Image result for zssf

Mkurugenzi wa mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF Sabra Issa Machano amesema uwekezaji wa miradi ya kiuchumi unaofanywa na mfuko huo umelenga mpango wa serikali wa kuwa na uchumi wa kati.

Amesema awamu ya kwanza ya uwekezaji wa nyumba za kuishi za Mbweni umepata wateja na hivi sasa ZSSF inaendelea na mipango ya kutaka kujenga nyumba za kisasa za watu wa kiwango cha chini eneo la Kwahani.

Akizungumza na wajumbe wa baraza la wawakilishi juu ya marekebisho ya sheria ya mfuko huo huko Mbweni amesema uwekezaji huo unaendelea kuimarisha kifedha mfuko huo.

Sabra amesema kuanzia January hadi March mwaka huu mfuko umewalipa viinua mgongo mwanachama 242 zaidi ya shilingi bilioni 3.8 na shilling bilioni 2.4 za pencheni kwa wanachama elfu nane, 292.

Nao wajumbe wa baraza la wawakilishi wameuomba mfuko huo kuwaelimisha wananchi juu ya marekebisho ya sheria hiyo kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya wanachama wake kukatwa mafao yao.

 

By Zanzibar Islamic News