MARADHI YANAYOTIBU HABBA SODA
Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat Sawdaa-1 (haba Soda – Chembe Nyeusi
Imefasiriwa na Iliyasa bint Maulaanah
Al-Bukhaariy anasimulia kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume Muhammad (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema.
((Habbat-Sawdaa inatibu kila kitu isipokuwa mauti)).
Yafuatayo hapa chini ni baadhi ya matatizo na magonjwa ambayo yanaweza kutibika kwa kirahisi kwa kutumia Habbat-Sawdaa.
Kwa faida ya Afya kwa ujumla:
Kunywa kijiko kimoja cha mafuta ya Habbat-Sawdaa asubuhi na usiku, au kunywa japo asubuhi kabla ya kifungua kinywa, unaweza kunywa kijiko kimoja cha mafuta peke yake au ukachanganya na kijiko kimoja cha asali safi.
Vipele (chunusi) Na Ngozi:
Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu) kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple). Paka katika sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.
Upara (Alopeshia):
Sugua mafuta ya Habbat-Sawdaa katika mabaka yanayokusumuba.
Pumu:
Tia ½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.
Kuumwa kwa Mgongo (Sehemu ya Chini):
Changanya asali pamoja na ¼ (robo) kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.
Mwiba Wa Nyuki Na Nyigu:
Tia ½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.
Kibofu cha Mkojo/Figo:
Kunywa maji ya moto yaliyochanganywa na½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa pamoja na asali kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Changanya vikombe viwili vya Habbat-Sawdaa iliyosagwa na ½ (nusu) kikombe cha asali safi. Kunywa kijiko kimoja cha mchanganyiko pamoja na kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Mchanganyiko unaweza kukaa kwa siku 15 na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.
Jiwe La Figo:
Kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyochanganwa pamoja na gilasi (bilauri) moja ya asali, vitunguu saumu vitatu vilivyosagwa na karafuu. Changanya vitunguu saumu pamoja na asali na Habbat-Sawdaa. Kunywa kijiko kimoja kabla ya kula chakula na kwa pendekezo kula limau (bila ya kumenywa). Rudia haya kwa wiki moja Insha-Allah jiwe litaondoka.
Maathiriko Ya Figo:
Changanya baadhi ya Habbat-Sawdaa pamoja na mafuta ya alizeti. Chukua mchanganyiko na weka katika sehemu ambapo figo limeathirika. Kunywa kijiko cha Habbat-Sawdaa asubuhi. Rudia haya kwa muda wa wiki moja Insha-Allah maathiriko yatatibika.
Mafua:
Chukua mbegu za Habbat-Sawdaa 21, ziweke katika kitambaa na roweka usiku. Tumia kama matone kwenye pua siku ya pili nusa poda ya Habbat-Sawdaa iliyomo katika kitambaa.
Kikohozi:
Tumia matone matatu au manne ya mafuta ya Habbat-Sawdaa kwenye kahawa au chai.
Bawasiri:
Kula unga wa Habbat-Sawdaa pamoja na maji.
Shinikizo la damu (high blood pressure):
Changanya kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, kijiko kimoja cha asali safi na kitunguu kiasi kidogo. Chukua mchanganyo kabla ya kufungua kinywa kwa siku ishirini.
Uwasho Na Maumivu Ya Jino Na Ufizi:
Chemsha Habbat-Sawdaa katika siki na itumie kwa kusukutulia meno na ufizi. Na jikinge kutumia dawa za msuwaki za kibiashara na tumia dawa za msuwaki ambazo zinatengenezwa kutoka kwenye nyuzi za mboga za mti wa siwak ambao kwa karne ulikuwa unatumiwa na Wahindi, Waafrika na Waarabu, ni msuwaki wa kiasili.
Kumbukumbu (memory):
Kunywa kijiko kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa na changanya na asali mara mbili kwa siku.
Utaratibu Wa Ulinzi Wa Mwili:
Kula kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa na asali mchana na usiku Kutoweza kuzuia haja ndogo (mkojo): Kunywa kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa pamoja na asali, kisha kunywa maji ya vugu vugu.
Jaundice:
Tumia Habbat-Sawdaa pamoja na maziwa.
Maumivu Sugu ya kichwa (Maumivu ya kichwa ya upande mmoja, maumivu ya kichwa):
Kaanga Habbat-Sawdaa na iweke katika kitambaa cha pamba, funga au weka tu kitambaa katika kikomo (kipaji cha uso). Roweka Habbat-Sawdaa ndani ya siki wakati wa usiku, siku ya pili ivuruge kufanya unga. Ingiza katika pua halafu vuta pumzi.
Ngozi kavu:
Changanya asali pamoja na robo kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.
Upepo:
Changanya asali pamoja na robo kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.
Minyoo:
Kunywa Habbat-Sawdaa pamoja na siki kuondoa minyoo.
————————————————————————————————————————–
Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat-sawdaa-2 (habba Soda – Chembe Nyeusi )
Imefasiriwa na Iliyasa binti Maulana
(Itumieni habba hii, hakika ndani yake muna shifaa (ponyo) ya kila aina ya ugonjwa isipokuwa mauti)). (Al-Bukhaariy)Kunyonyoka Nywele
Ataukanda unga wa Habbat-Sawdaa katika juisi ya chirichiri pamoja na kijiko cha siki nyepesi na kikombe cha mafuta ya zeituni, halafu asugue kichwani kwa mafuta hayo kila siku jioni pamoja na kukiosha kichwa kwa maji na sabuni kabla ya kupaka.
Maumivu ya Kichwa
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa , karafuu iliosagwa nusu ya kiwango cha Habbat-Sawdaa na anisuni (anise), halafu achanganye pamoja. Achukue kiasi cha kijiko kimoja (cha chai), wakati wa kuumwa na kichwa, na ale na maziwa lala (mala), pamoja na kupasugua mahala paumapo kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa .
Ukosefu Wa Usingizi
Atachukua kijiko cha Habbat-Sawdaa , achanganye na gilasi ya maziwa moto yaliochanganywa na asali, baada ya kupoa kiasi atakunywa.
Chawa Na Mayai Yake
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa uliosagwa vizuri aukande kwenye siki mpaka uwe kama marhamu, halafu ajipake kichwani – baada ya kunyoa nywele au kuisugua marhamu kwenye mashina ya nywele, halafu aketi katika mwanga wa jua kitambo cha robo-saa. Na hataosha kichwa ela baada ya masaa matano. Atafanya hivyo kila siku kwa muda wa wiki moja.
Kisunzi Na Maumivu Ya Sikio
Tone moja la mafuta ya Habbat-Sawdaa ndani ya sikio husafisha sikio, pamoja na kuyanywa na kusugua sehemu za panda na nyuma ya kichwa, humaliza kisunzi.
Upaa Na Mabaka
Utachukua kijiko cha unga wa Habbat-Sawdaa, siki kiasi cha kikombe kimoja na juisi ya kitunguu saumu kiasi cha kijiko kidogo, vyote hivyo utavichanganya na vitakua namna ya marhamu, utajipaka baada ya kunyoa sehemu ya nywele na kuchanja kidogo – kisha utafunga bendeji, utaiacha mpaka asubuhi, baadae utajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa,utaendelea hivyo kwa muda wa wiki moja.
Malengelenge ya Neva katika Ngozi
Atajipaka – sehemu ya malengelenge – mafuta ya Habbat-Sawdaa mara tatu kila siku mpaka iondoke kwa Uwezo wa Allah.
Maradhi Ya Wanawake Na Uzazi
Dawa kubwa inayosahilisha kuzaa ni Habbat-Sawdaa iliochemshwa ikachanganywa na asali na kiziduo cha babunaji (chamomile). H abat sawdaa ni kama burashi katika uke wa mwanamke yenye faida kubwa kwao pamoja na kutumua mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kila kinywaji cha moto kwa maradhi yote ya wanawake.
Meno Na Maumivu Ya Mafido na Koo
Kiziduo cha Habbat-Sawdaa na kutumia kwa kusukutua kwa kugogomoa, husaidia mno maradhi yote ya mdomo na koo, vivyo hivyo pamoja na kubugia kijiko cha Habbat-Sawdaa na kumeza kwa maji yenye vuguvugu kila siku na kujipaka mafuta yake sehemu ya koo kwa nje na kuusugua ufizi kwa ndani.
Maradhi Ya Tezi
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa na aukande kwa asali na mkate wa nyuki kila siku, kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Chunusi (Acne)
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa aukande katika mafuta ya ufuta (simsimu) pamoja na kijiko cha unga wa ngano. Vyote hivyo atajipaka usoni kuanzia jioni hadi asubuhi, halafu ataosha kwa maji yenye vuguvugu kwa sabuni. Ataendelea kufanya hivyo kwa muda wa wiki moja. Na awe akinywa mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kinywaji chochote cha moto.
Maradhi Yote ya Ngozi
Atachukua mafuta ya Habbat-Sawdaa, mafuta ya waridi (marashi jabali) na unga wa ngano asili, vyote hivyo kwa viwango sawa, ule unga wa ngano uwe zaidi kuliko mafuta, halafu aukande vizuri. Kabla ya kujipaka, apanguse sehemu yenye ungonjwa kwa kitambaa kilichoroweshwa siki nyepesi, halafu aketi kwenye jua, baadae ajipake dawa hio kila siku. Lakini ajizuie na kila chenye kuchochea hisia kama vile, samaki, mayai, maembe na mfano wake.
Sugu (Chunjua) (Wart)
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa aukande katika siki nzito na asugue kwa kitambaa cha sufi au katani mahala pa sugu asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja.
Kuung`arisha Uso Na Kuurembesha
Ataukanda unga wa Habbat-Sawdaa katika mafuta ya zeituni, na atajipaka usoni halafu apigwe na mwanga wa jua kidogo. Tiba hiyo ataifanya wakati wowote katika mchana na siku yoyote.
Kuunganisha Mvunjiko Haraka
Supu ya adesi (dengu), kitunguu maji pamoja na yai la kuchemsha na kijiko kikubwa cha unga wa Habbat-Sawdaa , utachanganya na supu hiyo japo siku baada ya siku; halafu anywe. Na atasugua sehemu zilizo karibu na mvunjiko kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa, na baada ya kufungua bendeji atajisugua kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa yenye vuguvugu; kila siku.
Mvilio Wa Damu (Contusion)
Atachemsha vizuri konde moja la Habbat-Sawdaa katika chombo cha maji, kisha atakiingiza kiungo kilichovilia damu ndani ya maji hayo- yenye vuguvugu- kwa muda wa robo-saa au zaidi pamoja na kukitaharakisha kiungo hicho. Baada ya hapo atajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa bila ya kufunga kitu. Lakini hatakiwi kukipa uzito kiungo hicho au kukitaabisha. Tiba hiyo ataifanya kila siku kabla ya kulala.
Baridi Yabisi (Rheumatism)
Atachemsha mafuta ya Habbat-Sawdaa na atasugua kwayo ile sehemu yenye ugonjwa, atasugua kwa nguvu kama kwamba yuwasugua mfupa wala sio ngozi! Na atayanywa baada ya kuyachemsha vyema na kuyachanganya na asali kidogo. Ataendelea na tiba hiyo huku akiwa ni mwenye imani na yakini kuwa Allah Atamponya.
(Ki) Sukari (Diabetes)
Utachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kikombe kimoja, manemane (myrrh) iliosagwa kiasi cha kijiko kikubwa, habbarrashad nusu kikombe, komamanga iliosagwa kiasi cha kikombe kimoja, mzizi wa kabichi uliosagwa baada ya kukaushwa kiasi cha kikombe kimoja na kijiko kidogo cha mvuje. Vyote hivyo atavichanganya na atakula kabla ya kula chakula kiasi cha kijiko kimoja, atakula na maziwa lala ili iwe rahisi kumeza.
Shinikizo la Damu (High Blood)
Kila unywapo kinywaji cha moto, tia matone machache ya mafuta ya Habbat-Sawdaa. Pia ujipake mafuta hayo mwili wote, japo wiki mara moja.
Uvimbe Wa Figo(Nephritis)
Atatengeneza kibandiko (cha kitambaa) kutokana na unga wa Habbat-Sawdaa uliokandwa katika mafuta ya zeituni, atabandika sehemu yenye maumivu ya figo pamoja na kubugia funda la kijiko cha Habbat-Sawdaa kila siku kabla ya kula chakula kwa muda wa wiki moja tu; uvimbe utakwisha insha Allah.
Kuvunjavunja Vijiwe Vya Tumboni
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kikombe kimoja kisha aukande katika kikombe cha asali, na atasaga kitungu u saumu punje tatu; atakua akichukua nusu yake akila kabla ya kula chakula kila siku. Pia itakua bora lau atakula limau kila baada ya kula dawa; kwani husafisha kabisa.
Kukojoa Kwa Maumivu (Dysuria)
Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa juu ya kinena kabla ya kulala pamoja na kunywa kikombe cha mafuta hayo yaliochemshwa na kutiwa asali; kila siku kabla ya kulala.
Kukojoa Bila Kukusudia
Atachukua Habbat-Sawdaa na maganda ya mayai yaliosafishwa na yakaokwa na kusagwa halafu yakachanganywa na Habbat-Sawdaa kisha yakaokwa na kusagwa halafu yakachanganywa na Habbat-Sawdaa kisha aingize kwenye maziwa; hatimae anywe kiasi cha kikombe kimoja kila siku na wakati wowote.
Jongo (Edema)
Ataweka kibandiko (cha kitambaa) cha unga wa Habbat-Sawdaa uliokandwa katika siki juu ya kitovu, kwanza ataweka kitambaa. Pia atakula Habbat-Sawdaa kijiko kimoja asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja.
Kifuko Cha Nyongo Na Vijiwe Vyake
Atachukua Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja, manemane iliosagwa robo kijiko na asali kiasi cha kikombe kimoja; vyote hivyo atavichanganya viwe mraba (kama jamu); halafu awe akila kila asubuhi na jioni.
Wengu
Ataweka kibandiko (kilichopashwa moto) cha Habbat-Sawdaa iliokandwa katika mafuta ya zeti katika ubavu wa kushoto; jioni. Na wakati huo huo ata kunywa kikombe cha kiziduo cha uwatu kilichochanganywa asali na mafuta ya Habbat-Sawdaa kidogo, ataendalea na dawa hiyo kwa muda wa wiki mbili mfululizo.
Maradhi Yote ya Kifua na Baridi
Atachukua mafuta ya Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kikubwa atie kwenye maji halafu ayaweke juu ya moto mpaka ianze kufuka moshi, hapo aanze kuuvuta ule moshi puani huku akiwa amejifunika kichwa ili ule moshi usiende upande mwingine. Atafanya hivyo kila siku kabla ya kulala, pamoja na kunywa kiziduo cha zaatari kilichochanganywa na unga wa Habbat-Sawdaa; asubuhi na jioni.
Moyo na Mzungukoa wa Damu
Kuwa na imani katika maneno ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wa sallam) Kwa sababu jambo hili ni katika muktadha wa imani. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wa sallam) alipotuambia kuwa Habbat-Sawdaa ni dawa ya kila ugonjwa, basi hakuna shaka hata chembe kuwa ni dawa ya maradhi yote yanayomfika mwanaaadamu. Mgonjwa wa moyo asikate tamaa kutokana na rehma ya Allah; ni juu yake akithirishe kutumia Habbat-Sawdaa kwa namna yoyote iwayo; iwe ni kwa kula nzima au kwa kunywa wakati wowote uwao.
Mchango (Msokoto Wa Tumbo) (Colic)
Atachemsha vyema anisuni, kamun na nana kwa vipimo sawa na atatia asali kidogo, halafu atie matone saba ya Habbat-Sawdaa ; atakunywa kinywaji hicho kikiwa na vuguvugu pamoja na kupaka mafuta ya Habbat-Sawdaa mahala panaposokota. Baada ya muda mchache maumivu yataondoka.
Kuhara
Atachukua juisi ya chirichiri iliochanganywa na unga wa Habbat-Sawdaa kijiko kikumbwa, atakunywa kiasi cha kikombe kimoja mara tatu kwa siku.
Uziwi
Atachemsha Habbat-Sawdaa pamoja na karafuu, na atakunywa bila ya kuongeza kitu; mara tatu kwa siku.
Gesi Na Maumivu
Atabugia unga laini wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja kabla ya kula chakula akifwatisha gilasi ya maji yenye vuguvugu iliotiwa asali ya muwa kiasi cha vijiko vitatu; atakariri kila siku kwa muda wa wiki moja
————————————————————————
Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat-sawdaa-3 (habba Soda – Chembe Nyeusi )
Imefasiriwa Iliyasa binti Maulana
Asidi (Acidness)
Motone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa yaliotiwa kwenye maziwa ya moto na asali; humaliza asidi.
Uvimbe Wa Tumbo
Atachukuwa unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja na kijiko cha urkusus (licorice) hivyo atavichanganya na juisi ya pea iliotengenezwa pamoja na kokwa zake; halafu anywe; ataona nafuu kubwa.
Maradhi Ya Macho
Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa sehemu za panda kandokando ya macho na kope, atafanya hivyo kabla ya kulala pamoja na kunywa matone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kinywaji chochote cha moto au katika juisi ya karoti.
Amiba (Vijidudu) (Amebiasis)
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja pamoja na kijiko cha kitunguusaumu kilichosagwa, atachangana katika kikombe cha juisi ya nyanya iliotiwa chumvi kidogo; atakunywa kila siku kabla ya kula chakula kwa muda wa wiki mbili mfululizo.
Kichocho (Bilharziasis)
Atakula Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja asubuhi na jioni, yawezekana kuila Habbat-Sawdaa katika chakula kama vile mkate pamoja na kujipaka mafuta yake katika ubavu wa kulia. Ataendelea na dawa hio kwa muda wa miezi mitatu mfululizo. Baadae atapata nguvu na nishati.
Kutoa Wadudu Tumboni
Atakula sandwichi moto ya vitu hivi: kijiko kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa, punje tatu za vitunguu, kijiko kimoja cha mafuta ya zeti, pilipilimanga kidogo na punje kumi za boga (calabash), asubuhi atakunywa kinywaji cha shimari au mafuta ya mbono mara moja pekee.
Utasa
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa, unga wa uwatu na mbegu ya figili kwa vipimo sawa, atakula kijiko kimoja asubuhi na jioni ilihali imekorogwa katika nusu kikombe cha asali, baadae atafuatisha kunywa kikombe kikubwa cha maziwa ya ngamia; basi inshaAllaah itakuwa kheri.
Tezikibofu (Prostate gland)
Atajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa chini ya mgongo na atajipaka chini ya korodani (mapumbu) na kusugua kwa mzunguko pamoja na kula unga wa Habbat-Sawdaa kijiko kimoja, na robo kijiko kidogo cha manemane katika nusu gilasi ya asali iliotiwa katika maji yenye vuguvugu; kila siku na wakati wowote apendao.
Pumu (Asthma)
Atanusa moshi wa mafuta a Habbat-Sawdaa asubuhi na jioni. Pia atakula unga wake asubuhi na jioni kabla ya kula chakula kila siku na pia kujipaka mafuta yake kifuani na kooni kabla ya kulala kila siku.
Kidonda
Atayachanganya matone kumi ya mafuta ya Habbat-Sawdaa, katika kikombe cha asali na kijiko kimoja cha maganda ya komamanga yaliyokaushwa na kusagwa. Atakula kila siku kabla ya kula chakula; baadae atakunywa gilasi ya maziwa yasiyotiwa chochote.
Saratani (Cancer)
Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa mara tatu kila siku na kula kijiko cha unga wake kila amalizapo kula katika kikombe cha juisi ya karoti. Ataendelea hivyo kwa muda wa miezi mitatu.
Nguvu Za Kiume
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja achanganye (apige) ndani ya mayai saba ya kienyeji; atafanya hivyo siku baada siku kwa muda wa mwezi mmoja. Basi hata kama ana miaka 120 atapata nguvu za barobaro!
Udhaifu kwa Ujumla
Atachukua unga wa habat sosa kiasi cha kikombe kimoja, uwatu mfano wake na ambari ilioyeyushwa kiasi cha kijiko kidogo, vyote atavichanganya katika chombo chenye asali iwe kama jamu; halafu awe akila kama jamu kila siku na wakati wowote apendao lakini kwa mkate wa ngano asili.
Kuleta Hamu Ya Kula
Kabla ya kuanza kula, jipatie Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kidogo na uitafune kwa meno yako, na unywe maji ya kawaida yaliochanganywa na siki kidogo.
Kutibu Ulegevu Na Uvivu
Atakunywa- kabla ya kula – juisi ya machungwa iliochanganywa matone kumi ya mafuta ya Habbat-Sawdaa. Ataendelea hivyo kwa muda wa siku kumi. Baada ya hapo ataona nishati na uchangamfu.
Nishati akilini Na Wepesi Wa Kuhifadhi
Atachemsha nanaa (mint leaf), aichanganye na asali na aingize matone saba ya mafuta ya Habbat-Sawdaa; anywe kinywaji hiki kikiwa na vuguvugu wakati wowote apendao. Basi ataionea namna fahamu itakavofanya kazi
103 responses to “MARADHI YANAYOTIBU HABBA SODA”
Ali Saleh Kombo,
January 3rd, 2011 at 11:31
Alhamdulillah namshukuru Allah kuniwezesha kuiona website hii ambayo nimefaidika vya kutosha kuhusu tiba hii ya Habbat Saudaa. Kwani ni salama ambayo ni kutoka kwa mtukufu wa daraja S.A.W. Ni vyema kuwa na imani na tiba hizi pia kuhimizana kuzitumia na mimi kuanzia sasa inshallah, nitafanya hivyo kwa kufuata sunna ya bwana mtume s.a.w.
wabillahi taufiq.
Haji kombo
December 18th, 2012 at 06:33
NAOMBA UNITUMIE KATIKA EMEIL YANGU HII DAWA YA NGOZI YALIO FANANA NA MBALANGA
nyasenga seiph
April 19th, 2019 at 08:40
Allah akulipeni mema duniani na akhera
Hassan
April 21st, 2011 at 08:44
je maji kujaa mapafuni, inweza kukausha
Gohil
May 5th, 2011 at 07:09
Jamani nisaidieni’
Wakati wa mapenzi nguvu za kiume ya punguwa
Abdul
August 16th, 2011 at 12:43
Alhamdulilaah alaa niimati Llah, tutumieni hizi ndio dawa! na tufuatanishe na adhkari.
Donath M. Shirima.
September 1st, 2011 at 05:40
Tiba ya Kuharisha.
Atachimba mzizi wa mpapai, aoshe vizuri kisha twanga, weka maji kikombe kimoja kisha chuja, changanya na asali vijiko vitano vya chakula, au sukari vijiko vitatu, kisha anywe kutwa mara tatu, kijiko kimoja cha chakula kwa mtoto mdogo kijiko kimoja cha chai, Inshaala kwa neema ya Mungu utapona.
N.B Sijwawahi kwenda hospitali kwa maradhi ya tumbo la kuharisha nina zaidi ya miaka 20 na tiba hii, na nimesaidia wengi kwa tiba hii. Aidha sukari na asali ni kwa ajili tu ya kupunguza ukali hivyo ratio hiyo ya asali na sukari siyo muhumu sana.
Donath M. Shirima.
September 1st, 2011 at 05:49
Asilimia kubwa ya maradhi ya mwanadamu yanatokana na matatazizo ya kisaikolojia. Hivyo tiba yoyote itafanya kazi endapo tu yule mwenye kutumia anaamini kuwa atapona. Naweza nikuambie nina miaka zaidi ya 13 sasa hivi nikijitibu kwa maji na mara chache sana kwa majani ya mlonge, mbegu na magome yake. Maji ni tiba namba moja kwa magonjwa mengi hasa ya kisaikolojia.
Donath M. Shirima.
September 1st, 2011 at 06:08
Nisiwe mnyimi wa shukurani. Nimshukuru huyu aliyeplan Website hii mahiri kwa tiba na ushauri.
suleiman Nyirenda
November 10th, 2011 at 08:54
nimefurahishwa na kuvutiwa na vyote vilivyoandikawa humu, hasa upande wa habbat sawda. Kimsingi mi nasumbuliwa na tatizo la sikio, nilikua nikisikia maumivi kipindi cha nyuma(mwezi wa pili mwaka huku), nikaenda hospital nikapatiwa dawa maumivu yakapungua lakini hivi karibuni maumivi yameongezeka na kuna kauvimbe kametokea kwa nje ya sikio kanauma pia. Je nitatumia vipi hiyo habbat sawda?
Moza Ally
January 5th, 2012 at 00:09
assalamu alaykum warahmatullah.Asanteni sana kwa wote walioweka web hii nzuri,kwa kweli ni nzuri itanisaidia mimi na kila mtu ambaye atapenda kutumia dawa hizi ambazo hazina cemical ndani yake.pia napenda kuuliza kuna dawa yeyote ya kifafa,ningependa kujua.asante.
loburas ewoi
February 17th, 2012 at 13:46
mimi niko kenya dawa inapatikana wapi?
skaska
December 15th, 2014 at 09:11
maduka ya dawa asilia na sunnah
peter
May 1st, 2012 at 10:40
dawa nitaipataje nipo dar es salaam
olomi
June 18th, 2012 at 12:55
asalam alekum,mim ndugu yangu mgongo unaniuma sana,kiuno,mpaka maumivu hayo nayasikia kwenye chembe ya moyo unaweza kunisaidia ndugu yangu?
skaska
June 18th, 2012 at 18:16
angalia zaidi katika hicho chuma ulichofungua kuna matibabu ya maradhi yote
Miraji I Mfinanga
July 4th, 2012 at 18:35
Niombacho kuelewa ni utaratibu WA jinsi ya kutunia habat sauda NA mayai saba ya kienyeji. Je,kunywa ni kila siku Kwa siku 30 au ni Siku1 ndani ya siku 30?? NA mayai yote saba yananywewa tote Kwa Mara moja au hunywewaje…?_
Kidulla
July 13th, 2012 at 22:34
Hata mimi ndugu zangu naomba kuelimishwa utaratibu wa jinsi ya kuyatumia hayo mayai saba ndani ya hizo siku 30. Kwa kweli katika maelezo ya matumizi ya dawa hii halikufafanuliwa hilo. Naomba msaada wenu.
abdallah
August 21st, 2013 at 10:47
Ass.aleykum, miraji vp tayar umeshapata jibu liswali lako hilo la kunywa mayai 7 yakuku wakienyeji na habat sawdaa.?
khamis
September 4th, 2015 at 17:06
Khamis naomba kuptiwa dawa y vdonda vya tumbo
skaska
September 5th, 2015 at 08:33
soma vizuri imo humo humo
shabani
July 24th, 2012 at 19:19
A.alykum. Naitwa Shabani. Natatizo la kukosa usingizi kwa muda mrefu sasa, nimehangaika sana bila mafanikio, naomba nipatiwe maelezo zaidi ya matumizi ya dawa nimeona habbat soda lakini sielewi ni kitu gani na nitakipata wapi, naomba mnisaidie kwa kunipa ufafanuzi zaidi nianze kuitumia pia naombee niambiwe nitaitumia kwa mda gani mpaka tatizo langu litakapokwisha, natanguliza shukrani zangu kwako na MUNGU akubaliki
Ahmadi
August 8th, 2012 at 23:18
Naomba nifaamiswe nini nifanye? Nasumbuliwa na maumivu ya misuri mwilini, ina ng’wenya na kupwita na ina sababisha kupunguza nguvu mwilini, na hamu ya kazi kwaujumla, mikono yapasua pia, naweza tumia dawa ipi?
mohammed nyawa
August 15th, 2012 at 08:00
nasumbuliwa na chembe cha moyo,kilizama ndani
jumaa fuime
September 23rd, 2012 at 11:39
nasumbuliwa na vidonda vya tumbo
Serelly
September 25th, 2012 at 20:56
Kuitaqidi dawa ni shirki, na kuacha dawa ni ujinga. Please be aware of this. Peace be upo you all.
MUUNGANO HUU HATUUTAKI.
JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.
“When peace fails apply force”
Nawasilisha.
SERELLY.
Latif
December 20th, 2012 at 16:25
Asalam .minaomba msaada wa ufafanuzi kuhusu utumiaji wa mayai na unga wahabasoda nikila siku ama kwa mwezi mara moja
mamii
February 8th, 2013 at 10:47
kiukweli inalipa
allyhib16
March 11th, 2013 at 17:32
unga wa habat soda na mayai saba unakunywa mabichi au baada ya kuchanganya unakaanga ndio ule
skaska
March 18th, 2013 at 07:21
angalia maelekezo
ISMAIL MUSSA
August 11th, 2014 at 08:30
A/ALYKHUM WARAHMATULLAH WABARAKATUL NIMEPENDA SN DARASA HII
Tony
March 28th, 2013 at 18:05
nahitaji hiyo dawa sana,nitaipataje?
skaska
March 29th, 2013 at 14:32
FUATA MAELEKEZO SHEIKH
RegganRimoy
August 23rd, 2016 at 14:51
Ni kweli kabisa Shirima.
Kidato Bakari Said
March 30th, 2013 at 14:22
Very educative, self explantory with simple instructions. May the Most High reward you abudantly. Amen.
allyhib16
March 30th, 2013 at 16:22
kijiko kimoja ndani ya mayai saba siku baada ya siku ina maana nile kila siku? au unamaana nile siku moja moja ndani ya mwezi mmoja?
Nasser Habsi
April 2nd, 2013 at 17:28
mwanzo nilikuwa sijui faida ya habati soda nashukuru sana kwa maelekezo yenu
kwa kweli ina faida sana…………nasser
bajuni
April 9th, 2013 at 21:32
mi nauliza hii dawa ya nguvu ya kiume unga Wa habat soda kijiko kimoja na mayai saba ya kienyeji unakunywa mara kwa siku au unatumia vipi
Saidyahyasultan
April 14th, 2013 at 11:29
Kwanza Alhamdulillah kwa kunipa mwingi hekma
doctor mm nna tatizo la moyo yaani moyo unapiga mapigo mengi ayd ya kawaida tatizo hili ni litibu kwa njia gani au kwa vipimo vya mpangilio gani?
Paulo Edward Lugodisha
April 27th, 2013 at 14:25
Nashukuru sana kwa website hii inamambo mazuri sana yahusuyo tiba. Pamoja na hivo naomba kuuliza sijaelewa vizuri kuhusu matumizi ya dawa ya nguvu za kiume. Je habbat soda ikishachanganya na mayai mchanganiko huo unatumikeje?
Mohamedi Mwijuma
May 12th, 2013 at 07:17
Nami nataka kujua hayo mayai saba na unga habbat soda ni kila siku au maramoja bali utmike kwa siku 30?
skaska
May 14th, 2013 at 08:11
fuata maelekezo sehemu uliyosoma
issa
May 27th, 2013 at 05:50
Mansh’ALLAH nimefaidika kiasi chakutosha ila baadhi ya majina ya vifaa si yafahamu kama vile:chirichiri,kamun,nana,uwatu,mbono n.k vinapatikana wapi hivo?
skaska
May 27th, 2013 at 12:30
wenye maduka ya dawa asilia ndio wanaozijua
Kashinde
May 29th, 2013 at 20:13
Nitaipata vipi hio dawa? Niko tanga kwa ajili ya uzazi.
skaska
May 30th, 2013 at 12:06
nenda maduka ya dawa za sunna
hamis
June 9th, 2013 at 17:44
tunashukulu kwa kutujulisha tiba bora kabisa
Ally juma
June 23rd, 2013 at 14:42
Nifafanukie unaposena mayai saba siku kwa siku unamaana kila siku? pia kijiko ulichosema hapo nikile kikubwa au kile kidogo cha chai? mimi ninapotumia mayai nahisi kuhema kwa taabu pressure, je´ni lazima nitumie njia hiyo? hakuna mbadala? nahitaji saana kutibu tatizo hili la ukosefu wa nguvu kwani ni la mda mrefu sana kiasi cha mimi kukata tamaa.
skaska
June 27th, 2013 at 11:43
ndio kila siku ni kijiko cha chai ahsante, lakini fuata maelekezo zaidi kwa wataalamu wa dawa za sunnah
Alice g
September 5th, 2013 at 18:07
Asante kwa msaada wako
Omar Muktar
September 11th, 2013 at 10:23
Many thanks for giving us this Lecture. My Allah increase you more knowledge wherever you are.
David Choka
September 15th, 2013 at 08:58
Nimefaidika sana na maelekezo yahusuyo HABBA SODA.Nakupa pongezi kwako.
Costantine
September 24th, 2013 at 18:52
Kwenye nguvu za kiume,huo muunganiko wa unga na mayai unakaangwa au ulinywewa?
Zuleikha
October 28th, 2013 at 10:32
mimi mdogo wangu anakaribia miaka miwili kiumri lakini ana tatizo katika koo inasemekana ana uvimbe na hospital wamesema kupasuliwa mpaka atimie miaka 4, hawezi kula chakula kizito,hawezi ata kuvuta pumzi vizuri na anakua anakoroma kaw vile anavuta pumzi kwa tabu, tufanyeje????????????
mary john
March 5th, 2014 at 11:00
Dawa nzuri ila fungus za koo na mdomoni tiba yake nini
Abu Zamakhshary
April 20th, 2014 at 00:33
jazaakumullahu khayr, wa baarakallahu fiikum.
rahaawewe
May 8th, 2014 at 23:43
Habatt Sawdaa inaitwaje kwa English plz!
rahaawewe
May 9th, 2014 at 20:07
Nimefurahi kwa elimu nzuri ya haya mafuta ahsante!
NI PESA NGAPI YAUZWA?
May 18th, 2014 at 15:31
shukran nitajaribu
CHAGGAN KIMARO
July 5th, 2014 at 10:15
THANKS,GOD BLEES YOU!!
Mussa
July 19th, 2014 at 01:06
Assalaam aleikum ndungu zanga ktk iman me nngelipenda kufafanuliwa vizuri katika uchanganyaji wa mayai 7 na unga wa habat sauda sijaelewa kabisa
Sayyid Athuman
August 9th, 2014 at 04:35
A/alykum wenzangu nimshukru sana na sifa njema Zinamstaiki Allah. Kwangu Mimi nimefahamu kiasi kidogo ukilinganisha mwenye. Kuisoma lakini ningependa kuwasiliana na nyinyi. Asante Mimi wenu Syd
makame hassan
August 23rd, 2014 at 07:46
assalamu aleikum naomba maelekezo zaidi ya hiyo namna ya kutibu nguvu za kiume sijaelewa maana hapo kwenye breket umeandika neon apige sijaelewa umekusudia nini
ramadhan mashaka
August 26th, 2014 at 17:13
Nguvu Za Kiume
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja achanganye (apige) ndani ya mayai saba ya kienyeji; atafanya hivyo siku baada siku kwa muda wa mwezi mmoja. Basi hata kama ana miaka 120 atapata nguvu za barobaro!.
naomba ufafanuzi hapa hiyo ni ya kunywa au unatumiaje?
Ruhogora
August 27th, 2014 at 20:43
THANKS
Idrissa madoud
August 31st, 2014 at 11:27
I’m Idrissa Maoud.
Asslaam Alaykum jamiyah! I have nothing to add rather than saying keep on and Allah protects you for this good work.
Salama Shewedi
September 4th, 2014 at 10:33
Jazaka llah. Habari hii nzuri Mungu atujalie tutibike na dawa hii. Alhamdulilah
michael
September 20th, 2014 at 08:13
Asanteni sana kwa kuelimisha watu ili wapone na wawe na afya njema MWENYEZI MUNGU NA AWE NANYI POPOTE MTAKAPO KUWAPO.
Makopa E.J
September 26th, 2014 at 11:18
Sijaelewa kwenye kutibu nguvu za kiume unapaka au unakunywa?
adrian mhangwa
September 28th, 2014 at 14:19
Kwa jina naitwa Adrian mimi nina matatizo ya vimbe katika matiti yangu niliwa naomba kuu liza habb soda inawe kunitibu?
skaska
September 29th, 2014 at 03:54
angalia maelezo zaidi pia pata ushauri wa daktari kwa ajili ya vipimo
lubna luckman
September 30th, 2014 at 20:53
aslm alkm nimependa hii dawa hivi kama mtu unakua na tatizo la mimba kutoka unatumia dawa gani
Abdallah Said
October 30th, 2014 at 18:56
Naomba maelekezo ya namna ya kutumia mayai saba na habbat soda. unachanganya mayai saba kila siku ? Au yale saba waeza kunywa mara moja?
mohamed jumanne
April 1st, 2015 at 14:35
Nijulishe dawa ya miguu kuuma
mattar mohammed
April 8th, 2015 at 14:10
A/hamdulillah nashukuru Sana baada ya kuiyona hadithi ya mtum saw na maelezo yenu yenye kutia moyo mzuri kwa jamii yote ambae amepata maradhi kama mtu Ana maradhi na hawezi kupata baadhi ya vitu ambavo mmvitaja jee afanye nini au nyinyi mnazo tayari hizo dawa
Hatibu R
June 22nd, 2015 at 09:58
Nina tatizo, ambapo uume wangu umesinyaa na kua mdogo. Nin tiba yake?
Hatibu R
June 22nd, 2015 at 10:02
Tatizo jingne ni kwamba ninapotoa mshindo wakati wa tendo, mbegu hazina spidi waka wa kutoka, yan haziruki, znatoka kawaida
amiry adnan
June 24th, 2015 at 11:05
Tiba Kifua kikuu
khamis omar
June 25th, 2015 at 05:47
niilezee jinsi ya kuchanganya habbat sauda na mayai hio shida yanitesa sana nahitaji msaada wenu
Mohammedamin
July 4th, 2015 at 22:45
niliathirika na figo nataka usaidizi
Kolde Suleiman
July 30th, 2015 at 20:38
Maa Shaa Allah! Its great invention n of high importance. May those concerned in publishing de same be granted Shifaa on this Earth n Janatul Fardowsa in de hereafter In Shaa Allah
Abdoul Karim
August 25th, 2015 at 23:35
Aslm alykum
Ningependa kujua dawa kuongeza nguvu za kiume mimi sijaelewa kijiko kimoja cha unga na mayayi 7 ninachanga vipi apo sheikh ninaomba ufafanuzi vizuri
skaska
September 5th, 2015 at 08:34
kuchanganya ni kuchanga tu
Kidula
September 7th, 2015 at 03:33
Hili suali linaendelea kuulizwa na watu tofauti kwa muda mrefu sana. Mimi naomba kwa wale wanaojua jibu lake watowe ufafanuzi ili liweze kuwasaidia hao wenye shida na nyinyi mtapata malipo makubwa kwa Allah kwa kumsaidia wenye maradhi kumpatia dawa.
THOMAS
November 22nd, 2015 at 11:09
Asante kwa maelezo.
ibrahim siafu
December 18th, 2015 at 01:37
sante sana ila nitafute tusaidiane
suleiman
December 22nd, 2015 at 22:04
assalam alaykum warahamatullah wabarakatuh, nashkur kwa maelezo mazuri juu ya matumizi ya habbat sauda kwenye kuleta shifaa……
naomba niulize swali kwenye kipengele cha matumizi ya habat sauda kwenye kuleta nguvu za kiume, jee?? kijiko hiko kimoja cha habbat sauda napochanganya na hayo mayai saba ya kuku wa kienyej, matumizi yake yanakuwaje na huo mchanganyiko unaweza kudumu kwa kipindi gani na unahitaj hali gani kuhifadhiwa ili usiharibike haraka.
Ahsante.
Semeni
January 19th, 2016 at 20:13
Thanx
salim
January 22nd, 2016 at 17:22
Mi naomba msaada wa kupata daktari natatizo la nguvu za kiume nimejaribu sana kutumia mayai ya kienyeji kwa kuchanganya na Unga wa habbat sauda lakini bado tatizo halijaisha inanitesa sana
ABDALLAH KIMEI
April 7th, 2016 at 11:25
jaribu na kwenda kusomewa kisomo cha ruqya ya kisheria kisha endelea kutumia dawa inshaallah utapona
RegganRimoy
August 23rd, 2016 at 14:39
Unavyochanganya habatisoda kwenye mayai saba ya kienyeji unakunywa mabichi au! 😮😮
skaska
August 31st, 2016 at 16:45
sasa ukiyapika huwezi kunywa ila utakula
Hajj hassan
September 4th, 2016 at 05:31
Jazzakha allahukheir kwa maanufaa ya mutupayo
Barack Khaled
October 31st, 2016 at 16:10
Mwenyezimungu awezidishie kwa kutoa elimu hii!
kelvin
November 3rd, 2016 at 13:03
Nipo arusha, wapi tapata hii habbat sawdaa? Hasa unga wake.
Rashidi
December 23rd, 2016 at 04:47
assalam alaykum warahamatullah wabarakatuh, nashkur kwa maelezo mazuri juu ya matumizi ya habbat sauda kwenye kuleta shifaa……
naomba niulize swali kwenye kipengele cha matumizi ya habat sauda kwenye kuleta nguvu za kiume, jee?? kijiko hiko kimoja cha habbat sauda napochanganya na hayo mayai saba ya kuku wa kienyej, matumizi yake yanakuwaje na huo mchanganyiko unaweza kudumu kwa kipindi gani na unahitaj hali gani kuhifadhiwa ili usiharibike haraka.
Ahsante
Buya Hussein Barisa
January 1st, 2017 at 09:39
Maneno mazuri sana na yenye manufaa. Mtume wetu Muhammad ( s.a.w ) aliposema habba soda ni tiba ya kila maradhi isipokuwa mauti na u zee. Na hii nadhani ni hadithi swahiih.
Sasa kupitia kwa maneno Haya ya Mtume wetu Muhammad, jee hata UKIMWI unatibiwa na io hiyo habba soda? Wanasayansi wamejaribu sana kutafuta dawa lakini wameshindwa kupata dawa ya UKIMWI. Kwa hivyo, kwa kuwa mimi ni muislamu naamini ya Kwamba Sisi waislamu dawa ya UKIMWI tuko nayo. Ni vile tuko wazembe kusoma, kuelewa, kufahamu, kufuata na kuyazingatia maneno ya Qura’n yetu tukufu na hadithi na sunnahw za Mtume wetu Muhammad ( s.a.w ).
Kwa hivyo kama ni Kweli Kwamba dawa ya UKIMWI Sisi waislamu tunayo jee , hii habba soda itumiwe kivipi au ichanganywe na dawa Zingine zipi ili itibu Huu ugonjwa sugu wa UKIMWI?
wahida mohamedy
January 22nd, 2017 at 08:49
as alaykhum… Dawa ya ukimwi ni kuacha uzizi na kujiheshimu nahisi kila jambo linamakusudio.
John Mbwele
February 14th, 2017 at 08:52
Assalm Alaykum Warahamatullah Wabarakatuh, Kuna mtu ameandika makala yeye kwenye mtandao ukisearch jina ni Fadhili Paulo amesema mafuta ya Habbat Soda inaua kabisa virusi vya Ukimwi je ni kweli mtaalam naomba jibu na dozi yake ikoje kama ni kweli.
Abdi Ayoub
May 30th, 2017 at 06:30
Shukran,JazaakumuLLAH khair.
John Mbwele
September 28th, 2017 at 11:30
Wahida Mohamedy sio wazinzi kama unavyodhania inaweza ikatokea bahati mbaya ukaupata bila kukusudia sindano jamaa zetu ambao wanao tunashirikiana kila siku kwenye ajali. Mimi naamini Dawa ipo sema Allah ameificha tu ili binadamu tufunzwe adabu kipindupindu kilichukua muda mrefu sana kupatikana dawa na kiliua watu sana hata kifua kikuu lakini Allah akaleta rehma zake dawa zikapatikana na huu UKIMWI naamini dawa ipo na itakuja kupatikana.
Salmatalhat
October 19th, 2017 at 04:04
Nikweli habat soda ina rudisha ute wa kwenye viungo?
swellemu_JNR
October 31st, 2017 at 09:22
kipi bora zaidi , mbegu ,mafuta amma unga???