Meli ya MV Mapinduzi

Meli ya abiria na mizigo M.V Mapinduzi imezama katika bahari ya visiwa vya Ushelisheli ikiwa na mabaharia 13 ambao wameokolewa.

Akizungumza na wandishi wa habari waziri mawasiliano na miundo mbinu Hamad Masoud Hamad amesema meli hiyo imezama njiani wakati ikielekea Yemen kwa ajili ya matengenezo.

Amesema tukio hilo limetokea wakati serikali imeshaiza meli hiyo kwa dola za Marekani laki nne na nusu kwa kampuni ya Badri inayomilikiwa na Abdalla Said ikiwa na usajili wa Zanzibar.

Hamad amesema meli hiyo ilipozama ilikuwa haina mzigo isipokuwa mabaharia 13 wenye uraia wa Pakistan waliokolewa wakiwa hai.

Waziri huyo amefahamisha kuwa meli hiyo ilitarajiwa kurejea Zanzibar kufanya kazi za usafirishaji wa mizigo na abiria baada ya kufanyiwa matengenezo nchini Yemen.

Meli hiyo inasemekana ilizama kutokana na upepo unaovuma katika bahari ha Hindi na serikali ya mapinduzi Zanzibar haitalazimika kumlipa fidia mmiliki wa meli hiyo