Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtupia lawama nzito Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuanza kwenda kinyume na makubaliano yaliounda Serikali ya Umoaja wa Kitaifa mwaka 2009.
Akihutubia mamia ya wanachama na mashabiki wa CCM waliohuidhuria mkutano wa hadhara uloiofanyika Jumba la Vigae huko Jang’ombe mjini Unguja leo , Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai amesema Maalim Seif ameanza kufanya vikao vya siri vinavyotishia kuvuruga amani na umoja wa kitaifa Visiwani humu.
Vuia ambaye ni kati ya wajumbe waasis walioshiriki katika mchakato wa mazunguzmzo ya upatanishi wa kisiasa Zanazibar ,amesema kama angeliijua mapema dhamira ya Maalim Seif katika mazungumzo ya kundwa kwa Serikali iliopo , angekuwa radhi kujitoa na kutokuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya muafaka.
Vuai ameiita kauli hiyo ni ya kichochezi na kwamba haikubaliki mbele ya jamii na kuwatolea wito viongozi wa kisiasa na kiserikali kuchunga ndimi zao ili kuyaenzi mazingira yalioleta maridhiano ya kisiasa.
Amesema Maalim Seifa kama anataka litote ili wagawane mbao ni heri akachukua mapema ubao wake na kuelekea Mtwambwe na kwamba CCM haiko tayaro kuona kuona amani ya Zanzibar ikichezewa kwa maslahi binafsi
1 responses to “CCM YAMTUPIA LAWAMA MALIM SEIF”
Sharif
March 6th, 2013 at 08:20
Mtajuwana wenyewe wanasiasa,ila sisi wananchi tunawombeni mtekeleze ahadi zenu ili mjiwekee mazingira mazuri huko kwa Mungu