaah سبحانه وتعالى katika Suratu An-Najm (53: 8).

“Kisha akakaribia (kwa Mtume) na akateremka.”

Huko siko kule kukaribia ambako kumetajwa katika kisa cha Al-Israa, Kwani kukaribia ambako kumo katika Suratu An-Najm, “Ni kukaribia kwa Jibriyl عليه السلام na kusogea zaidi kama alivyosema Mama wa Waumini ‘Aaishahرضي الله عنها na Ibn Mas’uud رضي الله عنه. Mtiririko wa maneno unafahamisha juu ya maana haya; “Amekukaribia na kusogea sana.” Katika Hadiyth ya Al-Israa, Kuna maana kuwa kukaribia huko ni kukaribia kwa Mola Mtukufu Aliyetukuka na kuwa karibu kwake zaidi. Hakuna kupingana katika Surat An-Najm. Lakini kutajwa huko ndani yake ni kuwa yeye alimuona mara nyingine mbele ya Sidratul-Muntahaa, Na huyo ni Jibriyl عليه السلام.

Mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم alimuona Jibriyl عليه السلام katika sura yake halisi mara mbili; ya kwanza hapa duniani na mara nyingine katika Sidratul-Muntahaa na Allaah سبحانه وتعالى Ndiye Mjuzi zaidi.

Lilituka lile tukio la Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kupasuliwa tena kifua chake kwa mara ya pili. Kwa ujumla katika safari hii aliona mambo mengi; miongoni mwa hayo ni kule kuletewa maziwa na pombe na kuchagua maziwa badala ya pombe, Na pakasemwa, “Umeongozwa katika fitrah na umechagua na kupata fitrah, Ama kwa hakika laiti ungechukua pombe Ummah wako wote ungepotea, “Katika safari hiyo alionyeshwa mito minne huko peponi, Mito miwili iko nje na mito miwili iko ndani. Mito miwili iliyo nje ni mito ya Nail (Nile) na Furaat (Euphrates), Na maana ya mambo hayo ni kuwa ujumbe wake utafanya makazi yake katika majanga yenye rutuba katika Nail na Furaat na  watu wake ndio watakaokuwa wasimamizi wa da’awah ya Kiislaam, Kizazi baada ya kizazi, na si kuwa maji ya mito miwili hiyo yanachimbuka kutoka peponi.

Alionyeshwa Malaika muangalizi wa moto wa Jahannam ambaye hacheki, mwenye uso usio na furaha wala bashasha. Alionyeshwa pepo na moto. Alionyeshwa walaji wa mali za yatima kwa dhulma, Waliokuwa na midomo kama ya ngamia, Wanatupiwa midomoni mwao vipande vya moto kama mawe na kisha kutolewa katika tupu zao za nyuma.

Alionyeshwa walaji wa ribaa waliokuwa na matumbo makubwa yaliyowafanya wasiweze hata kuondoka mahala walipokuwepo. Alipita na kuwaona watu wa Fir’awn wakionyeshwa moto na hali wakipita wakiukanyaga.

Alionyeshwa wazinifu, Mbele yao kulikuwa na nyama iliyonona vizuri na pembeni mwao kulikuwa na nyama duni iliyooza yenye uvundo. Wakawa wanakula ile nyama duni iliyooza yenye uvundo, na wanaiacha ile nzuri iliyonona. Alionyeshwa wanawake wanaonasibisha waume zao watoto ambao si wao (watoto wa zinaa) hawa walikuwa wametundikwa kwa matiti yao. Na aliona msafara wa kibiashara wa watu wa Makkah wakati wa kwenda na wakati wa kurudi kwake, Na aliwafahamisha watu hao juu ya ngamia aliyewatoroka na alikunywa maji yao yaliyokuwa yamefunikwa na hali ya kuwa wao wamelala na kisha akakiacha chombo kikiwa kimefunikwa na jambo hilo ndilo likaja kuwa dalili (hoja) ukweli wa madai yake asubuhi ya usiku wa Israa.

Ibnul Qayyim alisema. “Kulipopambazuka Mjumbe wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم akiwa kwa jamaa zake aliwaeleza yote Aliyoonyeshwa na Allaah Mtukufu Mwenye Kushinda, Miongoni mwa miujiza Yake mikubwa. Makuraishi walipinga na hawakutaka kabisa kuamini khabari hizo. Katika kutafuta ukweli wa maelezo yake walimtaka awaeleze ulivyo Msikiti wa Baytul Al-Muqaddas. Kwa uwezo wake Allaah سبحانه وتعالى Akamdhihirishia hiyo Baytul Al-Muqaddas machoni mwake, akawa anawaelezea alama zake moja baada ya nyingine na wakashindwa kukanusha kwa vile alikuwa akiwaambia ukweli. Mwisho akawaeleza kuhusu ule msafara wa wafanyabiashara aliokutana nao wakati wa kwenda na kurudi; akawaeleza ni lini msafara huo unategemea kufika; akawaeleza kuhusu ngamia aliyeuongoza msafara huo, Na mambo yakatokea kama alivyowaeleza. Hata baada ya kujulishwa yote hayo Ma-Quraysh walizidi kukanusha na kukufuru. Abu Bakr رضي الله عنه ameitwa “Swiddiyq” ‘Msadikishaji’ kwa sababu ya kulisadikisha tukio hili.

Yapo maelezo mafupi na marefu yaliyokuja katika kueleza sababu ya safari hii. Ipo pia kauli ya Allaah سبحانه وتعالى Mwenyewe inatosha kabisa kueleza sababu ya safari hii, Pale Aliposema:

“Ili Tumuonyeshe baadhi ya alama Zetu” (17:1).

Na huu ni utaratibu wa Allaah سبحانه وتعالى kwa Mitume, Pahala pengine ndani ya Qur-aan Anasema:

“Na namna hivi Tulimuonyesha Ibraahiym ufalme wa mbingu na ardhi (kuwa ni wa Mungu), Na ili awe miongoni mwa wenye yaqini.” [Al-An’aam: 75].

Na Alisema kumwambia Muusa عليه السلام:

“Tukuonyeshe miujiza (mingine) mikubwa mikubwa.” [Twaahaa: 23].

Na ameweka wazi makusudi ya huko kuonyeshwa, “Ili awe ni miongoni mwa wenye yaqini.” Kwa hivyo ni wazi basi kuwa elimu ya Mitume katika kumjua Mola wao inatokana na kuiona kwa macho miujiza Yake na kwa njia hiyo kuwa na yaqini na Allaah سبحانه وتعالى kwa kiasi kisichokuwa na mfano. Ni ukweli ulio wazi kuwa jambo la kujionea si sawa na la kusikia, Na hii ndio sababu Mitume عليهما السلام walivumilia mengi katika njia ya Allaah سبحانه وتعالى mambo ambayo si rahisi kuvumiliwa na watu wa kawaida. Nguvu zote za kidunia mbele ya Mitume ni kama ubawa wa mbu hawatishiki nazo hata chembe, Hata wanapofanyiwa vitimbi na wakati mwingine kuteswa.

Bila shaka msomaji ataona kuwa katika suratul Israa Allaah سبحانه وتعالى Amekitaja kisa cha Al-Israa katika Aayah moja tu, Kisha Akaingia katika kutaja fedheha za Mayahudi na maovu yao, Na kisha Akawazindua kwa kuwaeleza kuwa hii Qur-aan inaongoza kwenye mambo yanayohitaji misimamo madhubuti kabisa. Inawezekana msomaji akadhania hizi Aayah mbili hazina uhusiano wowote, Jambo hili si kweli, maana kwa maneno haya Allaah Mtukufu Anaashiria kuwa kwa hakika Israa ni tukio lilitokea Baytul Al-Maqdis na kuwa Mayahudi watanyang’anywa cheo cha kuwaongoza wanaadamu kutokana na matendo yao maovu ambayo wameyafanya. Matendo ambayo hayakubakisha nafasi ya wao kubakia katika cheo hicho na kuwa Allaah سبحانه وتعالى Atakihamisha cheo hicho kwa vitendo na kumkabidhi Mjumbe Wake Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم ambaye atamkusanyia vituo viwili vikuu vya Da’awah ya Ibrahiym عليه السلام. Wakati umefika wa kuhamishwa kwa uongozi wa kiroho kutoka Ummah ulioijaza historia yake kwa udanganyifu, Khiyana, Madhambi na uadui kwenda katika ummah mwingine utakaoaminika kwa wema na kheri. Mtume wa Ummah huo hakuacha kuwa anayesifika na wahyi wa Qur-aan inayoongoza kwenye msimamo ulio sahihi.

Kwa vipi utahama uongozi huu hali ya kuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم anazunguka katika majabali ya Makkah hali ya kuwa ni mwenye kufukuzwana kupigwa na watu wa kabila lake? Suala hili linaibua ukweli mwingine ambao ni kuwa mzunguko wa kwanza katika Da’awah hii ya Kiislaam umekaribia kufika mwisho na kukamilika, Na baada ya hapo utaanza mzunguko wa kwanza katika mapito yake. Kwa sababu hiyo ndio maana tunaona kuwa baadhi Aayah zinakusanya mambo yanayohusu makhofisho ya wazi na makemeo ya kutisha dhidi ya Mushirikina.

“Na pindi tukitaka kuuteketeza mji huwaamrisha wale wenye starehe na taanusi, lakini wao huendelea kutenda maovu humo. Basi hapo kauli huthibiti juu ya mji huo, nasi tukauangamiza kwa maangamizo makubwa.

“Na kaumu ngapi tumeziangamiza baada ya Nuuhu! Na Mola wako Mlezi anatosha kabisa kuwa ni Mwenye kuzijua na kuziona dhambi za waja Wake.” [Al-Israa: 16-17].

Pamoja na Aayah hizi zipo nyingine zilizowaweka wazi Waislaam na zinazoendelea kuwawekea misingi ya maendeleo na kanuni zake na vyanzo vyake ambavyo hujenga jamii ya Kiislaam. Kama vile tayari wamekwishafika kwenye ardhi iliyo tayari, waliyapanga vizuri mambo yao kwa pande zote na wakaunda umoja wenye mshikamano madhubuti.

Katika jamii yao, hali kadhalika kulikuwepo na Ishara ya kuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم atapata makimbilio na mahali pa amani ambako yatatulizana mambo yake na makimbilio hayo ndiyo yangekuwa kituo cha wito wake katika pande zote za dunia. Hii ni moja ya siri miongoni mwa siri za safari hii yenye kubarikiwa.

Tukio hili, ambalo kwa Muislam mwenye Iymaan barabara, hata kama lisingelikuwepo, Iymaan yake bado ingekuwa imara vilevile, ni tukio la kihistoria lenye kuzidisha kuujua uwezo wa Allaah سبحانه وتعالى na Utukufu Wake mkubwa usio na mithali. Ni tukio lenye mafunzo mengi ya kiimani na kiitikadi; ndani yake tumeona kumepatikana faradhi ya Swalaah, kumejulikana adhabu mbalimbali za matendo maovu ya hapa ulimwenguni, na hilo litaweza kutusaidia sana sisi kujiepusha na maovu hayo ili tusiishie kutumbukia ndani ya adhabu hizo kali. Tumeona utukufu na uzito wa Maswahaba kama Abu Bakr رضي الله عنه, na imetuzidishia heshima kubwa juu ya watukufu hao na kujua nafasi yao kubwa katika moyo wa mbora wa viumbe, kipenzi wa macho yetu, Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم. Tuchukue mazingatio yanayopatikana humo na kuyafanyia kazi katika maisha yetu na si tukio hili liwe la kuhadithiwa tu na watu kukusanyana kukisherehekea inapofika mwezi wa Rajab ambao kama tulivyoona mwanzoni kuna utata wa tukio hilo kuwa katika mwezi huo

—————————————————————–

Mjue Mtume Wako صلى الله عليه وآله وسلم Vizuri Uzidi Kumpenda

بسم الله الرحمن الرحيم

www.alhidaaya.com

BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa  aalihi wa aswhaabihil Kiraam, wa ba’ad,

Tumeona juhudi nyingi zinazofanywa na makafiri katika nyakati mbalimbali za kumtia kasoro na kumdhalilisha Mtume wetu mpenzi صلى الله عليه وآله وسلم bila shaka Muislamu yeyote anaathirika sana na kupata machungu na maudhi ya kutukanwa kipenzi chetu. Pamoja na kuwa mashambulizi ya kumtia dosari yamefanywa na yanaendelea kufanywa kila kukicha, lakini kila mashambulizi hayo yanapotokea, ndipo hisia na mapenzi ya Waislam wengi yanapofumuka zaidi na kuimarika kwa kipenzi chao Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم .

Matukio ya kutukanwa Mtume wetu na kudhalilishwa na kutuhumiwa, hayakuanza leo na hayakuanza kwake, ni kama vile wakati aliposingiziwa Mama wa Waumini ‘Aaishah رضي الله عنها na wanafiki wa Madiynah wakiongozwa na ‘Abdullaah bin Saluul aliyemsingizia uovu Mama wa Waumini ‘Aaishah رضي الله عنها katika kisa cha Ifk (uzushi/uongo) ambacho kilisababisha kuteremshwa Aayah tukufu za kumsafisha na uzushi huo muovu kuwa ametembea na Swahaba Swafwaan bin Al-Mu’attwal. Na hizo aya tokea siku zilizoteremshwa zama hizo zinasomwa hadi  leo, na zitaendelea kusomwa kila mahali, Misikitini, nyumbani, nyoyoni mwa Waislamu mpaka siku ya Qiyaamah kumsafisha Bibi ‘Aaishah Mama wa Waumini katika sifa chafu na ovu aliyozuliwa nayo na ambayo hadi sasa kuna wengi bado wanamtukana na hali wanadai wao ni Waislam. Katika tukio hilo Allaah سبحانه وتعالى Anasema:

((إِنَّ الَّذِينَ جَاؤُوا بِالْإِفْكِ عُصْبَةٌ مِّنكُمْ لَا تَحْسَبُوهُ شَرًّا لَّكُم بَلْ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُم مَّا اكْتَسَبَ مِنَ الْإِثْمِ وَالَّذِي تَوَلَّى كِبْرَهُ مِنْهُمْ لَهُ عَذَابٌ عَظِيمٌ))

((Hakika wale walioleta uongo ni kundi miongoni mwenu. Msifikiri ni shari kwenu, bali hiyo ni kheri kwenu. Kila mtu katika wao atapata aliyoyachuma katika madhambi. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao, atapata adhabu kubwa)) [An-Nuur: 11]

Kutokana na mafundisho hayo tuliyoyapata kutokana na kisa cha kusingiziwa mama wa waumini, nasi tunaamini kuwa kumepatikana kheri mbalimbali kwa tukio hili la kudhalilishwa Mtume wetu mpenzi صلى الله عليه وآله وسلم. Tumeona jinsi Waislam walivyoungana katika tumkio hilo na kugomea kununua bidhaa za hao Makafiri na pia kuandamana, kuandika barua kwa viongozi wao na mengi mengine ambayo yamesababisha khasara kubwa za mali kwa hao makafiri na pia kusheheneza khofu katika nafsi zao hadi sasa hivi wanatapatapa hawajui la kufanya! Na hayo ndiyo mapenzi ya dhati na umoja wa kweli. Hakika kwa uchache tumeonyesha jinsi tunavyompenda kipenzi chetu na jinsi tunavyoithamini dini yetu. Na bila shaka kungepatikana khasara kubwa kwa hao makafiri kama viongozi wa nchi za Waislam wangekuwa na misimamo thabiti na mikali zaidi katika tukio hili! Basi na tuzidi kumtambua huyu kiumbe bora kabisa umuhimu wake kwetu, tabia zake na wema wake ili tuzidi kuongeza mapenzi yetu kwake.

Hakuna sentensi itakayoweza kuelezea mema aliyokuja nayo Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na nafasi yake katika ulimwengu huu na athari zake ambazo hazitoweza kufutika hadi siku ya mwisho.

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:

((لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ))

((Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anayemtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho)) [Al-Ahzaab: 21]

UMUHIMU WAKE KWETU

1.     Mtume wa mwisho Waislamu tunaamini mitume yote walioletwa kabla na ujumbe wa Allaah سبحانه وتعالى tokea Adam عليه السلام hadi ‘Iysa عليه السلام kisha ndio Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ambaye katumwa kwa ajili ya Umma huu wa Kiislamu tunaojifakharia nao. Hakuna tena baada yeye Mtume mwingine atakayekuja hadi siku ya Qiyaamah, na Qur-aan ndio kitabu cha mwisho kabisa ambacho kimekamilisha vitabu vyote vya nyuma vilivyoteremshwa mbinguni na Mitume yake.

2.    Wa kwanza atakayefufuliwa kutoka kaburini siku ya Qiyaamah.

3.    Wa kwanza atakayevuka As-Swiraat.

4.    Wa kwanza atakayeingia peponi na sisi Umma wake tutafuatia kabla ya Umma nyingine zote.

5.    Ameletwa kama ni Rahma kwa ulimwengu wote.

6.    Hatajwi jina lake ila anaswaliwa (anaombewa rahma).

7.    Swalah zetu hazitimii ila baada ya kumtaja yeye kwa kumswalia.

8.    Amekuja na miujiza mikubwa, kama Qur-aan, Israa Wal-Mi’iraaj na miujiza mingi mingine tunayoisoma katika Siyrah yake.

9.    Imaam wa Mitume yote.

10.           Amefutiwa madhambi yake yote yaliyotangulia na ya mbele yake.

11.           Ni Mtume pekee atakayeweza kutuombea siku ya Qiyaamah. Atakapokuwa amesujudu chini ya ‘Arshi Ataambiwa: “Ewe Muhammad! Inua kichwa chako na omba unalotaka utapewa”. Atasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم “Umma wangu, Umma wangu, Ewe Mola Umma wangu”

.

12.           Allaah سبحانه وتعالى na Malaika Wake wanamswalia.

13.           Kumuona kwake katika ndoto ni kumuona hakika.

14.           Baina ya nyumba yake na Minbar yake ni kipande cha pepo ‘Rawdhatul-Jannah’.

15.           Amepewa Al-Kawthar (Mto wa peponi).

16.           Aliyepata wafuasi wengi kuliko Mitume yote mingine.

17.           Kiumbe bora kabisa na bwana wa mwanzo na wa mwisho.

18.           Kwa sababu ya heshima kubwa Aliyopewa na Allaah سبحانه وتعالى ni Mtume pekee asiyetajwa au kuitwa kwa jina lake katika Qur-aan, wengine wote wametajwa au kuitwa kwa majina yao.

19.           Amepewa wasila na fadhila na makazi matukufu Peponi.

20.           Siku ya Qiyaamah, watakapokanusha watu wa Mitume ya nyuma kuwa Mitume yao hawakuwafikishia ujumbe, Umma wake Mtume صلى الله عليه وآله وسلم (Sisi Waislamu) utashuhudia  kuwa Mitume wamefikisha ujumbe wao kutokana na dalili tuliyoipata katika Qur-aan.

TABIA ZAKE

Na si mwengine aliyemsifia kiumbe hiki bali ni Mwenyewe Mola Mtukufu Muumba wa mbingu na ardhi kwa kusema:

((وَإِنَّكَ لَعَلى خُلُقٍ عَظِيمٍ))

((Na hakika wewe una tabia tukufu)) [Al-Qalam: 4]

Swahaba Sa’ad bin Hishaam alipomuuliza Mama wa Waumini ‘Aaishah رضي الله  عنها kuhusu tabia yake Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alijibu:

كان خلقه القرآن. ألست تقرأ القرآن (( وَإِنَّكَ لَعَلى خُلُقٍ عَظِيمٍ )) أبي داود والنسائي

Tabia yake ilikuwa ni Qur-aan, kwani husomi katika Qur-aan ((Na hakika wewe una tabia tukufu?)) [Abu Daawuud na An-Nasaaiy]

Jina lake pekee linatosha kuelezea tabia zake kwani Muhammad maana yake ni “Mwenye kusifiwa”.

Kwa hiyo bila shaka anamiliki tabia njema zilizokamilika ambazo hakuna mtu yeyote mwingine aliyemiliki, ni cheo cha daraja ya juu kabisa hakuna atakayeweza kufikia.

Khuluqa yake ya mwanzo iliyojulikana kabla ya kupewa utume ni ukweli na uaminifu hata akapewa jina na kujulikana kwa kuitwa ‘Asswaadiqul-Amiyn’ (Mkweli Muaminifu).

Alikuwa mpole, mwenye huruma kwa kila mtu hata kwa walio dhaifu kama masikini. Upole wake haukuwa kwa binaadamu tu bali hata kwa wanyama. Alikuwa mwenye bashasha, mkarimu, mvumilivu wa maudhi yanayomfika, alipokuwa akinyanyaswa alikuwa mwepesi wa kusamehe hata kama ni kutoka kwa mtu mjeuri kabisa na ingawa alikuwa ana uwezo wa kulipiza.

Hajapata hata siku moja kutukana au kutamka maneno mabaya. Mazungumzo yake yote yalikuwa ni ya maana yenye kufahamika.

Ni mwenye heshima, mwenye haya, hata ilibidi wakati mwingine kwa shida ya haya zake ilibidi Allaah سبحانه وتعالى Amsemee badala yake, kama siku ya harusi yake na Bibi Zaynab bint Jahsh wakati Maswahaba walibakia kuzungumza baada ya karamu naye alikuwa anataka kupumzika na mkewe:

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتَ النَّبِيِّ إِلَّا أَن يُؤْذَنَ لَكُمْ إِلَى طَعَامٍ غَيْرَ نَاظِرِينَ إِنَاهُ وَلَكِنْ إِذَا دُعِيتُمْ فَادْخُلُوا فَإِذَا طَعِمْتُمْ فَانتَشِرُوا وَلَا مُسْتَأْنِسِينَ لِحَدِيثٍ إِنَّ ذَلِكُمْ كَانَ يُؤْذِي النَّبِيَّ فَيَسْتَحْيِي مِنكُمْ وَاللَّهُ لَا يَسْتَحْيِي مِنَ الْحَقِّ))

((Enyi mlioamini! Msiingie nyumba za Nabii ila mpewe ruhusa kwenda kula, sio kungojea kiwive. Lakini mtakapoitwa basi ingieni, na mkisha kula tawanyikeni, wala msiweke mazungumzo. Hakika hayo yanamuudhi Nabii naye anakustahini, lakini Mwenyezi Mungu Hastahi kwa jambo la haki)) [Al-Ahzaab: 53]

UNYENYEKEVU WAKE

Alikuwa mnyenyekevu kabisa, akichanganyika na kila mtu akiwa Mwarabu au kabila lolote ikiwa ni mweupe au mweusi akiwa ni tajiri au masikini, watu wazima au watoto, hata watoto alikuwa akiwasikiliza na kuzungumza nao. Akicheza na vijukuu vyake na kuwaachia hata wakati akiswali wakimpandia juu ya mgongo wake.

Hakuwa akivaa nguo za fakhari za kumtambulisha utukufu wake au kumtofautisha na Maswahaba zake, wala hakuwa anaishi katika nyumba ya fakhari, wala kumiliki fenicha au vitu vya fakhari. Kitanda chake kilikuwa cha kamba.

Hakuwa na matamanio ya dunia, alikinaika nayo. Hima yake kubwa ilikuwa ni akhera tu. Siku moja aliingia ‘Umar رضي الله عنه nyumbani kwake akasema ‘Umar: “Sikuona chochote cha kutazama” nikasema: “Muombe Mola wako kwani Allaah Amewafungulia wafursi na warumi na Amewapa dunia (mali) na wao hawamuabudu Allaah”. Akasema:

((Una shaka ewe Ibnul-Khatwaab, hao ni watu waliotanguliza mapambo katika maisha yao ya dunia)).

Pia alikuwa akisema:

((ما لي وللدنيا، ما أنا في الدنيا إلا كراكب استظل تحت شجرة، ثم راح وتركها)) صحيح سنن الترمذي

((Mimi na dunia ni wapi na wapi? Mimi si katika dunia ila kama mfano msafiri aliyepumzika chini ya mti, kisha akaondoka na kuuacha)) [Sunan At-Tirmidhiy].

Nyumbani kwake ilikuwa inawezekana kupita siku tatu bila ya moto wa kupikia chakula kuwashwa, ilikuwa ni kula tende na maji tu.

Alikuwa akitoa sadaka bila ya kukhofu umasikini, hata alipofariki hakuwa na chochote cha kumiliki wala dirham wala dinaar [Al-Bukhaariy]

Hakujiona kuwa ni mtu bora kuliko Maswahaba na juu ya kwamba ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikuwa haamui jambo peke yake bila ya kuchukua ushauri kwa Maswahaba zake.

UHUSIANO WAKE NA WATU WA NYUMBANI KWAKE

Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa ni mpole kwa ahli zake na  akimpa kila mmoja haki yake. Anapokuwa na wake zake hukaa nao na kuzungumza nao na kucheka nao, akicheza na mkewe Bibi ‘Aishah رضي الله عنها kama wakati mmoja alifanya naye mashindano ya kukimbia, mara nyingine alimbeba mgongoni ili atazame wanaume waliokuwa wakicheza mchezo wa vita msikitini.  Unapofika wakati wa Swalah huondoka ili kutimiza ibada hivyo kumpa Mola wake haki Yake, na alikuwa akimpa kila mtu haki yake.

Hakuwa mwenye makuu katika chakula, akila chochote alichopikiwa bila ya kulalamika.

Akisaidia kazi za nyumba kama kufagia na usafi mwingine. Hata na mfanya kazi wake alikaa naye kwa vizuri wala hakuwahi kumkaripia hata siku moja.

HEKIMA ZAKE

Alikuwa mwenye hikma katika kila hali. Anapokabiliwa na mambo mawili alikuwa akichagua lile lililokuwa jepesi maadam tu halikuvuka mipaka ya Allaah سبحانه وتعالى.

Hakujali kutoa hukumu kwa mtu yeyote hata kama ni mwanawe mpenzi maadam ni mkosa, alisema:

((والذي نفس محمد بيده ، لو أن فاطمة بنت محمد سرقت لقطعت يدها)) البخاري

((Naapa kwa Yule Ambaye Nafsi ya Muhammad iko katika mikono yake (Allaah)! Ikiwa Faatimah mtoto wa Muhammad ameiba basi nitamkata mkono wake)) [Al-Bukhaariy]

Bedui mmoja alikwenda msikitini akasimama kukojoa, Maswahaba walitaka kumkatiza na walikuwa tayari kumvamia, lakini Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliwakataza na akamuacha amalize haja yake, alipomaliza Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alimuambia:

((إن هذه المساجد لا تصلح لشيء من هذا البول ولا القذر، إنما هي لذكر الله وقراءة القرآن)) رواه مسلم

((Msikiti huu haufai kukojolewa au kuchafuliwa bali ni kwa ajili ya kumkumbuka Allaah na kusoma Qur-aan)) [Muslim]

Maelezo hayo ni mtazamo mdogo tu kutoka katika mwanga mkubwa wa utume wake Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم. Lau kama ni kuelezea yote basi ingelihitaji vitabu na vitabu kuandikwa. Na sio sisi tu Waislamu tuliyemtambua kwa tabia zake hizo bali hata makafiri wangapi waliosoma wasifu wake Mtume صلى الله عليه وآله وسلم walikubali kuwa hakika Muhammad alikuwa ni bwana wa tabia na ni mtu wa aina ya pekee aliyekamilika kwa kila upande wa sifa.

Tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atuzidishie mapenzi kwa Mtume wetu صلى الله عليه وآله وسلم na tuwe wenye kufuata tabia na nyendo zake hata tuweze kuwa karibu naye Peponi kama alivyosema mwenyewe:

عن جابر رضي اللَّه عنه أَن رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : (( إِن مِنْ أَحَبِّكُم إِليَّ ، وَأَقْرَبِكُمْ مِنِّي مَجلساً يَومَ القِيَامَةِ ، أَحَاسِنَكُم أَخلاقا)(( الترمذي حديث حسن

Imetoka kwa Jaabir رضي اللَّه عنه kwamba Mtumeصلى الله عليه وآله وسلم amesema: (Hakika walio vipenzi kwangu na watakaokuwa karibu na mimi siku ya Qiyaamah ni wale wenye tabia njema)) [At-Tirmidhiy – Hadiyth Hasan]

————————————————-

Kumpenda Kikweli Mtume (صلي الله عليه وسلم)

بسم الله الرحمن الرحيم

Shams Elmi (Abu ‘Ilmi)

Leo InshaAllaah tutaangalia mada ya kumpenda Mtume (صلي الله عليه وسلم) kutokana na umuhimu wake katika kukamilisha imani ya mja, na kutokana na kutofahamika vyema maana halisi ya kumpenda Mtume (صلي الله عليه وسلم) kwa Waislamu walio wengi.

Neno محبة ni neno la Kiarabu kilugha lina maana ya; Hisia za kumili kwa moyo. Na katika Sheria, ni kumili kwa moyo kunako ambatana na kiwiliwili, hisia, akili, matakwa, na matendo ya moyo yanayothibitishwa na matendo ya viungo. Na hiyo ndio Imani.

Imani kwa mtazamo wa Ahlus Sunnah wal Jama’ah ni kauli na matendo, yaani kauli ya moyo na ulimi, na matendo ya moyo na viungo. Kwa maana hii ya kisheria, mapenzi huwa na uhusiano moja kwa moja na Imani ya mtu.

Lakini kama mtu atatafsiri mapenzi kwa maana ile ya kilugha, yaani kumili kwa hisia za moyo tu, mapenzi ya mtu huyu yatakuwa na dosari kubwa, na yatakuwa yanahukumiwa na matamanio zaidi kuliko Imani, na huu ndio mtihani uliowasibu wengi katika Ummah wetu, wa kutotofautisha baina ya mapenzi ya kiimani, na mapenzi ya kumili kwa hisia za nyoyo.

Mtu anaweza kumpenda mtu mwengine kwa hisia hizo za kumili kutokana na vigezo vyake, lakini akawa bado anatofautiana naye katika mambo mengi, na wakati mwingine hakubaliani nae katika mitazamo yake na kauli zake, lakini bado moyo wake ukawa unamili kwa mtu huyo, tafsiri kama hii ya mapenzi ndio iliyowapotosha wengi miongoni mwa Waislamu kwa kudhani kuwa mapenzi ya aina hii, ni mapenzi yenye uhusiano na Imani.

Moja miongoni mwa misingi mikuu ya Imani ya Dini yetu ni kumpenda mtume wetu Muhammad (صلي الله عليه وسلم) kuliko tunavyozipenda nafsi zetu na ukimuuliza Muislamu yeyote duniani atakuthibitishia mapenzi makubwa aliyonayo kwa kipenzi chetu Mtume Muhammad (صلي الله عليه وسلم), lakini tunatofautiana katika uelewa wa jinsi ya kumpenda Mtume (صلي الله عليه وسلم) kwa mujibu wa tafsiri tulizozitaja hapo juu.

Wapo miongoni mwetu ambao ukimtaja tu Mtume (صلي الله عليه وسلم) anaweza kububujikwa na machozi kwa hisia kali alizonazo juu ya Mtume wetu (صلي الله عليه وسلم), mwengine atatoa sauti kali ya kumtakia rehma na amani Mtume (صلي الله عليه وسلم) kwa kusema kwa vishindo ‘Allaahumma salim alee’, au wengineo waliozuka siku hizi na kuleta itikadi yao ya kutukana Maswahaba, utawakuta anapotajwa Mtume, huitikia kwa vishindo ‘Allaaaahumma Swaliii ‘alaa Muhammad wa aaaali Muhammad’ lakini ndio hao hao wanautukana wake zake na Maswahaba zake!! Na si ajabu ukawakuta watu hao pamoja na mapenzi makubwa wanayoyaonyesha kwa Mtume (صلي الله عليه وسلم) hawatimizi Swalah tano kwa siku, wake zao na mabinti zao hawajisitiri, wana vimada nje, nyumba zao zimejaa taarabu za rusha roho, zimepambwa na vinyago na mapicha, wavuta sigara, wala mirungi, wakaa mabarazani kusengenya, panapoaziniwa na kukimiwa hawasimami kwenda kuswali na Waislam,  achilia mbali kupuuza kwao baadhi ya Sunnah muhimu kama vile kufuga ndevu n.k. Watu hawa wana mapenzi makubwa kwa Mtume (صلي الله عليه وسلم) lakini ni mapenzi ya aina gani ? je, haya ndio mapenzi ya kiimani?

Neno mapenzi katika Uislamu lina maana nzito sana, haifai kulichukulia kwa maana nyepesi nyepesi kwani lina uhusiano mkubwa na ‘Aqiydah ya Dini yetu; Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema katika Qur-aan:

(ومن الناس من يتخذ من دون اللــه أندادا يحبونهم كحب اللــه والذين آمنوا أشد حبا للــه) البقرة 165

“Na katika watu kuna wanaofanya waungu wasiyekuwa Mwenyezi Mungu, wanawapenda kama kumpenda, lakini walioamini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana.” 2:165

Kumpenda Allaah (سبحانه وتعالى) ni katika alama za Tawhiyd, kama ilivyobainisha Aayah, na kumpenda Allaah (سبحانه وتعالى) ndio msingi wa kumpenda Mtume (صلي الله عليه وسلم), huwezi kumpenda Mtume kabla hujatimiza mapenzi ya Allaah (سبحانه وتعالى) na huwezi kumpenda Allaah kwa kumkwepa Mtume (صلي الله عليه وسلم).

VIGEZO VYA KUMPENDA MTUME (صلي الله عليه وسلم)

1. KUTHIBITISHA SHAHADA YA UTUME WAKE

Ni kuthibitisha utume wa Mtume Muhammad (صلي الله عليه وسلم) kuwa ni mjumbe aliyetumwa kwa waja wote, kuthibisha kivitendo yote aliyoyaamrisha, na kujiepusha na yote aliyoyakataza na kuyakemea, kwa maana nyingine ni kumuabudu Allaah (سبحانه وتعالى) kama Alivyofundisha na kuelekeza Mtume, na Allaah Anathibitisha hayo kwa kusema:

(قل إن كنتم تحبون اللــه فاتبعوني يحببكم اللــه ويغفر لكم ذنوبكم واللـه غفور رحيم) العمران 31

“Sema, ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni, Mwenyezi Mungu Atakupendeni na Atakughufirieni madhambi yenu” 3:31

Allaah Anathibitisha kuwa, ili mja awe na Tawhiyd iliyokamilika ya kumpenda Allaah, basi ni lazima amfuate Mtume Muhammad (صلي الله عليه وسلم) na ndio kisha Allaah Atampenda mja huyo na kumsamehe. Hivyo basi, mapenzi ya kweli yanakuwa kwa kumfuata Mtume (صلي الله عليه وسلم) katika yote aliyokuja nayo na kumtii na ndipo Allaah Atampenda mja huyo, na atakayebahatika kupendwa na Allaah (سبحانه وتعالى) hakika huyo amefaulu kufaulu kulikokuwa kukubwa.

2. KUMUIGA MTUME (صلي الله عليه وسلم)

Mapenzi ya kweli ya Mtume (صلي الله عليه وسلم) yanakuwa ni kwa kumuiga kwa yote aliyokuja nayo, kumuiga katika tabia zake, katika maisha yake, katika nyumba yake, katika ibada zake, katika mahusiano yake na majirani, na katika maisha yake kwa ujumla, kama alivyotuambia Allaah (سبحانه وتعالى)

لقد كان لكم في رسول اللــه أسوة حسنة لمن كان يرجو اللــه واليوم الآخر وذكر اللــه كثيرا) الأحزاب 21

“Bila shaka mnao mfano mwema kwa mtume wa Mwenyezi Mungu kwa mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na kumtaja Mwenyezi Mungu sana.” 33:21

Kumuiga Mtume na kumfanya kuwa ruwaza njema ndio mapenzi ya dhati ya kumpenda Mtume (صلي الله عليه وسلم), lakini kumpenda mtume kwa kumsifu tu, na akawa hana nafasi katika maisha yako na maisha ya familia yako, basi huko si kumpenda bali ni kujifanya kumpenda na inawezekana ikawa ni kumcheza shere.

Katika Hadiyth iliyopokelewa na ‘Abdu-Rahmaan bin Quraad (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa “Mtume (صلي الله عليه وسلم) alikuwa anatawadha, na Maswahaba wakaanza kukinga maji yaliyokuwa yanatiririka kutoka katika wudhuu wa Mtume (صلي الله عليه وسلم) na wakijifutia katika miili yao kutafuta baraka za wudhuu ule kutoka kwa Mtume, Mtume (صلي الله عليه وسلم) akawauliza; “kwa nini mnafanya hivi? Wakasema; ni kwa ajili ya kumpenda Allaah na Mtume Wake, Mtume (صلي الله عليه وسلم) akawaambia, anayetaka kumpenda Allaah na Mtume Wake, au kupendwa na Allaah na Mtume Wake, basi aseme ukweli anapozungumza, na atekeleze amana yake anapoaminiwa, na awe jirani mwema kwa jirani yake” Al –Albaaniy ‘Mishkaatul Maswaabiyh

Mtume (صلي الله عليه وسلم) anawaelekeza Maswahaba zake, na ndio anatuelekeza sisi jinsi ya kumpenda mapenzi ya kweli, mapenzi yenye tija na yenye kuleta mabadiliko katika tabia za mja, Mtume alikuwa anawaelekeza Maswahaba kuwa kumpenda kwa kugombea maji yake ya wudhuu peke yake ili kupata baraka, hakutoshi, na kutakuwa hamna maana kama watu hao watakuwa waongo katika mazungumzo yao, hawatekelezi amana zao, wanaudhi majirani zao, mapenzi hayo ya kutafuta baraka tu na kuacha kumfuata Mtume (صلي الله عليه وسلم) yatakuwa ni mapenzi ya kumcheza shere Mtume (صلي الله عليه وسلم).

3. KUMFANYA HAKIMU KATIKA MIZOZO YOTE

Na katika dalili za kumpenda Mtume (صلي الله عليه وسلم) ni kumfanya hakimu katika mizozo yetu yote, na kuridhika na hukmu yake, na katika zama tulizonazo ambazo Mtume (صلي الله عليه وسلم) hayupo nasi, basi Qur-aan na Sunnah zake ndizo zitakazotumika katika kutatua mizozo yetu, na Allaah (سبحانه وتعالى) anatuambia katika Qur-aan:

(فلا وربك لا يؤمنون حتى يحكموك فيما شجر بينهم ثم لا يجدوا في أنفسهم حرجا مما قضيت ويسلموا تسليم) النساء 65

“Naapa kwa (haki ya) Mola wako. Wao hawawi wenye kuamini (kweli kweli) mpaka wakufanye hakimu katika yale wanayokhitalifiana, kisha wasione uzito nyoyoni mwao juu ya hukumu uliyotoa, na wanyenyekee kabisa” 4:65

Katika kutafsiri Aayah hii, Imam Ibnul Qayyim katika kitabu chake cha Sharhu Al-Manaazil anasema kuwa Aayah ii imekusanya ngazi tatu za Dini, amabzo ni: UISLAM, IYMAAN, NA IHSAAN, na atakayeikanusha na kuacha kuitekeleza basi atakuwa amekanusha ngazi zote za Dini.

Jambo la kuhuzunisha ni kuwa, Waislamu tulio wengi ambao tunasema tunampenda Mtume (صلي الله عليه وسلم), haturudi kwa Mtume katika kutatua mizozo yetu, bali kila mtu, kila kundi linarudi kwa sheikh wake, kwa madh-hab yake au kwa kutumia ra’aiy zao, na unapotoa ushahidi wa kauli ya Mtume (صلي الله عليه وسلم) kuhusu suala lenye mzozo basi unaweza kuambiwa mbona Imaam ash-Shaafi’iy, au Maalik kasema hivi, na mtu huyu huyu anapotajwa Mtume (صلي الله عليه وسلم) humtakia rehma kwa kishindo kudhihirisha mapenzi yake kwa Mtume (صلي الله عليه وسلم) na unapochelewa wewe kumtakia rehma Mtume basi hudiriki kukutuhumu kuwa humpendi Mtume (صلي الله عليه وسلم).

Katika Aayah nyingine Allaah Anasema:

( فإن تنازعتم في شيء فردوه الى اللــه والرسول إن كنتم تؤمنون بالله واليوم الآخر) النساء 59

“Na kama mkikhitalifiana katika juu ya jambo lolote basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho” 4:59

Aidha Allaah Anatuamrisha katika Aayah nyingine kurejesha mizozo yetu Kwake na kwa Mtume, lakini asilimia kubwa ya Waislamu hawaitekelezi Aayah hii, na kwa bahati mbaya hata wale wanaojinasibisha kutetea Sunnah za Mtume (صلي الله عليه وسلم) na mwenendo wa As-Salaf As-Swaalih baadhi yao wameshindwa kuitekeleza Aayah hii, na wanaona bora kuhukumiwa na mahakama za kitwaaghuut kuliko kukaa na kuyamaliza matatizo yao kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah.

Hali ya Ummah inahuzunisha, wako wanaotosheka kumsifu tu Mtume (صلي الله عليه وسلم) na kuridhika kuwa wameonyesha mapenzi yao kwa Mtume (صلي الله عليه وسلم), huku wakipinga Sunnah zake zizlizo dhaahir kwa utashi tu wa nafsi zao, na kuwatanguliza masheikh wao, na wakati mwingine kwa ajili tu ya kuwaonyesha Waislamu wenzao ukaidi wao na ubishi wao wa ushindani.

Bado hatumtendei haki Mtume wetu (صلي الله عليه وسلم), bado hatujafikia daraja ya kumpenda kwa dhati kuliko nafsi zetu, kuliko maslahi yetu, kuliko masheikh zetu, kuliko wafuasi wetu, na kuliko majina ya Taasisi na makundi yetu.

Allaah (سبحانه وتعالى) Anawasifu waumini wa kweli kwa kusema:

(إنما كان قول المؤمنين إذا دعوا الى اللــه ورسوله ليحكم بينهم أن يقولوا سمعنا وأطعنا وأولئك هم المفلحون) النور 51

“Haiwi kauli ya Waislamu wanapoitwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao, ila kusema “Tunasikia na tunakubali, na hao ndio watakaofuzu” 24:51

4. KUTOTANGULIZA JAMBO MBELE YAKE, NA KUINAMISHA SAUTI

Katika kumpenda Mtume (صلي الله عليه وسلم) ni kutotanguliza jambo lako, au rai yako, au kauli ya sheikh wako, au madh-hab yako, mbele ya kauli ya Mtume (صلي الله عليه وسلم) na kutonyanyua sauti yako, na fikra zako mbele ya mafundisho ya Mtume (صلي الله عليه وسلم), katika uhai wake na hata baada ya kifo chake (صلي الله عليه وسلم), kwa kuheshimu mafundisho yake na kuyaweka mbele na juu ya mafundisho yote, na kutonyanyua sauti yako juu ya kauli na hukmu ya Mtume (صلي الله عليه وسلم).

Siku moja Imaam Ash-Shaafi’iy (Radhiya Allaahu ‘anhu) alijiwa na mtu na akamuuliza mas-ala katika mas-ala ya Dini, Imaam akamwambia kuwa Mtume (صلي الله عليه وسلم). Amesema kadha, na akamsomea kipengele cha Hadiyth ya Mtume (صلي الله عليه وسلم). Yule muulizaji akamuuliza tena Imaam Ash-Shaafi’iy; na wewe Imaam unaonaje? Imaam Ash-Shaafi’iy akakasirishwa sana na yule mtu, na akamwambia, je unaniona mimi nipo kanisani hapa? Nakwambia amesema Mtume (صلي الله عليه وسلم) kadha unaniuliza rai yangu? Huku ndio kumpenda Mtume (صلي الله عليه وسلم) ukweli wa kumpenda.

5. KUWAPENDA NA KUWAHESHIMU WATU WA FAMILIA YAKE

Kumpenda Mtume (صلي الله عليه وسلم) ni kuipenda familia yake, wakiwemo wake zake na kuwapenda Maswahaba zake, huwezi kumpenda Mtume (صلي الله عليه وسلم) na ukawa unawachukia wakeze na Maswahaba zake, bali kwa kuwachukia wake za Mtume na Maswahaba zake utakuwa unamchukia Mtume mwenyewe, na ukiwatukana utakuwa umemetukana Mtume mwenyewe

6. KUTOMSIFIA KWA SIFA ASIZOSTAHIKI

Kumpenda Mtume (صلي الله عليه وسلم) hakuwi kwa kumsifia kwa sifa ambazo hastahiki, au ambazo zimepetuka mipaka ya utume wake. Wapo Waislamu ambao wanadai kumpenda Mtume (صلي الله عليه وسلم) na wanampachikia sifa ambazo zinakaribia kufikia sifa za Allaah (سبحانه وتعالى), na unapohoji juu ya uzushi huo na shirki hizo, basi utatuhumiwa kuwa wewe ni adui wa Mtume na humpendi.

Mtume (صلي الله عليه وسلم) alitabiri hali hii na akautahadharisha Ummah wake usije ukawa kama Manaswara waliomsifu ‘Iysaa bin Maryam mpaka wakamgeuza Mungu, Mtume (صلي الله عليه وسلم) Alisema:

(لا تطروني كما أطرت النصارى ابن مريم وإنما أنا عبد فقولوا : عبدالله ورسوله )

“Msinisifie kama walivyomsifu Manaswara ‘Iysaa bin Maryam hakika mimi ni mja, niiteni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.”

Lakini pamoja na tahadhari hizo za Mtume (صلي الله عليه وسلم) bado baadhi ya Waislamu hawaoni kuwa wamempenda Mtume (صلي الله عليه وسلم) mpaka wamsingizie sifa ambazo hana, na baadhi yao wamefikia hata kubadilisha Aayah ya Qur-aan ili ikubaliane na upotofu wao, Allaah (سبحانه وتعالى) aliposema kupitia ulimi wa Mtume (صلي الله عليه وسلم) katika kuthibitisha kuwa Mtume ni binadamu kama binadamu wengine isipokuwa yeye huteremshiwa wahyi, alisema:

(قل إنما أنا بشر مثلكم يوحي إلي أنما إلهكم إله واحد ) الكهف 110

“Waambie, Bila shaka mimi ni binadamu kama nyinyi (isipokuwa nimeletewa wahyi tu ndio tofauti yangu). Ninaletewa wahyi ya kwamba Mungu wenu ni mungu mmoja tu.” 18:110

Wapotoshaji hao waliona wamkosoe Allaah kwa kumshusha cheo Mtume, wao wakaona waiandike upya Aayah ili isomeke…

قل إن ما أنا بشر مثلكم يوحي إلي …

Kwa maana, sema hakika mimi si binadamu mfano wenu…

Hii ni kufru ya wazi kabisa ambayo inafanywa kwa jina la kumpenda Mtume (صلي الله عليه وسلم).

Na wengine wanadai kuwa Mtume (صلي الله عليه وسلم) anajua elimu ya ghayb na anajua lini itakuwa Qiyaamah, na kuwa Mtume (صلي الله عليه وسلم) ameumbwa kutokana na nuru ya Allaah, kama isemavyo kauli inayonasibishwa na ‘Abdul-Qaadir Al-Jaylaaniy katika kitabu cha ‘Sirru Al Asraar’ anasema: “Elewa Allaah Akuwafikishe kwa Anachokipenda na kuridhia, Allaah Aliumba roho ya Muhammad kwanza kutokana na nuru yake na uzuri wake, kama alivyosema Allaah: Nimeumba roho ya Muhammad kutokana na nuru ya uso wangu…”

na huo ni uongo dhaahir na kumsingizian Allaah ambacho Hajakisema.

Aidha wanadai kuwa siku ya kuzaliwa kwake Mtume (صلي الله عليه وسلم) ni siku bora kuliko hata usiku wa Laylatul Qadr, na wanadai kuwa roho ya Mtume (صلي الله عليه وسلم) huhudhuria katika maulidi na huwa anazungumza na mawaliiy.

Kwa ujumla, mambo mengi yamezushwa katika Dini hii kwa kumzushia Mtume (صلي الله عليه وسلم) mambo ambayo mengine tumeshindwa kuyaandika katika safu hii kutokana na kutunza heshima ya kipenzi chetu Mtume Muhammad (صلي الله عليه وسلم)

Ndugu zangu Waislamu, tumpende Mtume (صلي الله عليه وسلم) ukweli wa kumpenda, tumuingize katika maisha yetu, awe ni kiongozi wetu, ruwaza yetu, mshauri wetu, hakimu wetu, mwalimu wetu, tuyafundishe mafundisho yake kwa walimwengu wote, na tuuthibitishie ulimwengu kuwa, Mtume Muhammad (صلي الله عليه وسلم) ni Mtume aliyetumwa kwa watu wote na ni rehma kwa walimwengu wote.

Tunayo Dhimma kubwa ya kuhakikisha kuwa mafunzo ya Mtume (صلي الله عليه وسلم) yanafahamika vyema kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu, na njia nyepesi ya kufanikisha hilo ni sisi wafuasi wa Mtume (صلي الله عليه وسلم) kumpenda Mtume wetu ukweli wa kumpenda, na kuyaingiza mafundisho yake katika maisha yetu ya kila siku

—————————————————————

Nini Hikma Ya Kulala Upande Wa Kulia Kama Alivyotufundisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ?

19 Dhul-Hijjah 1428

Yote tunayoyapata kutoka katika Sunnah ya mwalimu wetu, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni mafunzo yenye faida kwetu ima faida ya nafsi zetu au faida katika mwili wetu au faida katika maisha yetu na kwa ujumla, bali kuna hikma kubwa kwenye mafunzo hayo:

عن البراء بن عازب رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه و قال صلى الله عليه وسلم : ((إذا أتيت مضجعك فتوضأ وضوءك للصلاة ثم ثم اضطجع على شقك الأيمن ثم قل :  أللهم  أَسْـلَمْتُ نَفْـسي إِلَـيْكَ، وَفَوَّضْـتُ أَمْـري إِلَـيْكَ، وَوَجَّـهْتُ وَجْـهي إِلَـيْكَ، وَأَلْـجَـاْتُ ظَهـري إِلَـيْكَ، رَغْبَـةً وَرَهْـبَةً إِلَـيْكَ، لا مَلْجَـأَ وَلا مَنْـجـا مِنْـكَ إِلاّ إِلَـيْكَ، آمَنْـتُ بِكِتـابِكَ الّـذي أَنْزَلْـتَ وَبِنَبِـيِّـكَ الّـذي أَرْسَلْـت”   واجعلهن آخر كلامك فإن مت مت على الفطرة)) البخاري و مسلم

Kutoka kwa Al-Baraa Bin ‘Aazib رضي الله عنهما kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema; utakapofika wakati wa kulala, tawadha kama wudhuu wa Swalah, kisha lala upande wako wa kulia, kisha sema:  “Allaahumma aslamtu nafsiy Ilayka, wa fawwadhwtu amriy Ilayka, wa wajjahtu wajhiya Ilayka, wa aljaatu dhwahriy Ilayka, raghbatan wa rahbatan Ilayka, laa maljaa wa laa manjaa Minka illa Ilayka, aamantu bi-Kitaabikal-ladhiy Anzalta, wa bi-Nabiyyikal-ladhiy Arsalta”

[Ewe Allaah,  nimeisalimisha nafsi yangu Kwako, na nimekuachia mambo yangu Wewe na nimeuelekeza uso wangu Kwako na nimeutegemeza mgongo wangu Kwako, kwa matajarajio na kwa kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila Kwako, nimekiamini kitabu Chako Ulichokiteremsha na Mtume Wako Uliyemtuma] Na fanya hivyo iwe ni maneno yako ya mwisho kwani utakapokufa utakufa katika Fitwrah [(Uislamu]))  [Al-Bukhaariy na Muslim]

Hatuna shaka na tunaamini  na kuyafuata  mafunzo yake kadiri tuwezavyo  kwani nani msemaye kweli kuliko Allaah (Subhanaahu wa Ta’ala) na Mjumbe Wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Mjumbe ambaye hasemi kwa matamanio yake ila ni wahyi utokao kwa Mola wetu Muumba Anayesema:

((وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَى)) (( إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَى))

((Wala hatamki kwa matamanio)) ((Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa)) [An-Najm: 3-4]

Basi hebu tuone hikma ya kutufunza kulala upande wa kulia.

Ubongo (Brain)

Ubongo sehemu yake huwa upande wa kulia na ndio ambao unauongoza Moyo ulioko upande wa kushoto.

Mapafu (Lungs)

Pafu la upande wa kulia wa mwili ni kubwa kuliko pafu la upande wa kushoto, kwa kuwa pafu la upande wa kulia lina sehemu 3 wakati ambapo la upande wa kushoto lina sehemu 2 tu.

Ini (Liver)

Ini liko upande wa kulia na ndilo tezi (gland) kubwa kubwa kabisa mwilini.

Nyongo (Gall Bladder)

Nyongo nayo nipo upande wa kulia na ina majukumu ya kutengeneza utomvu ambao unameng’enyua (digest) mafuta.

Matumbo (Intestines)

Matumbo (Intestines) Na Sehemu Ya Mwisho Wa Utumbo (colon)

Sehemu ya ‘mwisho wa Utumbo mkubwa’ (colon) na mwisho wa matumbo (intestines) yako upande wa kulia. (Appendix)

Moyo

Moyo uko upande wa kushoto na ndio pampu la taratibu ya mzungukuo(circulatory system)

Tumeona kwamba  kwamba viungo vya mwili vikubwa viko upande wa kulia katika mwili, kwa hiyo mtu anapolala upande wa kushoto, huathiri viungo hivi na huleta madhara katika siha ya Binaadamu. Na juu ya hivyo mtu anapolala upande wa kulia huwa haileti shinikizo katika vyumba vya mapumziko ya moyo ambazo hufanya wepesi kazi ya Taratibu ya Mzunguko (circulatory cycle).

Kwa hiyo mtu anayelala upande wa kulia anapoamka asubuhi huamka akiwa mwenye nguvu na  mchangamfu.

Hadiyth za  Mtume صلى الله عليه وآله وسلم tulizoamrishwa na mapendekezo ya kulala upande wa kulia

عن أبي  هريرة رضي الله عنه قال :” رأى رسول الله صلى الله عليه و سلم رجلاً مضطجعاً على بطنه فقال ((إن هذه ضجعة يبغضها الله و رسوله))”. رواه الترمذي  .

Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه ambaye kasema: Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alimuona mtu amelala kifudifudi, akasema: ((Kulala huku kunachukizwa na Allaah سبحانه وتعالى na Mtume Wake)) [At-Tirmidhy]

عن  عائشة أن رسول الله  صلى الله عليه وسلم   “كان   إذاصلى  ركعتي    الفجر    (يعني سنتها)  اضطجع على شقه   الأيمن” – صحيح البخاري

Imetoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah رضي الله عنها  kwamba “Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  akishaswali rakaa mbili za Alfajiri, [yaani Sunnah za Alfajiri]  hulala upande wa kulia” [al-Bukhaariy]

عن أبي أمامة قال: مر النبي صلى الله عليه وسلم على رجل نائم في المسجد منبطح على وجهه فضربه برجله وقال: (( قم أو اقعد فإنها نومة جهنمية))

مسند أحمد وسنن ابن ماجه

Kutoka kwa Abu Amaamah kasema; alipita Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwa mtu mmoja ambaye alikuwa amelala kifudifudi  msikitini akampiga hivi (teke) kwa mguu akasema: ((Inuka au kaa kwani kulala huku ni kama kulala kwa watu wa motoni))   [Musnad Ahmad na Sunan Ibn Maajah]

وعن حفصة رضي الله عنها قالت:” كان النبي صلى الله عليه وسلم إذا أخذ مضجعه جعل يده اليمنى تحت خده الأيمن” رواه الطبراني، صحيح الجامع

Kutoka kwa mama wa waumini Hafswah رضي الله عنها   ambaye kasema: “Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa anapotaka kulala huweka mkono wake katika shavu la kulia [At-Twabraaniy katika Swahiyh al-Jaami’y]

Amesema Imaam Ibn al-Qayyim (Allaah Amrehemu): Kulala kwake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ubavu wake wa kulia kuna siri, nayo ni kuwa Moyo unakuwa juu kwa upande wa kushoto, kwa hivyo, ikiwa atalalia ubavu wake wa kushoto basi usingizi utakuwa mzito; kwani atakuwa katika hali ya utulivu na ushwari na hivyo kuwa usingizi wake ni mzito. Na kama atalala kwa upande wa ubavu wake wa kulia, basi atakuwa katika hali ya wasiwasi na usingizi wake utakuwa si mzito kwa kuwa moyo utakuwa katika hali ya wasiwasi na atahitajia utulie na moyo kupondokeka kwake.

——————————————————-

Kauli Za Maimaam Wanne Kuhusu Kushikamana Na Sunnah Na Kuacha Kufuata Rai Zao

Shaykh Muhammad Naaswirud-Diyn Al-Albaaniy

Imefasiriwa na  www.alhidaaya.com kutoka kitabu cha: ‘Swiffatus-Swalaatun-Nabbiy (Sifa ya Swalah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kilichoandikwa na Shaykh Al-Albaaniy (Rahimahu-LLaah)

Itakuwa ni manufaa makubwa ikiwa tutazieleza baadhi ya kauli zao hapa, kwani labda hii itamuonya mtu au itawakumbusha wale ambao wanafuata rai za Maimaam au madhehebu maalum, bali wanaofuata kwa upofu wale Waalimu au Mashaykh na wale walio chini ya daraja ya hao Maimaam wanne wakubwa[1]wakishikilia madhehebu yao au rai zao kama kwamba zimeteremeshwa kutoka mbinguni! Na hali Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:

((اتَّبِعُواْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلاَ تَتَّبِعُواْ مِن دُونِهِ أَوْلِيَاء))

((Fuateni mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake))[2]

WASEMAVYO MAIMAAM

1) ABU HANIYFAH  (Rahimahu-Llaah)

Wa kwanza wao ni Abu Haniyfah Nu’maan bin Thaabit.

Wafuasi wake wamesimulia kauli zake mbali mbali pamoja na maonyo tofauti ambayo yote lengo lake ni moja, nalo ni: Wajibu wa kuikubali Hadiyth na kuachilia mbali kufuata rai za Maimaam ambazo zinakhitilafiana nayo.

1. “Ikiwa Hadiyth imeonekana kuwa ni sahiyh, basi hiyo ndiyo madhehebu yangu”[3]

2. “Hairuhusiwi[4] kwa mtu yeyote kukubali rai zetu ikiwa pindi hawatojua wamezipata kutoka wapi”[5]

Katika usimulizi mwengine:”Imekatazwa[6] mtu ambaye hajui dalili zangu kutoa hukmu[7] kutokana na maneno yangu”

Usimulizi mwengine imeongezwa: “…Kwani sisi ni wanaadamu, tunasema jambo siku moja na kulirudisha (kulikataa) siku ya pili yake”.

Na katika usimulizi mwengine: “Ole Ewe Ya’quub![8] Usiandike kila kitu unachosikia kutoka kwangu kwani huwa natoa rai moja leo na kesho huikataa. Au hutoa rai moja kesho na kuikataa keshokutwa”.[9]

3. “Ninaposema jambo linalokhitilafiana na kitabu cha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) au yaliyosimuliwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), basi mpuuze usemi wangu”.[10]

2) MAALIK IBN ANAS (Rahimahu-LLaah)

Imaam Maalik bin Anas yeye amesema:

1. “Hakika mimi ni mwanaadamu: Ninafanya makosa (mara nyingine) na ninakuwa sahihi (mara nyingine). Kwa hiyo, tazameni rai zangu: zote ambazo zinakubaliana na Kitabu (Qur-aan) na Sunnah, zikubalini; na zote ambazo hazikubaliani na Kitabu (Qur-aan) na Sunnah, basi zipuuzeni”. [11]

2. “Kila mmoja baada ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), atakuwa na kauli yake utakaokubaliwa na kukataliwa, isipokuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”[12]

3. Ibn Wahb amesema: “Nilimsikia Maalik akiulizwa kuhusu takhliyl ya vidole vya miguu (kuvichanganua vidole ili kupitisha maji) wakati wa wudhuu. Akasema: “Watu si lazima kufanya hivyo”. Sikumkaribia hadi zogo la watu lilipopunguka. Nilipomwambia: “Tunajua kuwa ni Sunnah kuhusu jambo hilo”. Akasema: “Jambo gani hilo? Nikasema: “Laith ibn Sa’d, ibn Lahiy’a na ‘Amr ibn Al-Haarith wamesimulia kwetu kutoka kwa Mustawrid bin Shaddaad Al-Quraishiy ambaye amesema: “Nilimuoma Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisugua baina ya vidole vyake vya miguu kwa kidole change kidogo”. Akasema: “Hadiyth hii ni hasan (njema); sikuwahi kuisikia  abadan ila leo”. Kisha baadaye nikamsikia akiulizwa kuhusu jamo hili hili, naye akaamrisha kufanya takhliyl ya vidole vya miguu”[13]

3) ASH-SHAAFI’IY  (Rahimahu-LLaah)

Ama kutoka kwa Imaam Ash-Shaafi’iy, kauli zake zilizonukuliwa ni nyingi na nzuri mno.[14]na wafuasi wake walikuwa ni bora kabisa katika kufuata.

1. “Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zinamfikia na kumkwepa kila mmoja wetu. Kwa hiyo kila ninapotaja rai yangu au nikiunda sheria, na ikiwa ipo dalili kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), inayopinga rai yangu, basi rai iliyo sahihi ni aliyosema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na hiyo ndio rai yangu”[15]

2. “Waislamu wamekubaliana pamoja  kwamba ikiwa Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) imebainishwa dhahiri kwa yeyote, hairuhusiwi[16] kwake kuiacha kwa kufuata kauli ya mwengine yeyote[17]

3. “Ukiona katika maandishi yangu jambo ambalo ni tofauti na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), basi zungumza kwa kurejea Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na acha niliyoyasema mimi”

Katika usimulizi mwengine: “…basi ifuate (Sunnah) na usitazame tena pembeni kufuata kauli ya mwengine yeyote”[18]

4. Hadiyth ikipatikana kuwa ni sahiyh, basi hiyo ndiyo madhehebu yangu”[19]

5. “Wewe (Imaam Ahmad)[20]ni mwenye elimu zaidi kuhusu Hadiyth kuliko mimi. Kwa hiyo Hadiyth ikiwa ni sahiyh basi nijulishe, ikiwa ni kutoka Kufah, Basrah au Syria, ili nichukue rai ya Hadiyth madamu tu ni sahiyh”[21]

6. “Katika kila jambo, ambako wenye kusimulia wakipata ripoti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo ni kinyume na niliyoyasema, basi narudisha usemi wangu nyuma, ikiwa wakati wa maisha yangu au hata baada ya kufa kwangu”[22]

7. “Ukinisikia nasema kitu, na kinyume yake ni Hadityh Sahiyh kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), basi tambua kuwa akili yangu imetoweka”[23]

8. “Kwa kila ninalosema, ikiwa upo usimulizi ulio Sahiyh, basi Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inakuja mwanzo, kwa hiyo usifuate rai yangu”[24]

9. “Kila kauli kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni rai yangu pia, japokuwa hujaisikia kutoka kwangu”[25]

4) AHMAD BIN HANBAL (Rahimahu-LLaah)

Imaam Ahmad alikuwa wa mbele miongoni mwa Maimaam kukusanya Sunnah na kuzishikilia sana hadi   alichukizwa kuona kitabu kilichokuwa na yaliyegeuzwa na rai kiandikwe[26] kwa sababu hii akasema:

1. Msifuate rai yangu, wala msifuate rai ya Maalik, au Ash-Shaafi’iy au ya Awzaa’iy, wala Ath-Thawriy, lakini chukueni kutoka walikotoa”[27]

Katika usimulizi mmoja: “Msiige dini yenu kutoka kwa mtu yeyote katika hawa, bali chochote kilichotoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake, chukueni, kisha kwa At-Taabi’iyn (Waliofuata) ambako mtu ana khiari”.

Mara moja kasema: “Kufuata[28]ina maana kwamba mtu anafuata yaliyokuja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake, baada ya  At-Taabi’iyn (Waliofuata) anayo khiari” [29]

2. “Rai ya Awzaaiy, rai ya Maalik, rai ya Abu Haniyfah, zote ni rai, na ni sawa katika macho yangu. Lakini, dalili ni yale masimulizi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake”[30]

3. “Yeyote atakayekanusha kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) basi yumo katika ukingo wa kuangamia”[31]

Hizi ndizo kauli za wazi kabisa za Maimaam (Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala Awe radhi nao), kuhusu kushikamana  na Hadiyth na kukataza kufuata rai zao bila ya kuwa na dalili iliyo dhahiri kabisa.

Kwa hiyo, yeyote aliyeshikamana na lolote la Sunnah ambayo imeshuhudiwa kuwa ni Sahiyh hata kama imepinga kauli ya baadhi ya Maimaam, hatokuwa anapingana na madhehebu yao, wala hatopotoka katika njia zao, bali mtu huyo atakuwa anawafuata wote na atakuwa amekamata kile kilichoaminiwa zaidi akishika mkono ambao hautavunjika. Lakini hii haitakuwa hali ya yule anayeziweka kando Sunnah Sahiyh kwa sababu tu zimepingana na rai za Maimaam, bali mtu huyo atakuwa sio mtiifu kwao na amepingia kauli zao hizo za juu.  Na tunaona Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:

((فَلاَ وَرَبِّكَ لاَ يُؤْمِنُونَ حَتَّىَ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لاَ يَجِدُواْ فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُواْ تَسْلِيمًا))

((La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenyekee kabisa.))[32]

((فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ))

((Basi na watahadhari wanaokhalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu iumizayo))[33]

Kwa vile hii ni uthibitishaji kuwa kwa nini Abu Haniyfah mara nyingine alikhitilafiana na Hadiyth zilizokuwa Sahiyh bila ya kukusudia na ni sababu barabara ya kukubaliwa, kwani Allaah Haikalfishi nafsi kwa yale isiyoweza kubeba. Hairuhusiwi kumtukana kwa sababu hiyo kama walivyofanya watu wajinga. Bali ni wajibu kumheshimu, kwani yeye ni mmoja wa Maimaam wa Waislamu ambao wameihifadhi hii dini hadi ikafikishwa kwetu kutoka katika kila matawi yake. Na kwa vile yeye analipwa (Na Allaah Subhaanahu wa Ta’ala) kwa hali yoyote ile; ikiwa ni Sahiyh au amekosea. Wala hairuhusiwi kwa wafuasi wake wapenzi kuendelea kushikilia kauli zake ambazo zinakhitilafiana na Hadiyth zilizo Sahiyh kwani kauli hizo sio madhehebu yake kama kauli zake hapo juu zilivyosema. Kwa hiyo hii ni mipaka miwili; ukweli na uongo katika yake. ((Na waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala Usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu)) [Al-Hashr 59:10]

An-Nuur: 24:63


[1] Hii ni aina ya taqliyd (kufuata kwa upofu [kiujinga]) ambayo Imaam At-Twahaawiy alihusisha aliposema: “Hafuati rai ila ni mtu mkaidi au mjinga” (kufuata kama kipofu)

[2] Al-A’raaf:3

[3] Ibnul-‘Aabidiyn katika al-Haashiyah (1/63) na katika inshaa yake   Rasm al-Mufti (1/4 kutoka Mkusanyiko wa Inshaa za Ibnul-‘Aabidyin). Shaykh Swaalih Al-Fulaaniy katika alIyqaadhw al-Himaam (uk.62) na wengineo. Ibnul-‘Aabidiyn amenukuu kutoka Sharh al-Hidaayah ya Ibn Al-Shahnah Al-Kabiyr, mwalimu wa Ibn Al-Himaam, kama ifuatavyo:

“Ikiwa Hadiyth iliyo kinyume na Madhehebu imeonekana kuwa ni sahiyh basi mtu atende kwa kufuata hiyo Hadiyth na aifanye kuwa ni madhehebu yake. Kuifanyia kazi Hadiyth hakutombatilisha mtu kuwa sio mfuataji wa madhehebu ya Hanafi, kwani imeripotiwa kuwa Abu Haniyfah alisema: “Ikiwa Hadiyth imeonekana kuwa ni sahiyh, basi hiyo ndiyo madhehebu yangu”. Na hii imeelezewa na Imaam Ibn ‘Abdul-Barr kutoka kwa Abu Haniyfah na kutoka kwa Maimaam wengine”.

Hii ni sehemu ya ukamilifu wa elimu na ucha Mungu wa Maimaam, kwani wameonyesha kwa kusema kwamba wao hawakuwa na maarifa  (elimu) kamili ya Sunnah zote. Na Imaam Ash-Shaafi’iy amefafanua wazi wazi (tazama mbele). Hutokea wanapokwenda kinyume na Sunnah huwa ni kwa sababu hawakuitambua. Ndipo walipotuamrisha tushikilie Sunnah na tuizingatie kuwa ni sehemu ya madhehebu yao. Allaah Awashushie Rahma Yake kwao wote.

[4] Sio halaal

[5] Ibn ‘Abdul-Barr katika Al-Intiqaa’ fiy Fadhwaail Ath-Thalaathah Al-Aimmah Al-Fuqahaa (uk.145), Ibn Al-Qayyim katika ‘I’laam Al Muqi’iyn (2/309), ibn ‘Aabidiyn katika tanbihi zake kwenye Al-Bahr Ar-Raa’iq (6/293) na katika Rasm Al-Mufti (uk. 29,32) na Sha’raaniy katika Al-Miyzaan (1/55) pamoja na usimulizi wa pili. Usimulizi wa mwisho ulikusanywa na ‘Abbaas Ad-Dawriy katika At-Taariykh ya Ibn Ma’iyn (6/77/1) ikiwa na isnaad sahiyh kutoka kwa Zafar, mwanafunzi wa Imaam Abu Haniyfah. Usimulizi uliofanana upo kutoka kwa wafuasi wa Abu Haniyfah; Zafar, Abu Yuusuf na ‘Aafiyah bin Yaziyd;  taz. Al-Iyqaadhw (uk.52). Ibn Al-Qayyim alithibitisha kwa nguvu usahihi wake kutoka kwa Abu Yuusuf katika I’laam Al-Muwaqi’yn (2/344). Nyongeza ya usimulizi wa pili unarejewa na mwandishi wa Al-Iyqaadhw (uk. 65) kwa Ibn ‘Abdul-Barr, ibn Al-Qayyim na wengineo.

Ikiwa hivi ndivyo wanavyosema kwa mtu asiyejua dalili zao, jibu lao litakuwa nini kwa yule anayetambua kuwa dalili zinapingana na kauli yao, lakini bado anatoa hukumu iliyopinga dalili? Kwa hiyo, fuata usemi huu, kwani pekee unatosheleza kuvunja ufuataji rai kwa ujinga. Ndio maana nilipomlaumu mmoja wa Mashaykh (Muqallid) wa madhehebu katika kutoa fatwa (hukm) kwa kutumia maneno ya Abu Haniyfah bila ya kujua dalili, aligoma kuamini kuwa huo ni kauli ya Abu Haniyfah!

[6] Haraam

[7] Fatwa

[8] Mwanafunzi mashuhuri wa Imaam Abu Haniyfah, Abu Yuusuf  (Rahimahu-Llaah)

[9] Hii ni kwa sababu Imaam kawaida hutoa rai yake kutokana na Qiyaas (analogia). Kisha tena hupata analogia iliyo na nguvu zaidi, au Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) humfikia. Kwa hiyo huikubali hiyo na kuipuuza rai yake ya nyuma. Maneno ya Sha’araaniy katika Al-Miyzaan (1/62) yamewekwa kwa mukhtasari kama ifuatavyo:

“Imani yetu na ya kila mtafiti wa Imaam Abu Haniyfah (Rahimahu-Llaah) ni kwamba, aliishi hadi iliporikodiwa Sharia. Na safari za wahifadhi wa Hadiyth katika miji mbali mbali na mipakani kwa ajili ya kukusanya na kuzipata. Angeliipokea na kupuuza analogia zote ambazo alizozitumia, idadi za qiyaas katika madhehebu yake zingelikuwa kidogo kama zilivyo katika madhehebu mengine. Lakini kwa vile dalili za Sharia zimetapakaa kwa Waliotangulia na waliowatangulia, na haizikukusanywa wakati wa maisha yake, ilihitajika kuwepo qiyaas nyingi katika madhehebu yake kulingana na Maimaam wengine. Maulamaa wa baada ya hapo, kisha wakafanya safari kutafuta na kukusanya Hadiyth kutoka nchi mbali mbali na miji na wakaziandika. Hivyo baadhi ya Hadiyth za Sharia zimeelezea nyingine. Hii ni sababu ya kuweko idadi kubwa ya qiyaas katika madhehebu yake wakati kwenye madhehebu mengine ilikuwa ni idadi ndogo”

Abul-Hasanaat Al-Luknawi amenukuu maneno yake kikamilifu katika An-Naafi’ Al-Kabiyr (uk.135) akiandika na kupanua tanbihi zake. Kwa hiyo yeyote anayependa kutafuta maelekezo yake afanye humo. [10]Al-Fulaaniy katika Al-Iyqaadhw Al-Himaam (uk.50), ikifuatilia kwa Imaam Muhammad na kisha kusema: “Hii haimhusu mujtahid, (mwenye kujitahidi kwa elimu yake na kutoa hukmu) kwa vile hakujifunga katika rai zao, bali inamhusu muqallid (mwenye kufuata).

[11]Ibn ‘Abdul Barr katika Jaami’ul Bayaan Al’Ilm (2/32), ibn Hazm   akinukuu kutoka kwake katika Usuul-Al-Ahkaam (6/149) na hali kadhaalika Al-Fulaaniy (uk. 72).

[12] Hii inajulikana sana miongoni mwa Maulamaa wa baadaye kuwa ni kauli ya Maalik. Ibn ‘Abdul-Haadi alikiri kuwa ni Sahiyh katika Irshaad As-Saalik (227/1); Ibn ‘Abdul Barr katika Jaami’ul-Bayaan Al-‘Ilm (2/91) na Ibn Hazm katika Usuul Al-Ahkaam (6/145, 179) alisimulia kama ni kauli ya Al-Hakam ibn ‘Utaybah na Mujaahid; Taqid-Diyn As-Subki alisimulia  katika Al-Fataawa (1/148) kama ni kauli ya Ibn ‘Abbaas akishangazwa kwa uzuri wake kisha akasema: “Haya maneno yameanzia kwa Ibn ‘Abbaas na Mujaahid, na Maalik (Rahimahu-Llaahu) aliyachukua, na akawa mashuhuri kwayo”. Inavyoelekea kwamba Imaam Ahmad kisha akachukua kauli hii kutoka kwao, kama Abu Daawuud alivyosema katika Masaaiil ya Imaam Ahmad (uk 276). “Nilimisikia Ahmad akisema: Kila mmoja anapokelewa na anakatiliwa katika rai zake, isipokuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”

[13] Kutoka kwa Utangulizi wa Al-Jarh wat-Ta’diyl ya Ibn Abi Haatim (uk.      31-32)

[14] Ibn Hazm anasema katika Usuul al-Ahkaam (6/118)

“Hakika, Mafuqahaa wote ambao rai zao zilikuwa zikifuatwa zilipingwa  kwa taqliyd na waliwakataza wafuasi wao kufuata  rai zao kijinga. Aliyekuwa mkali kabisa miongoni mwao ni Ash-Shaafi’iy (Rahimahu-LLaah), kwani yeye alirudia kutilia mkazo zaidi kuliko yeyote mwengine kufuata usimulizi ulio Sahiyh na kukubali dalili yoyote iliyoamriwa. Vile vile alidhihirisha wazi na kujitenga kuwa hana hatia ikiwa atafuatwa yeye tu pekee na aliwatangazia hayo wale waliokuwa naye. Tunaomba hii imnufaishe mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na thawabu zake ziwe za juu kabisa kwani alikuwa ni sababu ya mema mengi”.

[15] Imesimuliwa na Al-Haakim ikiwa ina isnaad ya kuendelea hadi kwa Ash-Shaafi’iy kama ilivyo katika Taariykh Dimashq ya Ibn ‘Asaakir (15/1/3), I’laam Al-Muwaqi’yn (2/363,364) na Al-Iyqaadhw (uk. 100)

[16] Halaal

[17] Ibn al-Qayyim (2/361) na Al-Fulaaniy (uk. 68)

[18] Al-Haraawiy katika Dhamm Al-Kalaam (3/47/1) Al-Khatiyb katika Al-Ihtijaaj bi Ash-Shaafi’iy (8/2), Ibn ‘Asaakir (15/9/10), An-Nawawiy katika Al-Majmuu’ (1/63), Ibn al-Qayyim (2/361), na Fulaani (uk 100) usimulizi wa pili ni kutoka Hilyah Al-Awliyaa ya Abu Nu’aym.

[19]An-Nawawiy katika Al-Majmuu’ (1/63), Sha’raaniy (1/57), akitoa chanzo chake kama Al-Haakim na Al-Bayhaqiy na Al-Fulaaniy (uk. 107). Ash-Sha’raaniy kasema: “Ibn Hazm kasema: “Kwamba imeonekana ni sahiyh naye au kwa Imaam mwengine”. Kauli yake nyingine imethibitisha ufahamu huu.

An-Nawawiy amesema: “Wafuasi wetu walitenda kutokana na hili katika mambo ya tathwiyb (mwito wa Swalah baada ya adhana), shuruti za kutoka katika ihraam kwa ajili ya ugonjwa, na mambo mengine yaliyojulikana vyema katika vitabu vya madhehebu. Miongoni wafuasi wetu ambao wameripotiwa kuwa walitoa hukumu kutokana na chanzo cha Hadiyth (yaani kuliko kuchukua kauli ya Ash-Shaafi’iy) ni Abu Ya’quub Al Buwiity na Abul-Qaasim Ad-Daariki. Wafuasi wa Muhaddithiyn (Wakusanyao Hadiyth), Imaam Abu Bakr Al-Bayhaqi na wengineo walitenda kwa kufuata kauli hii. Wafuasi wengi wetu wa zamani, walipokumbana na jambo ambalo ilikuweko Hadiyth na madhehebu ya Ash-Shaafi’iy yalikuwa ni kinyume nalo, basi walitenda  kwa kufuta Hadiyth na kutowa fatwa (hukmu) pia wakisema: “Madhehebu ya Ash-Shaafi’iy ni kila kinachokubaliana na Hadiyth”. Shaykh Abu ‘Amr (Ibn As-Swalaah) alisema: “Yeyote miongoni mwa Ash-Shaafi’iy akiona Hadiyth inayopinga madhehebu yake, alichukulia kama alitimiza shuruti za ijtihaad kwa kawaida, au katika maudhui au jambo lile khaswa ambalo alikuwa huru kutenda kwa kufuata Hadiyth; kama sio. Lakini hata hivyo aliona vigumu kupingana na Hadiyth baada ya utafiti zaidi, hakuweza kupata uthibitishaji wa kukinaisha wa kupinga Hadiyth. Kwa hiyo, alibakia kutenda kwa kufuata Hadiyth ikiwa Imaam mwingine mwenye kujitegemea mbali na Ash-Shaafi’iy, basi alitenda kuifuata. Na hii huwa ni kithibitisho chake cha kuacha madhehebu ya Imaam wake katika jambo hilo”. Alichosema (Abu ‘Amr) ni Sahiyh na lililokubalika. Na Allaah Anajua zaidi.

Kuna uwezekano mwingine ambao Ibn As-Swalaah alisahau kutaja: Afanyeje mtu ikiwa hakumpata mtu yeyote ambaye alitenda kwa kufuata Hadiyth? Hii imejibiwa na Taqiud-Diyn As-Subkiy katika makala yake ‘Maana Ya Kauli ya Ash-Shaafi’iy: Ikiwa Hadiyth ikipatikana kuwa ni sahiyh, basi ndio madhehebu yangu’ (uk.102, Mjalada 3). “Kwangu, lililo bora kabisa ni kufuata Hadiyth. Mtu na awaze kwamba yuko mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama vile ameisikia kutoka kwake, je, atakwenda demani (kufuata mweleko wa upepo) acheleweshe kutenda kwa kuifuata? Hapana! WaLLaahi, na kila mmoja anabeba jukumu kutokana na ufahamu wake”.

Mjadala wake uliobakia umetolewa kuchambuliwa  katika I’laam Al-Muwaqi’iyn (2/303,370)  na katika kitabu cha Al-Fulaaniy, (Kichwa cha habari kamili) Al-Iyqadhw Himam Uul Al-Abswaar, lil-iqtidaa bisayyid Al-Muhaajiriyn wal-Answaar, wa Tahdhiyrihim ‘an Al-Ibitidaa’ Ash-Shaai’ fit-Quraa wal-Amswaar, min taqlyid Al-Madhaahib ma’a Al-Hamiyyat Wal-‘Aswabiyyat Bayna Fuqahaa Al-A’swaar”

Kitabu hicho ni cha pekee katika maduhui hii, ambacho kila mpenda haki akisome kwa ufahamu na kutafakari.

[20] Akimwambia Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu-LLaah)

[21]Imesimuliwa na Ibn Abi Haatim katika Aadaabu Ash-Shaafi’iy (uk.94-5), Abu Nu’aym katika Hulya Al Awliyaa (9/106), Al-Khatiyb katika Al-Ihtijaaj bish-Shaafi’iy (8/1) na kutoka kwake Ibn ‘Asaakir (15/9/1), Ibn ‘Abdul-Barr katika Al-Intiqaa’ (uk.75), Ibn Al-Jawziy katika Manaaqib Al-Imaam Ahmad (uk.499) na Haraawiy (2/47/2) katika njia tatu kutoka kwa ‘Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal kutoka kwa baba yake kwamba Ash-Shaafi’iy alimhusisha nayo katika I’laam (2/325) kama alivyofanya Al-Fulaaniy katika Al-Iyqaadhw (uk.152) na kisha akasema: “Al-Baihaqy amesema: “Hii ndio maana yeye, yaani Ash-Shaafi’iy alitumia Hadiyth sana, kwa sababu alikusanya elimu kutoka kwa watu wa Hijaaz, Syria, Yemen na Iraq. Kwa hiyo alikubali yote aliyoona kuwa ni sahiyh bila ya kutegemea au kuangalia yale yaliyokuwa nje ya madhehebu ya watu wa nchi yake,wakati ukweli ulipodhihirika kwake kutoka sehemu nyingine. Wengineo kabla yake, walijiwekea mipaka kwa waliyoyakuta katika madhehebu ya watu wa nchi yao bila ya kujaribu kuhakikisha usahihi wa yale yaliyokuwa kinyume nayo. Allaah Atusamehe sote”

[22] Abu Nu’aym (9/107), Harawiy (47/1), Ibn al-Qayyim katika I’laam Al-Muwaqqi’iyn (2/363) na Fulaani (uk. 104)

[23] Ibn Haatim katika Al-Adaab (Uk. 93), Abul-Qaasim Samarqandi katika Al-Amaali, kama katika uchaguzi kutoka kwa Abu Hafsw al-Mu’addab (234/1), Abu Nu’aym (9/106), na Ibn ‘Asaakir (15/10/1) ikiwa ni sanad sahiyh.

[24] Ibn Abi Haatim, Abu Nu’aym na Ibn ‘Asaakir (15/9/2)

[25] Ibn Abi Haatim (uk 93-4)

[26] Ibn Al-Jawziy katika Al-Manaaqib (Uk. 192)

[27] Al-Fulaaniy (uk.113) na Ibn Al-Qayyim katika I’laam

[28] Ittibaa’

[29] Abu Daawuud katika Masaail ya Imam Ahmad (Uk 276-7)

[30] Ibn ‘Abdul-Barr katika Jaami’ Bayaan Al-‘Ilm

[31] Ibn Al-Jawziy (uk 182)

[32] An-Nisaa:4:65

[33] An-Nuur: 24:63

——————————————————–

Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat Sawdaa-1 (haba Soda – Chembe Nyeusi

Imefasiriwa na Iliyasa bint Maulaanah

Al-Bukhaariy anasimulia kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume Muhammad (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema.

((Habbat-Sawdaa inatibu kila kitu isipokuwa mauti)).

Yafuatayo hapa chini ni baadhi ya matatizo na magonjwa ambayo yanaweza kutibika kwa kirahisi kwa kutumia Habbat-Sawdaa.

Kwa faida ya Afya kwa ujumla:

Kunywa kijiko kimoja cha mafuta ya Habbat-Sawdaa asubuhi na usiku, au kunywa japo asubuhi kabla ya kifungua kinywa, unaweza kunywa kijiko kimoja cha mafuta peke yake au ukachanganya na kijiko kimoja cha asali safi.

Vipele (chunusi) Na Ngozi:

Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu) kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple). Paka katika sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.

Upara (Alopeshia):

Sugua mafuta ya Habbat-Sawdaa katika mabaka yanayokusumuba.

Pumu:

Tia ½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.

Kuumwa kwa Mgongo (Sehemu ya Chini):

Changanya asali pamoja na ¼ (robo) kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.

Mwiba Wa Nyuki Na Nyigu:

Tia ½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.

Kibofu cha Mkojo/Figo:

Kunywa maji ya moto yaliyochanganywa na½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa pamoja na asali kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Changanya vikombe viwili vya Habbat-Sawdaa iliyosagwa na ½ (nusu) kikombe cha asali safi. Kunywa kijiko kimoja cha mchanganyiko pamoja na kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Mchanganyiko unaweza kukaa kwa siku 15 na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.

Jiwe La Figo:

Kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyochanganwa pamoja na gilasi (bilauri) moja ya asali, vitunguu saumu vitatu vilivyosagwa na karafuu. Changanya vitunguu saumu pamoja na asali na Habbat-Sawdaa. Kunywa kijiko kimoja kabla ya kula chakula na kwa pendekezo kula limau (bila ya kumenywa). Rudia haya kwa wiki moja Insha-Allah jiwe litaondoka.

Maathiriko Ya Figo:

Changanya baadhi ya Habbat-Sawdaa pamoja na mafuta ya alizeti. Chukua mchanganyiko na weka katika sehemu ambapo figo limeathirika. Kunywa kijiko cha Habbat-Sawdaa asubuhi. Rudia haya kwa muda wa wiki moja Insha-Allah maathiriko yatatibika.

Mafua:

Chukua mbegu za Habbat-Sawdaa 21, ziweke katika kitambaa na roweka usiku. Tumia kama matone kwenye pua siku ya pili nusa poda ya Habbat-Sawdaa iliyomo katika kitambaa.

Kikohozi:

Tumia matone matatu au manne ya mafuta ya Habbat-Sawdaa kwenye kahawa au chai.

Bawasiri:

Kula unga wa Habbat-Sawdaa pamoja na maji.

Shinikizo la damu (high blood pressure):

Changanya kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, kijiko kimoja cha asali safi na kitunguu kiasi kidogo. Chukua mchanganyo kabla ya kufungua kinywa kwa siku ishirini.

Uwasho Na Maumivu Ya Jino Na Ufizi:

Chemsha Habbat-Sawdaa katika siki na itumie kwa kusukutulia meno na ufizi. Na jikinge kutumia dawa za msuwaki za kibiashara na tumia dawa za msuwaki ambazo zinatengenezwa kutoka kwenye nyuzi za mboga za mti wa siwak ambao kwa karne ulikuwa unatumiwa na Wahindi, Waafrika na Waarabu, ni msuwaki wa kiasili.

Kumbukumbu (memory):

Kunywa kijiko kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa na changanya na asali mara mbili kwa siku.

Utaratibu Wa Ulinzi Wa Mwili:

Kula kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa na asali mchana na usiku Kutoweza kuzuia haja ndogo (mkojo): Kunywa kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa pamoja na asali, kisha kunywa maji ya vugu vugu.

Jaundice:

Tumia Habbat-Sawdaa pamoja na maziwa.

Maumivu Sugu ya kichwa (Maumivu ya kichwa ya upande mmoja, maumivu ya kichwa):

Kaanga Habbat-Sawdaa na iweke katika kitambaa cha pamba, funga au weka tu kitambaa katika kikomo (kipaji cha uso). Roweka Habbat-Sawdaa ndani ya siki wakati wa usiku, siku ya pili ivuruge kufanya unga. Ingiza katika pua halafu vuta pumzi.

Ngozi kavu:

Changanya asali pamoja na robo kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.

Upepo:

Changanya asali pamoja na robo kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.

Minyoo:

Kunywa Habbat-Sawdaa pamoja na siki kuondoa minyoo.

————————————————————————————————————————–

Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat-sawdaa-2 (habba Soda – Chembe Nyeusi )

Imefasiriwa na Iliyasa binti Maulana

(Itumieni habba hii, hakika ndani yake muna shifaa (ponyo) ya kila aina ya ugonjwa isipokuwa mauti)). (Al-Bukhaariy)Kunyonyoka Nywele

Ataukanda unga wa Habbat-Sawdaa katika juisi ya chirichiri pamoja na kijiko cha siki nyepesi na kikombe cha mafuta ya zeituni, halafu asugue kichwani kwa mafuta hayo kila siku jioni pamoja na kukiosha kichwa kwa maji na sabuni kabla ya kupaka.

Maumivu ya Kichwa

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa , karafuu iliosagwa nusu ya kiwango cha Habbat-Sawdaa  na anisuni (anise), halafu achanganye pamoja. Achukue kiasi cha kijiko kimoja (cha chai), wakati wa kuumwa na kichwa, na ale na maziwa lala (mala), pamoja na kupasugua mahala paumapo kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa .

Ukosefu Wa Usingizi

Atachukua kijiko cha Habbat-Sawdaa , achanganye na gilasi ya maziwa moto  yaliochanganywa na asali, baada ya kupoa kiasi atakunywa.

Chawa Na Mayai Yake

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa uliosagwa vizuri aukande kwenye siki mpaka uwe kama marhamu, halafu ajipake kichwani – baada ya kunyoa nywele au kuisugua marhamu kwenye mashina ya nywele, halafu aketi katika mwanga wa jua kitambo cha robo-saa. Na hataosha kichwa ela baada ya masaa matano. Atafanya hivyo kila siku kwa muda wa wiki moja.

Kisunzi Na Maumivu Ya Sikio

Tone moja la mafuta ya Habbat-Sawdaa ndani ya sikio husafisha sikio, pamoja na kuyanywa na kusugua sehemu za panda na nyuma ya kichwa, humaliza kisunzi.

Upaa Na Mabaka

Utachukua kijiko cha unga wa Habbat-Sawdaa, siki kiasi cha kikombe kimoja na juisi ya kitunguu saumu kiasi cha kijiko kidogo, vyote hivyo utavichanganya na vitakua namna ya   marhamu, utajipaka baada ya kunyoa sehemu  ya nywele na kuchanja kidogo – kisha utafunga bendeji, utaiacha mpaka asubuhi, baadae utajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa,utaendelea hivyo kwa muda wa wiki moja.

Malengelenge ya Neva katika Ngozi

Atajipaka – sehemu ya malengelenge – mafuta ya Habbat-Sawdaa mara tatu kila siku mpaka iondoke kwa Uwezo wa Allah.

Maradhi Ya Wanawake Na Uzazi

Dawa kubwa inayosahilisha kuzaa ni Habbat-Sawdaa iliochemshwa ikachanganywa na asali na kiziduo cha babunaji (chamomile). H abat sawdaa  ni kama burashi katika uke wa mwanamke yenye faida kubwa kwao pamoja na kutumua mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kila kinywaji cha moto kwa maradhi yote ya wanawake.

Meno Na Maumivu Ya Mafido na Koo

Kiziduo cha Habbat-Sawdaa na kutumia kwa kusukutua kwa kugogomoa, husaidia mno maradhi yote ya mdomo na koo, vivyo hivyo pamoja na kubugia kijiko cha Habbat-Sawdaa na kumeza kwa maji yenye vuguvugu kila siku na kujipaka mafuta yake sehemu ya koo kwa nje na kuusugua ufizi kwa ndani.

Maradhi Ya Tezi

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa na aukande kwa asali na mkate wa nyuki kila siku, kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Chunusi (Acne)

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa aukande katika mafuta ya ufuta (simsimu) pamoja na kijiko cha unga wa ngano. Vyote hivyo atajipaka usoni kuanzia jioni hadi asubuhi, halafu ataosha kwa maji yenye vuguvugu kwa sabuni. Ataendelea kufanya hivyo kwa muda wa wiki moja. Na awe akinywa mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kinywaji chochote cha moto.

Maradhi Yote ya Ngozi

Atachukua mafuta ya Habbat-Sawdaa, mafuta ya waridi (marashi jabali) na unga wa ngano asili, vyote hivyo  kwa viwango sawa, ule unga wa ngano uwe zaidi kuliko mafuta, halafu aukande vizuri. Kabla ya kujipaka, apanguse sehemu yenye ungonjwa kwa kitambaa kilichoroweshwa siki nyepesi, halafu aketi kwenye jua, baadae ajipake dawa hio kila siku. Lakini ajizuie na kila chenye kuchochea hisia kama vile, samaki, mayai, maembe na mfano wake.

Sugu (Chunjua) (Wart)

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa aukande katika siki nzito na asugue kwa kitambaa cha sufi au katani mahala pa sugu asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja.

Kuung`arisha Uso Na Kuurembesha

Ataukanda unga wa Habbat-Sawdaa katika mafuta ya zeituni, na atajipaka usoni halafu apigwe na mwanga wa jua kidogo. Tiba hiyo ataifanya wakati wowote katika mchana na siku yoyote.

Kuunganisha Mvunjiko Haraka

Supu ya adesi (dengu), kitunguu maji pamoja na yai la kuchemsha na kijiko kikubwa cha unga wa Habbat-Sawdaa , utachanganya na supu hiyo japo siku baada ya siku; halafu anywe. Na atasugua sehemu zilizo karibu na mvunjiko kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa, na baada ya kufungua bendeji atajisugua kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa yenye vuguvugu; kila siku.

Mvilio Wa Damu (Contusion)

Atachemsha vizuri konde moja la Habbat-Sawdaa katika chombo cha maji, kisha atakiingiza kiungo kilichovilia damu ndani ya maji hayo- yenye vuguvugu- kwa muda wa robo-saa au zaidi pamoja na kukitaharakisha kiungo hicho. Baada ya hapo atajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa bila ya kufunga kitu. Lakini hatakiwi kukipa uzito kiungo hicho au kukitaabisha. Tiba hiyo ataifanya kila siku kabla ya kulala.

Baridi Yabisi (Rheumatism)

Atachemsha mafuta ya Habbat-Sawdaa na atasugua kwayo ile sehemu yenye ugonjwa, atasugua kwa nguvu kama kwamba yuwasugua mfupa wala sio ngozi! Na atayanywa baada ya kuyachemsha vyema na kuyachanganya na asali kidogo. Ataendelea na tiba hiyo huku akiwa ni mwenye imani na yakini kuwa Allah Atamponya.

(Ki) Sukari (Diabetes)

Utachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kikombe kimoja, manemane (myrrh) iliosagwa kiasi cha kijiko kikubwa, habbarrashad nusu kikombe, komamanga iliosagwa kiasi cha kikombe kimoja, mzizi wa kabichi uliosagwa baada ya kukaushwa kiasi cha kikombe kimoja na kijiko kidogo cha mvuje. Vyote hivyo atavichanganya na atakula kabla ya kula chakula kiasi cha kijiko kimoja, atakula na maziwa lala ili iwe rahisi kumeza.

Shinikizo la Damu (High Blood)

Kila unywapo kinywaji cha moto, tia matone machache ya mafuta ya Habbat-Sawdaa. Pia ujipake mafuta hayo mwili wote, japo wiki mara moja.

Uvimbe Wa Figo(Nephritis)

Atatengeneza kibandiko (cha kitambaa) kutokana na unga wa Habbat-Sawdaa uliokandwa katika mafuta ya zeituni, atabandika sehemu yenye maumivu ya figo pamoja na kubugia funda la kijiko cha Habbat-Sawdaa kila siku kabla ya kula chakula kwa muda wa wiki moja tu; uvimbe utakwisha insha Allah.

Kuvunjavunja Vijiwe Vya Tumboni

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kikombe kimoja kisha aukande katika kikombe cha asali, na atasaga kitungu u saumu punje tatu; atakua akichukua nusu yake akila kabla ya kula chakula kila siku. Pia itakua bora lau atakula limau kila baada ya kula dawa; kwani husafisha kabisa.

Kukojoa Kwa Maumivu (Dysuria)

Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa juu ya kinena kabla ya kulala pamoja na kunywa kikombe cha mafuta hayo yaliochemshwa na kutiwa asali; kila siku kabla ya kulala.

Kukojoa Bila Kukusudia

Atachukua Habbat-Sawdaa na maganda ya mayai yaliosafishwa na yakaokwa na kusagwa halafu yakachanganywa na Habbat-Sawdaa kisha yakaokwa na kusagwa halafu yakachanganywa na Habbat-Sawdaa kisha aingize kwenye maziwa; hatimae anywe kiasi cha kikombe kimoja kila siku na wakati wowote.

Jongo (Edema)

Ataweka kibandiko (cha kitambaa) cha unga wa Habbat-Sawdaa uliokandwa katika siki juu ya kitovu, kwanza ataweka kitambaa. Pia atakula Habbat-Sawdaa kijiko kimoja asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja.

Kifuko Cha Nyongo Na Vijiwe Vyake

Atachukua Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja, manemane iliosagwa robo kijiko na asali kiasi cha kikombe kimoja; vyote hivyo atavichanganya viwe mraba (kama jamu); halafu awe akila kila asubuhi na jioni.

Wengu

Ataweka kibandiko (kilichopashwa moto) cha Habbat-Sawdaa iliokandwa katika mafuta ya zeti katika ubavu wa kushoto; jioni. Na wakati huo huo ata kunywa kikombe cha kiziduo cha uwatu kilichochanganywa asali na mafuta ya Habbat-Sawdaa kidogo, ataendalea na dawa hiyo kwa muda wa wiki mbili mfululizo.

Maradhi Yote ya Kifua na Baridi

Atachukua mafuta ya Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kikubwa atie kwenye maji halafu ayaweke juu ya moto mpaka ianze kufuka moshi, hapo aanze kuuvuta ule moshi puani huku akiwa amejifunika kichwa ili ule moshi usiende upande mwingine. Atafanya hivyo kila siku kabla ya kulala, pamoja na kunywa kiziduo cha zaatari kilichochanganywa na unga wa Habbat-Sawdaa; asubuhi na jioni.

Moyo na Mzungukoa wa Damu

Kuwa na imani katika maneno ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wa sallam) Kwa sababu jambo hili ni katika muktadha wa imani. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wa sallam) alipotuambia kuwa Habbat-Sawdaa ni dawa ya kila ugonjwa, basi hakuna shaka hata chembe kuwa ni dawa ya maradhi yote yanayomfika mwanaaadamu. Mgonjwa wa moyo asikate tamaa kutokana na rehma ya Allah; ni juu yake akithirishe kutumia Habbat-Sawdaa kwa namna yoyote iwayo; iwe ni kwa kula nzima au kwa kunywa wakati wowote uwao.

Mchango (Msokoto Wa Tumbo) (Colic)

Atachemsha vyema anisuni, kamun na nana kwa vipimo sawa na atatia asali kidogo, halafu atie matone saba ya Habbat-Sawdaa ; atakunywa kinywaji hicho kikiwa na vuguvugu pamoja na kupaka mafuta ya Habbat-Sawdaa mahala panaposokota. Baada ya muda mchache maumivu yataondoka.

Kuhara

Atachukua juisi ya chirichiri iliochanganywa na unga wa Habbat-Sawdaa kijiko kikumbwa, atakunywa kiasi cha kikombe kimoja mara tatu kwa siku.

Uziwi

Atachemsha Habbat-Sawdaa pamoja na karafuu, na atakunywa bila ya kuongeza kitu; mara tatu kwa siku.

Gesi Na Maumivu

Atabugia unga laini wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja kabla ya kula chakula akifwatisha gilasi ya maji yenye vuguvugu iliotiwa asali ya muwa kiasi cha vijiko vitatu; atakariri kila siku kwa muda wa wiki moja

————————————————————————

Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat-sawdaa-3 (habba Soda – Chembe Nyeusi )

Imefasiriwa Iliyasa binti Maulana

Asidi (Acidness)

Motone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa yaliotiwa kwenye maziwa ya moto na asali; humaliza asidi.

Uvimbe Wa Tumbo

Atachukuwa unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja na kijiko cha urkusus (licorice) hivyo atavichanganya na juisi ya pea iliotengenezwa pamoja na kokwa zake; halafu anywe; ataona nafuu kubwa.

Maradhi Ya Macho

Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa sehemu za panda kandokando ya macho na kope, atafanya hivyo kabla ya kulala pamoja na kunywa matone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kinywaji chochote cha moto au katika juisi ya karoti.

Amiba (Vijidudu) (Amebiasis)

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja pamoja na kijiko cha kitunguusaumu kilichosagwa, atachangana katika kikombe cha juisi ya nyanya iliotiwa chumvi kidogo; atakunywa kila siku kabla ya kula chakula kwa muda wa wiki mbili mfululizo.

Kichocho (Bilharziasis)

Atakula Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja asubuhi na jioni, yawezekana kuila Habbat-Sawdaa katika chakula kama vile mkate pamoja na kujipaka mafuta yake katika ubavu wa kulia. Ataendelea na dawa hio kwa muda wa miezi mitatu mfululizo. Baadae atapata nguvu na nishati.

Kutoa Wadudu Tumboni

Atakula sandwichi moto ya vitu hivi: kijiko kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa, punje tatu za vitunguu, kijiko kimoja cha mafuta ya zeti, pilipilimanga kidogo na punje kumi za boga (calabash), asubuhi atakunywa kinywaji cha shimari au mafuta ya mbono mara moja pekee.

Utasa

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa, unga wa uwatu na mbegu ya figili kwa vipimo sawa, atakula kijiko kimoja asubuhi na jioni ilihali imekorogwa katika nusu kikombe cha asali, baadae atafuatisha kunywa kikombe kikubwa cha maziwa ya ngamia; basi inshaAllaah itakuwa kheri.

Tezikibofu (Prostate gland)

Atajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa chini ya mgongo na atajipaka chini ya korodani (mapumbu) na kusugua kwa mzunguko pamoja na kula unga wa Habbat-Sawdaa kijiko kimoja, na robo kijiko kidogo cha manemane katika nusu gilasi ya asali iliotiwa katika maji yenye vuguvugu; kila siku na wakati wowote apendao.

Pumu (Asthma)

Atanusa moshi wa mafuta a Habbat-Sawdaa asubuhi na jioni. Pia atakula unga wake asubuhi na jioni kabla ya kula chakula kila siku na pia kujipaka mafuta yake kifuani na kooni kabla ya kulala kila siku.

Kidonda

Atayachanganya matone kumi ya mafuta ya Habbat-Sawdaa, katika kikombe cha asali na kijiko kimoja cha maganda ya komamanga yaliyokaushwa na kusagwa. Atakula kila siku kabla ya kula chakula; baadae atakunywa gilasi ya maziwa yasiyotiwa chochote.

Saratani (Cancer)

Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa mara tatu kila siku na kula kijiko cha unga wake kila amalizapo kula katika kikombe cha juisi ya karoti. Ataendelea hivyo kwa muda wa miezi mitatu.

Nguvu Za Kiume

Atachukua  unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja achanganye (apige) ndani ya mayai saba ya kienyeji; atafanya hivyo siku baada siku kwa muda wa mwezi mmoja. Basi hata kama ana miaka 120 atapata nguvu za barobaro!

Udhaifu kwa Ujumla

Atachukua unga wa habat sosa kiasi cha kikombe kimoja, uwatu mfano wake na ambari ilioyeyushwa kiasi cha kijiko kidogo, vyote atavichanganya katika chombo chenye asali iwe kama jamu; halafu awe akila kama jamu kila siku na wakati wowote apendao lakini kwa mkate wa ngano asili.

Kuleta Hamu Ya Kula

Kabla ya kuanza kula, jipatie Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kidogo na uitafune kwa meno yako, na unywe maji ya kawaida yaliochanganywa na siki kidogo.

Kutibu Ulegevu Na Uvivu

Atakunywa- kabla ya kula – juisi ya machungwa iliochanganywa matone kumi ya mafuta ya Habbat-Sawdaa. Ataendelea hivyo kwa muda wa siku kumi.  Baada ya hapo ataona nishati na uchangamfu.

Nishati akilini Na Wepesi Wa Kuhifadhi

Atachemsha nanaa (mint leaf), aichanganye na asali na aingize matone saba ya mafuta ya Habbat-Sawdaa; anywe kinywaji hiki kikiwa na vuguvugu wakati wowote apendao. Basi ataionea namna fahamu itakavofanya kazi

—————————————————————-

Makosa Wanayofanya Mahujaji Mara Kwa Mara

Imetayarishwa na AL HIDAAYA

MAKOSA YANAYOHUSU IHRAAM:

Mahujaji wengine wanavuka kituo kilichoteuliwa kwa ajili ya ihraam katika njia za msafara wao bila ya kuwa katika hali ya ihraam au bila ya kuwa katika ihraam hapo. Wanaendelea hadi wanafika Jiddah au sehemu nyingine katika mipaka ya vituo ambako huko ndio wanaingia  katika hali ya ihraam.

Hivi ni kinyume na  amri ya Mjume wa Allah  (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo inaamrisha kuwa kila Hujaji anapaswa aingie kwenye ihraam katika kituo kilichoko katika njia ya msafara wake.

Inapomtokea mtu hivyo, ni lazima arudi katika kituo chake cha  ihraam ili aingie katika ihraam. Au itambidi afanye kafara kwa kuchinja kondoo atakapokuwa Makkah na kuigawa nyama yote kuwalisha  masikini.

Hii inawahusu Mahujaji wote, wanaopita kituo wakiwa wamesafiri kwa njia ya angani, baharini au nchi kavu.

Ikiwa mtu hakupitia vituo vitano vilivyoteuliwa kwa ajili ya ihraam katika kila pande ya njia ya msafara, basi ni lazima aingie katika ihraam akiwa katika sehemu iliyo karibu na kituo cha ihraam kilichopo njiani kwake.

MAKOSA YANAYOHUSU TWAWAAF

1.       Kuanza twawaaf katika chanzo kingine kisichokuwa sehemu ya Hajarul-Aswad na hali ni fardhi kuanzia twawaaf hapo.

2.       Kufanya twawaaf ndani ya Hijr Ismaa’iyl.  Hii itamaanisha kwamba ni kuzungua sehemu tu ya Ka’abah na sio Ka’abah yote kwa vile Hijr Ismaa’iyl ni sehemu mojawapo ya Ka’abah yenyewe. Kufanya hivyo itakuwa imeachwa kufanywa twawaaf, na hivyo itakuwa twawaaf haikukamilika mzunguko wake. Twawaaf kama hii haifai.

3.       Kufanya ramal (yaani kupiga hatua ndogo ndogo za haraka) katika twawaaf zote saba na hali ramal inatakikana kufanywa katika mizunguko mitatu tu ya mwanzo ya twawaaful-quduum.

4.       Kusukumana na watu na kusabisha zahma, kuwaumiza watu kutaka kulifikia Hajarul-Aswad ili kulibusu. Vitendo kama hivi vinaleta madhara kwa Waislamu na haturuhusiwi kufanya hivyo.

Itambulike kuwa twawaaf inabakia kuwa sahihi bila ya kulibusu Hajarul-Aswad. Ikiwa mtu hawezi kulifikia  au kulibusu Hajarul-Aswad, inamtosheleza Hujaji anapofika sambamba nalo kuashiria tu kwa mkono na kusema ‘Allahu Akbar’ japokuwa yuko mbali nalo.

5.       Hujaji kufuta au kusugua mkono wake katika Hajarul-Aswad akitegemea kupata baraka. Hili ni jambo lisilokuwa na dalili katika sheria ya Kiislam, hivyo ni bid’ah (uzushi). Sunnah ni kuligusa tu au kulibusu inapokuweko uwezekano wa kufanya hivyo bila ya taabu yoyote.

6.       Kugusa pembe nne za Ka’abah au kuta zake, kusugua na kujipangusa nayo kwa kutegemea kupata baraka. Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakugusa sehemu yoyote ya Ka’abah isipokuwa Hajarul-Aswad na Ruknul-Yaman.

7.       Kusoma du’aa zilizotajwa kuwa ni maalum kwa kila twawaaf moja, na utakuta kuna vijitabu vidogo vidogo vyauzwa huko Makkah vyenye du’aa maalum kwa kila twawaaf, du’aa hizo za kwenye hivyo vijitabu hazina ushahidi wala asli katika mafunzo ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa chache sana. Ni bora mtu aombe yale yaliyothibiti na pia yale anayoyahitajia yeye zaidi kuliko kukariri du’aa za kwenye hivyo vijitabu ambazo hawaelewi hata maana zake. Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakueleza bayana du’aa yoyote isipokuwa ni kusema ‘Allahu Akbar’ anapofikia Hajarul-Aswad na kila anapomaliza twawaaf moja baina ya Ruknul-Yaman na Hajarul-Aswad akisoma:

رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ

Rabbanaa Aatinaa Fid-Duniyaa Hasanataw-Wafil- Aakiharati Hasanataw-Waqinaa ‘Adhaaban-Naar.

((Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto)) [Al-Baqarah:201]

Sehemu nyingine katika mzunguko wa twawaaf, anaweza kusoma Aaya za Qur-aan, du’aa zilizothibitika katika Sunnah, Kumtukuza, Kumsifu, Kumpwekesha, Kumshukuru Allah, Kuomba maghfira, kumswalia    Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) n.k .

8.         Kupandisha sauti kupita sauti za wengine aidha anapoongoza watu katika hizo du’aa ambazo watu wamejipangia au anapomfuata anayemuongoza. Kufanya hivyo kunasababisha kubabaisha mahujaji wengine ambao wanasoma du’aa zao pole pole, wasiweze kupata khushuu katika ibada yao wanapofanya twawaaf.

9.        Kujilazimisha kuswali Maqaam Ibraahiym wakati kuna zahma za watu. Hii ni kinyume na Sunnah, pia husababisha maudhi na misongomano ambayo huishia kuumizana na Mahujaji wengine. Inatosheleza kuswali Rakaa mbili baada ya kumaliza twawaaf mahali popote katika Masjidil-Haraam.

MAKOSA YANAYOHUSU SA’Y

1.       Kwenye kupanda  kilima cha Swafaa na Marwah, baadhi ya mahujaji wanaelekea Ka’abah na kuiashiria kwa mikono wakisema ‘Allahu Akbar‘ kama vile wanavyosema takbira ya Swalah. Kuashiria hivyo ni makosa kwa sababu Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinyanyua mikono yake tu kuomba du’aa. Hapo unaweza kumtukuza Allaah (Subhaanahu kwa Ta’ala), kuomba du’aa yoyote ile upendayo huku umeelekea Ka’abah. Inapendekezeka kusoma dhikr ambayo Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliisoma katika Swafaa na Marwa nayo ni:

لا إِلهَ إلاَّ  اللهُ وَحْدَهُ  لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ،

لا إِلَهَ إلا اللهُ وَحْدَهُ أَنْجَزَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ

Laa Ilaaha Illa-Allaah Wahdahu Laa Shariyka Laah, Lahul-Mulku Walahul-Hamd Wa Huwa ‘Alaa Kulli Shay-in Qadiyr.  Laa Ilaaha Illa-Allaah Wahdahu, Anjaza Wa’dahu Wanaswara ‘Abdahu Wahazamal-Ahzaaba Wahdahu))

((Hapana Mola Apasae kuabudiwa kwa haki ila Allah, hali ya kuwa peke Yake, wala Hana mshirika Wake, ni Wake Ufalme na ni Zake sifa njema Naye juu ya kila kitu ni Muweza.  Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allah hali ya kuwa peke Yake, Ametekeleza ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi peke Yake))

2.     Kuchapuza mwendo katika masafa yote baina ya vilima viwili. Sunnah ni kuchapuza mwendo baina ya milingoti miwili ya kijani na kutembea mwendo wa wakawaida kwengine kote.

MAKOSA YANAYOTENDEKA MINAA

1.    Mahujaji kupoteza muda wao katika mahema kwa kupiga soga badala ya kufanya dhikr au badala ya kuelimishana hapo mambo ya dini na hasa yanayohusu utekelezaji sahihi wa ibada hii ya fardhi. Mahujaji wengi kabisa wanafika huko kutekeleza fardhi hii wakiwa hawana elimu ya kutosha ya jinsi ya kuitekeleza ibada hii. Kwa hiyo kuelimishana ni jambo litakaloleta faida kubwa badala ya kupoteza muda kwa mambo yasiyofaa.

Wengine wanafanya mambo ya bid-ah kama kusoma uradi kwa pamoja, na kusoma adhkaar zisizokuwa zenye dalili kutoka katika mafunzo ya Sunnah.

MAKOSA KATIKA KISIMAMO CHA ‘ARAFAH

1.          Baadhi ya mahujaji wanapiga kambi nje ya maeneno ya ‘Arafah na kubakia hapo hadi jua kuzama, kisha wanaelekea Muzdalifah bila ya kusimama ‘Arafah kama inavyopasa. Hili ni kosa kubwa ambalo linabatilisha Hijja yao kwani kusimama ‘Arafah ni kilele cha Hajj na pia ni fardhi kubakia ndani ya eneo la ‘Arafah na si nje ya eneo lake.

2.          Kuondoka ‘Arafah kabla ya jua kuzama hairuhusiwi kwa sababu Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alibakia ‘Arafah hadi jua kuzama kabisa.

3.          Kujilazimisha katika zahma ya watu kupanda mlima wa ‘Arafah hairuhusiwi, kwa sababu inasababisha madhara na madhara kwa Mahujaji wengine. Eneo lote la ‘Arafah linahesabiwa kuwa ni kisimamo cha’Arafah, na si kupanda mlima wa ‘Arafah wala kuswali katika huo mlima au karibu yake kuwa ndio idhaniwe kuwa mtu amepata  kisimamo cha ‘Arafah.

4.          Kuomba du’aa akiwa anaelelekea mlima wa ‘Arafah ni makosa kwa sababu Sunnah ni kuelekea Qiblah wakati wa kuomba du’aa.

5.          Kulundika chungu ya mchanga au vijiwe siku ya ‘Arafah katika sehemu fulani, jambo ambao haliko katika sheria ya Allah.

MAKOSA KATIKA ENEO LA MUZDALIFAH

1.     Baadhi ya Mahujaji wanapofika tu Muzdalifah na kabla ya kuswali Swalah za Magharibi na ‘Ishaa huanza kukusanya vijiwe vya kurusha katika nguzo za huko Minaa.

Mawe hukusanywa popote katika maeneo ya al-Haram Inajulikana kwamba Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuamrisha mawe ya Jamaratul-‘Aqabah yaokotwe Muzdalifah. Maswahaba walimuokotea yeye mawe asubuhi baada ya kuondoka Muzdalifah na kuingia Minaa. Aliokotewa mawe yaliyobakia yote kutoka Minaa pia.

2.     Baadhi ya Mahujaji huyaosha mawe. Sio pendekezo kufanya hivyo wala sio Sunnah.

MAKOSA KATIKA SEHEMU ZA KURUSHIA MAWE

Baadhi ya Mahujaji wanadhania kwamba kurusha mawe katika nguzo za Jamarah ni kumpiga shaytwaan, hivyo wanarusha mawe kwa nguvu na ghadhabu. Kurusha mawe kuna maana zifuatazo:

1.     Imekusudiwa kuwa ni njia ya kumkubuka Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), ni jambo la kiibada.

2.     Wengine wanarusha mawe makubwa, viatu au mbao. Kufanya hivyo kote ni kuzidisha mambo ya dini ambayo Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameharamisha. Vile vile ni kusababisha madhara ya Mahujaji wengine kwani mtu anaweza kurusha jiwe kubwa kwa mbali likampiga Hujaji aliye mbele yake badala ya kupiga nguzo.  Vijiwe vidogo vyenye ukubwa wa harage au kunde au choroko au punje za mahindi ndio bora zaidi kuvitumia.

3.     Kusababisha zahma, kusukumana na kugombana na wengine katika maeneo hayo ya nguzo hairuhusiwi. Inavyopasa ni kuwa na upole na kurusha vijiwe bila ya kumjeruhi mtu mwingine.

4.     Kurusha vijiwe vyote kwa mara moja ni makosa. Maulamaa wamesema kwamba hii itahesabika kuwa ni kama kurusha kijiwe kimoja. Sharia imetaja kurusha kijiwe kimoja baada ya kimoja na huku Hujaji anasema ‘Allahu Akbar’ kila kijiwe kimoja kinaporushwa.

5.     Kumuwakilisha mtu kurusha mawe, kwa sababu tu ya khofu ya zahma au tabu na mashaka, na hali Hujaji mwenyewe anao uwezo wa kufanya mwenyewe ibada hii hairuhusiwi. Wagonjwa tu na wale walio dhaifu ndio wanaruhusiwa kumuwakilisha mtu kufanya kitendo hiki.

MAKOSA KATIKA KUZURU KABURI LA MTUME (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)

1.     Kugusa na kusugua mikono katika kuta na nondo za chuma, kufunga nyuzi katika mihimili yake na vitendo vingine vya namna hiyo wakati wa kuzuru kaburi la Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kutegemea kupata baraka. Hivyo ni bid’ah. Baraka zinapatikana kwa kufuata amri za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na Mjumbe Wake (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na si kufuata mambo ya kuzushwa yasiyo na maana wala manufaa.

2.     Kwenda katika mapango ya Mlima wa Uhud au mapango ya mlima wa Hiraa au Thawr karibu na Makkah na kutundika vitambara au kuomba du’aa huko. Haya hayamo katika mafunzo ya kutekeleza fardhi hii. Na yote hayo ni kujitakia mashaka na tabu kwani ni mambo ya bid’ah katika dini na wala hayana msingi katika Sheria.

3.     Vile vile kuzuru sehemu nyingine kwa kudhania kuwa sehemu hizo ni athari za mabakio ya Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Mfano sehemu ambayo ngamia wake alikaa, au kisima cha ‘Uthmaan na kukusanya udongo sehemu hizo kwa kutegemea kupata baraka, yote ni mambo ya bid’ah.

4.     Kuwaita waliokufa wakati wa kuzuru makaburi ya Al-Baqi’i au makaburi ya mashuhadaa wa Uhud na kurusha sarafu ili kutegemea kupata baraka za sehemu waliozikiwa watu ni makosa makubwa kabisa bali ni shirki kama walivyosema Maulamaa. Ni dhahiri pia katika Qur-aan na Sunnah ya Mjumbe Wake (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba aina zote za ibada ziwe kwa ajili ya Allaah Pekee. Hairuhusiwi kumuomba mwingine au kuchinja, kuweka nadhiri au aina yoyote ya ibada isipokuwa ziwe kwa ajili ya Allah kwani Anasema:

((وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاء))

((Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Allah kwa kumtakasia Dini)) [Al-Bayyinah:5]

Vile vile Anasema:

((وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّهِ أَحَدًا))

((Na hakika misikiti ni ya Allah, basi msimuabudu yeyote pamoja na Allah)) [Al-Jinn: 18]

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Awazidishie Waislamu elimu ya dini, na Atuepushe katika makosa, kuvuka mipaka ya sheria Yake na kufuata mambo ya bid’ah, hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kujibu du’aa zetu. Aamiyn.

FAHARASA
Ihraam Hali ya kuingia katika tendo la kufanya ibada ya Hajj, au pia nguo za Hajj zinaitwa hivyo.
Ramal Kwenda mwendo wa mbio mbio kwa hatua ndogo ndogo katika mizunguko mitatu ya mwanzo kwenye twawaaf
Twawaaf Mzunguko katika Ka’abah
Hajarul Aswad Jiwe jeusi lilioko pembeni mwa Ka’abah
Hijr Ismaa’iyl Chumba cha Ismaa’iyl
Twawaaful-Quduum Twawaaf ya kuingia (mwanzo unapowasili)
Rukn Al-Yaman Pembe katika Ka’abah inayoelekea Yemen
Khushuu Unyenyekevu
Maqaam Ibraahiym Jiwe alilokanyaga Nabii Ibraahiym na kusimama kuomba Du’aa baada ya kujenga Ka’abah
Masjidul-Haraam Msikiti Mtukufu
Sa’y Kutembea baina ya Swafa na Marwa
Al-Haram Sehemu Takatafiu
Ram-y Kurusha mawe
Jamaratul-‘Aqabah Mnara ulio karibu na Makkah
Jamarah Mnara katika Minaa

—————————————————-

Mwanzo Wa Maumbile – Kabla Ya Kuumbwa Ardhi Na Mbingu

Imeandikwa na Alhidaaya.com

Kabla ya kuanza visa vya Mitume na tuanze na utangulizi katika kujua hali ilivyokuwa kabla ya kuumbwa ardhi na mbingu.  Zifuatazo ni Aya na Hadithi zinazothibitisha maumbile ya mwanzo kabisa.

Anasema Allaah سبحانه وتعالى

}}اللَّهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ{{

{{Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu, na Yeye ndiye Mlinzi juu ya kila kitu}} Az-Zumar: 62

Amesema vile vile

}}خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالأََرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ الرَّحْمَانُ فَاسْأَلْ  بِهِ خَبِيرًا{{

{{Ambaye ameziumba mbingu na ardhi, na viliomo ndani yake kwa siku sita. Kisha akatawala juu ya A’rshi, Arrahman, Mwingi wa Rehema! Uliza khabari zake kwa wamjuaye}}  Al-Furqaan: 59

Ama Yeye Allaah سبحانه وتعالى ni wa mwanzo na wa  milele  na hakuna kilichokuwepo kabla Yake.

}}هُوَ الأََوَّلُ وَالأَخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ{{

{{Yeye ndiye wa Mwanzo na ndiye wa Mwisho, naye ndiye wa Dhaahiri na wa Siri, naye ndiye Mjuzi wa kila kitu}}  Al-Hadiid:3

Hadithi inatuelezea alipokuwa Allaah سبحانه وتعالى kabla ya kuumba ardhi na mbingu.

((عن عامر العقيلي أنه قال يا رسول الله أين كان ربنا قبل أن يخلق السموات والأرض قال كان في عماء ما فوقه هواء وما تحته هواء ثم خلق عرشه على الماء))   الإمام أحمد

(( Imetoka kwa ‘Amir Al-‘Aqiyliy kwamba alimuuliza Mtume صلى الله عليه وسلم  Ewe Mjumbe wa Allaah, alikuwa wapi Mola wetu kabla ya kuumba mbingu na ardhi? Akasema: Alikuwa katika sehemu tupu (empty space) juu yake hewa na chini yake hewa kisha akaumba ‘Arshi  katika maji ))  Imaam Ahmad

Na kabla ya kuumba chochote kwanza Allaah سبحانه وتعالى  kwa Ujuzi Wake Aliiumba kalamu na Akaiamrisha  hiyo kalamu iandike katika ubao wa ‘Lawhun Mahfuudh”  makadirio ya kila kitu.

((عن عبادة بن الصامت رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم إن أول ما خلق الله القلم ثم قال له اكتب فجرى في تلك الساعة بما هو كائن إلى يوم القيامة))   رواه الإمام أحمد وأبو داود والترمذي

((Kutoka kwa ‘Ubaadah bin As-Swamit رضي الله عنه alisema; kasema Mtume صلى الله عليه وسلم kitu cha mwanzo kabisa alichokiumba Allaah سبحانه وتعالى ni kalamu kisha akaiamrisha  iandike, ikaanza kuandika tokea saa hiyo (mambo yote yatakayotokea) mpaka siku ya Kiyama))  Imaam Ahmad, Abu Dawuud na At-Tirmidhy

Makadirio hayo yaliandikwa miaka khamsini kabla ya  kuanza kuumba mbingu na ardhi

)) عن عبد الله بن عمرو بن العاص قال سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول كتب الله مقادير الخلائق قبل أن يخلق السموات والأرض بخمسين ألف سنة قال وعرشه على الماء))  مسلم .

((Kutoka kwa Abdullah Bin ‘Umar bin Al-‘Aas kasema, nimemsikia Mtume صلى الله عليه وسلم anasema Allaah سبحانه وتعالى ameandika makadirio ya viumbe kabla ya kuumba mbingu na ardhi  miaka khamsini alfu, akasema na ‘Arshi Yake ilikuwa katika maji)) Muslim

}}هُوَ الَّذِي خَلَق السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَكَانَ عَرْشُهُ عَلَى الْمَاء{{

{{ Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji }}  Huud:7

Kwa hiyvo kutokana na hadithi hizo na qauli za Maulamaa wengi, kwamba kitu cha kwanza ilikuwa ni ‘Arshi katika maji, kisha kalamu ambayo iliandika makadirio yote, kisha tena ndio mbingu na ardhi.  Wallaahu A’alam.

Na hadithi ya Imaam Bukhari inathibitisha vile vile hayo:

((عن عمران بن حصي قال: قال أهل اليمن لرسول الله صلى الله عليه وسلم جئناك لنتفقه في الدين ولنسألك عن أول هذا الأمر فقال كان الله ولم يكن شيء قبله: وفي رواية معه وفي رواية غيره:  وكان عرشه على الماء وكتب في الذكر كل شيء وخلق السموات والأرض : وفي لفظ  :ثم خلق السموات والأرض ))البخاري

((Kutoka kwa ‘Umar bin Haswiin ambaye kasema,  walikuja wageni   kutoka Yemen walimuuliza  Mtume صلى الله عليه وسلم : tumekuja kijifunza dini na kukuuliza jambo la mwanzo, (yaani kabla  ya kuumbwa kitu)   akasema, Alikuwa Allaah, na hakukuwa na kitu kabla Yake, (Na Riwaya nyingine)  na ‘Arshi Yake ilikuwa katika maji, akaandika makadirio ya kila kitu, (Na kauli nyingine ) kisha akaumba mbingu na ardhi))   Al-Bukhaariy

Aya zifuatazo zinasema kuwa maumbo ya mwanzo yaliyoumbwa na Allaah سبحانه وتعالى  ambayo yalitendeka kwa siku sita .

}}إِنَّ رَبَّكُمُ اللّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ أَلاَ لَهُ الْخَلْقُ وَالأَمْرُ تَبَارَكَ اللّهُ رَبُّ الْعَالَمِين{{

{{Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote}}

Al-A’araaf :54

}}اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْش{{

{{Mwenyezi Mungu ndiye aliye umba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa siku sita, na akatawala kwenye Kiti cha Enzi}}  As-Sajda :4

Wataalamu wetu walizungumzia kuhusu siku sita hizi kama ni sawa sawa na siku zetu au ni siku Zake Allaah سبحانه وتعالى ?

Wengine wamesema ni siku za Allaah سبحانه وتعالى  kama alivyosema:

}}وَإِنَّ يَوْمًا عِندَ رَبِّكَ كَأَلْفِ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ{{

{{Na hakika siku moja kwa Mola wako Mlezi ni kama miaka elfu mnavyo hisabu nyinyi}}   Al-Hajj:47

Sheikh Al-Jazairiy amesema inaweza pia kuwa ni siku hizi zetu za kawaida kwani Allaah سبحانه وتعالى Ni Muweza wa kila kitu:

}}إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَنْ يَقُولَ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ{{

{{Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa}}

Yasiin :82

Hadithi hii Sahihi imesimuliwa na Muslim inaelezea taratibu za maumbile katika wiki yalivyokuwa:

((عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه  قَالَ أَخَذَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِيَدِي فَقَالَ خَلَقَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ التُّرْبَةَ يَوْمَ السَّبْتِ وَخَلَقَ فِيهَا الْجِبَالَ يَوْمَ الأَحَدِ وَخَلَقَ الشَّجَرَ يَوْمَ الإِثْنَيْنِ وَخَلَقَ الْمَكْرُوهَ يَوْمَ الثُّلاثَاءِ وَخَلَقَ النُّورَ يَوْمَ الأََرْبِعَاءِ وَبَثَّ فِيهَا الدَّوَابَّ يَوْمَ الْخَمِيسِ وَخَلَقَ آدَمَ عَلَيْهِ السَّلاَم بَعْدَ الْعَصْرِ مِنْ يَوْمِ الْجُمُعَةِ فِي آخِرِ الْخَلْقِ فِي آخِرِ سَاعَةٍ مِنْ سَاعَاتِ الْجُمُعَةِ فِيمَا بَيْنَ الْعَصْرِ إِلَى اللَّيْلِ)) مسلم

((Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه   kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم alionyesha kwa mkono wake akasema, Allaah سبحانه وتعالى Ameumba   udongo siku ya Jumamosi, Akaumba majabali siku ya Jumapili, Akaumba miti siku ya Jumatatu, Akaumba makirihisho (yaani mambo ya kukirihisha yote, na vidudu (Germs)  na maradhi) siku ya Jumanne, Akaumba mwangaza siku ya Jumatano, Akaeneza wanyama siku ya  Alkhamisi, Akaumuumba Adam عليه السلام baada ya Alasiri siku ya Ijumaa katika mwisho wa kuumba kwenye  saa ya mwisho   ya Ijumaa baina ya Alasiri na Usiku)) Muslim

Qatada alisema, Mayahudi walisema kwamba Allaah سبحانه وتعالى  aliumba maumbile yote kwa siku sita kuanzia siku ya Jumapili kisha Akamalizia Ijumaa kwa hiyo alichoka akapumzika  siku ya Jumamosi ndio maana wakaifanya Jumamosi kuwa ni siku yao ya mapumziko. Na Allaah سبحانه وتعالى Akawakatalia kauli yao hiyo kwa kuteremsha Ayah hii:

( At-Tabari 22:376)

}}وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالأََرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ{{

{{Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilio baina yao mnamo siku sita; na wala hayakutugusa machofu}}  Qaaf 50:38

Uthibitisho mwengine wa kuwa Allaah سبحانه وتعالى  hakuchoka kuumba chochote:

}}أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَلَمْ يَعْيَ بِخَلْقِهِنَّ بِقَادِرٍ عَلَى أَنْ يُحْيِيَ الْمَوْتَى بَلَى إِنَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ{{

{{Je! Hawaoni ya kwamba Mwenyezi Mungu, aliye ziumba mbingu na ardhi, na hakuchoka kwa kuziumba, kuwa ni Muweza wa kuwafufua wafu? Kwani? Hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu}}   Al-Ahqaaf:33

Wallaahu A’alam

Vimekusanywa kutoka:

1)Tafsiyr Ibn Kathiyr

2) At-Twabariy

3) Aysarut-tafaasiyr (Sh Abubakkar Al-Jazaairiy)—————————————————————————————————————

TOBA YA KWELI

Kuomba msamaha kwa M/Mungu ni tabia au uaminifu wa kinaa ya mwanadamu kuamini kwamba yupo duniani kwa ajili ya matakwa ya Allah na atarudi kwa Allah muda wake ukifika kinyume cha hayo ni kiburi na kutoamini kuwa iko siku ya ufufuo .

Baba yetu Nabii Adam (A.S) kishatufunza jambo hili na ni tendo la awali la kiumbe mtu kuomba msamaha na baadae kukiuka amri ya Mola basi vyenginevyo yule anaejiona si katika wanaadamu kitabia anafuatana na tabia ya iblis ya kiburi kwa muumini yoyote anaeshindana na amri za M/Mungu baada ya kumbainikia yale yaliohimizwa huyo hufanya jeuri tuu na kulewa na uhai na tabia hii humfanya kiumbe kuwa si wa maana ni mchupa mipaka mazuri mengi yaliofanywa na wanadamu wameyaona faida yake hapa hapa duniani licha ya akhera kwenyewe hivyo hivyo na uovu wote na mfanyiwe na mwanadamu hapa duniani baadhi ya matokeo yake yameleta madhara kwa mfanyaji au jamii iliyonyamaza isikerwe . Watu katika maisha ya sasa hivi wamekuwa wakiheshimu vialama vilivyowekwa na wanadamu zaidi ya kuheshimu yale ambayo kayataja na kuyaamuru M/Mungu katika Qur-ani.

Mwanadamu hukata tamaa na maisha pale yanapomgeukia lakini hana budi kujiuliza lakini mimi nilifanya nini wakati faraja iliponipa uso, makosa yetu yameendelea yamezidi mema yetu, na roho zetu zimejaa matumaini ya kuishi zaidi siyo kufikiria kama siyo sasa hivi basi halafu bado hatufikiri jinsi tumbo la ardhi lilivyomeza vipenzi vyetu kama siyo baba, mama, kaka, dada, na kama si ndugu mwana, kama si mke mume na kama si jamaa rafiki, hao wote tungependa tuwe nao , tusafiri nao , tusali nao , tule nao futari na tusherehekee nao pamoja harusi . Wako wapi leo , njia ndio hiyo hiyo kwa zamu bila ya kupanga foleni bila ya kujua saa wala pahala . Kwa maana hiyo kwanini hatuishi kwa wasiwasi maana hatujui dakika ipi zamu yako au yangu , ikiwa mtume Muhammad (S.A.W) katangulia mbele ya haki na wewe na mimi ndie kiongozi wetu iko shaka tena kuwa tutabakia maisha . Saa ngapi tutaomba kusamehewa madhambi yetu ikiwa hata ndani ya mwezi huu mtukufu wa ramadhani baadhi tunatenda dhambi wangapi waliodhulumu kupitia milango ya biashara wakala viapo vya harama vya manunuzi ???

Ni wangapi vijana wanaoshindwa kuheshimu hata mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ??? wanaendelea kunywa kunusa vilivyoharamishwa , wangapi hawaogopi wanapikiwa futari na watu waliowaweka kinymba tu bila ya kuwaoa, au wanapeleka futari huko sambamba na kulikohalalika kwao, dhambi zitatendwa sana ndio tunatakiwa tuyakimbilie maghfira haraka kabla ya kuja kunyakuliwa roho na malaika wa mauti, baadhi tumetupa wazazi wetu hata wanahudumiwa na watu wa nje na hali tupo wazima na tuna uwezo japo mdogo wa kujikimu licha ya tulivyotajirishwa , wangapi tunavaa vizuri na kuwaacha mama au baba zetu na matambara maana mtu mzima anastahili vivazi hivyo . Wangapi miongoni mwetu wamesafiri wako ugenini si wa salamu au kalamu kwa wazazi wao ??? na hata hawataki hata wajulikane kama wako wapi ili wasipelekewe barua na maombi ya dhiki na wazazi wao na ndugu zao . Yoyote atakaejisahau nae atasahauliwa atalipwa na wanawe pia vile upandavyo ndivyo utakavyovuna si kila jambo linalosemekana leo lipo , basi uhodari wako ni mtihani wa maisha na kila umuonae ni mpungufu sio ujinga wake nae anaonjwa katika subira.

Kwenye aya 12 ya surrat ashuraa.M/Mungu anatukumbusha kwa kutuambia “Funguo za mbingu na aridhi ziko katika kadhi yake humfungulia  ridhiki amtakae na humfikishia yeye ndiye ajuaye kilakitu.”Mwisho wa tafsiri.

Tujitahidi wale wenye midomo mirefu dhidi ya wazee wetu tuzikomeshee akili na ndimi zetu .Maana tupo mzee akitusemeza hunungunikia mdomoni ,tupo tunao waeleza wazee wetu na kuwaliza hasa wakati tunajua huyu mzee kwa hali yake ya utuuzima hajiwezi tena basi maskini mengi huyamalizia pale pale alipolala au kukaa ,hapo sisi husahau zao wakati wa uchanga na udogo wetu humfokea, tukanungunika , tukafinya usoo , mwisho wa habari tukamwacha kama alivyo kutwa nzima haya yanajulikana  na baadhi ya wazazi waliofikia hali hii ,hata wakiwa na njaa huwogopa kuwaomba chakula watoto wao maana atafoka na kumkemea ,pengine atamsubiri jirani amnongonezee na alicholetewa akifiche asije mwanawe akajuwa maana akijuwa matusi mapya dhidi yake yatamwandama

Waombe maghafira walofikia kiwango hiki na tuliobaki M/Mungu asitufikishe kuwanyanyapaa wazee wetu kiasi hicho.

M/Mungu atuzidishie imani na Wazee wetu ,atujalie huduma zetu kwao ziwe funguo njema zakuipata pepo chini ya radhi zao . Amiein

KUMBUKA NDUGU YANGU MTUPA MZEE HANA MWISHO MWEMA .   M/MUNGU AKUHIDI WEWE NA SISI AMEEEIN.

Ni mwenzenu All Hajj Udiii katika njia ya kukumbushana.(Muomba Toba

PAKISTAN YAZINDUA TOVUTI MBADALA YA FACEBOOK YA WAISLAM

Print E-mail
Sunday, 30 May 2010
Sample ImagePakistan imezindua tovuti mbadala ya Facebook baada ya tovuti hiyo kupigwa marufuku nchini humo kutokana na kuanzisha shindano la vijikatuni vya kumvunjia heshima Mtume Mohammad SAW.
Tovuti hiyo mpya inayojulikana kama Millatfacebook inawaunganisha zaidi ya Waislamu Billioni moja laki tano pamoja na wafuasi wa dini nyinginezo. Aidha tovuti hiyo ya kijamii ya Waislamu inatoa huduma mbadala ya tovuti ya Kimarekani ya Facebook ambayo inalaumiwa kwa kutoheshimu faragha ya watumizi wake. Mamia ya maelfu ya wananchi wa Pakistan wamekuwa wakiandamana wiki za hivi karibuni kupinga ukurasa wa Facebook uliowahimiza watumizi wake kutuma taswira zinazomvunjia heshima Mtume Mohammad SAW. Serikali ya Pakistan iliwaamuru wanaotoa huduma za intaneti kuizuia tovuti ya Facebook baada ya mawakili wa Kiislamu kushinda kesi iliyoitaka serikali kupiga marufuku tovuti hiyo ya kijamii yenye makao yake Marekani. Anwani ya tovuti mpya ya Kijamii ya Waislamu ni http://www.millatfacebook.com

ITIMAI YA KISLAMU

ASALAM ALEYKUM st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

Assalaam Alaykum

ZAWADI YA IJITIMAI

Wengi wa watu wa zama zetu za leo tumekuwa niwagumu wakuamini kutokea kwa mambo japokuwa tunajiita Waumini. Tupo tunaojishughulisha tuu kama tuliosahau kumbe hakuna sahau hapo ila ni kuwaficha walimwengu wenzetu wasitujue malengo yetu.

Basi huweza hata kusema uwongo kukinga maslahi ya kidunia tupo wengine tunaosahau ghafla baada ya yakufanikiwa yale yalokuwa yakitutesa na kutuhangaisha kimaisha. Lakini tuliponyooshewa mambo  tuliyageuza mambo tukichunguza tutajiona ni vichekesho tuuu  kwani hatuangalii umri na tunasahau vifo ambavyo kila siku vipo. Ndiyo Maana Mtu hufanya Maasi makubwa na kuyaendeleza siku ya pili kwa pumbao la kuamka tena na tena  lazima tuwe ni Watu wenye kufikiri na  kushukuru yale ambayo Mola ametuvuwa nayo, lakini kwanini huyaingia kichwa kichwa na mengine huyarejea kwa jeuri ya hali ya juu ?

Kwenye Jamii wapo Watu wenye kuwapa Nasaha Wenziwao mara kwa mara wengine huwaita watu wa (DAAWAAH) lakini watu hawa hata waonekanapo majiani au kuingia nyumba za Ibada huonekana ni  Wepesi mno.Watu kwa zama zetu hizi huwa tayari  wanaona wamebobeya katika kuwaidhiwa mambo na tayari huchaguwa nani wakumsikiliza na nani wakumpuuza  sehemu rahisi sana  wakuyagunduwa haya katika misikiti (na hata ndani ya chat humu utaona) yetu takribani Watu wasimamao na kutowa Dawaah ya Angalau dakika mbili baada ya sala huangaliwa ni nani?

Wapo wanaowapendeza Watu  basi umma wa Waumini hutulia tuli yaani watayari kumsikiliza, lakini wapo wasimamao na kuomba angalau dakika tano wakumbushane na Waumini, Sihasha! akaachwa peke yake na Imamu alompa ruhusa ya kuongea labda na wanaosali rakaa mbili za sunnah aghalabu watu wa daawaah huwa na matumaini yakufikisha Ujumbe kwa Waumini wenziwao  ni vyema kuwapa moyo na kuwasikiliza tusiondoke kwa sura ya kufedhehesha Muumini hatuelewi kaja na mada gani  tena kawaomba waumini wenzake kuzungumza kwa dakika tano Muondokoo tunao ondoka ni kama kusema Aaa! Hana lolote huyo.

Ni kweli baadhi yao ni Wana genzi katika fani hii lakini tendo hilo liangaliwe kama kijana mwenyewe angelijituma sehemu iliyo haramu angelitupa moyo upi? Wakati huyu kajituma kafika katika nyumba ya Ibada (kheri).

Inawezekana baadhi tuna dharura baada ya sala  kazi za watu au miadi iliyo mema basi hatuwezi kulaumika kwa kweli nyengine zinakubalika .Pamoja na kukumbushana huku lakini vyema pia kwa wale watowao daawah wakakumbuka juu ya viwango vya daawaah wazitoazo.

Jamii wanayoihubiria na nidhamu wanayoisimamia aidha na muda wanaotumia hii itamsaidia Mtowa daawah kujenga sura yenye mvuto maalum kwa Jamii  kwani Hekima na Rai ni mambo  muhimu katika hadhara ya Waumini ni vizuri lugha ambayo yenye mvuto ijibainishe na mkabala uwe wa kuangalia rika za Waumini.

Hatusemi asiye na sifa hizi au zaidi ya hizi asiwasilishe ujumbe lakini kila kile tunachohisi kuwa ni mvuto tuegemee Aya hata moja ambayo hutosha  ambayo ikiwakilishwa vyema basi humjaza Imani Msikilizaji kwa maana hiyo tuendelee kujifunza mbinu hizi za kuwakabili wenzetu na pia Waumini wasiwache au kuwachagua nani wakukaa kumsikiliza na yupi apandapo kiririni Watu wakumte kanzu wapige viatu chini safari tena angalau yakwenda kuendelea na shughuli za maisha lakini pengine yakuwahi chance katika nafasi ya dama liliposimamia wakati wa wito wa Adhana .Lazima tupime Uzito wa mambo yetu ya kila siku kitako kile kina thawabu  na thamani ya thawabu haipimwi kwa uzito wa mawe ya kilo za madukani mwetu , na kwa wale wenye kukurupuka tuu na kuanza kutowa  dawaah bila ya Idhini  ya wakuu wa msikiti hiyo haifai na tuombe rukhusa kesha na tuendelee na mawaidha tuliyoyakusudia hii itasaidia sana kujenga nidhamu yetu  kwani idhini ni faraja kubwa kwa aliyeomba na mwenye kuombwa

Na siyo vyema kuigeuza misikiti kama ni nyumba ya mtu au kikundi cha Watu Fulani Msikiti ni nyumba ya MWENYEZI MUNGU (S.W.). Maimamu nao ni vyema wakawa na tabia zamfano ili Jamiii iwaheshimu na kuwakubali wawe na lugha lainii, Suhuba nzuri, Uaminifu, Ukinaifu, Utulivu na usimamiaji mzuri wa kazi zake za Uimamu.

Tupo miongoni mwetu tunaoingilia nidhamu za misikiti  na kuparurana na Maimamu au kwakudhania tuu au tabia aliyonayo kweli Imamu huyo kazi hii siyo yakuingangania kama kiwango cha Uadilifu kidogo mno tutabeba dhima nzito kwa unganganizi.

Alhamdulillah tuwashukuru Maimamu wetu wengi kwa juhudi kubwa zao wanayoichukuwa kwa kuichunga misikiti lakini vyema wakawa imara pale haki na sheria ya msikiti inapoingiliwa. Kinyume chake, tupo  wale wenye tabia ya swalaa swalaa swalaa kumhimiza mkimu swalaa bila ya Idhini ya Imamu, lakini wapo wale wenye  tabia ya mafuta kidogo na kwa kuwasubirisha au kutaka aina ya watu Fulani wafike kwanza ndiyo atowe Idhini ya watu kwenda kusali, Sio kufuata wakati au wingi wa Maamuma waliokwisha fika msikitini basi hadi tunongonezane nakuanza kumsema  tena Imamu  minongono mbali  hiyo itatufanya tuwanze kusimangana misikitini na hiyo huleta Dhambi kwa wanaosema, lakini tusiyaache yakapevuka MWENYEZI MUNGU NDIYE AJUWAYE ZAIDI ATATUONGOZA.

YARABBI IKINGE JAMII YETU YA KIISLAMU KUTOKANA NA MAWAZO POTOFU TUJALIE UKUMBUSHO TUNAOKUMBUSHANA KUWA WENYE MANUFAA NA WAJALIE KHERI NAWALIPE MALIPO YAO WATU WA DAAWAAH NA WAJALIE WALIOANDAA JITIMAI WAWEZE KULETA JENGINE ZAIDI YAHILI, YARABBII TUJALIE KUFUATA NJIA YA HAKI NA TUONYESHE BATIL POPOTE ILIPO TUIKIMBIE NA UTUWEZESHE KUIKIMBIA BATIL NA KUIFUATA HAKI ILIPO  (AMIIIN).

WABILLAHI TAWFIQ

Ndugu yenu katika kuamsha jamii na kukumbushana  All Hajj Udii

(YARABBI TOBAA).

_____________________________________________________________________________________________________________________

UADILIFU WA MASHABA

Zipo baadhi ya hadithi zenye utatanishi au zenye kubeba maana zaidi ya moja, ambazo wakristo katika tovuti zao huzitumia kwa kuzifasiri hadithi hizo kwa maslahi yao, au kwa maana wanayoitaka wao, kinyume na maana yake ya kweli, kwa ajili ya kuupiga vita Uislamu.

Kinachoskitisha zaidi ni kuwa wapo baadhi ya Waislamu ambao kwa kutaka maslahi yao, bila kujali athari wanayoiacha, utawakuta wakipoteza wakati wao mkubwa wakifanya utafiti na kunukuu hadithi za aina hizo huku wakitaja baadhi ya makosa ya kibinadamu yaliyowahi kutendwa na baadhi ya Masahaba (Radhiya Llahu anhum), kisha wanayakuza makosa hayo na kuyafanya kuwa ni dalili ya ubaya wa Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

Yareti kama wakati wao wangeliupoteza katika kufanya utafiti juu ya maadui wa Mwenyezi Mungu kama vile Abu Jahal au mnafiki Abdullahi bin Saluul au Firauni au Haaman au Abu Lu’ulua al Majusiy, aliyemuuwa Khalifa wa pili wa Waislamu Umar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu). Bali kinyume na hivyo, utawaona wanaunyamazia uadui wao watu hao, juu ya kuwa ukafiri wao umethibiti ndani ya Qurani tukufu na ndani ya mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na badala yake wanaziunguza juhudi zao katika kujaribu kuwapaka matope Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

Kwa kufanya hivyo wanawapa makafiri silaha kali pamoja na ushahidi wanaoutaka katika kuupiga vita Uislamu na kuwapiga vita waliotuletea dini hii, kwa sababu kwa kuwatuhumu Masahaba bila ya uhakika wala ushahidi ulio wazi, ni kuutuhumu Uislamu waliotuletea Masahaba hao (Radhiya Llahu anhum) baada ya kuupokea kutoka kwa sahibu yao Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

Hadithi ya hodhi

Miongoni mwa hadithi wanayoitumia katika ubabaishaji wao huo ni ile hadithi maarufu ya Hodhi, na namna Malaika watakavyowarudisha watu watakaotaka kunywa ndani ya hodhi hilo la Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), wakidai kuwa hadithi hiyo inawakusudia Masahaba hawa (Radhiya Llahu anhum) sahibu zake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na marafiki zake na wenzake alioanza nao tokea siku ile ya mwanzo ya kuwalingania watu katika dini hii tukufu.

Imepokelewa katika hadithi hiyo kuwa Siku ya Kiama, wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) atakapokuwa anawanywisha watu maji kutoka katika hodhi lake, watakuja Malaika na kuwaondoa makundi kati yao, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) atakaposema:

“Hawa ni katika Masahaba wangu.”

Malaika watajibu:

“Je Unajuwa waliyoyazuwa baada yako?”

Na katika riwaya nyingine, Malaika watasema:

“Walirtaddi hawa wakarudi nyuma.”

Anasema Ibni Abdul Barr: “Maana hasa ya hadithi hizi ni kuwa kila mwenye kuzusha mambo katika dini, atakuwa miongoni mwa watakaofukuzwa penye hodhi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).”

Tukiendelea na kuichambuwa Shubha hii inayowakanganya baadhi ya watu wakadhani kuwa watakao ondolewa penye hodhi ni hawa Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) waliosimama naye tokea siku za mwanzo kisha wakaendelea kusimama naye katika shida zake zote na vita vyote dhidi ya makafiri; vita vya Badar, vita vya Bani Qaynuqaa, vita vya Uhud, vita Khandaq, Fathi Makka, Hunayn na vita mbali mbali. Hawa ambao baada ya kufariki kwa sahibu yao Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) waliendelea kuisimamia dini hii kidete na kuipigania kwa hali zao na mali zao mpaka ikaenea ulimwengu mzima.

Daraja yao

Daraja ya Masahaba na heshima yao katika dini ni jambo lisilokubali kujadiliwa na Muislamu yeyote mkweli mwenye kupenda haki, kwa sababu hawa ndio ambao Mwenyezi Mungu aliwahusisha kwa kuwafanya kuwa sahibu zake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), wakamsadiki na kumfuata na kumnusuru na wakaifuata nuru aliyokuja nayo, na wakafanya kila juhudi kwa kujitolea roho zao na mali zao kwa ajili ya kuipigania dini hii tukufu mpaka ilipokamilika.

Hawa ndio wale waliosifiwa na Mwenyezi Mungu walipoambiwa kuwa wao ni umma bora kupita zote zilizoletwa kwa ajili ya watu. Na Mwenyezi Mungu Akaridhika nao.

Masahaba ni waaminifu wa umma huu walioibeba sheria na kuieneza ulimwenguni kote mpaka ikatufikia sisi hivi sasa. Hii Qur’ani tuliyo nayo na haya mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) yametufikia kupitia kwao (Radhiya Llahu anhum).

Kwa hivyo kitendo cha kuwatilia shaka Masahaba hawa watukufu katika uadilifu wao ni katika kuipiga vita dini na kuwafanya watu wasiamini masdari za dini tulizopokea kutoka kwa Masahaba hao watukufu (Radhiya Llahu anhum). Kwa sababu Qurani tukufu na Mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), yote tumeyapata kupitia kwao.

Ndiyo maana maulamaa wa Kiislamu wanatutaka tuwe na msimamo imara dhidi ya kila mwenye kuwatuhumu Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

Inasikitisha kuona kuwa wapo miongoni mwa Waislamu wenye kuwatuhumu baadhi ya Masahaba, na wanafanya hivyo makusudi kwa ajili ya kukifikia kile wanachokitaka tu, na wakazitumia hizi hadithi za hodhi katika kujaribu kuwapaka matope Masahaba hawa watukufu (Radhiya Llahu anhum).

Katika kujaribu kuharibu sifa za Masahaba (Radhiya Llahu anhum), wakazitumia hadithi mfano wa hii inayosema:

“Wakati mimi nimesimama, litakuja kundi, nitakapowajuwa, atatoka mtu kutoka kwangu na kusema: ‘Twendeni’, Nitasema: ‘Wapi?’ Atasema: ‘Motoni wallahi.’ Nitasema: ‘Wana makosa gani?’ Atasema: ‘Hawa wamertaddi na kurudi nyuma baada yako..”

Bukhari na wengine

Sifa zao ndani ya Qurani

Maulamaa wanasema:

Wa kwanza kutoa hukmu Yake kuwa Masahaba (Radhiya Llahu anhum), ni watu waadilifu ni Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala na Mtume wake (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kama ilivyoandikwa ndani ya Qurani tukufu na kama ilivyokuja kwa njia Mutawaatirah katika Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na miongoni mwa hukmu hizo ni kauli Yake Subhanahu wa Taala Aliposema:

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاء عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاء بَيْنَهُمْ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلا مِّنَ اللَّهِ وَرِضْوَانًا سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ذَلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَى عَلَى سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا

Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio toa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa.

Al Fat’h – 29

Na Akasema:

وَالسَّابِقُونَ الأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللّهُ عَنْهُمْ وَرَضُواْ عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَداً ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ

“Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.”

At Tawba 100

Na Akasema:

لَـكِنِ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُواْ مَعَهُ جَاهَدُواْ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ وَأُوْلَـئِكَ لَهُمُ الْخَيْرَاتُ وَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

Lakini Mtume na wale walio amini pamoja naye walipigania Jihadi kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio watakao pata kheri nyingi, na hao ndio wenye kufanikiwa.

At Tawba – 88

لَقَدْ رَضِيَ اللَّهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا

Na Akasema:

Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waumini walipo fungamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa Ushindi wa karibu.

Al Fat’h – 18

Sifa zao ndani ya Sunnah

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

“Kheri ya watu ni wa karne yangu kisha wanaowafuata kisha wanaowafuata.”

Bukhari na Muslim

Na kauli yake (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliposema:

“Msiwatukane Sahaba wangu. Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hata mmoja wenu atajitolea katika njia ya MwenyeziMungu kugawa dhahabu ukubwa wake mfano wa jabali Uhud, basi hatofikia gao lao wala hata nusu ya gao lao”.

Bukhari na Muslim

Na akasema:

“Allah Allah! (nakuusieni) juu ya Sahaba wangu. Msiwageuze kuwa malengo yenu baada ya kuondoka kwangu. Kwani mwenye kuwapenda basi kwa kunipenda mimi (ndiyo) amewapenda, na mwenye kuwachukia basi kwa kunichukia mimi (ndiyo) amewachukia. Na mwenye kuwaudhi ameniudhi (na) mimi, na mwenye kuniudhi mimi amemuudhi Allah, na mwenye kumuudhi Allah, anakaribia Kumnyakuwa.”

Attirmidhy

Zipo hadithi nyingi za namna hii zenye kuwasifia na kueleza juu ya fadhila zao mbali mbali na mitihani waliyopambana nayo, na kututaka wafuasi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kuwaheshimu na kuwakirimu na kutowaudhi wala kuwageuza kuwa ni malengo yetu tunayoyatumia kila tunapotaka kuipitisha batil yetu. Na nasaha zote hizi zinatoka kwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala na kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

Katika kauli za maulamaa

Amesema Imam Ibni Najjar:

“Aliyesifiwa namna hii na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala, itakuwaje tena asiwe muadilifu. Ikiwa mbele ya mahakama wanatosha mashahidi wawili tu kuthibitisha uadilifu wa mtu, itakuwaje basi ikiwa ushahidi unatoka kwa Muumba wa mbingu na ardhi Subhanahu wa Taala.”

Shar’hi ya Kawkab Al Muniyr (2/475)

Anasema Al Khatwiyb Al Baghdaadiy

“Usafi wa Masahaba (Radhiya Llahu anhum) na uadilifu wao hauna lazma ya kusifiwa na wanadamu baada ya kusifiwa na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Aliyeangalia ndani ya nafsi zao akatujulisha juu ya ukweli wao.

Na hata kama Mwenyezi Mungu asingetujulisha juu ya sifa zao na kuridhika Kwake nao, basi kule kupigana kwao Jihaad kwa mali zao na nafsi zao, wamewaua baba zao na watoto wao waliopigana upande wa makafiri, haya yanatokana na yakini waliyokuwa nayo ndani ya nyoyo zao juu ya nusra ya Mwenyezi Mungu iliyowajia.”

Al Kifayah fiy Ilm Annhihaayah – 48-49

Kwa hivyo kuzichukulia zile hadithi za hodhi kuwa waliokusudiwa ni hawa Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) waliomsadiki na kumuamini, wakamsaidia na kumnusuru, kunakuwa ni kuzikataa aya zote na riwaya zote zilizo sahihi zenye kutubainishia fadhila zao na heshima yao mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume wake (Swallah Llahu alayhi wa sallam).

Kuwatuhumu Masahaba (Radhiya Llahu anhum) ni mfano wa kuukataa ushahidi wa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala, kwa sababu itakuwaje Mwenyezi Mungu atujulishe juu ya watu Alioridhika nao na kutujulisha juu ya fadhila zao na kwamba atawaingiza katika Pepo

Sharh (maelezo) Ya Hadiyth Nambari 14 An-Nawawy – Damu Ya Muislam Haimwagiki Ila Kwa Mambo Matatu
HadiythNa: Alhidaaya.com

الحديث الرابع عشر” لا يحل دم امريء مسلم إلا بإحدى ثلاث” عن ابْنِ مَسْعُودٍ رضي اللهُ عنه قالَ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((لاَ يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ إلاّ بإحْدَى ثَلاَثٍ: الثَّيِّبُ الزَّاني، وَالنَّفْسُ بالنّفْسِ، وَالتَّارِكُ لِدِيِنِهِ الْمُفَارِقُ لِلْجَماعَةِ)). رَوَاهُ الْبُخَارِيّ وَمُسْلِمٌ
HADITHI YA 14

DAMU YA MUISLAMU ISIMWAGWE ISIPOKUWA KWA SABABU TATU

Kutoka kwa Ibn Mas’uudرضي الله عنه ambaye alisema: Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:

((Damu ya Muislamu haipasi kumwagwa isipokuwa katika hali tatu: Mzinzi Muolewa (Mtu mzima aliyeoa/olewa), uhai kwa uhai (nafsi kwa nafsi) na kwa yule anaeeacha dini na akajifarikisha na jama’ah (kundi) (amejitenga na watu wa dini yake)) [Imesimuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim]

Hadiyth hii inaelezea utakatifu wa maisha ya Muislam kama ilivyo katika sheria ya Kiislamu. Kwa ujumla roho ya Muislam haitolewi ila ikiwa atatenda uhalifu unaoleta madhara katika jamii. Uhalifu huo uwe mbaya sana hadi umfanye kuwa hastahiki tena kuishi. Uhalifu huu umetajwa kwa ujumla katika Hadiyth hii.
Makafiri wasioamini akhera huwa ni vigumu kwao kuifahamu hukmu hii ya Kiislam ya kuuawa. Uislam, kuuawa kuna maana kuwamba ni kumalizika kwa maisha ya kidunia, lakini huyo anayeuliwa huenda akalipwa Pepo hivyo awe na maisha bora zaidi kuliko ya duniani na Muislamu hutegemea hivyo. Na ndio maana wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mwanamke alimuendea Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na akakiri madhambi yake ya uzinifu na akauawa kwa kupigwa mawe.

Hadiyth hii inaelezea kidogo na kuambatana na maelezo ya Hadiyth Namba 8 ifuatayo ambayo maisha ya mtu huwa ni ya usalama katika haki ya Uislam.

الحديث الثامن”أمرت أن أقاتل الناس” عن ابنِ عُمَرَ رضي الله عنهما أنَّ رسُوَل الله صلى الله عليه وسلم قال: ((أُمِرْتُ أَنْ أُقاتِلَ النَّاسَ حتَّى يَشْهَدُوا أنْ لا إلَهَ إلاَّ اللهُ وأنَّ محمداً رسوُل اللهِ، ويُقِيمُوا الصَّلاَةَ، ويُؤتُوا الزَّكاةَ، فإذا فَعَلوا ذَلِكَ عَصَموا منِّي دِماءَهُمْ وأمْوَالَهُمْ إلا بِحَقِّ الإِسْلامِ، وحِسابُهُم على اللهِ تعالى)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ

HADITHI YA 8
NIMEAMRISHWA NIPIGANE NA WATU

Kutoka kwa Ibn ‘Umar رضي الله عنهما ambaye alisema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم kasema :

((Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka washahadie kuwa hakuna mungu isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى na Muhammad ni Mjumbe wa Allaah سبحانه وتعالى, na mpaka watakaposwali, na wakatoa Zakah, na wakifanya hivyo, watakuwa wamepata himaya kwangu ya damu yao na mali yao isipokuwa kwa haki ya Uislam. Na hesabu yao itakuwa kwa Allaah ((سبحانه وتعالى[Imesimuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim]

Muislam lazima aheshimu maisha, mali na heshima ya Muislam mwenzake kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hijjatul-Widaa’ (Hijja ya ya mwago)
((أيها الناس, ان دماءكم وأموالكم حرام عليكم الى أن تلقوا ربكم كحرمة يومكم هذا في شهركم هذا في بلدكم هذا, ألا هل بلّغت؟ اللهم فاشه))
((Enyi Watu, damu zenu (kuua), mali zenu (kunyang’anya, kuiba) ni haraam kwenu hadi mtakapokutana na Mola wenu…)
Maisha ya Muislam yana heshima mbele ya Allaah.

Ingawa Muislam anapaswa kuheshimika kama ilivyo katika sheria, lakini kwa hali nyingine, huenda akafanya kitendo kiovu hadi kikamfanya kuwa hastahiki tena kuishi.

HALI TATU ZILIZOTAJWA ZINAZOSTAHIKI KUULIWA MUISLAMU

1- الثَّيِّبُ الزَّاني
At-ThayyibAz-Zaaniy – Mzinzi Muolewa (Mtu mzima aliyeoa/olewa)

Mzinifu ni mwenye kutenda zinaa yaani kutenda kitendo cha ndoa cha haraam. Adhabu yake ni kama ifuatayo:

– Mzinifu aliyeoa au kuolewa – kupigwa mawe hadi afariki.

– Asiyeoa au kuolewa – kupigwa mijeledi (bakora) 100 hadharani kisha mwanaume ahamishwe nje ya mji kwa muda wa mwaka mmoja.

Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Ametuwekea njia ya halali ya kutimiza matamanio ya kinafsi na kujitosheleza, nayo ni ndoa. Kisha pia Ameonya kuwa Muislam asikaribie kabisa zinaa, na Ametuwekea njia mbali mbali za kumhifadhi mtu asifikie kuingia katika kitendo hicho, njia hizo ni:

1- Hijaab
2- Kutokuchanganyika wanawake na wanaume. Na kutokaa mwanamke na mwanamume wasio maharimu faragha.
3 – Ametuonya tusikaribie kabisa zinaa Anaposema:

وَلاَ تَقْرَبُواْ الزِّنَى إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاء سَبِيلاً ﴿32﴾32. Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya. [Al-Israa: 32]
Pia Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Ametupa sifa za Waja Wa Ar-Rahmaan ambao ni wale wasiofanya uovu huu pamoja na nukta ya pili ya kuua,

وَعِبَادُ الرَّحْمَنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا ﴿63﴾ وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا ﴿64﴾ وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا ﴿65﴾ إِنَّهَا سَاءتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴿66﴾ وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَلِكَ قَوَامًا ﴿67﴾ وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ وَمَن يَفْعَلْ ذَلِكَ يَلْقَ أَثَامًا ﴿68﴾ يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا ﴿69﴾ إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُوْلَئِكَ يُبَدِّلُ اللَّهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿70﴾ وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّهِ مَتَابًا ﴿71﴾ وَالَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ الزُّورَ وَإِذَا مَرُّوا بِاللَّغْوِ مَرُّوا كِرَامًا ﴿72﴾ وَالَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ لَمْ يَخِرُّوا عَلَيْهَا صُمًّا وَعُمْيَانًا ﴿73﴾ وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿74﴾ أُوْلَئِكَ يُجْزَوْنَ الْغُرْفَةَ بِمَا صَبَرُوا وَيُلَقَّوْنَ فِيهَا تَحِيَّةً وَسَلَامًا ﴿75﴾ خَالِدِينَ فِيهَا حَسُنَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴿76﴾

63. Na waja wa Ar-Rahmaan Mwingi wa Rehma ni wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama!
64. Na wale wanaokesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama.
65. Na wale wanaosema: Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi.
66. Hakika hiyo ni kituo na makao mabaya
67. Na wale ambao wanapotumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo
68. Na wale wasiomwomba mungu mwengine pamoja na Allaah, wala hawaui nafsi Aliyoiharimisha Allaah isipokuwa kwa haki, wala hawazini – na atakaye fanya hayo atapata madhara,
69. Atazidishiwa adhabu Siku ya Qiyaama, na atadumu humo kwa kufedheheka.
70. Isipokuwa atakayetubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Allaah Atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Allaah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu
71. Na aliyetubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kweli kweli kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).
72. Na wale ambao hawatoi ushahidi wa uongo, na pindi wapitapo penye upuuzi, hupita kwa hishima yao
73. Na wale ambao wanapokumbushwa Ishara za Mola wao Mlezi hawajifanyi viziwi nazo, na vipofu.
74. Na wale wanaosema: Mola wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wacha Mungu.
75. Hao ndio watakaolipwa makao ya juu kwa kuwa walisubiri, na watakuta humo maamkio na salamu
76. Wadumu humo – kituo na makao mazuri kabisa
[Al-Furqaan]

2- وَالنَّفْسُ بالنّفْسِ
Nafsi (uhai) kwa nafsi (uhai)

Mwenye kumuua mwenzake bila ya sheria naye anapaswa kuuliwa.

Hii iko wazi kabisa katika Qur-aan kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِصَاصُ فِي الْقَتْلَى الْحُرُّ بِالْحُرِّ وَالْعَبْدُ بِالْعَبْدِ وَالأُنثَى بِالأُنثَى فَمَنْ عُفِيَ لَهُ مِنْ أَخِيهِ شَيْءٌ فَاتِّبَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ وَأَدَاء إِلَيْهِ بِإِحْسَانٍ ذَلِكَ تَخْفِيفٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَرَحْمَةٌ فَمَنِ اعْتَدَى بَعْدَ ذَلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿178﴾ وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَاْ أُولِيْ الأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿179﴾

178. Enyi mlioamini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasi katika waliouawa – muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke. Na anayesamehewa na ndugu yake chochote basi ashikwe kulipa kwa wema, na yeye alipe kwa ihsani. Huko ni kupunguziwa kulikotokana na Mola wenu Mlezi, na ni rehema. Na atakayevuka mipaka baada ya haya, basi yeye atapata adhabu iumizayo.
179. Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili msalimike
[Al-Baqarah: 178-179]

Lakini kuna visivyohesabiwa katika sheria hii mojawapo imetajwa katika aayah yenyewe nayo ni,

Ya kwanza:

Jamaa za mtu aliyeuliwa wanaweza kuchukua fidia ya pesa (blood-money) kutoka kwa muuaji.

Ya pili:

Ni baba anapomuua mtoto.

Maulamaa wengi wao wameona kwamba baba asiuliwe kwa kitendo hicho. Rai hii imesimuliwa na ‘Umar ibnul-Khatwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu). Na Hadiyth iliyosimuiwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo inasema:
((لاَ يُقادُ الوَالِدُ بالْوَلَد ))((Hakuna adhabu/malipo kwa baba kwa sababu ya mwana)) [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad na wengineo]
Lakini Imaam Maalik ambaye hakuitambua hadiyth hii kaona kwamba ikiwa baba amemuua mwana makusudi, bila ya makosa yoyote, basi naye auliwe.

Ya tatu:

Ni hali ya mtu aliye huru anapomuua mtumwa.

Hii ni rai ya wengi wa Maulamaa. Abu Haniyfah na wafuasi wake wamaona kwamba ikiwa mtu atamuua mtumwa wake mwenyewe, asiuliwe, lakini mtu akimuua mtumwa wa mtu mwengine basi auliwe.

Ama wengine wameona kuwa mtu huru akimuua mtumwa yeyote basi naye auliwe.

Ya nne:

Muislamu anapomuua asiye Muislamu.
Aayah nyingine zinazohusiana na kipengele hicho:

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ أَن يَقْتُلَ مُؤْمِنًا إِلاَّ خَطَئًا وَمَن قَتَلَ مُؤْمِنًا خَطَئًا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ وَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَى أَهْلِهِ إِلاَّ أَن يَصَّدَّقُواْ فَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ عَدُوٍّ لَّكُمْ وَهُوَ مْؤْمِنٌ فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ وَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُمْ مِّيثَاقٌ فَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَى أَهْلِهِ وَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةً فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ تَوْبَةً مِّنَ اللّهِ وَكَانَ اللّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿92﴾ وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَآؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا ﴿93﴾ 92. Na haiwi Muumini kumuua Muumini ila kwa kukosea. Na mwenye kumuua Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipokuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini, basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na akiwa ni miongoni wa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Allaah. Na Allaah ni Mjuzi na Mwenye hikima
93. Na mwenye kumuua Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Allaah Amemkasirikia, na Amemlaani, na Amemuandalia adhabu kubwa. [An-Nisaa: 92-93]

3. وَالتَّارِكُ لِدِيِنِهِ الْمُفَارِقُ لِلْجَماعَةِ
Yule anaeacha dini na akajifarikisha na jama’ah (kundi) (amejitenga na watu wa dini yake).

Mtu akisilimu au akiwa ni Muislamu harusiwi tena kutoka. Dini si kitu cha mchezo, mtu kuingia na kutoka atakavyo. Mwenye kutoka katika Uislam huitwa “Murtad” na hukmu yake ni kuuliwa. Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
((من بدل دينه فاقتلوه))((Mwenye kubadilisha dini yake (ya Kiislamu) muueni)).
[Al-Bukhaariy 6922, Abu Dawuud 4329, At-Tirmidhiy 1483].

Maelezo mengineyo ya Hadiyth hii:

Mauaji yatekelezwe na wahusika wa serikali na sio mtu binafsi; mfano kaka aliyeuliwa ndugu yake asitoke kwenda kulipiza kisasi mwenyewe bila ya kupelekwa kesi yake mahakamani kisha tena Hakimu (Qaadhi) ndiyo atoe hukmu. Ikiwa mtu atafanya hivyo basi naye itapasa apewe adhabu, lakini sio adhabu ya kuuliwa kwa vile kamuua mtu ambaye alistahiki kuuliwa.

Hilo la mwenye kubadili na kuuliwa, lina maelezo mengi na ufafanuzi mrefu ambao mnaweza kuupata katika makala ya KURITADI iliyomo ndani ya ALHIDAAYA katika kiungo kifuatacho:

Kurtadi (kutoka Katika Dini)

FAIDA TUNAZOPATA KATIKA HADIYTH HII:

· Maisha Ya Muislam ni ya thamani na yanalindwa na sheria. Hakuna mwenye haki ya kuchukua maisha yake Muislam hadi awe amefanya jarima ambayo itahitajia adhabu ya kuuawa.

· Kufanya Maana Ya Hadiyth Dhwa’iyf
Hadiyth

Maulamaa wanasema kuwa: Hadiyth dhaifu ni ile isiyokuwa na sifa zinazokubalika. Na wengine wakasema kuwa Hadiyth dhaifu ni ile isiyostahiki kuitwa Sahihi wala Hasan (njema).

Zipo aina nyingi ya Hadiyth dhaifu zikiwemo:

Mursal:

Nazo ni zile zilizonyanyuliwa moja kwa moja kutoka kwa Taabi’iy mpaka kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم

Taabi’iy ni Muislamu aliyeishi wakati wa Maswahaba رضي الله عنهم akawaona lakini hajamuona Mtume صلى الله عليه وآله وسلم

Kwa mfano Tabi’iy aseme:

“Mtume wa Mwenyezi Mungu صلى الله عليه وآله وسلم amesema……”

Wakati yeye hajawahi kuonana na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم

Maulamaa wamekhitalifiana juu ya kuzitumia Hadiyth za aina hii mafungu manne:

1- Imaam Abu Haniyfah na Imaam Malik na baadhi ya wanavyuoni wanasema kuwa Hadiyth hizi zinafaa kutumika.

2- Imaam An-Nawawi akieleza juu ya Jamhur kubwa ya Maulamaa na pia akimnukuu Imaam Shaafi’iy anasema kuwa Hadiyth za aina hii zinaweza kutumika kama ni hoja lakini si hoja ya moja kwa moja (ya kutegemewa).

3- Imaam Muslim anasema; “Hadiyth Mursal kwetu sisi na kwa wengi kati ya wanavyuoni si hoja hata kidogo.

4- Wengine wakasema kuwa inaweza kuwa hoja pale tu ikiwa imepokelewa kutoka kwa Tabi’iy mkubwa, kisha Hadiyth hiyo iwe imefanyiwa kazi na Swahaba yeyote au na wanavyuoni wengi.

Munqati’i:

Hizi ni zile Hadiyth zilizokatika Isnadi zake, yote sawa kukatika huko kuwe mwanzo au mwisho wa majina ya wapokezi.

Al Mudallas:

Nazo ni zile Hadiyth ambazo muelezaji aeleze kuwa amehadithiwa na mtu aliyeishi katika zama moja kisha ikathibiti kuwa hawajapata kuonana. Au ahadithie kama kwamba amehadithiwa na mtu huyo wakati ukweli ni kuwa hakuhadithiwa na mtu huyo, kwa mfano aseme:

“Amenihadithia Fulani.” Au: “Nilimsikia Fulani.” Wakati ingekuwa sahihi kama angesema:

“Amesema Fulani.” Au: “Kutoka kwa Fulani.”

Maulamaa wanasema kuwa Mudallis (muelezaji wa Hadiyth hizi) hazikubaliwi riwaya zake hata kama aliwahi mara moja tu katika maisha yake kusema uongo katika hadiyth.

Wengine akiwemo Imaam Shaafi’iy wakasema kuwa; ni zile Hadiyth alizodallis tu hazikubaliki, lakini zile alizozielezea kwa njia sahihi zinakubalika.

Mudh twarib:

Nazo ni zile Hadiyth nyingi zinazogongana (Contradiction). Hadiyth aina hii zimedhoofishwa kwa sababu ya kugongana kwake na kutokuwa thabit.

Munkar:

Nazo ni zile zilizohadithiwa na ‘Dhaifu’ (asiyeaminika) kisha zikakhitilafiana na Hadiyth zilizohadithiwa na Thiqah (mwenye kuaminika).

Al Mudha’af:

Nazo ni zile zilizodhoofishwa na baadhi ya Maulamaa kutokana na udhaifu wa wapokezi wake, wakati baadhi nyingine ya Maulamaa wakasema kuwa ni sahihi.

Al Matruk:

Nazo ni zile zilizohadithiwa na mtu anayetuhumiwa kwa uongo katika Hadiyth au hata katika mazungumzo yake. Au anayetuhumiwa kuwa ni Faasiq wa maneno au vitendo. Matruk pia ni yule mwenye kusahau sana au mwenye kukosea sana.

Wakati gani Hadiyth dhaifu inakuwa na nguvu?

Hadiyth dhaifu inapata nguvu pale tu ikiwa rawi wake (mwenye kuhadithia) anatuhumiwa kuwa ameanza kusahau sahau Sharti awe Thiqah hatuhumiwi kwa Uongo wala kwa Ufaasiq wala kwa kusahau sana. Kisha Hadiyth alozungumza juu yake ziwe zimepokelewa kwa njia nyingi sana, na hapo inapanda darja na kuwa ‘Hadiyth Hasan.’

Na hii ni kwa sababu imepokelewa kwa njia zinazokubalika tena kwa njia ya rawi asiyetuhumiwa kwa uongo au kwa sababu ovu za kumdhoofisha.

Kuzifanyia kazi Hadiyth dhaifu:

Maulamaa wamekhitalifiana katika hukumu za kuzifanyia kazi Hadiyth za aina hii katika makundi matatu:

1.Wapo wanaosema kuwa Hadiyth hizi hazifai kuzifanyia kazi kabisa, yote sawa iwe katika kuamrisha mambo ya Fadhila au katika Hukmu. Na hii ni kauli ya Yahya bin Ma’iyn na Abubakar bin Al-‘Arabiy na pia Al-Bukhaariy na Muslim.
2.Wengine wakasema kuwa Hadiyth hizi zinaweza kufanyiwa kazi.
3.Na wengine wakasema kuwa Hadiyth hizi zinaweza kufanyiwa kazi katika mambo ya Fadhila na katika kuwaidh watu tu. Na kwamb zisitumike katika kutoa hukmu au katika ibada, tena ziwe zimekamilisha baadhi ya masharti kama vile asituhumiwe mmojawapo wa wapokezi wake kwa uongo au ufuska nk. Na pia udhaifu wa Hadiyth usiwe mkubwa sana, na pia mtu anapoelezea Hadiyth ya aina hii awajulishe watu kuwa ina udhaifu ndani yake.
Anasema Dr. Muhammad Ajjaj Al Khatwiyb katika kitabu chake ‘Al-Mukhtaswar Al-Wajiyz fiy ‘Uluum al Hadiyth:

“Mimi naunga mkono rai ya mwanzo inayosema kuwa Hadiyth dhaifu zisifanyiwe kazi kabisa. Zipo Hadiyth za kutosha zilizo sahihi katika mambo ya fadhail na mawaidha kiasi ambapo haina haja ya kuingiza Hadiyth zenye shaka zinazoweza kuwa ni maneno ya uongo aliyozuliwa Mtume wa Mwenyezi Mungu صلى الله عليه وآله وسلم

Pia Fadhail na Tabia njema ni katika mambo muhimu sana katika dini kwa hivyo haina haja kuzitumia Hadiyth dhaifu kwa ajili yake.”

Rai ya Dr. Muhammad Al Ajjaj ni bora zaidi kwa sababu mtu atawezaje kuiamini Hadiyth iliyosimuliwa na Mudallis, mtu mwenye kubadilisha majina ya mashekhe au ya miji akijua kuwa anawadanganya wasikilizaji wake, au muongo ‘Kadhaab’ anayependa kuwadanganya watu katika mambo ya kidunia ambaye hatoshindwa kuwadanganya katika mambo ya dini.

Na vipi mtu ataweza kuifanyia kazi Hadiyth Mudhtwarib inayogongana na Hadiyth sahih au Hadiyth Matruk iliyodhoofishwa kwa ajili ya tabia ovu za msimulizi kwa ajili ya uongo na ufuska n.k.

Na Allah Anajua zaidi
uzinifu, uuaji, na kuritadi ni madhambi makubwa kabisa katika sheria ya Kiislam, sheria ambayo inalinda maisha na uhai wa mtu. Hivyo, sheria hiyo itakuwa kali na kumuadhibu adhabu inayostahi yeyote atakayefanya madhambi hayo yasiyostahi nafasi ya mtu huyo katika jamii safi yenye nidhamu na ustaarabu.

· Moja ya malengo ya adhabu ya kifo ni kulinda utakatifu na maisha ya Waislam, Kama ambavyo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anavyosema:

((Enyi mlioamini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasi katika waliouawa – muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke. Na anayesamehewa na ndugu yake chochote basi ashikwe kulipa kwa wema, na yeye alipe kwa ihsani. Huko ni kupunguziwa kulikotokana na Mola wenu Mlezi, na ni rehema. Na atakayevuka mipaka baada ya haya, basi yeye atapata adhabu iumizayo}} {{ Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili msalimike)) [Al-Baqarah: 178-179]

WA ALLAAHU A’ALAMQu’Uluum At-Tajwiyd – Sayansi Ya Tajwiyd Hukmu Za Tajwiyd “…na soma Qur-aan kwa utaratibu na utungo” عُلومُ التَّجْوِيدِ (Kitabu cha) ‘Uluum At-Tawjiyd Sayansi Ya Tajwiyd Assalaamu ‘Alaykum wa RahmatuLlaah wa Barakaatuh, Karibuni kujifunza Sayansi Ya Tajwiyd (Maarifa Ya Elimu Ya Tajwiyd) Ili uweze kulisoma somo hili unahitaji kuwa na Adobe Reader Version 8. Ingia katika kiungo kifuatacho uweze kuishusha (download). Adobe Reader Tunawaomba na tutashukuru mkiweza kutuma maoni yenu au makosa yoyote mtakayoyakuta humo kupitia anuani ya tajwiyd@alhidaaya.com Hati Miliki (Copy Right): Kitabu hiki cha Tajwiyd si cha kuuzwa bali kinatarajiwa kugaiwa bure pindi kitakapochapishwa. Hivyo ni ruhusa kutolesha nakala na kugawa bure popote itakapohitajika. Kwa hali yoyote ile isifanyiwe mauzo. Tunawaomba ndugu zetu msitusahau katika du’aa zenu. •01-Tunzo •02-Dibaji •03-Utangulizi Wa Mwandishi •04-Historia Ya Elimu Ya Tajwiyd Na Viraa (Visomo) •05-Umuhimu Wa Elimu Ya Tajwiyd •06-Faida Ya Kuwa Na Elimu Ya Tajwiyd •07-Fadhila Za Kusoma Qur-aan •08-Aina Za Viraa (Visomo) •09-Adabu Za Kusoma Qur-aan •10-Sajdatut-Tilaawah (Sijda Ya Kisomo) •11-Makosa Makubwa Ya Dhahiri Na Madogo •12-Isti’aadhah Na BismiLLaah •13-Makhaarij Al-Huruuf (Sehemu Zitokapo Herufi) •14-Matamshi Ya Herufi Za Hijaaiyyah (Alfabeti) •15-Mukhtasari Wa Sehemu Kuu Za Makhaarij Al-Huruuf •16-Sifa Ze Herufi •17-Mukhtasari Wa Sifa Za Herufi Zote •18-Kusimama Na Kuanza •19-As-Sakt (Kipumziko) •20-Mukhtasari Wa Alama Za Kusimama •21-Namna Ya Kutamka Herufi Ya Mwisho Wa Neno •22-Hukmu Za Nuun Saakinah Na Tanwiyn •23-Hukmu Za Miym Saakinah •24-Idghaam Al-Mutamaathilayni, Al-Mutajaanisayni, Al-Mutaqaaribayni •25-Al-Qalqalah •26-Tafkhiym Na Tarqiyq •27-Hukmu Za Raa •28-Hukmu Za Laam •29-Hamzatul-Qatw’ Na Hamzatul-Waswl •30-Iltiqaau Saakinayan •31-Ahkaam Za Madd •32-Al-Madd At-Twabiy’iy •33-Al-Madd Al-Far’iy •34-Al-Huruuf Al-Muqqattwa’ah •35-Chati Ya Madd •36-Makosa Yanayotatiza Kwa Ujumla •37-Adabu Za Kukhitimisha Qur-aan •38-Hitimisho •39-Du’aa •40-Vitabu Vya Marejeo •41-Ufafanuzi Wa Maneno r-aan Neno Kwa Neno

تَرْجَمَةُ  مَعاَنِي كَلِماَتِ الْقُرْآنِ الْكَرِيمِ

بِالُلغَّةِ السَّوَاحِيلِيَّةِ كََلِمَةً بِكَلِمَةٍ

Tarjuma Ya Maana Ya Maneno  Ya

Qur-aan Tukufu Kwa

Kiswahili Neno Kwa Neno

Assalaamu ‘Alaykum

Karibuni kujifunza ‘Tarjuma ya Qur-aan Tukufu Neno Kwa Neno Kwa Lugha Ya Kiswahili’.

Ili uweze kuisoma Qur-aan hii unahitaji kuwa na Adobe Reader Version 8.

Ingia katika kiungo kifuatacho uweze kuishusha (download).

Adobe Reader

Tunawaomba na tutashukuru mkiweza kutuma  maoni yenu au makosa yoyote mtakayoyakuta humo kupitia anuani ya quraan.nenokwaneno@alhidaaya.com

Hati Miliki (Copy Right): Qur-aan hii sio ya kuuzwa bali inatarajiwa kugaiwa bure pindi itakapochapishwa. Hivyo ni ruhusa kutolesha nakala na kugaiwa bure popote itakapohitajika. Kwa hali yoyote ile isifanyiwe mauzo.

Tunawaomba ndugu zetu msitusahau katika du’aa zenu.

Jazaakumu Allaahu Khayra

Enyi Mlioamini!m melazimishwa kufunga (Saumu)kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu”(2:183)

Na Ramadhan Himid, Zanzibar.

WAISLAMU hivi sasa wapo katika heka heka za kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan lakini la muhimu ambalo waislamu hao wanatakiwa kulikumbuka ni ule utii wa hali ya juu kwa Mola wao waliouonyesha wakati wa mwezi huo mtukufu.

Kwa maana hiyo Mungu yule yule aliekuwa akiheshimiwa kwa utii mkubwa ndani ya Ramadhan, bado yupo milele na milele hivyo wakati wote anahitaji kuheshimiwa kwa kufuata yale aliyoyaamrisha na kuacha yale aliyoyakataza.

Mwezi huo mtukufu ulikuwa ni darasa tosha kwa baadhi ya dada zetu wanaopenda kuvaa nguo zisizoendana na maagizo ya Dini ya Kiislamu na hivyo yale mabaibui waliyokuwa wakiyavaa wakati wa mfungo wa Ramadhan , waendelee na tabia hiyo kwa kuwa Mungu aliyekuwepo wakati wa Ramadhan ndiye yule yule aliyeko milele .

Wanawake wenye tabia kama hiyo ya kuvaa watakavyo wasijidanganye kwamba Mungu wa Ramadhan hatamani kuona miili yao, na hivyo kumalizika kwa Ramadhan waachwe wafanye tu watakavyo.

Tusimchezee Mungu kwani mwanamke akionekana unyoya mmoja tu wa nywele zake na mtu ambaye si maharimu wake, kwa maana mumewe au jamaa zake kama baba yake au mama yake siku ya Kiyama atavutwa nywele zake hadi kwenye mashimo ya moto, sasa seuze kila siku kutembea uchi.

Kwa kweli dada zetu ndani ya Ramadhan walikuwa wakipendeza kwa kuvaa mavazi ya heshima kiasi kwamba vile vishawishi vya zinaa vilikuwa sitrahisi kuchemka mwilini mwa mwanamume.Subiri Ramadhan imalize utawaona kama wanagombea umisi kila mmoja anamshinda mwenzake kwa kuvaa uchi.Lahaulah.

Basi bila shaka tumeshuhudia wenyewe kwa jinsi imani zetu zilivyonawirika ndani ya mfungo wa Ramadhan.Waliokuwa hawasali miezi mengine yote waliacha uvivu wao wakajitakasa kwa Mola wao.

Kama vile haitoshi Wengi tulikuwa tukikesha usiku kucha kusali Sala za usiku kama Tahajud, Sunna za Haja, Witri na kadhalika pamoja na kuleta kila aina ya maghafira kiasi kwamba mioyo yetu wakati alipokuwa akitajwa Mola wetu Allah (S.W) na Mtume wake Muhammad (S.A.W) ilijawa na hofu kubwa kuashiria kuwa kweli tuliiva kiimani.

Tupo pia tuliolia usiku kucha kutubia madhambi yetu tuliyoyafanya, na Mungu atulipe shufaa njema kutokana na nia zetu, lakini tukumbuke kuwa mwisho wa Ramadhan sio mwisho wa Ibada.

Si hivyo tu bali wapo pia wale waliojaliwa kukaa itikafu misikitini kwa kipindi cha kumi zima la mwisho wa mfungo wa Ramadhan huku wakimhimidi Mola wao pamoja na kumtaka msamaha mwema hapa duniani na kesho Akhera.

Mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa mwaka huu wa 1430 AH ndio unaelekea ukingoni, kama wasemavyo maulama na wahadhiri mbali mbali wa dini hii ya Kiislamu kwamba jambo la muhimu kwetu kabla ya kusherehekea Sikukuu ya Idd-el-Fitr ni kujitathmini kwa kiasi gani tunaweza kuendeleza yale mafunzo mema tuliyoyapata ndani ya Ramadhan?

Na hapa ndipo panapo tatizo, maana hata ukianza kufanya tathmini ndogo Misikitini utagundua kuwa hata wale waliokuwa wakisali kwa wingi kipindi hiki cha Ramadhan idadi inaanza kupungua mwishoni mwa kumi hili la mwisho muhimu la kuachwa huru na moto.

Kwa kweli inasikitisha kuona kuwa baadhi yetu tumeanza kupungua Misikitini kama kwamba Mungu wa Ramadhan ndio anaondoka na hivyo tutaonana nae tena mwaka akipenda Inshaallah.

Tumesahau ile hadithi ya Mtume (S.A.W) isemayo kwamba ‘Mcheni Mwenyezi Mungu popote mulipo na ishini na watu kwa wema, na jitakaseni kwa wema punde tu munapoteleza kwenye maovu”.

Katika hadithi hiyo ya Mtume (S.A.W) anatilia mkazo juu ya kumcha Mungu pahala popote ama mazingira yeyote mtu aliyopo bila kujali kuwa huu ni mfungo wa Ramadhan au huu ni mwezi wa kula mchana.

Kwa kumuabudu Mungu mwezi mtukufu wa Ramadhan tu pekee tusitegemee hata siku moja kuwa Mungu wetu atatuepusha na Moto wa Jehannam.

Wako wapi wale waislamu waliorehemewa na Mola wao kumi la mwanzo wa mwezi wa Ramadhan, wako wapi pia wale waislamu waliofutiwa madhambi yao katika kumi la pili la Ramadhan na je wako wapi wale walioachwa huru na moto. Hawapo tena Ramadhan imekwisha na hivyo wanafunga virago vyao vya kambi ya Ramadhan hadi mwakani.

Lakini je ni nani kati yetu ana uhakika kuwa atafika Ramadhan ijayo mwaka 1431AH, basi tusihada

Umuhimu wa Siku ya Quds kwa mtazamo wa Imam Khomeini (M.A)
Written by Baraza
Thursday, 17 September 2009 10:07
Baada ya kupita karibu miaka mia moja, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalivunja kimya cha ulimwengu kuhusiana na suala la Palestina; na kwa kutumia muelekeo unaozingatia uhalisia wa mambo, uliosimama juu ya misingi ya itikadi na mafundisho ya Kiislamu ambayo ndiyo dira ya kila Muislamu mwenye fikra huru, yakabuni mkakati sahihi na wa muda mrefu wa kudai kurejeshwa haki zilizoghusubiwa za taifa la Palestina, na ambao utavuruga mahesabu ya Wazayuni yaliyopangwa kwa zaidi ya karne moja; na badala yake kuleta suhulu ya kiadilifu itakayowezesha kuwarejeshea wanamapambano hao (Wapalestina) wa kupigiwa mfano katika historia ya kupigania uadilfu na ardhi ya mababu zao. Hakuna shaka yoyote kuwa wananchi wa mataifa mengine hawatokosa kufaidika na hidaya itakayopatikana kwa kuwepo mlingano wa nguvu, ambayo si kitu kingine bali ni uthabiti wa kudumu katika eneo, na watafanya jitihada kwa ajili ya kufanikisha malengo matukufu ya Mapinduzi makubwa ya Imam Khomeini(M.A).Kutangaza Imam Khomeini siku ya Kimataifa ya Quds kuliweka wazi msimamo wa Mapinduzi ya Kiislamu katika sura ya mpango wa kistratijia, wa kukabiliana na mpango wa Wazayuni, wa kutaka kuwafuta kikamilifu Wapalestina pamoja na madhihirisho yote ya Kiislamu ya ardhi ya Palestina. Hatua hiyo inaonyesha tadbiri ya mwanasiasa mweledi ambaye wito wake wa kupambana na batili katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa ugeni wa Mwenyezi Mungu umebaki katika kumbukumbu ya historia ya Waislamu; siku hiyo ya mshikamano wa Waislamu na wenye fikra huru wote duniani, ni ya kukabiliana na utawala ambao kichwani mwake una ndoto ya kupanua mipaka yake ulimwenguni, na ambao kubakia kwake kunahatarisha amani na usalama wa dunia. Umuhimu wa kuzungumzia suala la Palestina na kubuni fikra ya kuanzisha moja ya siku za kimataifa kuwa ni Siku ya Quds, unatokana na kuwa kwake siku hiyo nembo kubwa ya kidini iliyovuka mpaka wa mitazamo finyu ya utaifa na ukabila kwa ajili ya kutumikia malengo matukufu ya Palestina. Hatua hiyo ya Imam Khomeini imepelekea kuitoa fikra ya kuushughulikia mgogoro wa Palestina katika ngazi rasmi na za kiserikali na kuielekeza kwenye ngazi ya wananchi, mataifa na fikra za walio wengi duniani. Nayo Intifadha ya wananchi wa Palestina ni mojawapo ya madhihirisho ya kupigania haki kwa mtazamo wa Kiislamu, ikiwa imepata ilhamu na kufuata mfano wa Mapinduzi ya Kiislamu, na ikazidi kupata nguvu na mwamko maradufu kutokana na mafanikio makubwa iliyopata harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Lebanon ya kuwatimua Wazayuni katika ardhi yao.

Tukio la Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran liliandaa mazingira ya kujiri mageuzi na mabadiliko makubwa katika miundo ya kiutamaduni na kisiasa katika upeo wa kieneo na kimataifa; na kutokana na moyo wake wa kukabiliana na dhulma na kupambana na madola ya utumiaji mabavu, Mapinduzi hayo yanatafautiana na mapinduzi mengine mengi yaliyotokea katika kipindi cha historia.

Moja kati ya vipengee muhimu vya Mapinduzi ya Iran ni kutetea kwake malengo matukufu ya taifa la Palestina. Lengo hilo lilipata umuhimu zaidi kutokana na kusadifu ushindi wa Mapinduzi hayo na kufikiwa makubaliano ya mkataba wa Camp David; mkataba ambao ulisainiwa kati ya utawala wa Kizayuni na Waarabu kwa hima ya Marekani. Wakoloni walikuwa wakidhani kwamba baada ya muda si mrefu wangeweza kuziweka nchi nyingine za Kiislamu chini ya satua na ushawishi wao, na kwa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni, kulifanya suala la Palestina lionekane kidogo kidogo kuwa limemalizika.

Kutokea Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kulivuruga mahesabu yote ya wakoloni. Na kutokana na uongozi, uamshaji na msimamo imara wa Imam Khomeini (M.A), mbinu za mapambano na Israel zikachukua muelekeo mpya. Kutokana na kulielewa barabara suala la Palestina na kutambua nafasi kuu ya wananchi na athari ya kuchukua hatua za mtawalia na za kishujaa za kuupinga utawala wa Israel, Imam Khomeini aliwafanya Wazayuni hao wakabiliwe na hali ngumu zaidi. Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ulidhihirisha wazi kwamba kulikubali suala la msingi la kutambua haki za taifa za Palestina na kulirejeshea haki zake hizo, ndiyo njia pekee ya ufumbuzi wa mgogoro huo wa kihistoria. Kwa kutumia tajiriba ya Mapinduzi ya wananchi wa Iran na kufuata kigezo cha mapambano yenye mpangilio maalumu katika kuhamasisha matabaka tofauti ya jamii, Wapelestina walianzisha harakati iliyoratibiwa kwa umakini zaidi, ya maandamano makubwa ya akina mama, watoto, viongozi wa dini na wanafikra wakiwa katika safu moja ya kukabiliana na mtutu wa bunduki kwa kutumia mawe, virungu na hata mikono mitupu; na kwa kutumia vituo vya misikiti na Sala za Ijumaa wakaleta mabadiliko makubwa katika sura na mwenendo wa mapambano. Kuingia kwa awamu hii muhimu ya mapambano na kujitokeza kivitendo wananchi na kwa uelewa kamili, kuliliweka suala la Palestina katika hali tofauti kabisa ambayo ilipelekea kuanza kwa vuguvugu la Intifadha. Intifadha ya kwanza ambayo ilikuwa maarufu kama “Intifadha Kubwa” ilianza mwaka 1987 na kuendelea hadi mwaka 1991. Intifadha ya pili iliyoanza mwaka 2000 ilijulikana kama “Intifadha ya al Aqsa”.

Vuguvugu na harakati hiyo ilikuwa kielelezo cha kukatishwa tamaa wananchi wa Palestina kutokana na mazungumzo yasiyokuwa na tija yoyote eti ya amani ambayo pia yalikuwa matokeo ya kukata tamaa ya misaada ya nchi za Kiarabu, ambazo zilipuuza kadhia ya Palestina na wananchi wa eneo hilo waliofukuzwa kwenye makazi na nchi yao. Hali hiyo ya kupuuzwa kadhia ya Palestina ilionekana waziwazi kwenye mkutano wa viongozi wa nchi za Kiarabu uliofanyika Amman mji mkuu wa Jordan Novemba 1987, ambapo kwa mara ya kwanza kabisa suala la Palestina lilipewa umuhimu wa daraja la pili na suala lililopewa kipaumbele zaidi lilikuwa la kuisaidia Iraq katika vita vyake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Wananchi wa Palestina walikatishwa tamaa na harakati ya PLO ambayo ilikuwa imetupilia mbali mapambano kama njia ya kukomboa Palestina na kujibana katika juhudi zisizokuwa na faida za kisiasa na kimataifa kwa shabaha ya kutatua kadhia ya Palestina kwa upande mmoja kuelekea kwenye sababu nyingine zinazohamasisha mwamko na vuguvugu, yaani Uislamu, na matumaini ya Wapalestina ya kupata mafanikio chaguo hilo katika upended mwingine vilikuwa miongoni mwa sababu muhimu za kuanza harakati ya Intifadha ya Pili. Ni wazi kuwa ni humali kutokea mapinduzi bila ya kutegemea wananchi, kwani sababu nyingine zinazochangia harakati hiyo haziwezi kufanya miujiza.

Kadhia ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, kama zilivyokuwa nchi nyingi ne za Kiislamu, iliathiriwa na fikra na uongozi wa Imam Khomeini MA. Hata hivyo Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalikuwa na taathira kubwa zaidi huko Palestina kuliko sehemu nyingine yoyote kwa sababu Waislamu wa Palestina waliokuwa chini ya ukandamizwaji na ukatili wa Wazayuni, walikuwa wamepoteza matumaini na kusambaratika zaidi kuliko mataifa yote ya Kiislamu. Uungaji mkono wa hayati Imam Khomeini uliwafunza Wapalestina kwamba wanaweza kusimama kidete kwa kupata ilhamu ya mafundisho ya Uislamu na hatimaye kumshinda adui, japokuwa suala la kuikomboa Baitul Muqaddas kutoka kwenye makucha ya utawala huo ghasibu, linahitajia muda.

Vuguvugu na harakati ya Intifadha haikuishia kwenye maeneo ya mijini na kambi za wakimbizi ambao wana uelewa wa masuala ya kisiasa, bali ilisambaa na kuenea kwenye maeneo ya vijijini. Awali mapambano ya Wapalestina yalihusiana tu na marekebisho ya kijamii na kamwe hayakuwa na sifa za mapinduzi. Wanaharakati wa Intifadha walikuwa wakiamini kwamba watu waliokuwa madarakani hawawezi kukidhi mahitaji ya kizazi cha vijana. Kwa msingi huo, hali ya kukata tamaa ya vijana wa Kipalestina ilifikia hadi kwamba walitambua ya kuwa hawakuwa na kitu chochote cha kupoteza; na huu ndio uliokuwa mwanzo wa vuguvugu na harakati ya Intifadha. Matokeo yake ni kuwa, siasa za kivitendo za Imam Khomeini na taathira zake katika harakati ya Intifadha ya wananchi wa Palestina zinaweza kushuhudiwa katika mambo yafuatayo.

1 – Uratibu wa mambo kimapinduzi na kujitolea wananchi na wanachuoni: Kuwepo uratibu wa kienyeji na usio wa kiserikali wa harakati kubwa za kiraia kupitia misikiti kote nchini Iran, ilihesabiwa kuwa nguvu iliyoleta mabadiliko makubwa ya kijamii nchini.

Imam Khomeini MA kwa kutegemea nguvu hiyo hakufuata mbinu za mapambano ya kisiasa iliyozoeleka ulimwenguni yaani kuundwa chama na mkusanyiko uliopangwa wa kisiasa na kijeshi, bali alitumia uhusiano wa kawaida sana na wa kienyeji na kuizindua jamii ya wananchi, kwani hayo ndiyo yalikuwa malengo ya mapambano yake. Kwa hakika kufungamana makundi mbalimbali na uongozi katika harakati nchini Iran hakukuthibiti kupitia taasisi za kimapambano na kiidara ambazo zilibunia kupitia ushindi wa mapinduzi bali kutokana na ushujaa wa Imam Khomeini MA pamoja na maneno yake yaliyoeleweka vyema na makundi yote katika jamii yakiwemo hata yale ya watu wasiojua kusoma na kuandika. Intifadha ya Palestina iliundwa katika awamu ya historia ya mapambano ya nchi hiyo, ambapo mapambano ya kivyama na kidiplomasia yalikuwa yameshindwa kabisa kuwarudishia haki yao wananchi wa Palestina katika kipindi cha miongo kadhaa iliyopita. Wakati huohuo aidiolojia isiyokuwa ya kidini na ya kigeni pia ilifeli kuwadhaminia Wapalestina matakwa na mahitaji yao. Mapinduzi ya Kiislamu yalithibitisha mianya mikubwa iliyokuwepo kati ya madola ya kibeberu na harakati halisi za mapambano za wananchi na jambo hilo lilionekana wazi katika uungaji mkono wa Marekani kwa Shah wa Iran katika kukabiliana na mapinduzi huru zaidi ya karne. Harakati ya intifadha ya wananchi wa Palestina pia ilikabiliwa na hali kamahiyo mbele ya migongano mikubwa iliyokuwepo kati ya madola na mifumo ya kisiasa iliyokuwa ikiunga mkono utawala haramu wa Israel. Uungaji mkono wa mifumo hiyo kwa jinai za utawala wa Kizayuni katika kukabiliana na wananchi waliopigania haki zao za kujiainishia mustakbali na kujitawala kwao, ni dalili ya wazi ya kuthibitisha madai hayo.

2- Mbinu ya Mapambano: Kipindi cha mwamko katika mapambano ya Intifadha ya Palestina kilikuwa hatua ya mwanzo kama ilivyokuwa katika Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Japokuwa baadhi ya sababu zake zilitofautiana na zile za Mapinduzi ya Kiislamu, lakini kizazi kipya cha Palestina kiliingia katika medani ya harakati za kisiasa na kijamii huku kikikabiliwa na maisha ya kudunishwa na kuishi chini ya dhulma za uzayuni.

Mbinu za mapambano zilizokuwa zikitumika wakati huo hazikufua dafu kwa ajili ya kuvuka kipindi na mkwamo huo bali hata mbinu na aidiolojia za hapo awali zilikuwa moja ya sababu kubwa za kukwama mapambano ya ukombozi ya Wapalestina.

Utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kutumia nguvu za kijeshi na kueneza propaganda chafu katika fikra za Wapalestina ulitaka kuonyesha kwamba ni muhali kupatikana mabadiliko huko Palestina. Hata hivyo katika kipindi hicho ambapo utawala huo ghasibu ulikuwa ukifanya jitihada za kuimarisha nafasi yake katika eneo la Mashariki ya Kati, wanamapambano wa Kiislamu nchini Iran walifanikiwa kumuondoa mdarakani msaliti wa malengo ya Wapalestina Shah Muhammad Ridha Pahlavi. Tukio hilo lilileta nuru ya matumaini katika mwenendo wa mapambano huko Palestina. Japokuwa kizazi kipya kilirithi masaibu na matatizo chungu nzima lakini kilikuwa na fursa makhsusi ambayo ilifungua upeo wenye mwanga katika mustakbali wa tabaka hilo. Fursa hizo ni pamoja na umuhimu unaotolewa na Waislamu kote duniani kuhusu mustakbali wa Quds Tukufu, mwamko wa mataifa ya Mashariki ya Kati, uungaji mkono wa Imam Khomeini na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa taifa la Palestina na muhimu zaidi ya yote, kigezo na mfano hai wa mapambano ya wananchi katika eneo lililokua ‘kisiwa cha amani na utulivu kwa Wamagharibi’ hususan Marekani, yaani Iran.

Katika upande mwingine, kizazi kipya cha Palestina kilisifika kwa kuwa na upeo mpana zaidi wa elimu na maarifa kutokana na kuvumilia kwake mashinikizo mengi. Kilifanya uchambuzi wa kina kuhusu uwezo wa mirengo na harakati za Palestina kwa kutilia maanani hali ya huko nyuma na ya sasa na kufanya ulinganisho kati ya hali hizo mbili. Wananchi wenye hasira katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ambao walikuwa wakikusanyika misikitini na katika vituo vya kidini, walikuwa wakipambana na vifaru kwa kutumia mawe na kujiunga na harakati ya mapambano ya wananchi ya Intifadha.

Mbinu hiyo ya mapambano ina matunda muhimu licha ya kusababisha hasara na gharama kubwa. Kiasi kwamba hata wataalamu wa vita vya kisaikolojia wameshindwa kukabiliana nayo. Moja na matunda hayo ni kuondoa woga na hali ya kukata tamaa katika safu za wanamapambano na kuihamishia katika kambi ya adui. Mbinu hii ndiyo njia pekee ya mapambano ambayo ilimtia kiwewe adui na kumuelekeza kwenye ukanda wa maangamizi na kushindwa tena kwa mikono yake mwenyewe.

3- Hatua ya hayati Imam Khomeini ya kuitangaza Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ilitoa bishara ya harakati tofauti ya kurejesha mapambano ya taifa la Palestina katika njia sahihi. Tunapotazama kwa ujumla ujumbe wa Imam kuhusu siku hiyo tunaelewa vyema umuhimu wa mtazamo wake kuhusu kadhia hiyo. Anasema katika ujumbe huo kwamba:

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu.

Ninatoa wito kwa Waislamu wote duniani na serikali za Kiislamu kuungana kwa ajili ya kukata mkono wa utawala huo ghasibu na wasaidizi wake. Ninatoa wito kwa Waislamu wote duniani kuichagua Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ambayo ni miongoni mwa siku za lailatul Qadr na inaweza kuwa na umuhimu mkubwa mno kwa mustakbali wa wananchi wa Palestina, kuwa Siku ya Quds na kufanya marasimu ya kutangaza mshikamano wa kimataifa wa Waislamu katika kutetea haki za kisheria za wananchi wa Palestina”.

Kwa hakika mapambano dhidi ya Uzayuni hususan Israel, ilikuwa moja ya nguzo kuu za fikra za kisiasa za hayati Imam Khomeini.

Moja ya nukta zenye umuhimu mkubwa katika kadhia hii ni zingatio makhsusi la Imam kwa mitazamo ya pamoja ya wanafikra huru duniani kutoka makundi na mirengo yote. Mwelekeo huu uliofauka ya mipaka ya kidini na utaifa unatayarisha uwanja mzuri kwa wanadamu kutafakari kwa kina kuhusu kadhia ya Palestina na kuleta uwiano na umoja katika jamii ya Kiislamu na pia kuifungamanisha jamii ya kimataifa na suala la Palestina. Imam Khomeini anasema: Siku ya Quds ni siku ya kimataifa na si siku inayoihusu Quds peke yake…”

. Neno la Mwisho

Endapo tutatupia jicho matukio ya kisiasa na kiutamaduni ya eneo la Mashariki ya Kati hususan katika masuala muhimu likiwemo suala la Palestina, tunang’amua kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu yakiwa kama kigezo na umbo jipya la mapambano ya kiraia (ya wananchi) yameweza kuwa na nafasi muhimu baina ya Waislamu na harakati za mapambano katika meneo mbalimbali ulimwenguni na hivyo kuwa na taathira chanya katika kuleta mwamko baina ya Waislamu na wanadamu wenye fikra huru kwa ujumla. Kuhusiana na hilo, nafasi maalumu iliyonayo Palestina katika mazungumzo na miamala ya Imam Khomeini-ambapo kilele cha kuzingatia suala hilo ni kuichagua siku na kuipa jina la Siku ya Kimataifa ya Quds-ni jambo la kutaamali, kutadabari na kuchunguza; kwani bila shaka taathira ya muamala huu una umuhimu wa hali ya juu kwa suala la Palestina.

1- Ubunifu wa Imam Khomeini (Quddisa Sirruh) katika kuichagua Siku ya Kimataifa ya Quds ni sisitizo la upinzani wa ulimwengu wote wa Kiislamu dhidi ya uwepo wa utawala vamizi kwa jina la ‘’Israel’’. Siku hii imekuwa ni chimbuko la kusafisha nyoyo na aina fulani ya kuwa na mtazamo mmoja katika Ulimwengu wa Kiislamu ambao ni dhihirisho la wito wa Imam Khomeini wa kuweko umoja wa kalima. Ni kwa namna hii ambapo hatua ya kwanza hupigwa kwa ajili ya umoja wa Kiislamu na kuweko njia kwa ajili ya kufikia katika umma mmoja ambao hauna ubaguzi na tofauti za kimadhehebu.

2- Siku ya Quds ni vita vikubwa kabisa vya kisaikolojia dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na ni moja ya wenzo mkubwa kabisa wa mashinikizo ambao yamkini ukatumiwa dhidi ya tamaa na uchu wa utawala huo ghasibu. Siku ya Kimataifa ya Quds ni tukio muhimu ambalo hutia alama ya ulizo juu ya uhalali wa utawala huo. Kukaririwa kila mwaka kwa tukio hili sambamba na kuufanya ulimwengu wa Kiislamu kuwa na muelekeo kwa fikra za kiistratejia za Imam Khomeini, harakati hiyo huwaonyesha walimwengu kwamba, utwala huo si halali na wakati huo huo huzing’arisha nyoyo za wumini kwa matukufu ya Palestina. Katika upande mwingine, kuonekana picha za mamia kwa maelfu ya waandamanaji katika pembe mbalimbali za dunia hupelekea kutokea ukosefu wa amani wa kisaikolojia ndani ya mipaka ya utawala huo ghasibu.

iwe na pumzi tunazovuta bila ya kulipia bili. Tusimuasi Mungu kwa makusudi tukidhani kuwa tunamtogoza wakati yeye akisema kuwa basi fayakun.

Wale waliokula mchana wa mwezi wa Ramadhan kwa kujificha mbele ya kadamu nasi wakajiona wajanja waliorevuka, wajue tu kwamba hawakuwaonea haya binadamu wenziwao bali pia hawakumuonea haya Mungu wao ambaye anaona kila kitu kinachotendeka katika ulimwengu huu.

Waislamu wa namna hiyo waliojitoa mshipa wa fahamu kwa kutoa kila aina ya visingizio ili wasifunge na wajiulize wamezidi nini , ndio wamenenepa kwa kula sana mchana kutwa au ni hasara tu kwa Mola wao kesho Akhera?,Bila shaka hawana walichokivuna ila hasara ya Jahanam.

Hivyo ni vyema kukumbushana juu ya jambo hili kuwa kumalizika kwa mwezi wa Ramadhan si mwisho wa Ibada, kwani Ibada inaendelea kila siku tokea mtu anapoamka mpaka anapolala.

Tumuombe Mwenyezi Mungu atutakabalie funga zetu na atuzidishie imani juu ya kuendeleza mafunzo mema tuliyoyapata katika mwezi huo mtukufu.

WAJIBU WA MUISLAM

Na AlHajj Udii

Kabla ya kujuwa wajibu wetu hatuna budi kujitambua sisi wenyewe kwanza. Hivyo ni lazima kujiuliza masuala matatu ya msingi yafuatayo:-

1          Kwanza:          Sisi nani na tumeletwa na nani??

2          Pili:                 Tumeletwa hapa duniani kwa ajili ipi???

3          Tatu:                Nini khatima ya maisha yetu  ya duniani???

Jawabu ya suala la kwanza tunalipata katika Qur-an(95:4)

“Bila ya shaka tumemuumba Mwanaadamu kwa  umbo lilo bora  zaidi”.

Kumbe sisi ni wanaadamu  tumeumbwa kwa umbile lililo bora zaidi, na  ubora  wa umbile hilo unatokana na akili,fikra na mawazo tuliyopewa katika kuamuwa maamuzi yetu . Hivyo Mwanaadamu akitumia akili yake vizuri huongoka na akawa bora kuliko kiumbe chochote ulimwenguni na kinyume cha hivyo hupotoka na akawa chini ya walio chini kama aya inavyo tufahamisha (95:5).

“Halafu tukamrudisha chini kuliko walio chini”

Vilevile ayya ya 30 ya surrat Baqarah inatufahamisha .

“Wakumbushe watu khabari hii :Wakati MOLA wako alivyowambia Malaika “Mimi ninaleta viumbe wengine kukaa katika ardhi”(nao ndio wanaadamu) wakasema Malaika “utaweka watakaofanya uharibifu humo na kumwaga damu,  hali sisi tunakutukuza kwa sifa zako na utakatifu wako ?”Akasema (M/MUNGU) “Hakika mimi nayajua msiyo yajua”

Ayya hii inatufahamisha kuwa Mwanadamu hakuzuka tuu kwa bahati mbaya ,isipokuwa ameletwa na M?MUNGU Bwana wa viumbe vyote .

Jee, M/MUNGU ametuleta duniani bila ya malengo yoyote ?.

Jawabu ya suala la pili Qur-an (51:56)

“Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu”.

Katika ayya hii M/MUNGU ametuwekea wazi lengo hasa la kuwepo kwetu duniani . Jawabu ya suala la tatu . Katika suala la khatima ya maisha yetu ya ulimwenguni ni kwamba : waislamu tunaamini tutakufa ,tutafufuliwa , tutakusanywa na tutahesabiwa (tutahukumiwa)(45:26)

Kwa yale tuloyatenda ulimwenguni .Kwa hakika maisha ya duniani ni mafupi na yakupita na maisha ya kweli yako huko akhera . Qur-an (87:16-17)

“Lakini nyinyi mnayapenda maisha ya dunia . Hali yakuwa (maisha ) ya akhera ni bora na yenye kudumu”  .

Siku ya malipo watu watagawika sehemu mbili .Qur’an (79:37-41) “Ama yule aloasi Na akapenda zaidi maisha ya dunia .Basi kwa hakika jahannamu ndiyo itakayokuwa makazi yake ,Na ama yule aliyeogopa kusimamishwa mbele ya MOLA wake ,akaikataza nafsi yake na matamanio( maovu )Basi pepo ndiyo itakayokuwa makazi yake.

Nasifa za watu wa peponi tunazipata katika sura ya (56:15-37) “Watakaa juu ya viti vya faharii , kuelekeana kuzungumza ,na watakunywa vinywaji vya kila namna ,hawataumwa na vichwa wala kutokwa na akili , Watakula matunanda wayapendayo na nyama za ndege kama watakavyo tamani .Watapata W/ke wazuri wenye macho mazuri na makubwa  mithili ya lulu . Humo hawatasikia maneno ya upuuzi na  ya dhambi isipokuwa maneno ya salama na Amani .Watakuwa katika vivuli vya mikunazi isiyo na miba na migomba iliyopangiliwa pamoja na maji yanayominika .Na wake watukufu (waliokuwa nao duniani)wataumbwa kwa umbo bora zaid.Na M/MUNGU anamalizia kwa kusema  “Tutawafanya vijana kama kwamba ndio kwanza wanaolewa ,watapendana na waume zao waliohirimu moja.”.

Ama watu wa Motoni sifa zao(adhabu) zimetajwa katika sura mbali mbali kama vile sura ya 56,69,88 n.k , kwa ufupi hali itakuwa mbaya sana maana ni adhabu juu ya adhabu .M/MUNGU ataamrisha “Mtupeni motoni katika mnyororo wenye dhira sabini”chakula ni maji ya usaha na miba , watakuwa katika upepo wa maji ya chemkayo ,na kivuli cha moshi mweusi sana si chakuleta baridio wala starehe na kinywaji cha humo nimaji ya chemkayo .

Naturudi katika maada yetu ambayo tuihusisha moja kwa moja na jawabu ya suala la pili (51:56)

“Siku waumba majini na watu ila wapate kuniabudu”

Huu ni wajibu wa Waislamu, lakini kabla kuangalia Suala zima lakuabudu ni lazima tujuwe maana ya dini “Dini ni mfumo wowote wa maisha anaofuata mwanaadamu katika kuendesha maisha yake ya kibinafsi na jamii kwa ujumla katika nyanja zote za maisha”

Sasa sisi waislam ambao tumeamuwa kufuata mfumo wa kiislamu ambao ndiyo mfumo wa haki “Bila ya shaka dini (ya haki ) mbele ya M/UNGU ni Uislam………”(3:19). Hatuna budi kuufuata mfumo huo kikamilifu.

“enyi mlioamini !Ingieni katika hukumu za Uislam zote, wala msifuate nyayo za shetani , kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahirii”. (2:208)

Suala linajitokeza , Vipi tutaweza kumuabudu  Allah (s.w)na kuuingia Uislam wote.

Jawabu:- Elimu ndio zana pekee aliyotunukiwa Mwanaadamu ili aitumie katika kutekeleza wajibu wake.Naye Mtume(s.a.w) wahyi na amri ya kwanza aliyopewa na Mola wake ni kusoma kwa ajili ya Allah (s.w) Qur’ani (96:1-5).

Ni wazi kuwa Muislam mwenye tabia ya  kujielimisha katika mambo muhimu ya maisha kwa lengo la kupata ufanisi katika kumuabudu Allah(s.w) atatofautiana sana kiutendaji na kiuchaji na yule ambae hana sifa ya kujielimisha kama tunavyojifunza katika Qur’ani(39:9)

“…Je! Wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojuwa ?Wanaotanabahi ni  wale wenye akili tu.”  Vilevile (58:11) “…..Allah atawainua daraja wale walioamini miongoni mwenu na walio pewa elimu watapewa watapata daraja zaidi.” Pia “….Kwahakika wanaomuogopa Allah miongoni mwa waja wake ni wale wataalamu (waliosoma)”

Aya zilizopo hapo juu zinatuekea wazi dhana nzima ya kuabudu ,itafanikiwa ikiwa Waislam tutajifunza na kuifanyia kazi elimu tuliyonayo , ukizingatia maneno ya Mtume (s.a.w) “Kutafuta elimu ni faradhi kwa kila muislamu  MwanamumenaMwanamke.

Kwani madhara gani yatajitokeza endapo waislamu hawatakuwa na utamaduni wa kujisomea ?

Madhara makubwa yatajitokeza katika jamii ,kama tunavyoona katika jamii yetu ya Kizanzibar na Kiislam kwa jumla:-

1                  Waislamu kutoufanyia kazi Uislam wao .(hawaujui)

2                  Waislamu wengi wanabaki kuwa waislam majina tuu .

3                  Waislamu wanaona tabu (wanaona haya) kujitambulisha kuwa wao waislamu.

4                  Waislamu kufuata mila zisizokuwa za Kiislam.

5                  Kuutupa (kuugawa) Uislam na siasa (amakueweka tofauti na siasa)

6                  Uislam unashindwa kuwa juu ya dini zote kama kama Allah(s.w)alivyoahidi.

Kutokana na matatizo tuliyokwisha ya orodhesha hapo juu, ni dhahiri kuwa lengo la kuabudu halitofanikiwa, na hapo waislamu wanabaki na dhana ya kuwa Uislamu (au ibada),ni nguzo tano .Shahada, Swalaa,Zakah,Funga na Hijja.Hili ni wazo potofu.

Mana haiwezekani M/Mungu kutuwambia kuwa lengo la kuumbwa kwetu ni kumuabudu katika maisha yetu yote alafu ibada yenyewe iwe :-

1     Swala tano (5) za faradhii ambazo tunatumia saa moja kuzisali katika masaa 24.

2     Zakah  ambayo hutolewa na Mtu mwenye uwezo katika kiwango na muda  maalum.

3     Funga ambayo tunafunga mwezi mmoja(1) katika miezi kumi na mbili (12).

4     Hijja ambayo hutekelezwa   na Mtu mwenye uwezo ,mwaka mara moja .

Ukweli utabaki palepale kuwa nguzo tano za Uislamu ni msingi wa ibada ,hivyo mafunzo yanayopatikana humo kupitia msingi huo ndio hasa yatakayokamilisha ujenzi wa nyumba  ya Uislam.

Swala: Humkataza mtu maovu na machafu yote . hivyo Waumini  hatuna budi kuachana na maovu na machafu yote .

Zakah : Humtakasa mja kutokana na mali yake, nafsi yake  na jamii kwa ujumla .

Funga:Funga humfanya muumini kuwa mcha mungu .

Hijja: Inatufunza Umoja na Usawaa pamoja na Utii kwa Allah (s.w) kubwa zaid ni dhana nzima ya kukumbushana mema na kukatazana mabaya funzo hili tunalipata katika Uwanja wa  Arafa.

Maafa makubwa yameikuta jamii ya Waislam wa  Kizanzibari  , ambapo hata tunashindwa hata kujielewa kuwa ni waumini au siwaumini wa dini ya Kiislamu. Mafundisho ,mila na desturi za kitwaghuti  tumezikumbatia na Uislam tumeupiga teke ,tumesahau wajibu wetu na sasa tunakufuru  ,shime Waislamu  turudi  kwa Mola wetu ,tufuate Qur’an na Sunna za Mtume wetu (s.a.w).Tuanzishe mashule ya Kiislamu ,yatakayofuata utamaduni wa Kiislamu kwa ajili yakutowa mafunzo Kiislamu .Ndugu zangu waislamu .Waislamu kutafuta elimu ndiyo roho ya Uislamu.Kukumbushana mema na kukatazana mabaya ndiyo chakula cha n! yoyo za Waislamu .Kufuata mafundisho ya Mtume (s.a.w) ndio mafanikio ya Waislamu .  Kumtumikia ,kumnyenyekea  na kumuabudu M/Mungu ndio wajibu wa Waislamu .

Qur’an (103:2-3)

“ Hakika binaadamu yuko katika hasara. Isipokuwa wale walioamini na Wakafanya vitendo vizuri wakausiana (kufuata)haki na wakausiana (kushikamana) na subira (kustahamiliana) .” YARABII TUJALIE NA SISI  KATIKA WALIOAMINI NA WENYE MAFANIKIO KATIKA HUKUMU YAKO .

AMIIIIEN .

WABILLAHI  TAWFIQ

Ndugu yenu Alhajii- Udiii katika njia ya kuamshana .

Advertisements