MATOKEO YA URAIS WA ZANZIBAR KATIKA MAJIMBO

MATOKEO YA UCHAGUZI WA URAIS WA ZANZIBAR KWA MJIMBO YOTE YA ZANZIAR

FUONI CCM 6,351 69.0%, CUF 2,777 30.2%, AFP 9 0.1%, JAHAZI ASILIA 9 0.1%, NCCR MAGEUZI 8 0.1%, NRA 33 0.4, TADEA 14 0.2%.

MTONI CCM 3,746 43.4%, CUF 4,852 56.2%, AFP 6 0.1%, JAHAZI ASILIA 11 0.1%, NCCR MAGEUZI 5 0.1%, NRA 4 0.0%, TADEA 11 0.1%.

DOLE CCM 4,777 69.9%, CUF 2007 29.4%, AFP 12 0.2%, JAHAZI ASILIA 16 0.2%, NCCR MAGEUZI 8 0.1%, NRA 7 0.1%, TADEA 7 0.1%.

DIMANI CCM 6,226 55.5%, CUF 4,898 43.7%, AFP 13 0.1%, JAHAZI ASILIA 23 0.2%, NCCR MAGEUZI 55 0.1%, NRA 11 0.1%, TADEA 23 0.2%.

KIEMBESAMAKI CCM 2,734 71.8%, CUF 1,041 27.4%, AFP 5 0.1%, JAHAZI ASILIA 5 0.1%, NCCR MAGEUZI 3 0.1%, NRA 10 0.3%, TADEA 8 0.2%.

MWANAKWEREKWE CCM 4,338 60.4%, CUF 2,812 39.2%, AFP 4 0.1%, JAHAZI ASILIA 7 0.1%, NCCR MAGEUZI 4 0.1%, NRA 10 0.3%, TADEA 3 0.0%.

BUBUBU CCM 4,458 51.8%, CUF 4119 47.4%, AFP 3 0.0%, JAHAZI ASILIA 7 0.1%, NCCR MAGEUZI 4 0.1%, NRA 12 0.1%, TADEA 3 0.0%.

MFENESINI CCM 3,755 62.2%, CUF 2,246 37.2%, AFP 11 0.2%, JAHAZI ASILIA 7 O.1%, NCCR MAGEUZI 4 0.1%, NRA 7 0.1%, TADEA 8 0.1%.

MAGOGONI CCM 3,877 44.1%, CUF 4,867 53.4%, AFP 5 0.1%, JAHAZI ASILIA 13 O.1%, NCCR MAGEUZI 4 0.1%, NRA 7 0.1%, TADEA 8 0.1%.

MPENDAE CCM 4,870 57.5%, CUF 3,546 41.8%, AFP 7 0.1%, JAHAZI ASILIA 8 0.1%, NCCR MAGEUZI 4 0.0%, NRA 28 0.2%, TADEA 13 0.2%.

KWAHANI CCM 4,994 78.1%, CUF 1,346 21.1%, AFP 8 0.1%, JAHAZI ASILIA 12 0.2%, NCCR MAGEUZI 1 O.0%, NRA 15 0.2%, TADEA 19 O.3%.

MJIMKONGWE CCM 1,589 25.1%, CUF 4,717 74.5%, AFP 9 0.1%, JAHAZI ASILIA 8 0.1%, NCCR MAGEUZI 4 0.0%, NRA 28 0.3%, TADEA 13 0.2%.

AMANI CCM 4,367 64.9%, CUF 2,312 34.4%, AFP 10 0.1%, JAHAZI ASILIA 20 0.3%, NCCR MAGEUZI 6 0.1%, NRA 6 0.1%, TADEA 4 0.1%.

RAHALEO CCM 4,043 66.2% CUF 2,216 35.2% AFP 4 0.1% JAHAZI ASILIA 14 0.2% NCCR MAGEUZI 9 0.1% NRA 6 0.1% TADEA 8 O.1%.

KIKWAJUNI CCM 4,534 90.5% CUF 1,860 28.9% AFP 6 0.1% JAHAZI ASILIA 10 0.2%, NCCR MAGEUZI 0 0.0%, NRA 12 0.2%, TADEA 90.1%.

DONGE CCM 6,320 88.4%, CUF 7,73 10.8%, AFP 9 0.1%, JAHAZI ASILIA 28 0.4%, NCCR MAGEUZI 5 0.1%, NRA 5 0.1%, TADEA 11 0.2%.

UZINI CCM 7,158 89.9%, CUF 7,36 9.2%, AFP 14 0.2%, JAHAZI ASILIA 26 0.3%, NCCR MAGEUZI 7 0.1%, NRA 8 0.1%, TADEA 12 0.2%.

CHWAKA CCM 7,365 81.1%, CUF 1,610 17.7%, AFP 36 0.4%, JAHAZI ASILIA 30, NCCR MAGEUZI 9 0.1%, NRA 18 0.2%, TADEA 13 0.1%.

KOANI CCM 7,247 69.3%, CUF 3099 29.7%, AFP 9 0.1%, JAHAZI ASILIA 30 0.3%, NCCR MAGEUZI 26 0.2%, NRA21 0.2%, TADEA 18 0.2.

MAKUNDUCHI CCM 6,544 83.0%, CUF 1,256 15.9%, AFP 13 0.2%, JAHAZI ASILIA 15 0.2%, NCCR MAGEUZI 6 0.6, NRA 46 0.6%, TADEA 5 0.1%.

MUYUNI CCM 6,052 81.5%, CUF 1,316 17.7%, AFP 9 0.1%, JAHAZI ASILIA 15 0.2%, NCCR MAGEUZI 4 0.1%, NRA 14 0.2%, TADEA 13 0.2%.

KITOPE CCM 5,183 80.5%, CUF 1,186 18.4%, AFP 13 0.2%, JAHAZI ASILIA 21 0.3%, NCCR MAGEUZI 11 0.1%, NRA 8 0.1%, TADEA 14 0.2%.

BUMBWINI CCM 3,662 60.2%, CUF 2,377 39.1%, JAHAZI ASILIA 8 0.1%, NCCR MAGEUZI 4 0.1%, NRA 10 0.2%, TADEA 10 0.2%.

MAGOMENI CCM 5,200 59.9%, CUF 3,494 39.8%, JAHAZI ASILIA 10 0.1%, NCCR MAGEUZI 8 0.1%, NRA 13 0.1%, TADEA 18 0.2%.

MATEMWE CCM 3,531 66.0%, CUF 1,641 30.7%, AFP, 36 0.7%, JAHAZI ASILIA 65 1.2%, NCCR MAGEUZI 30 0.5%, NRA 16 0.3%, TADEA 28 0.5%.

NUNGWI CCM 3,791 51.4%, CUF 3,473 47.1%, AFP 31 0.4%, JAHAZI ASILIA 34 0.3%, NCCR MAGEUZI 8 0.1%, NRA 17 0.3%, TADEA 17 0.3.

MKWAJUNI CCM 3,583 60.4, CUF 2220 32.4%, AFP 34 0.6%, JAHAZI ASILIA 46 0.8%, NCCR MAGEUZI 10 0.2%, NRA 27 0.5%, TADEA 16 0.3.

JANG’OMBE CCM 5,762 71.1%, CUF 2295 28.3%, AFP 3 0.0%, JAHAZI ASILIA 6 0.1%, NCCR MAGEUZI 7 0.1%, NRA 12 0.1%, TADEA 15 0.2%.

CHUMBUNI CCM 5,345 60.0%, CUF 3475 39.0%, AFP 12 0.1%, JAHAZI ASILIA 17 0.2%, , NCCR MAGEUZI 8 0.2%, NRA 17 0.2%, TADEA 17 0.2%.

MICHEWENI CCM 1,548 22.1%, CUF 5,370 76.8%, AFP 5 0.1%, JAHAZIO ASILIA 13 0.2%, NCCR MAGEUZI 12 0.2%, NRA 8 0.2%, TADEA 40 O.6.

TUMBE CCM 573 3.2%, CUF 6,265 91.3%, AFP 123 1.8%, JAHAZI ASILIA 13 0.2%, NCCR MAGEUZI 3 0.0%, NRA 5 0.1%, TADEA 3 0.0%.

KIWANI CCM 1,605 29.8%, CUF 3,743 69.5%, AFP 9 0.2%, JAHAZI ASILIA 9 0.2%, NCCR MAGEUZI 6 0.1%, NRA 7 0.1%, TADEA 9 0.2%

ZIWANI CCM 921 13.5%, CUF 5,901 86.3%, AFP 2 0.0%, JAHAZI ASILIA 5 0.1%, NCCR MAGEUZI 5 0.1%, NRA 4 0.1%, TADEA 1 0.0%.

WAWI CCM 2024 25.0%, CUF 6,036 74.4%, AFP 13 0.2%, JAHAZI ASILIA 11 0.1%, NCCR MAGEUZI 12 0.1%, NRA 7 0.1%, TADEA 6 0.1%.

CHONGA CCM 2,150 34.1%, CUF 4,108 65.2%, AFP 10 0.2%, JAHAZI ASILIA 16 0.3%, NCCR MAGEUZI 8 0.1%, NRA 6 0.1%, TADEA 3 0.0%.

OLE CCM 8,93 13.7%, CUF 5,775 86.2%, AFP 6 0.1%, JAHAZI ASILIA 13 0.2%, NCCR MAGEUZI 4 0.1%, NRA 6 0.1%, TADEA 5 0.1%.

CHAKE CHAKE CCM 1,575 21.9%, CUF 5,530 77.7%, AFP 12 0.2%, JAHAZI ASILIA 5 0.1%, NCCR MAGEUZI 5 0.1%, NRA 2 0.0%, TADEA 4 0.1%.

MTAMBWE CCM 307 5.4%, CUF 5,415 74.4%, AFP 1 0.0%, JAHAZI ASILIA 6 0.1%, NCCR MAGEUZI 2 0.0%, NRA 3 0.1%, TADEA 4 0.1%.

KONDE CCM 6,53 10.1%, CUF 5,751 89.9%, AFP 5 0.1%, JAHAZI ASILIA 10 0.1%, NCCR MAGEUZI 10 0.1%, NRA 1 0.0%, TADEA 4 0.1%.

MTAMBILE CCM 961 16.1%, CUF 4,9818 83.5%, AFP 3 0.1%, JAHAZI ASILIA 5 0.1%, NCCR MAGEUZI 3 0.1%, NRA 5 0.1%, TADEA 6 0.1%.

WETE CCM 1,159 25.5%, CUF 6,317 83.3%, AFP 1 0.0%, JAHAZI ASILIA 6 0.1%, NCCR MAGEUZI 8 0.1%, NRA 2 0.0%, TADEA 2 0.0%.

KOJANI CCM 562 8.2%, CUF 6,262 91.5%, AFP 2 0.0%, JAHAZI ASILIA 13 0.2%, NCCR MAGEUZI 3 0.0%, NRA 1 0.0%, TADEA 1 0.0%.

GANDO CCM 8,84 14.4%, CUF 5,239 85.4%, AFP 1 0.0%, JAHAZI ASILIA 8 0.1%, NCCR MAGEUZI 3 0.1%, NRA 1 0.0%, TADEA 2 0.0%.

MGOGONI CCM 615 9.8%, CUF 5,614 89.1%, AFP 5 0.1%, JAHAZI ASILIA 12.0%, NCCR MAGEUZI 5 0.1%, NRA 3 0.0%, TADEA 0 0.0%

November 2, 2010 skaska Leave a comment Edit this 

Categories: Uncategorized
———————————————————————————-

DR. SHEIN KUAPISHWA KESHO

Dr. Shein

Wananchi wa Zanzibar kesho watashudia kitendo cha kihistoria cha kuapishwa rais wa kwanza wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi atakaongoza serikali ya umoja wa kitaifa katika kipindi cha miaka mitano.

Katika sherehe hizo Dr. Ali Mohammed Shein atakula kiapo cha kuiongoza serikali hiyo kufuatia mabadiko ya katiba ya Zanzibar mbele ya umma wa Zanzibar huko katika uwanja wa amani wakati wa asubuhi.

Dr. Shein aliekuwa mgombea urais wa Zanzibar kutoka CCM alitangazwa rais mteule baada ya kupata ushindi wa asilimia 50.1 dhidi ya mpinzani wake wa karibu kutoka CUF Seif Sharif Hamad aliepata asilimia 49.1 ya kura za urais za uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi jana katika hoteli ya Bwawani Dr. Shein ameahidi kuwatumikia wanzanzibari kwa heshima na busara katika mfumo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Hata hivyo amesema serikali ya umoja wa kitaifa bado ni changamoto kwa wazanzibar, lakini ataheshimu maamuzi ya wananchi ya kukubali serikali hiyo ili kuijenga Zanzibar mpya…

Wakati huo huo rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume anaemaliza muda wake amewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa utulivu na ustahamilivu walionesha wakati wote wa kupiga kura na kutangazwa matokeo.

Amesema ustarabu huo ni ishara ya utamaduni mpya wa siasa unaonesha waafrika wanaweza kuendesha uchaguzi wa amani, utulivu na kufuata sheria.

 

 

November 2, 2010 skaska Leave a comment Edit this

Categories: Uncategorized
—————————————————————————————–

CUF KUMTEUWA MALIM SEIF KUWA MAKAMO WA RAIS WA KWANZA ZANZIBAR

Ismail Jussa

Chama cha wananchi CUF, kimesema kitapendekeza jina la katibu mkuu wa chama hicho kuteuliwa kuwa makamo wa kwanza wa rais wa Zanzibar katika serikali ya umoja wa kitaifa.

Akizungumza katika hafla fupi ya kuwasalimia wafuasi wa CUF waliodai kusherehekea ushindi wa Zanzibar mpya huko Mtendeni kiongozi mwandamizi Ismail Jussa amesema chama hicho kitahakikisha jina la Hamad linapendekezwa kuwania nafasi hiyo

Akizungumzia matokeo ya urais wa Zanzibar Jussa amesema kabla ya kutangazwa viongozi wa chama walipitia matokeo yote na kuwambia wafuasi hao matokeo yaliotangazwa na tume ndio waliokuwa sahihi.

Hata hivyo amesema katika upigaji wa kura kulikuwa na kasoro ndogo ndogo, lakini chama kimeridhika na kumuagiza mgombea wake wa urais Hamad kukubali matokeo hayo.

Aidha Jussa amewataka wafuasi wa CCM kushiriki kwa wingi katika sherehe za kuapishwa kwa rais mteule wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein katika uwanja wa Amani mjini hapa
————————————————————————————————-

KIKWETE ANGOZA NAFASI YA URAIS

Rais Jakaya Kikwete 

MGOMBEA wa urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete anaongoza kura za urais katika majimbo 14 ya uchaguzi yaliyokwishatangazwa hadi jana jioni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Katika majimbo hayo, Rais Kikwete amepata kura 162,439, huku Dk. Willibrod Slaa wa Chadema akipata kura 60,155.

Wagombea wengine akiwamo Profesa Ibrahimu Lipumba wa CUF, amepata 33,819 akifuatiwa na Peter Mziray wa APPT-Maendeleo aliyepata kura 1,806. Hashimu Rungwe wa NCCR-Mageuzi amepata kura 711, Fahmy Dovutwa wa UPDP kura 366 na Mutamwega Mgahywa wa TLP kura 341.

Akitangaza matokeo hayo jana Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Lewis Makame, alitaja majimbo hayo 14 ya awali ambayo matokeo yake yameshafika Tume na kuhakikiwa kuwa ni: Micheweni, Konde, Singida Mjini, Korogwe Mjini, Njombe Kusini, Tumbe, Babati Mjini, Mtwara Mjini na Magogoni.

Mengine ni Bukoba Mjini, Siha, Mpanda Vijijini, Chilonwa na Longido. Singida Mjini, Rais Kikwete anaongoza kwa kupata kura 19,246 akifuatiwa na Dk. Slaa aliyepata kura 5,266. Profesa Lipumba ana kura 922, Mziray kura 93, Mgahywa 24 na Dovutwa kura 22.

Korogwe Mjini Rais Kikwete anaongoza kwa kupata kura 10,761 akifuatiwa na Dk.Slaa mwenye kura 3,135. Profesa Lipumba ana kura 394, Mziray 110, Rungwe 19, Mgahywa tano na Dovutwa sita.

Na katika jimbo la Njombe Kusini, Kikwete ana kura 22,337 na Dk. Slaa 6,848. Mziray ana kura 250, Profesa Lipumba 80, Rungwe 32, Mgahywa 12 na Dovutwa 36, ambapo pia katika jimbo la Mtwara Mjini Kikwete ana kura 18,087.

Profesa Lipumba kura 6,198, Dk. Slaa 4,415, Mgahywa 77, Mziray 161, Rungwe 56 na Dovutwa 33. Longido, Kikwete ana kura 17,067, Dk. Slaa 2,702, Profesa Lipumba 114, Mziray kura 157, Rungwe 10, Mgahywa nne na Dovutwa saba.

Chinolwa, Kikwete ana kura 19,780, Dk. Slaa 2,439, Mziray 319, Lipumba 179, Rungwe 25, Mgahywa na Dovutwa wamefungana kwa kura 18.

Mpanda Vijijini, Kikwete ana kura 7,817, Dk. Slaa 3,669, Lipumba 378, Mziray kura 128, Rungwe 26, Mgahywa kura 17 na Dovutwa 13. Siha, Kikwete ana kura 15,570, Dk.Slaa 7,226, Mziray kura 241, Lipumba 83, Rungwe 18, Dovutwa 14 na Mgahywa kura 11.

Tumbe, Lipumba ana kura 7,021, Kikwete 633, Rungwe kura 127, Slaa 59, Mziray kura 33, Mgahywa kura 36 na Dovutwa 45.

Jaji Makame pia alitangaza matokeo ya jimbo la Micheweni ambapo Profesa Lipumba ana kura 5,674, Kikwete 1,561, Rungwe 168, Dk. Slaa 115, Mgahywa kura 68 na Dovutwa 98. Konde, Lipumba ana kura 6,181, Kikwete 775, Rungwe 66, Slaa 45, Dovutwa 27, Mgahywa 27 na Mziray 20.

Magogoni, Lipumba ana kura 6,044, Kikwete kura 696, Rungwe 79, Dk.Slaa 50, Dovutwa 27, Mgahywa kura 23 na Kuga 22.

Bukoba Mjini, Dk. Slaa kura 16,604, Kikwete kura 15,410, Profesa Lipumba kura 449, Mziray kura 117, Rungwe na Mgahywa wamefungana kwa kura 14 huku Dovutwa akiambulia kura tisa.

Matokeo zaidi ya majimbo mengine yataendelea kutangazwa leo na NEC, kadri itakavyoyapata na kuyahakiki kutoka majimboni.

November 2, 2010 skaska Leave a comment Edit this 

Categories: Uncategorized
————————————————————————————————-

WAPINZANI WANYAKUTA MAJIMBO YA BUNGE TANZANIA BARA

WAGOMBEA kadhaa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama Cha Wananchi (CUF) wamewabwaga wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwemo mawaziri na viongozi wengine waandamizi waliokuwa katika Serikali iliyopita.

Mwenyekiti wa Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, pia wameshinda ubunge mkoani Kilimanjaro.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto, ametangazwa kuwa ni mshindi katika uchaguzi wa ubunge kwenye jimbo la Kigoma Kaskazini.

Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya (bongo flava), Joseph Mbilinyi (Mr II au Sugu) ameshinda katika uchaguzi wa ubunge jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chadema.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Lindi Mjini, Ahamad Sawa jana alitangaza ushindi kwa CUF baada ya kukamilika kuhesabu kura zilizopigwa.

Alisema CCM ambayo ilikuwa na mgombea, Mohammed Abdulaziz, alishindwa kwa kupata kura 11,402 huku mpinzani wake wa CUF Salumu Barwani akipata kura 13,155.

Kutoka Tarime, Samson Chacha anaripoti kwamba mgombea wa CCM Nyambari Nyangweni, amewabwaga wagombea wenzake kutoka vyama vya upinzani kwa kupata kura 28,064.

Mgombea wa Chadema, Mwikwabe Waitara alipata 27,334, wa NCCR-Mageuzi Peter Wangwe (7,811), wa CUF, Charles Mwera (7,368), wa UDP Mchungaji Jacob Mwita (185) na wa TLP, Nyaronyo Kicheere (145).

Jasmin Shamwepu, anaripoti kutoka Dodoma, kuwa Msimamizi wa uchaguzi Dodoma Mjini Suzan Bidya, alimtangaza mgombea wa CCM, David Malole, kuwa mshindi kwa kura 52,243 sawa na asilimia 73.

Aliwashinda wagombea wengine, wa Chadema, Enock Muhembano aliyepata kura 15,806 sawa na asilimia 22, wa CUF Haruna Kamwelwe kura 1,903 sawa na asilimia 2.7.

Mgombea wa NCCR–Mageuzi, Mohamed Kabutali, alipata kura 714 sawa na asilimia moja na wa UPDP, Bona Masawe kura 589 sawa na asilimia 0.83.

Kutoka Shinyanga, Shangwe Thani, anaripoti kwamba msimamizi wa uchaguzi Meatu, Upendo Sanga, alimtangaza mgombea wa Chadema, Meshack Opurukwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo, baada ya kupata kura 13,850 na wa CCM, Salum Khamis (12,824).

Kutoka Musoma, taarifa rasmi iliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Musoma Mjini, ilithibitisha ushindi wa Vincent Nyerere wa Chadema, kuwa mbunge mpya baada ya kumshinda Vedasto Manyinyi wa CCM.

Nyerere alipata kura 21,335 (56.71%), Manyinyi 14,072 (39.38%), Mustapha Wandwi wa CUF 253 (0.71%) Chrisant Nyakitita wa DP 53 (0.15%) na Tabu Machibya wa NCCR–Mageuzi, 19 (0.05%).

Kutoka Mbeya, Merali Chawe anaripoti kuwa Nec ilimtangaza mgombea ubunge wa CCM Mbarali, Dickson Kilusi kuwa mshindi baada ya kupata kura 34,869 dhidi ya wa Chadema, Kazamoyo Kangwa (16,090), TLP, Getrude Dwila (487) na Mwantange Damas wa UDP aliyeambulia kura 237.

Kutoka Ruvuma, Mbunge aliyemaliza muda wake Peramiho, Jenista Mhagama ameshinda tena kiti hicho kwa kupata kura 28,753 dhidi ya mpinzani wake, Mchungaji Chilokota aliyepata kura 2,562.

Katika udiwani, CCM ilizoa kata 17 na Chadema moja. Tunduru Kaskazini, Ramo Makani wa CCM alishinda kwa kupata kura 19,573 na kuwashinda wagombea wengine watatu: Mzee Rajabu wa CUF kura 17,365; Randi Daudi wa Chadema kura 604 na Makamanya Simbili wa UDP kura 72. Kwa udiwani, CCM ilipata kata 16, CUF nne na Chadema moja.

Tunduru Kusini, Mtutura Abdallah Mtutura wa CCM alirejea bungeni kwa kuzoa kura 16,856 dhidi ya kura 10,930 za Mohamed Mambo wa CUF.

Kwa udiwani, CCM ilizoa viti 13 na CUF kimoja. Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo wa Chadema alishinda tena kwa kuzoa kura 28,797 akifuatiwa na Justine Salakana wa CCM aliyepata kura 16,792.

Wengine ni Seif Madongo wa CUF 97; Godfrey Malisa wa TLP 55; Issack Kireti wa SAU 42; Faustine Sungura wa NCCR-Mageuzi 42 na Ndesanyo Godlisen wa UDP 34.

Watu waliojiandikisha walikuwa 112,479; waliojitokeza kupiga kura ni 46,053; kura halali ni 45,759 na zilizoharibika ni 294. Katika jimbo hilo, Chadema ilishinda kata 17 na CCM nne za udiwani.

Mwanga, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe ameshinda kwa kura 20,730 dhidi ya Shafii Msuya wa Chadema aliyepata kura 4,719.

Mgombea mwingine Khadija Hajia wa CUF alipata kura 556; wakati waliojiandikisha ni 63,669; waliopiga kura ni 26,005 na kura 284 ziliharibika.

Kutoka Singida Hudson Kazonta, anaripoti kwamba Msimamizi wa Uchaguzi Singida Mjini, Yona Maki alimtangaza Mohamedi Dewji wa CCM, kuwa mshindi baada ya kupata kura 21,169, dhidi ya wapinzani wake watatu.

Dewji alipata ushindi huo na kuwaacha mbali wapinzani hao; Josephat Isango (Chadema) kura 3,457, Rashidi Mindicar wa CUF (648) na Omari Sombi wa AFP (190).

Maki alisema idadi ya wapiga kura waliojitokeza ni sawa na asilimia 40.4 tu, hivyo ni ndogo ikilinganishwa na watu 64,515 ya waliojiandikisha kwenye Daftari.

Arusha Mjini, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Batilda Burian, ameshindwa na mgombea wa Chadema, Godbless Lema.

Dk. Burian alipata kura 37,460 huku Lema akizoa kura 56,551, na Maximillian Lyimo wa TLP akipata kura 722 na Balawi Balawi wa CUF 150.

Waliojiandikisha katika jimbo hilo ni watu 240,822, na waliopiga kura ni 96,313. CCM imeshinda kata tisa, sawa na Chadema wakati TLP ina kata moja.

Arumeru Magharibi, Godluck ole Medeye wa CCM ameshinda kwa kura 35,544, akifuatiwa na Jackson ole Kisambo wa Chadema kura 27,425.

Katika jimbo hilo, CCM imepata kata 33 na Chadema kata nne. Katika urais, Rais Jakaya Kikwete amepata kura 33,470 na Dk. Willibrod Slaa kura 27,587.

Mkinga, Mgombea wa CCM, Dustan Kitandula ameibuka na ushindi wa kura 16,967 dhidi ya mgombea pekee wa upinzani kutoka CUF, Bakari Mbega aliyejizolea kura 11,252.

Nyamagana, mgombea wa Chadema, Ezekiel Wenje amepata kura 38,171 dhidi ya Lawrence Masha wa CCM aliyepata kura 27, 883.

Kibaha Vijijini, mgombea wa CCM, Hamoud Jumaa ameshinda kwa kura 11,361, akifuatiwa na Agnes Emmanuel wa Chadema, 2,201 na Abdallah Zugo wa CUF kura 1,086.

Katika urais, Jakaya Kikwete kura 11,711; Dk. Willibrod Slaa 2,021; Profesa Ibrahim Lipumba 1,001. Kwa upande wa udiwani, CCM imeshinda kata 11 kati ya 12 na kata moja ya Janga haijafanya uchaguzi.

Kutoka Pangani, kura zilizopigwa ni 15,412, halali 15,085 na zilizoharibika ni 327. Mshindi ni mgombea wa CCM, Salehe Pamba 9,342 dhidi ya mgombea wa CUF, Omari Ally 4,521 na wa Chadema, Abdallah Omari 1,222.

November 2, 2010 skaska Leave a comment Edit this 

Categories: Uncategorized
—————————————————————————————–
Dr. Shein akikumbatiana na Malim Seif mara baada ya kutangazwa mshindi katika hoteli ya Bwawani 

Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein jana alifanikiwa kunyakua ushindi kwenye uchaguzi uliofanyika Jumapili akimshinda mgombea wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad.

Dk Shein, ambaye anamalizia kipindi chake kama makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano, sasa anakuwa rais wa saba wa Zanzibar, ambayo inaundwa na visiwa vya Pemba na Unguja akimbadili Abeid Amani Karume pia wa CCM.

Lakini Dk Shein atakuwa na changamoto kubwa ya kuwa kiongozi wa kwanza kuongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa na atashirikiana na Maalim Seif, ambaye kwa mujibu wa marekebisho ya katiba baada ya kufikiwa kwa maridhiano, anakuwa makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar.

Akitangaza matokeo hayo, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec), Khatib Mwinyichande alisema Dk Shein alipata kura 179,809 ambazo ni sawa na asilimia 50.1.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, Maalim Seif, ambaye amegombea urais kwa mara ya nne, alipata kura 176,338 ambazo ni sawa na aslimia 49.1 ya kura zote 358,815.

Alisema kuwa vyama vilivyosimamisha wagombea urais katika uchaguzi huo ni pamoja na AFP, CCM, CUF, Jahazi Asilia, NCCR-Mageuzi, NRA na Tadea.

“Matokeo yanaonyesha kuwa mgombea wa NRA amepata kura 480 sawa na asilimia 0.1, wa CCM kura 179,809 sawa na asilimia 50.1, wa CUF kura 176,338 sawa na asilimia 49.1, Jahazi Asilia kura 803 sawa na asilimia 0.2, NCCR kura 363 sawa na asilimia 0.1, NRA kura 525 sawa na asilimia 0.1 na Tadea kura 497 sawa na asilimia 0.1,” alisema Mwinyichande.

Tofauti na ilivyokuwa kwenye chaguzi zilizopita, jana hali ilikuwa shwari wakati mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec) akitangaza matokeo ya urais. Shangwe zilizofuata baada ya Dk Shein kutangazwa kuwa mshindi, hazikunakshiwa kwa vijembe vya kuudhi wapinaani kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwenye chaguzi zilizopita.

Hata Maalim Seif alikuwepo wakati wa hafla hiyo na akakubali kwenda mbele kutoa hotuba ya kukubali matokeo ambayo ilijaa hekima na busara ikieleza umuhimu wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande hizo mbili kuu, huku ikitaharidha kuhusu vitendo vinavyoweza kuvuruga maridhiano hayo.

“Kwa mara ya kwanbza uchaguzi umefanyika kwa amani, bila ya vitisho. Kampeni ziliendeshwa kiungwana na kwa ustaarabu,” alisema Maalim Seif ambaye aliwahi kuwa waziri kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

“Nachukua nafasi hii kumpongeza kwa dhati kabisa Dk Ali Mohamed Shein kwa kupata ridhaa ya Wazanzibari atuongoze kwa miaka mitano inayokuja.

“Dk Shein ana uwezo, uzoefu na mahaba kwa nchi yake. Tunatumaini ataongoza kwa busara na hekima kwa lengo la kuunganisha nchi yetu. Naamini kuwa Wazanzibari walifanya maamuzi sahihi Julai 31.

Tarehe hiyo waliamua kuunda serikali shirikishi.” [Dk Shein na Mr Seif wakipongezana mara baada ya tume ya uchaguzi kutoa matokeo] Seif, ambaye alikuwa akizungumza kwa utulivu, alisema uamuzi huo umeweka enzi mpya ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kwamba Wazanzibari wamempa Dk Shein jukumu la kuongoza kwa mara ya kwanza serikali ya umoja.

Lakini mkongwe huyo wa siasa visiwani Pemba na Unguja hakusita kutoa tahadhari kwa Dk Shein na CCM wakati akitaja mambo makuu matatu muhimu. “Kwanza ni shukrani kwa Tume ya Uchaguzi kwa kuendesha uchaguzi ambao ulikuwa na afadhali kulinganisha na chaguzi nyingine,” alisema.

“Lakini kuna dosari ambazo ni lazima zirekebishwe. Mwenye matatizo si wewe mkurugenzi… ni baadhi ya maofisa wako.” Alieleza matatizo ambayo maofisa wa uchaguzi wamekuwa wakiyafanya akisema yanasababisha watu wasiwe na imani na tume. “Jambo la pili ni kwamba Dk Shein ni rais mteule.

Ametangazwa tu kuwa mshindi, lakini hakuna mshindi. Washindi ni Wazanzibari wote na Shein ni mteule tu.” Dk Shein alionya katika suala lake la tatu kuwa baada ya matokeo hayo kusiweo na siasa za kubezana.

“Siasa za kubezana zitachafua hali ya hewa kabisa,” alionya Maalim Seif akimtaka Dk Shein afikishe ujumbe huo kwa viongozi wenzake wa CCM na wanachama wao.

Naye Dk Shein, ambaye huzungumza kwa utaratibu na mpangilio, alimshukuru Maalim Seif kwa hotuba yake, aliyoielezea kuwa ilijaa busara na hekima na kuahidi kutekeleza yote ambayo kiongozi huyo wa CUF aliyazungumzia.

“Nafahamu fika kuwa kazi hii ni nzito… Mungu anisaidie, anipe hekima na busara ili niifanye kwa uadilifu,” alisema Dk Shein. Shein sasa atakuwa na changamoto jipya la kuwa rais wa kwanza kuongoza Zanzibar akishirikiana na chama kikuu cha upinzani, CUF baada ya pande hizo mbili kufikia maridhiano ambayo yalilifanya Baraza la Wawakilishi kuridhia kupitisha sheria inayoruhusu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Kwa mujibu wa muundo mpya wa Serikali ya Zanzibar, mshindi wa uchaguzi mkuu ndiye ataingia Ikulu akiwa rais na mgombea aliyeshindwa atakabidhiwa nafasi ya makamu wa kwanza wa rais.

Muafaka huo ulifikiwa baada ya viongozi wakuu wa vyama hivyo viwili, Rais Amani Abeid Karume kukutana kwa faragha Ikulu na katibu mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad Novemba 4, 2009.

Taarifa iliyotolewa baada ya faragha hiyo ilieleza kuwa wawili hao walizungumzia haja ya kudumisha amani na utulivu pamoja na kuwa na maelewano na ushirikiano baina ya wananchi wote wa Zanzibar.

—————————————————————————–

MGOMBEA WA URAIS WA ZANZIBAR ANAONGOZA KATIKA MAJIMBO 12 YA MJINI MAGHARIBI

Dr. Ali Mohammed Shein

Chama cha mapinduzi CCM kinaongoza katika kura za urais wa Zanzibar kwenye majimbo 12 kati ya 15 ya mkoa wa mjini magharibi, huku chama cha wananchi CUF kikiongoza katika majimbo matano ya wilaya ya Wete.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyichande amesema mgombea wa CCM Dr. Ali Mohammed Shein ameshinda katika majimbo ya Fuoni, Dole, Dimani, Kiembesamaki, Mwanakwerekwe, Bububu, Mfenesini na Mpendae.

Majimbo mengine aliyoshinda Dr. Shein ni Amani, Rahaleo, Kikwajuni na Kwahani wakati mgombea wa CUF Seif Sharif Hamad ameshinda katika majimbo ya Mtoni, Magogoni na Mji Mkongwe.

Wagombea wengine wa vyama vya AFP, TADEA, NCCR-MAGEUZI, NRA, JAHAZI ASILIA na TADEA wamepata kura chini ya asilimia mbili katika majimbo hayo.

Na huko kisiwani Pemba mwandishi wetu alioko katika afisi ya uchaguzi wilaya ya Wete amesema kwa mujibu wa matokeo yaliotolewa na afisi hiyo kwa majimbo ya Kojani, Wete, Konde, Gando na Mtambwe, mgombea wa CUF Hamad anaongoza katika majimbo hayo

Tume ya uchaguzi Zanzibar imesitisha kwa muda kutangaza matokeo ya urais wa Zanzibar katika majimbo yaliobakia hadi saa 3.00 asubuhi hii, lakini matokeo ya uwakilishi na udiwani yameanza kutangazwa katika afisi za uchaguzi za wilaya.

Uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa mfumo wa vyama vingi kwa mara ya kwanza umefanyika kwa amani na utulivu ikilinganishwa na chaguzi tatu zilizopita.

——————————————————————————————-

TUME YA UCHAGUZI TANZANIA IMEAHIRISHA UCHAGUZI WA MAJIMBO MANNE YA ZANZIBAR

Tume ya taifa ya uchaguzi NEC katika wilaya ya magharibi imeahirisha uchaguzi wa wabunge katika majimbo matatu ya wilaya ya magharibi kwa muda usiojulikana.

Akizungumza na Zenji Fm radio msimamizi wa uchaguzi NEC wilaya ya magharib Amina Talib Ali ameyataja majimbo hayo ni Magogoni, Mtoni na Mwanakwerekwe.

Amesema kuahirishwa kwa uchaguzi huo kunatokana na upungufu wa karatasi za kupigia kura zilizopokelewa kwa wagombea hao na kutaja upungufu huo ni wa kibinadamu

Hata hivyo Amina amewataka wapiga kura katika majimbo hayo kutovunjika moyo na kuwataka kuzitunza shahada za kupigia kura hadi pale itakapotangazwa tarehe nyingine ya kufanyika uchaguzi huo.

Wakati huo huo tume ya uchaguzi ya taifa NEC imeahirisha uchaguzi katika jimbo la Wete kutokana na jina la mgombea ubunge wa chama cha TLP kutoonekana katika karatasi ya kupigia kura.

Hata hivyo kazi za upigaji kura katika mkoa wa Kaskazini Pemba zimendelea vizuri licha ya kujitokeza matatizo katika baadhi ya vituo vya kupigia kura.

Katika jimbo la Ole kumejitokeza upungufu wa karatasi za kupigia kura kwa wabunge na rais wa jamhuri ya muungano Tanzania hali iliyosababisha kuchelewa kuanza kwa upigaji kura.

———————————————————————————————-

ZANZIBAR YAFANYA UCHAGUZI KWA AMANI NA UTULIVU

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania umeanza vizuri, licha ya kuwepo kwa kasoro ndogo zilizosababisha baadhi ya majimbo ya matatu ya ubunge na wadi tisa kwa Zanzibar kutofanyika kutokana na hitilafu za karatasi za kupigia kura. Miongoni mwa wadi zilizoahirishwa uchaguzi huo ni Kajengwa, Mangapwani, Mchangani, Kwahani Miembeni, Nyerere na wadi tatu za Pemba na majimbo yaliohirishwa uchaguzi ni Mtoni, Mwanakwerekwe na Magogoni. Mwandishi wetu alietembelea vituo vya kupigia kura Mwanakwerekwe amesema baadhi ya mawakala wamelalamikia uhaba wa vitabu vya kupigia vya urais wa jamhuri ya muungano. Wakala wa CUF katika kituo cha Mwanakwerekwe amesema vitabu vilivyotarajiwa kuwepo katika vituo hivyo ni vitano, lakini vimefika vitatu hivyo kuna uwezekano kwa watu wengine kukosa kupiga kura. Akizungumzia suala hilo mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Tanzania Rajab Kiravu amesema tayari makamishna wa tume hiyo wanafuatilia matatizo hayo katika vituo vya Tanzania bara na Zanzibar…

Nae mgombe mwenza wa chama cha ATPP-MAENDELEO Rashid Mchenga amesema iwapo baadhi ya wananchi watakosa kupiga kura kutokana na uchache wa vitabu uchaguzi utarejewe kulingana na sheria Hata hivyo akizungumza na Zenji Fm radio amesema uchaguzi umefanyika kwa amani na utulivu na kuwataka wagombea kukubali matokeo kwa maslahi ya taifa lao…

Na huko Tanzania bara baadhi ya wapiga kura mjini Dar es Salaam walilalamika tatizo la kutokuwemo kwa majina yao katika orodha ya wapiga kura. Kazi za kuhesabu kura zinatarajiwa kuanza katika vituo vyote vya kupigia kura na matokeo yake yatabandikwa katika vituo hivyo

—————————————————————————————–

TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR IMEAHIRISHA UCHAGUZI KATIKA WADI NNE ZA MKOA WA MJINI MAGHARIBI

Tume ya uchaguzi Zanzibar imeahirisha uchaguzi wa madiwani katika wadi nne za mkoa wa mjini magharibi kutokana na kukosewa kwa uchapishaji wa karatasi za kupigia kura kwa wagombea hao.

Akizungumza na waandishi wa habari huko hoteli ya Bwawani mkurugenzi wa tume hiyo Salum Kassim Ali amezitaja wadi hizo ni Mchangani jimbo la Mji mkongwe, Kwahani jimbo la Kwahani, Miembeni jimbo la Kikwajuni na wadi ya Nyerere jimbo la Magomeni.

Amesema hali hiyo inatokana na baadhi ya majina ya wagombea kuonekana katika wadi ambazo hawahusiki kupigiwa kura na baadhi ya wapiga kura kulazimika kupiga kura wadi sio zao.

Hata hivyo mkurugenzi huyo amesema uchaguzi wa madiwani katika wadi hizo utafanyika Jumapili ijayo  tarehe 28 mwezi ujao na hakutakuwa na kampeni wala uteuzi wa wagombea.

Wakati huo huo Ali amesema vifaa vya kupigia kura zikiwemo karatasi za kupigia kura tayari vimeshasambazwa katika vituo vyote vya kupigia kura vya Unguja na Pemba vipatavyo elfu moja, 291.

Uchaguzi mkuu wa nne wa Zanzibar wa mfumo wa vyama vingi unatarajiwa kufanyika kesho ambapo jumla ya wapiga kura laki nne elfu saba, 658 watapiga kura kuwachagua wagomea urais wa Zanzibar, muungano, wawakilishi, wabunge na madiwani.

————————————————————————————————

TANZANIA YAINGIA KATIKA UCHAGUZI MKUU

Wananchi wakiwa katika foleni ya kupiga kura

Wananchi wa Tanzania wanapiga kura katika uchaguzi mkuu wa rais, bunge, uwakilishi na udiwani  Jumapili ya tarehe 31 Octoba mwaka 2010.

Uchaguzi huo wa nne wa vyama vingi vya siasa kwa upande wa Zanzibar unaonekana kuwa na mchuano mkali kati ya mgombea wa urais wa CCM Dr. Ali Mohammed Shein na mgombea wa CUF Seif Sharif Hamad.

Jumla ya wapiga kura laki nne, elfu saba, 658 kwa upande wa Zanzibar watapiga kura kuwachagua wagombea urais wa jamhuri ya muungano Tanzania, urais wa Zanzibar, wabunge, wawakilishi na madiwani katika vituo vya kupigia kura vipatavyo elfu moja, 291 Unguja na Pemba.

Na huko Tanzania bara wapiga kura watawachagua wagomea urais wa jamhuri ya muungano, wabunge na madiwani. Kampeni za uchaguzi huo mkuu zinatarajiwa kumalizika rasmi hapo kesho

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetenga zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kugharamia uchaguzi mkuu wa Zanzibar.

—————————————————————————————-

MAALIS SEIF AHIDI KUKUBALI MATOKEO YA UCHAGUZI

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF Seif Sharif Hamad amesema yuko tayari kukubali matokeo ya uchaguzi na kuwataka wafuasi wa chama hicho kutiofanya vurugu wakati wa kutangazwa matokeo hayo.

Hata hivyo mgombea huyo ametoa wito kwa tume ya uchaguzi Zanzibar kuendesha uchaguzi wa haki na huru na kuwasimamia maafisa wake wa wilaya ambao wanatiliwa shaka ya kutaka kuchafua uchaguzi.

Akizungumza katika mkutano wa mwisho wa kampeni za uchaguzi huko viwanja vya Maisara Maalim Seif amesema wakati umefika kwa wazanzibar kuachana na siasa za chuki na kuanza kutafuta njia za kujiiinua kimaendeleo.

Amesema wazanzibar wana kila sababu ya kuendeleza maridhiano ya kisiasa yanayolenga kuijenga Zanzibar mpya

Kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa itakayoundwa baada ya uchaguzi amesema endapo ataingia madarakani atahakikisha serikali hiyo inawajumuisha wazanzibari wote bila kujali udini na ukabila.

Amesema ataingoza Zanzibar kwa kutumia utawala wa sheria na hakuna kiongozi hata mmoja atakaekuwa juu ya sheria ili kuona kila mwananchi anapata haki yake.

Aidha mgombea huyo amesema endapo wananchi watamchagua serikali yake itaimarisha uchumu kwa asilimia 15 utakaolenga kuinua maisha ya wananchi kwa kuongeza nafasi za ajira.

——————————————————————————————

RAIS KIKWETE KUONDOA SUALA LA MAFUTA KWENYE MUUNGANO

Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dr. Jakaya Kikwete ameahidi kulipatia ufumbuzi tatizo la uchimbaji wa mafuta ya Zanzibar katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Amesema matatizo mengi yaliodaiwa kuwa kero ya muungano tayari yameshapitiwa ufumbuzi, kupitia kamati ya pamoja ya waziri mkuu na waziri kiongozi na maeneo yaliobakia ikiwemo suala la uchimbaji wa mafuta ya Zanzibar kuondolewa katika muungano litapatiwa jawabu

Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo Zenji Fm radio imetangaza moja kwa moja rais Kikwete pia ameahidi kuimarisha sekta ya uwekezaji ili kulipatia ufumbuzi tatizo la ajira.

Amesema tatizo la ajira kwa vijana bado ni kubwa nchini, lakini amesema endapo atachaguliwa tena kuiongoza Tanzania serikali yake itawavutia wawakezaji kwa kuwawekea mazingira mazuri.

Rais Kikwete amesema mpango huo utakwenda sambamba na kuwawezesha wakezaji wazalendo kwa kuwapatia mikopo ya kuwekeza katika viwanda, huduma na biashara ili kusaidia ukuwaji wa uchumi.

Aidha Dr. Kikwete amesema serikali yake itaanzisha benki ya wakulima na kuongeza fedha katika taasisi za fedha zinazotoa mikopo yenye masharti nafuu ili kuwawezesha wananchi kujiajiri na kuwajiri wengine…….)

Chama hicho kimeonyesha wasiwasi wa kuwepo kwa vitendo vya rushwa baada ya wagombea wao kushawishiwa hali iliyosababishwa kushindwa kurejea fomu za kuwania nafasi hizo.

Mwenyekiti wa CUF taifa Prifa Ibrahim Harouna Lipumba amesema wagombea wao hawakurejesha fomu katika mazingira ya kustajabisha na iwapo TAKUKURU ingefanya kazi inavyopaswa wagombea wao wasingelinunuliwa.

Akizungumza na BBC Profisa Lipumba amesema ……

Chama cha wananchi CUF kinatarajia kuzindia kampeni zake mwishoni mwa wiki hii huku kikipishana kwa siku moja na chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

————————————————————————————————–

 

Profisa Ibrahim Lipumba

Chama cha CUF wakamilisha kampeni za uchaguzi, Tanzania Bara

Leo Chama cha Wananchi , CUF, huko Tanzania kinakamilisha kampeni zake za uchaguzi wa urais , ubunge na wa madiwani katika nchi hiyo kwa upande wa Bara.

Watakuwa na mkutano wa hadhara mjini Dar es Salaam ambao utahutubiwa na mtetezi wa urais wa chama hicho kwa urais wa Jamhuri ya Muungano, Profesa Ibrahim Lupumba, na pia  mtetezi wa chama hicho kwa urais wa Visiwani Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad.

Mwenzangu Othman Miraji muda mfupi uliopita alifanya mahojiano kwa njia ya simu na Profesa Lupumba…vipi anatathmini kampeni yake, imekwenda vipi?

Interview Othman/Ibrahim Lupumba

Mhariri:Aboubakary Liongo

Na huko Zanzibar Tume ya Uchaguzi ya leo ilikuwa na mkutano kuwaarifu waangalizi wa ndani na nje kuhusu walikofikia katika matayarisho ya uchaguzi mkuu unaowadia jumapili hii ijayo.

Kutoka visiwani Zanzibar Mohamed Abdulrahman ametuletea ripoti ifuatayo

————————————————————————————————

MGOMBEA URAIS ZANZIBAR KUPITIA NCCR-MAGEUZI AHIDI KUJENGA CHUO KIKUU PEMBA

Haji Ambar Khamis

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha NCCR-Mageuzi Hajji Ambari Khamis ameahidi kujenga kiwanda cha matunda na uchongaji wa matofali huko Uwandani katika jimbo la Wawi endapo ataingia ikulu.

Amesema wananchi wa Uwandani na Ole ni wazalishaji wa embe na tungule lakini hizana soko la kuridhisha hasa wakati wa msimu kuwepo kwa viwanda vya kusindikia matunda vitawasaidika kujiongeze akipato.

Akizunguma katika mkutano wa kampeni Khamis amesema kuwa iko haja kujenga kiwanda cha mashine za kukatia matofali huko Uwandani, kutokana kuwa na raslimali nyingi ya mawe na kuendelea kukata kwa kutumia msumeno ni kuhatarisha maisha yao.

Aidha mgombea huyo pia ameahidi kujenga chuo kikuu katika mkoa wa Kusini Pemba,pindi atakapopata ridhaa ya kuchakuliwa kuwa rais wa Zanzibar

October 28, 2010 skaska Leave a comment Edit this
Categories: Uncategorized

ZANZIBAR YAKARIBISHA WANGALIZI WA UCHAGUZI

Khatib Mwinyichande

Wangalizi wa uchaguzi kutoka taasisi za ndani na kimataifa wametakiwa kutoegemea upande wowote wa vyama vya siasa kwa vile ushauri wao unategemewa kuimarisha mfumo wa uchaguzi nchini.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyichande amesema hayo katika mkutano wa kuwakaribisha wangalizi wa uchaguzi kutoka taasisi huko hoteli ya Bwawani.

Amesema tume ya uchaguzi Zanzibar imekuwa na uzowefu mkubwa wa kuendesha shughuli za uchaguzi, lakini itahakikisha mapendekezo yatakaoyotelewa na taasisi hizo mara baada ya upigaji kura yatazingatiwa ili kuimarisha chaguzi zijazo.

Aidha Mwinyichande amewaonya wangalizi hao kutokuwa waamuzi wa mwisho hasa katika utangazaji wa matokeo na kusema tume ya uchaguzi ndio yenye mamlaka pekee ya kutangaza matokeo ya mwisho

Jumla ya wananchi laki nne, elfu saba, 658 Jumapili ijayo wanatarajiwa kumchagua rais wa Zanzibar kati ya wagombea saba wa vyama vya siasa waliojitokeza kuwania nafasi hiyo, rais wa jamhuri ya muungano Tanzania, wabunge, wawakilishi na madiwani.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetenga zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kugharamia uchaguzi mkuu wa Zanzibar.

————————————————————————————

MWENYEKITI WA TLP AGUSTINE LYATONGA ADAI KUFANYIWA RAFU KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI

AGUSTINE LYATONGA

Mgombea ubunge jimbo la Vunjo ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour TLP, Agustine Mrema, amenusurika kujeruhiwa na kundi la vijana aliodai wafuasi wa Chama cha Mapinduzi CCM.

Akizungumza na Zenji Fm radio Mrema amesema mbali ya kunusurika katika tukio hilo, gari lake liliharibiwa vibaya kwa kupigwa mawe na vioo vyote vya mbele vya gari yake vimepasuliwa.

Amesema tukio hilo, limetokea Jumamosi iliyopita katika eneo la njia panda la Himo, Moshi wakati Mrema alipokuwa akipita barabara kuu karibu na eneo ambalo mgombea ubunge wa CCM, Crispin Meela, alikuwa akifanya mkutano wa kampeni za kuomba kura

—————————————————————————————–

WAANGALIZI WA UCHAGUZI WAMEANZA KUSAMBAZWA KUANGALIA UCHAGUZI MKUU 2010

Kamati ya kuangalia mwenendo wa uchaguzi Tanzania TEMCO imesema inashindwa kutekeleza shughuli za uangalizi wa chaguzi zinazofanyika nchini kutokana na uhaba wa fedha.

Mratibu wa TEMCO DR. Benson Banner amesema taasisi hiyo inayofanya kazi muhimu, lakini haipokei fungu lolote la fedha kutoka serikalini na badala yake hutegemea wahisani wenye masharti magumu.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari wa utowaji wa taarifa ya mwenendo wa uchaguzi mwaka 2010 mjini Zanzibar amesema hali hiyo imeifanya TEMCO kuwa na wangalizi wachache ikilinganishwa na ukubwa wa maeneo ya uchaguzi Tanzania.

Dr. Banner amesema taasisi za ndani zina uwezo mkubwa wa kuendesha shughuli za uangalizi wa chaguzi zinazofanyika nchini ikilinganishwa na taasisi za kimataifa, lakini bado haiziwezeshwi kifedha na serikali

Nae makamo mwenyekiti wa tume hiyo Maryam Abdulrahman amesema TEMCO inatarajia kutuma wangalizi wa uchaguzi elfu saba, 210 katika majimbo yote ya Tanzania bara na Zanzibar kuangalia mwenendo wa uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu.

Amesema wangalizi hao wa muda mrefu na mfupi watatumwa majimboni na kwenye vituo vya kupigia kura kuangalia undeshaji wa kampeni, upigaji na kuhesabu kura, utowaji wa matokeo, malalamiko na ukataji wa rufaa ambapo taarifa zake zitatolewa ndani ya siku tano baada ya upigaji wa kura.

TEMCO ni taasisi ya ndani inayoundwa na taasisi mia moja na 52 imekuwa ikiangalia mwenendo wa uchaguzi Tanzania tokea mwaka 1995.

————————————————————————————-

CHAMA CHA NLD, ZANZIBAR KUMUUNGA MKONO MGOMBEA WA URAIS ZANZIBAR KUPITIA CCM DR. ALI SHEIN

Chama cha siasa cha NLD, kimekuwa chama cha kwanza cha upinzani kutangaza kumuunga mkono mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dr. Ali Mohammed Shein katika uchaguzi mkuu ujao. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, naibu katibu mkuu wa NLD, Zanzibar Rashid Ahmme Joy amesema chama hicho kimeamuwa kumuunga mkono mgombea huyo kutokana na sera zake zenye kulenga siasa za umoja na kuweka mbele maslahi ya Zanzibar. Amesema chama hicho bado kina wasiwasi na wagombea wengine wa vyama vya kwamba hawatoweza kuendeleza siasa za umoja kwa kile alichodai kuwa na ulafi wa madaraka… “Sisi tutamuunga mkono mgombea atakaeleta mabadiliko na wagombea wa vyama vya upinzani watakapokuja hujui watafanya nini, hivyo mgombea wa CCM Dr. Shein ameonesha mwelekeo wa kufuata sera za siasa za umoja wa nchi”. Alisema Joy. Joy ambae kwa muda wa miezi kadhaa hajaonekana hadharani kutokana na kuugua shindikizo la damu amesema hali yake inaendelea vizuri na wiki mbili zijazo anatarajia kushiriki katika harakati za siasa. Hivyo amewaahidi wafuasi na wapenzi wa chama cha NLD ataendelea kuwepo katika ulingo wa kisiasa kwa lengo la kuleta mabadiliko ya mfumo wa siasa wa vyama vingi hasa Zanzibar. Chama cha NLD hakijasimamisha mgombea wa nafasi ya urais Zanzibar kutokana na Joy alietarajiwa kugombea nafasi hiyo kuugua siku chache baada ya tume ya uchaguzi Zanzibar kuanza kazi za utowaji wa fomu kwa wagombea wa nafasi hiyo kupitia vyama vya siasa. Hivi karibuni chama kingine cha upinzani cha APPT-MAENDELEO kimetangaza kumuunga mkono mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananachi CUF Seif Sharif Hamad. END

————————————————————————————————

CHADEMA YATAKA RAIS KIKWETE AWEKEWE PINGAMIZI

Chama cha Demokraisa na maendeleo CHADEMA kimewasilisha malalamiko kwa msajili wa vyama vya siasa kikitaka mgombea wa urais wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM rais Jakaya Kikwete awekewe pingamizi katika kinyanganyiro cha uchaguzi wa urais.

Hoja kuu ya CHADEMA kuweka pingamizi ni kwa serikali kupandisha mishahara ya wafanyakazi waliokusudia kugoma wakati wa mkutano wa uchumi wa dunia, lakini rais Kikwete wakati huo alisema hawezikupandisha mishahara.

Kaimu katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika amesema hatua ya sasa ya serikali kupandisha mishahara ya watumishi wa umma inahesabiwa kama yenye kutaka ungwaji mkono na wafanyakazi.

Mnyika amedai suala la nyongeza wa mishahara kwa wafanyakazi halikuongezwa na bunge kama vile ilivyopendekezwa hivyo suala hilo linatumiwa kama kampeni za mgombea huyo na kwenda kinyume na sherria ya gharama za uchaguzi

————————————————————————————

Chama cha NCCR –Mageuzi kimezindua rasmi ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010 jijini Dar es salaam ikiainisha Ajenda 12 ikiwemo kuundwa kwa katiba mpya ,kuimarisha uchumi , huduma za jamii na kuanzisha mpango wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho Hashim Rungwe amesema uimarishwaji wa uchumi na kukuza raslimali za nchi zitatiliwa mkazo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa Jems Mbatia amewashauri wagombea wa nafasi mbali mbali za kisiasa kufanya kampeni zinazolenga kujenga umoja wa kitaifa .

Uzinduzi rasmi wa Kampeni za Chama cha NCCR Mageuzi kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao zimepangwa kufanyika Septemba 11 baada ya kukamilika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

————————————————————————————————–

MGOMBEA URAIS KUPITIA SAU ASHINDWA KUREJESHA FOMU

Ikiwa leo ni siku ya mwisho kurejesha fomu za kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar, mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama Cha Sauti ya Umma (SAU) Haji Mussa Kitole ameshindwa kurejesha fomu za kuwania nafasi hiyo kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Kitole awali alikataliwa kupewa fomu ya kuwania nafasi hiyo na ZEC kutokana na kuwa chama hicho kimetoa wagombea urais wawili wenye kutaka kuwania urais wa Zanzibar wakati sheria za ZEC zinaeleza chama kitowe mgombea mmoja wa nafasi hiyo.

Vyama ambavyo vimerejesha fomu leo katika afisi hiyo ni NCCR-MAGEUZI, TADEA, AFP, NRA, Jahazi Asilia huku chama cha SAU kikiwa bado hakijarejesha fomu hiyo.

Akizungumza na Zenji fm radio afisa wa habari wa tume ya uchaguzi Zanzibar Idriss Haji Jecha amesema hadi kufikia saa 9.45 cha cha SAU bado hakijarejesha fomu ambapo muda wa mwisho ulikuwa saa 10.00 jioni.

Amesema katika urejeshaji wa fomu hizo hakukuwa na kasoro zozote na fomu zilizorejeshwa zilikuwa safi.

SAU ndio chama pekee kilichoshindwa kuwasilisha fomu zake kwa tume ya uchaguzi ambapo vyama vyengine vilivyorejesha fomu zake jana ni pamoja Juma Ali Khatib (46) -TADEA, saa 4:13 asubuhi, Said Soud Said (62) AFP,saa 5:00, Haji Ambar Khamis (44) NCCR–Mageuzi, saa 5:30, Kassim Bakari Ali (43) Jahazi Asilia, saa 7.06, na Haji Khamis Haji (60) NRA saa 8:20 mchana.

Wengine waliorejesha fomu zao kwa ZEC wa mwanzo ni ni Mgombea wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ((67) alirejesha Agosti 16 majira ya saa 9:00 mchana wakati mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Dk Ali Mohammed Shein (62) alijesha fomu yake Agosti 18 majira ya saa 8:30 mchana.

Akizungumza katika kikao hicho baada ya kupokea fomu hizo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Khatib Mwinchande alisema kwao wao kujitokeza kwa wagombea wengi ni kupanuka kwa demokrasia nchini.

Mwenyekiti huyo aliwaomba wagombea wote ambao watateuliwa na tume kuingia katika mchakato wa kutaka urais baada ya kuhakikiwa fomu zao kuingia katika kampeni za kistaarabu zisizo na matusi ili kuepusha Zanzibar kuingia katika sura mbaya ya kukosekana amani.

Iwapo wagombea urais kutoka vyama hivyo hawatawekewa pingamizi uchaguzi mkuu kwa nafasi ya urais unatarajiwa kufanyika Octoba 31 mwaka huu utakuwa na wagombea saba.

——————————————————————————————————

Chama cha NCCR –Mageuzi kimezindua rasmi ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010 jijini Dar es salaam ikiainisha Ajenda 12 ikiwemo kuundwa kwa katiba mpya ,kuimarisha uchumi , huduma za jamii na kuanzisha mpango wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho Hashim Rungwe amesema uimarishwaji wa uchumi na kukuza raslimali za nchi zitatiliwa mkazo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa Jems Mbatia amewashauri wagombea wa nafasi mbali mbali za kisiasa kufanya kampeni zinazolenga kujenga umoja wa kitaifa .

Uzinduzi rasmi wa Kampeni za Chama cha NCCR Mageuzi kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao zimepangwa kufanyika Septemba 11 baada ya kukamilika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

————————————————————————————————

MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KUPITIA CCM DR. SHEIN AREJESHA FOMU

Dr. Ali Mohammed Shein

Mgombea wa urais Zanzibar kupitia CCM Dr. Ali Mohammed Shein amesema ataitumikia Zanzibar kwa ufanisi mkubwa na kuweka mbele maslahi ya wananchi.

Akizungumza na wana CCM huko Kisiwandui muda mfupi baada kurudisha fomu za kuwania nafasi hiyo katika tume ya uchaguzi Zanzibar amesema atashirikiana vizuri na viongozi watakaokubali kufanyakazi kwa maslahi ya Zanzibar.

Aidha Dr. Shein ameonya kuwa hatamvumilia kiongozi yoyote ambae atakwenda kinyume na matakwa ya Wazanzibar endapo ataingia madarakani ……

Dr. Shein amesema katika uchaguzi ujao, CCM imejiandaa kuendesha kampeni za kistaarabu zenye kuwaelekeza wananchi malengo ya chama hicho ili wakipe ridhaa tena ya kuiongoza Zanzibar.

Nae naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar Saleh Ramadhan Ferouz amewataka wafuasi wa chama hiho kupuuza matamshi yanayotolewa na baadhi ya watu kwamba kumtilia kura kiongozi wa upinzani ni sawa na kumpigia mgombea wa CCM.

Amesema watu hao wanaopotosha wana CCM kwa kusambaza vipeperushi vyenye ujumbe huo, amewataka wafuasi wa chama hicho kuwa makini juu ya mbinu hizo zinazofanywa na vyama vya upinzani.

Dk . Shein anakuwa mgombea wa pili kurejesha fomu zake kwa tume ya uchaguzi Zanzibar kati ya wagombea wanane waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba 31 mwaka huu.

August 27, 2010 skaska Leave a comment Edit this
Categories: Uncategorized
————————————————————————————–

TANZANIA YATAKIWA KUBADILISHA KATIBAProfis Lipumba

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya muungano Tanzania kupitia chama cha wananchi CUF Profia Ibrahim Harouna Lipumba amesema wakati umefika kwa watanzania kurekebisha katiba ili kuruhusu mgombea binafsi na kupanua wigo wa demokrasia nchini.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni wa chama hicho kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao mjini Dar es Salaam Profisa Lipumba amesema kutokuwepo kwa fursa hiyo kunanyima mianya ya demokrasia na kuwacha watu wenye sifa za kuongoza kutokana na kutojiunga na vyama vya siasa.

Aidha Profisa Lipumba amesema endapo atachaguliwa kuwa rais amesema atapunguza umasikini unaowakabili watanzania……

Hii ni mara ya nne kwa profisa Lipumba kuwania urais wa Jamhuri ya muungano Tanzania kupita CUF tangu mfumo wa vyama vingi kuanza mwaka 1992.

August 27, 2010 skaska Leave a comment Edit this
Categories: Uncategorized
————————————————————————————–

CHADEMA KUMUWEKEA PINGAMIZI RAIS KIKWETE

Dr. Wilbord Slaa

Kaimu katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA John Mnyika amesema chama hicho kinaendelea na taratibu zake katika afisi ya msajili wa vyama vya siasa na tume ya uchaguzi ya taifa kupinga kile alichodai mgombea wa urais kupitia CCM rais Jakaya Kikwete kukiuka sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010.

`      Wakati CHADEMA ikiendelea na harakati hizo naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania Bara Peuce Msekwa amesema mgombea huyo hajavunja kifungu chochote cha sheria na inasubiri suala hilo liwasilishwe katika afisi husika ili itowe utetezi wake.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa mgombea urais wa wa CHADEMA Dr. Wilbord Slaa amepanga kuwasilisha pingamizi kwa msajili wa vyama vya sisasa nchini John Tendwa kwa madai mgombea urais wa CCM rais Jakaya Kikwete amevunja kifungu nambari 21  cha sehria ya gharama za uchaguzi.

———————————————————

TUME YA UCHAGUZI TANZANIA KUSHTAKIWA

Chama cha Sauti ya Umma SAU kimetishia kuishtaki tume ya taifa ya uchaguzi NEC kufuatia tume hiyo kukitoa chama hicho kushiriki kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi utakaofanyika Octoba 31 mwaka huu.

Chama kingine kilichozuiliwa kushiriki katika uchaguzi huo ni Democratic Party D.P ambavyo vinadaiwa kutotimiza masharti ya kuingia katika kinyanganyiro hicho.

Jana ni siku ya mwisho kwa tume hiyo kuwateuwa wagombea wa nafasi hiyo na majina yao kubandikwa katika afisi za tume nchini ili kutolewa pingamizi.

Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Jaji Lewis Makame amesema tume hiyo imezingatia masharti ya uchaguzi kwa kukiengua chama cha SAU

Hata hivyo vyama vya Democrasia Makini, NRA na Jahazi Asilia havikurejesha fomu zao na hivyo kuondolewa kushiriki katika uchaguzi huo

———————————————————————————–

UFISADI ZANZIBAR MDOGO

Chama cha Jahazi Asilia kimesema suala la ufisadi kwa Zanzibar bado ni dogo ikilinganishwa na nchi nyingine duniani kutokana na kuwa na vyanzo vichache vya mapato.

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho Kassim Ali Bakar amesema hayo huko tume ya uchaguzi Zanzibar wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.

Amesema Zanzibar inategemea zaidi sekta ya utalii na karafuu kama mihimili wa uchumi, hali iliyosababisha kuwa na pato dogo lisilozidi shilingi bilioni moja kwa mwezi

Mgombea huyo amesema endapo chama chake kitaongeza Zanzibar katika uchaguzi ujao kitaanza kupiga vita ufisadi huo mdogo kabla ya kuanzisha vianzio vikubwa vya ukusanyaji wa mapato.

Aidha amesema mabadiliko ya katiba yaliofanywa hivi karibuni na baraza la wawakilishi yamekisaidia chama hicho kuifanya Zanzibar kuwa na sera yake ya kiuchumi badala ya kutumia sera ya muungano.

Bakar amesema matatizo yaliomo ndani ya muungano yanaendelea kuathiri uchumi wa Zanzibar na kuonekana tofauti na uchumi wa Tanzania bara, hivyo asema suluhisho lake ni kuunda serikali tatu.

Amesema mwelekeo wa Jahazi Asilia katika mfumo mpya wa serikali ijayo ya umoja wa kitaifa ni kuendeleza uzanzibari na maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa hivi karibuni

Hadi sasa jumla ya wagombea saba wa vyama vya siasa  wamejitokeza kuchukua fomu za  kuwania urais wa Zanzibar ambao ni kutoka chama cha CCM, CUF, AFP, SAU, NCCR-Mageuzi na Jahazi Asilia, huku chama cha NRA kimejitoa kutokana na mgombea wake Rashid Ahmmed Joy kuugua shindikizo la damu.

———————————————————————————

RAIS OBAMA APONGEZA KURA YA MAONI ZANZIBAR

Rais Barack Obama

Rais wa Marekani Barack Obama amempongeza rais Jakaya Kikwete kwa kukamilisha mpango wa maridhiano ya kisiasa Zanzibar na kufanikiwa kwa kura ya maoni ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.

Rais Obama ametoa salamu hizo za pongezi kwa rais Kikwete kupitia kwa ujumbe maalum uliowasilishwa na balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso katika mazungumzo yao yaliofanyika ikulu mjini Dar es Salaam.

Katika salamu hizo rais Obama amesema ni jambo la kutia moyo katika kipindi kifupi cha mwaka mmoja ongozi wa serikali ya awamu ya nne na tume ya uchaguzi Zanzibar na taasisi nyingine zimefanikisha kura ya maoni kwa kuridhia serikali ya umoja wa kitaifa kwa zaidi ya asilimia 60.

—————————————————————————–

RAIS KARUME ATIA SAINI MAREKEBISHO YA KATIBA YA ZANZIBAR

Rais Aman Abeid Karume

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume ametia saini muswada wa sheria wa marekebisho ya kumi ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yenye lengo la kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Akizungumza na Zenji fm radio katibu wa baraza la wawakilishi Ibrihim Mzee Ibrahim amesema muswada huo uliopitishwa na baraza la wawakilishi tarehe tisa mwezi huu yametiwa saini na rais Augus 13.

Amesema marekebisho hayo tayari yameshaingizwa katika katiba ya Zanzibar kuanzia tarehe 13 mwezi huu na kinachosubiriwa ni kutolewa kwa nakala mpya ya katiba

Hata hivyo Ibrahim amesema mfumo wa undwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa umeshatandikwa na kinachosubiriwa ni nia njema na kuaminiana kwa wanasiasa juu ya utekelezaji wa serikali hiyo.

———————————————————————–

DR. SHEIN APUNGUZA JOTO KWA WANA CCM

Makamo wa rais Dr. Ali Mohammed Shein

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Dr. Ali Mohammed Shein amesema serikali ya CCM haitakubaliana na kiongozi atakaekuwa serikalini kwa kutumia madaraka kwa maslahi yake binafsi.

Akizungumza na wagombea wa ubunge, uwakilishi na udiwani huko hoteli ya Bwawani  amesema ukimya wake hautamfanya kuwa mlegevu katika utekelezaji wa majukukumu yake.

Dr. Shein ambae ni mgombea urais wa Zanzibar amewaahidi wanachama hao endapo atapata ushindi atahakikisha anaendesha nchi kwa misingi ya haki, upendo na maelewano huku suala la nidhamu ndio msingi wa wananchi kujikwamua kimaisha.

Amesema viongozi wenye tabia ya kuendeleza chuki na kupenda madaraka hatowapa nafasi kwa vile mambo hayo  yanachangia kuzusha mifarakano ndani ya jamii ya wazanzibari..

Aidha Dr. Shein amewataka wana CCM kusafisha nyoyo zao na kuondokana na chuki na ubinafsi zilizojitokeza katika kinyanganyiro cha urais, ubunge, uwakilishi na udiwani katika kura za maoni.

Amesema wanachama wa CCM wanapaswa kukusanya nguvu zao katika kukipatia ushindi chama hicho na utaratibu wa kura za maoni ulikuwa muhimu katika kutafuta viongozi ndani ya chama.

Nae naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar Saleh Ramadhan Ferouz amesema chama hicho kitaendesha kampeni za zinazotarajiwa kuanza mwezi ujao kuelezea mafanikio ya ilani ya uchaguzi na sio kuelezea kero.

Amesema CCM imeweza kutekeleza ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2005 kwa asilimia kubwa hasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kiuchumi na kijamii pamoja na kutekeleza utawala bora ambapo katika kipindi hicho hakukuwa na mfungwa wa kisiasa

————————————————————————–

SEIF KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS

Seif Sharif Hamad

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF Seif Sharif Hamad amevitolea wito vyombo vya ulinzi na usalama kutoegemea upande wowote wakati wa uchaguzi na badala yake kuheshimu maamuzi ya wananchi.

Amesema chaguzi zilizopita baadhi ya vyombo vya dola vimejingiza katika harakati za uchaguzi na kusahau majukumu yao ya kulinda usalama, hivyo amezitaka taasisi hizo kujiepusha na vitendo hivyo vinavyoweza kuchafua uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar katika afisi za tume ya uchaguzi Hamad amesema vikosi vya ulinzi na usalama havina jukumu la kuamuwa nani anaongeze nchi, lakini katiba ndio inayotoa fursa kwa wananchi kuchagua viongozi wanaowataka….

Aidha Hamad amesema chama cha CUF kitaendesha kampeni za kiungwana ili kuendeleza maridhiano ya kisiasa na hakitaruhusu mgombea wake kutoa maneo ya matusi au kuchafua kampeni za uchaguzi.

Amesema katika kampeni hizo chama chake kitafuata ilani ya uchaguzi ya kushindana kwa hoja na kuvitaka vyama vingine kujiepusha na kampeni za kupakana matope.

Wakati huo huo mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia chama cha Wakulima Said Soud nae amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo katika afisi za tume ya uchaguzi Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hizo amesema chama chake kitashiriki katika uchaguzi huo ili kuotoa ushindani kwa vyama vingine vya siasa

Maalim Seif na Soud ni miongoni mwa wagombea wa nne waliojitokeza kuchukua fomu leo baada ya wiki iliyopita Haji Ambar Khamis kutoka NCCR-MAGEUZI na Juma Ali Khatib kutoka TADEA kuchukua fomu.

Uchaguzi mkuu wa Zanzibar ambao unatarajiwa kuwashirikisha wagombea wa nafasi ya urais sita unatarajiwa kufanyika Octoba 31 mwaka huu na mshindi atakaeshinda atalazimika kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

————————————————————————–

ZANZIBAR HAIJAKIUKA KATIBA YA MUUNGANO

Naibu mwanasheria mkuu George Masaju amesema marekebisho ya katiba ya Zanzibar yaliofanyika wiki hii hayajavunja kifungu chochote cha katiba ya jamhuri ya muungano Tanzania.

Akitoa ufafanuzi juu ya kile kinachodaiwa mkanganyiko wa mabadiliko ya kumi ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yaliofanyiwa marekebisho na baraza la wawakilishi Zanzibar.

Amesema mabadiliko hayo hayajavunja katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Masaju amesema mabadiliko hayo yanampa madaraka rais wa Zanzibar kugawanya mipaka iliyo ndani ya visiwa hivyo na hayataathiri vipengele vilivyomo ndani ya muungano wa Tanzania

Mabadaliko ya katiba hayo ni kifungu cha kwanza cha katiba ya Zanzbiar ambapo awali kilikuwa kikisomeka Zanzibar ni sehemu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania baada ya marekebisho kifungu hicho kitasomeka Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zilizounda jamhuri ya muungano wa Tanzania
————————————————————————

Tume ya uchaguzi Zanzibar imekataa kutoa fomu za kuwania urais wa Zanzibar kwa chama cha SAU kutokana na kujitokeza wagombea wawili wanaowania nafasi hiyo kupitia chama kimoja.

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Salim Kasim amesema  wagombea hao waliojitokeza kuchukua fomu ni Haji  Ramadhani Haji barua yake iliwasilishwa Ogasti 12 na Haji Musa Kitole barua yake iliwasilishwa Agosti 13.

Amesema kwa mujibu wa sheria za uchaguzi kila chama kitalazimika kuteuwa mgombea mmoja kushiriki katika uchaguzi huo, hivyo tume imeshindwa kutoa fomu kwa wagombea wa urais kupitia chama hicho.

Hata hivyo mkurugenzi huyo amesema fomu hizo zinaweza kutolewa kwa chama hicho endapo kitawasilisha barua ya kufuta jina moja kati ya wagombea hao wawili

Haji Mussa Kitole na Haji Ramadhan Haji wote kutoka chama cha SAU wakiwa na barua tofauti wakati kitole akiwa na barua ya Mwenyekiti, Ramdhan alikuja na barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho wote wakidai kupitishwa na chama chao.

Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Zanzibar, Salim Kassim Ali aliwaambia waandishi wa habari kwamba haiwezekani kutolewa fomu mbili kwa chama kimoja kwa kuwa sheria za uchaguzi zimeeleza mgombea mmoja kutoka chama husika ndie anayepaswa kupewa fomu na sio zaidi ya hapo.

“Tume ya uchaguzi tumepokea barua mbili kutoka chama kimoja lakini sheria inasema kila chama kitateuwa mgombea mmoja wa kiti cha urais na lakini baada ya kupokea barua mbili sisi tulichowashauri ni kwamba walete mgombea mmoja ambaye awasilishe barua tume ya uchaguzi ili apewe fomu ya kuwania urais” alisema Kassim.

Hata hivyo wagombea hao walikuwa na maoni tofauti huku kila mmoja akijitetea kwamba ameteuliwa kihalali na chama chake na kutaka mwenzake arudi katika chama ili kupata ridhaa ya mkutano mkuu ambao ndio wenye maamuzi ya mwisho.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Khatib Mwinyichande aliwataka wagombea wote walipopewa fomu za urais kutimiza masharti yaliowekwa katika ujazaji wa fomu hizo ikiwa pamoja na kurejesha kabla ya Agosti 30 mwaka huu zikiambianishwa na dhamana wa shilingi millioni mbili na wadhamini wasiopungua 200 katika mikoa mitano ya Unguja na Pemba
—————————————————————————-

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimejitokeza kumuunga mkono mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF, Seif Sharif Hamad katika uchaguzi mkuu ujao.

Mgombea urais wa Tanzania wa CHADEMA Dr. Wilbord Slaa amesema uwamuzi huo umechukuliwa kwa lengo la kukiongezea nguvu chama hicho ili kushindana na CCM katika uchaguzi wa urais wa Zanzibar

Dr. ambae alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini huko Kibandamaiti mjini hapa amedai Tanzania imejaa ufisadi unaosababisha watanzania kupoteza haki zao zikiwemo ardhi ambao hayana mtetezi.

Amesema suala la maisha bora linalodaiwa na viongozi walioko madarakani bado halijaleta maslahi kwa wananchi hivyo linahitaji mabadiliko hasa katika kudhibiti mfumko wa bei za bidhaa.

Dr. Slaa amesema CHADEMA bado inaendelea kutetea sera ya kuwa na serikali tatu ili wazanzibari na watanzania bara wawe na maamuzi katika mambo yao wanayowahusu.

Amesema chama chake kitaisimamia sera hiyo kwa vile nchi nyingi duniani zilizoungana hazina mfumo wa serikali mbili kama ilivyo Tanzania hali ambayo inainyima Zanzibar fursa za kimataifa ikiwemo misaada na mikopo

CHADEMA kimekuwa chama cha siasa cha pili kutangaza hadharani kumuunga mkono mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia CUF Malim Seif Sharif Hamad baada ya chama cha APPT-maendeleo kutangaza kufanya hiyo
——————————————————————–