WATOTO Yatima katika kijiji cha SOS, mjini Zanzibar wameshiriki katika chakula cha futari  na mke wa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, katika kijiji chao Mombasa mjini Zanzibar.
 
Mama Mwanamwema, alishiriki katika chakula hicho juzi usiku akiwa pamoja na mama Asha Suleiman Iddi, pamoja na Umoja wa wake wa Viongozi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Abdalla Mwinyi Khamis